Jumanne, 12 Novemba 2019

USIFANYE HARAKA KUFUNGUA HUDUMA, KUHAMA KANISANI AMA KUACHA KAZI NA KUFUNGUA BIASHARA.

Ujumbe huu ni sehemu ya kitabu chetu ninachoendelea naho cha: NAFASI YA VIUNGO VYA MWILI WA MWANADAMU KATIKA ULIMWENGU WA ROHO.

Na Malimu Oscar Samba:
12. Uwe na Subira, Saburi ni kitu muhimu sana, kuna wakati unakuwa katika vita vya kumiliki na kutawala lakini unakuta eneo unalotaka kumiliki au kuweka maskani yako bado hakuna nafasi, usiwe na haraka, wala usifanye haraka, endelea kuwa na uvumilivu, jambo la kuwekwa kwa adui chini ya miguu yako ni swala la mchakato, sio la siku moja, na swala la kukuwekea mazingira ya kuishi katika miliki yako kiroho iwe ni kihuduma, kiuchumi ama kiutumishi na kindoa na kadhalika linahitaji muda !



Mfano, Nuhu alipokuwa kwenye safina maana yake nje kulikuwa na gharika tena kali, hakuwa na mahali pa kuweka mguu wake, maana hata njiwa alipotimwa alikosa mahali pa kukanyaga na hata ujani hakuweza kuuchuma, ikiwa na maana kuwa mazingira hayakuruhusu kwa wao kutoka safinani !

Ona hapa; Mwanzo 8:9 bali yule njiwa hakuona mahali pa kutua kwa wayo wa mguu wake, akamrudia Nuhu safinani, maana maji yalikuwa juu ya uso wa nchi yote; naye akanyosha mkono, akamtwaa, akamwingiza mle safinani.

Usifanye haraka kuondoka kanisani au chini ya mchungaji wako kiongozi na kwenda kufungua huduma, ni hatari maana bado maji hayajakauka, na ishara ya kwamba maji hajakauka ni kukosa kibali na amani moyoni, na kutakuwa na vita ambavyo bado vinatokota, japo vimepungua, au kwa jinsi ya kawaida twawezasema kuwa mvua hainyeshi tena, maana baada ya siku harubaini gharika ilikoma, lakini maji hayajakauka bado, yaani ghadhabu haijaisha bado, hasira haijaisha bado !

Sasa huna mahali pa kukanyaga, usiwe na haraka katika kukimbilia kufungua biashara yako kwa kuacha kazi, au kujitenga na mwenzako ili ujitegemee, maana maji bado yangalipo juu ya uso wa nchi, utazama na hutaweza kuogelea ! Subiria ya ishe !

Hapa ndipo watu wengi wa Mungu hukosea, hutaka kuvuka mto Yoridani na kuelekea Kanani kabla haujakauka, hutaka kuvuka bahari ya Shamu kwa miguu ingali haijagawangika ! Usijifanye shujaa sana maana utafia njiani, subiria igawanyike kwanza, ni hatari kuvuka barabara magari yakiwa bado yanaenda kasi, usivuke mto usio na daraja ! Tumepoteza wengi kwa ujinga huu !

Anakimbilia kuolewa au kuoa kwa njia ya mkato na kuzama majini kabisa, anakimbilia kufanya jambo hajui maji bado hayajakauka, na wengine hutoka kwenye safina mvua ingali inanyesha, hawa ni hatari zaidi ! Vita vya kumiliki na kutawala huhitaji sana subira na uvumilivu wa hali ya juu !

Ona hatua iliyofuata kwa Nuhu na Njiwa wake, nawe njiwa wako ni Roho Mtakatifu, mtangulize kwanza, akuletee habari za hapo unapotaka kuhamia au kwenda au kufanyia maamuzi akija na jani, sawa, vuta tena subira;10 Akangoja na siku saba tena; kisha akamtoa yule njiwa katika safina mara ya pili,
      11 njiwa akamjia jioni, na tazama, alikuwa na jani bichi la mzeituni kinywani mwake, ambalo amelitunda, basi Nuhu akajua ya kwamba maji yamepunguka juu ya nchi. (Sio yamekauka, "yamepungua".)

Hapa napo unatakiwa kuwa mstaimilivu, japo watu wengi hapa huamua kutia nanga na kushuka safinani, nikiwa na maana kama ni kazi kuacha na kufungua yao, kama ni kiutumishi kuaga na kwenda shambani, hapana ! Muda bado, usikimbilie kuolewa au kuoa, subiria hatua ijayo, maana hiyo njiwa hatarudi, ikiwa na maana kuwa Roho Mtakatifu atakutangulia eneo husika, atafika hujafika, ili ukienda umkute !

Huduma nyingi ni kwamba Roho yupo ndani ya mtumishi, ila hayupo kwenye utumishi wake, maana hakutanguli eneo la tukio, kwani muhusika katua kwenye maji, kakanyaga majini, njiwa hakuona mahali pa kuweka unyanyo au wayo wa mguu wake, ndio maana karudi na jani, alionyesha kuwa kuna hauweni ila majira bado ! Sasa wakikwama kiutumishi au biashara ikiwa ngumu hukimbilia kuomba ! Pole, maana Nuhu angekosea majira ya kutua hakika angekwama tu !

Najua ni kweli maisha ya kwenye safina sio mazuri kwako, ila vumilia, maana ni heri hayo maisha kuliko kukosa mahali pa kuweka mguu ! Ukiona unatangatanga kwenye makanisa, au leo una biashara hii kesho ile, leo ni mtume kesho nabii, kesho kutwa mchungaji, uwe na hakika hujapata mahali pa kuweka unyayo wako, ile unatua kila mti ni sawa maana maji yamepungua ila sasa hujapata mahali pa kutulia, yaani "kuseto" maana unyanyo hauwezi kukanyaga juu ya maji na ukaweza kuteka na kumiliki ni sharitti maji ya kauke kwanza !

 Tazama hatu ijayo, inaaza na akangoja siku saba tena, inawakilisha uvumilivu na majira yaliyofungwa kwa siku saba, hapa haina kanuni ya kuomba sana ila ni ya uvumilibu sasa, kama ni maombi usikazane kwa jina la Yesu maji kauka, la ! Bali jiombee uweze kuwa na uvumilivu, kama unao tayari endelea kumshukuru Mungu na kuhudumia wanyama na ndege kweye safina, yaani tenda vyema hapo ulipo !

Ona sasa;  12 Akangoja na siku saba tena, akamtoa yule njiwa; naye asimrudie tena kamwe.
Ukiendelea kusoma ndipo utafurahia sana faida za kusubiria mazingira yakae sawa, ili unyanyo wako ukanyage sasa, utamuona akitoa sadaka ya shukrani, pia maisha yaliendelea vyema, uwepo wa Mungu ulikuwa pamoja naye, ndiposa akafunga naye agano ! Katika haya mazingira ndipo unaweza kulima na vukuna, na kujenga nyumba na kuishi ndani yake !

Ukilazimisha hata mifugo uliyonayo kwenye safina kama wanyama na wadudu wa nchi kavu watakufa, na hata wale wa majini maana kama maji ni mengi hawawezi kuishi, lakini pia kama ulitoka mvua bado inanyesha au hatua ambayo hata jani la mti halipatikani uwe na hakika hata ndege wenyewe hawataishi, maana ni shariti wapate pa kutua !

Nina manisha nini sasa ? Ni kwamba kuna mazingira ukilazimiaha kutoka kwenye safina ambayo imekuifadhi na gharika ni lazima au utakuwa ukihatarisha karama, na vipwa vyako ! Kwani ukuwahi kuwaona watu wanaofanya vizuri sana kiutumishi wakiwa chini ya mtumishi fulani, na kuwa na mafanikio kiasi ambacho wengi huwaona kuwa watakuja kufika mbali sana !

Ila toka walipotoka na kujitenga wamenywea na kupoa kama sio wale tena ! Uwe na hakika, walitoka muda bado, sasa mafuriko yamezimisha ule moto, na kuuwa vile vipawa vyote !

Hukuwahi kumuo na mfanyakazi mzuri sana alipokuwa kwenye kampuni au shirika fulani na watu kumpongeza ila alipofanya haraka tu kujitegemea akizania kuwa akitoka atangara kama hapo awali ndipo ulipokuwa mwanzo wa kupotea kwake ! Ni kwamba hakujua kuwa alipaswa kutulia ndani ya safina, japo kweli hana uhuru wa mambo yake, lakini saa bado !

(Cha ajabu kurudi tena kwenye safina ni jambo gumu sana, lina hitaji neema, mbili, kama sio tatu, ya kutambua kuwa amekosena na kumuwezesha kuwa na unyenyekevu wa kurudi, na itakayomfungulia mlango arudipo, maana kama lango la safina limefungwa na Nuhu hana funguo, neema inahitajika, lakini hata Nuhu akiwa nao, huweza kugoma, maana: " inategemea ameondokaje," pia Ma-Nuhu wegine hawajui kusamehe na kuachilia, wanaweza kukwambia rudi au kukupokea na kukufungulia mlango wa barazani, usiingie ndani, yaani ushirika ukakosa, ukashangaa upo upo kama vile haupo, kuhudumu kama zamani hakupo tena, ni kama vile umetengwa, lakini afadhali uwekwe hata kando ya ndani ya safina kuliko kufungiwa lango kabisa !)

Nakumbuka kisa cha mtumishi mmoja aliyekuwa katika majira kama haya, anasema kuwa kuna kipindi alikuwa na msukumo sana wa kutaka kuanza huduma, siku moja akaota ndoto kuwa yupo kando ya mto na maji yanaenda kasi sana, alimuona mtu mweusi tii akimuimiza vuka vuka, akiangalia hakuna dara, aligoma na kuendelea kutembea kando hadi alipopata jiwe la kukanganya naye kuvuka !

Alipoamka Mungu alimwambia kuwa hiyo sauti inayokuimiza kuanza huduama sio yangu subiria hadi darajani ! Ni muhimu sana kuijua hii siri ! Kuna muda Paulo alikaa  Uharabuni miaka mitatu bila kuhubiri ! Ni kwamba alikuwa akijifunza na kusubiria maji yakauke ! Hapo safinani unajifunza na subiria maji ya kauke !

Ni kweli nako kuna vita, maana sasa wanyama waliopo humo ni wengi, wengine ni mbwa-mwitu kwa simba, lakini bado vumilia ! Wanafunzi wa Yesu kulipokuwa na dhoruba majini hawakukimbilia kufanya maamuzi ya kujitupa majini, bali walichota maji, walipozidiwa walimwamsha Yesu !

Na wewe mwamshe Yesu huku ukichota maji, wakati Yesu anakemea upepo wewe chota maji, kisha mtafika ngambo na utatoka tu majini ! Unajua ngambo ipo, ndipo utakapo pata mahali pa kuweka unyanyo wako, au mguu wako, ukilazimisha ziwani au majini utakwama tu, maana huko kuna mamba na viboko wa kali !

Kama hujaokoka na unataka kuokoka tafadhali fuatisha nami kwa imani sala hii ya toba, Sema: Mungu Baba, nisamehe, nimetambua ya kuwa ni mwenye dhambi, sasa ninatubu, ninakuamini na kukupokea moyoni mwangu kama Bwana na mwokozi wa maisha yangu, nakuomba ufute jina langu kwenye kitabu cha huku na uliandike sasa kwenye kitabu cha uzima wa milele, Ameni.

Hongera kwa kuokoka, na tafuta sasa kanisa la watu waliokoka ukasali hapo, na ujitambulishe kuwa umeoka hivi karibuni ili wakulee zaidi kiroho, kwa mawasiliano au sadaka M-PESA, maombi na ushauri, ni +255759859287, E-Mail: ukombozigospel@gmail.com, Tupo Arusha Tanzania. Na Mwalimu Oscar Samba. Zaidi endelea kutembelea; www.ukombozigospel.blogspot.com .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni