Awali ya yote pokea salamu zangu, leo ninataka kukufikirisha tu walau kwa kiduchu, kuwa maisha unayoishi leo ndio yenye hatima ya maisha yako ya baadae.
Kulikuwa na tajiri mmoja na masikini mmoja jina lake Lazaro, tajiri huyu hakumjua wala kumcha Mungu, ila Lazaro alikuwa ni mtu mwema.
Kulikuwa na tajiri mmoja na masikini mmoja jina lake Lazaro, tajiri huyu hakumjua wala kumcha Mungu, ila Lazaro alikuwa ni mtu mwema.
Ikatokea siku wote wakafa, njia ambayo mimi na wewe ni shariti tuipitie, Lazaro alienda Mbinguni, na tajiri motoni;
Luka 16:22 Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.
23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.
24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.
25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.
26 Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.
27 Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu,
27 Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu,
28 kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso.
29 Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.
30 Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu.
Luka 16:31 Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.
Luka 16:31 Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.
kwa nini?
Jibu ni kwamba matendo yao hapa ulimwenguni yaliamua hatima yao, na wewe leo, maisha yako yataamua utakavyoishi baadae, nakushauri kuamua sasa kuokoka ili kuwa katika maisha salama baadae milele.
Kule kuzimu tajiri aliomba ndugu zake wafikishiwe injili, nami na kwambia wakina Musa wa leo ni mimi ninayekutamkia ukweli huu kama Ibrahimu alivyo wataka kutusikiliza, fahamu hakuna mbingu nje ya kuokoka.
Kama upo tayari kuokoka, tafadhali fuatisha maneno haya nami kwa imani, Sema; BWANA YESU, NINAKIRI KUWA MIMI NIMKOSAJI, NINAOMBA UNISAMEHE, NA UIFUTE JINA LANGU KWENYE KITABU CHA HUKUMU NA ULIANDIKE KWENYE KITABU CHA UZIMA, NAKUAMINI KAMA BWANA NA MOKOZI WANGU, Amen.
Hongera kwa kuokoka, tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo, nimekuombea ili Bwana akuimarishe zaidi, kwa hitaji la maombi au faraja ya kiroho tafadhali wasiliana nami, simu; +255 759 859 287, Email: ukombozigospel@gmail.com, Asante.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni