NAMNA YA KUMJUA NABII WA KWELI NA WA UONGO. Mwalimu Oscar Samba wa Ug Minisry.
Ujumbe huu ni sehemu ya kitabu changu cha Wito na huduma ya Nabii,
(a) WA UONGO:
1. Tazama Misingi yao ya Kihuduma, Hawana msingi wa neno, Hofu ya Mungu haipo pamoja nao, mambo muhimu ya kiroho kama Ubatizo, Toba ya dhambi, Ujazo wa Roho Mtakatifu, Msisitizo wa kudumu katika imani ya kweli, msisitizo katika maombi ya kufunga na kuomba katika Roho na Kweli, au matumizi ya jina la Yesu hayatakuwa yakitumika kama ilivyo amriwa, na kamwe hawezi kuitumia Damu ya Yesu.
Kumbuka hata akijifanya kujitahidi kubatiza, hataweza kutumia utatu mtakatifu au maji mengi, na kuwafunza watu wake katika Roho kuhusu huo ubatizo.
Mambo hayo yatazame sana katika huduma ambayo unaitilia shaka.
2. Chunguza Matunda yao, Yesu alituhusia na kutufahamisha kuwa tutawatambua kwa matunda yao, akibainisha kuwa mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, alikadhalika mti mbaya huzaa yaliyo mabaya.
Mathayo 7:15 Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.
16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?
Alhamisi, 1 Agosti 2019
Alhamisi, 11 Julai 2019
Mtu moja kauliza Hivi ! Hivi wakisema sisi hatupo chini ya sheria tupo chini ya Neema nini maana yake hasa?
Nami nimemjbu kwa kifupi sana, na kwa kirefu kipo kitabu chetu kiitwacho, YESU KAMA KWELI NA NEEMA, Jibu:
Ni kuongozwa na Roho Mtakatifu; Wagalatia 5:23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.
25 Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa RohMtu moja kauliza Hivi !
Hivi wakisema sisi hatupo chini ya sheria tupo chini ya Neema nini maana yake hasa?
Nami nimemjbu kwa kifupi sana, na kwa kirefu kipo kitabu chetu kiitwacho, YESU KAMA KWELI NA NEEMA, Jibu:
๐ Ni kuongozwa na Roho Mtakatifu; Wagalatia 5:23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.
25 Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.
Kazi moja wapo ya sheria ni kukujulisha lipi baya na jema, sasa neema inakujulisha baya na jema, na kukuwezesha au na kukupa nguvu ya kuepukana na baya , ukisoma Warumi tano hadi nane utaelewa zaidi !
Laini penye Roho Mtakatifu, pana sheria ! Ila utofauti yake ni kwamba ni katika Roho, ndiposa huitwa sheria ya Roho wa Uzima, ikimaanisha kuwa kuna neema ndani yake; Warumi 8:2 Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.

Jumatano, 3 Julai 2019
MUNGU ANAPOKAA KIMYA, WEWE FANYA YA FUATAYO, AMA TENDA HIVI:
Na Mwalimu Oscar Samba:
Wasomaji wa Biblia wanafahamu kuwa yapo maombi kadha wa kadha ambayo hayakuwahi kujibiwa, na mengine yalijibiwa lakini yalichukuwa muda mrefu tofauti na mtazamo wa wa husika ila Mungu alikuja kuyajibu.
Ibrahimu na mkewe ni kielelezo kikubwa katika hili, kwa hiyo, ikupe kufahamu kuwa wewe sio wa kwanza, sio hapo tu lakini twafahamu katika sura ya kutokujibiwa yapo hata maombi ya Yesu ambayo hayakujibiwa !
Alihitaji kikombe kimuepuke, na Mungu Baba kugoma kuyajibu ! Hadi alipobadili maombi, Musa na Yeremia nao wana orodha ya maombi ambayo hayakujibiwa !
Walijitetea kadri walivyoweza ili wasitumike lakini Mungu hakuzingatia hoja zao ! Kuna ndugu wa wiwili kipindi cha Yesu ambao ni wanafunzi wake, waliomba kuketi mkono wa kuume katika Ufalme wa Mbinguni ila maombi yao yalisogezwa

JINASUWE KWENYE ROHO AU VIFUNGO VYA KURITHI, FAMILIA, KABILA NA UKOO.
Ujumbe huu ni matokeo ya kiu ya kijana fulani anayesoma kidato cha Sita kunitaka nimfundishe maana amekuwa akisumbuliwa na mkuu wao wa ukoo ambaye humtokea na kumtangazia kumkwamisha kimasomo, japo yeye hamjui maana ni wa miaka mingi, ila hujitambulisha hivyo, na amekuwa akipitia wakati mgumu kitaaluma, hata kugubikwa na usingizi mzito mwalimu aingiapo darasani na kadhalika !
Pia ni nimeelezea jambo hili kiupana sio kitaaluma tu, natumai litakusaidia namna ya kujinasua kindoa, kiuchumi, na hata kimaisha, unapojiona umeokoka ila maisha yako yamekwama kama ndugu zako, una ugonjwa ambao husumbua jamii zako, unatatizo la kindoa kama nduguzo, unakataliwa na ndugu, huna kibali kwao, uwe na hakika hizi roho zipo kazini.

Jumamosi, 29 Juni 2019
MNGOJE BWANA KAMA MKULIMA ANGOJAVYO MAVUNO
Na Mwalimu Oscar Samba:
Kwenye pwenti ya kumngoja Bwana kwa Saburi; Mpendwa Mwenzangu katika Bwana ! Mwenye kungoja kwa Saburi huwa na taraja, ndani yake mna imani dhabiti, hana mashaka wala manongono, ni kama vile mkulima angojavyo mazao !
๐Hana haraka, ana hakika yaja majira ya mavuno, kwanza hulikwatua ama huliandaa shamba hata kabla ya mvua kunyesha, hutia mbegu chini majira ya mvua ya kupandia, wakati wa palizi hana haraka ya kuvuna bali hufanya palizi, huwekea mbolea na kuyalinda dhidi ya wadudu, kisha huja wakati wa kuchanua, napo hana haraka, anajua kuna majira ya ngano au suke, ama mahindi yake kukomaa; Marko 4:26 Akasema, Ufalme wa Mungu, mfano wake ni kama mtu aliyemwaga mbegu juu ya nchi;
27 akawa akilala na kuondoka, usiku na mchana, nayo mbegu ikamea na kukua, asivyojua yeye.
28 Maana nchi huzaa yenyewe; kwanza jani, tena suke, kisha ngano pevu katika suke.
29 Hata matunda yakiiva, mara atapeleka mundu, kwa kuwa mavuno yamefika.
Aina hii ya uvumilivu, ndio tunaotakiwa kuwa nao, ili kutuwezesha kuyafikilia mema yetu, mwisho wa maandiko nikupayo kuna onyo kuhusu manongono ! Hii ikupe kuwa makini na mwenendo huu, wenye ishara ya kukosa au kupungukiwa saburi, (Zakaria alimngoja Bwana kweli, ila kuna namna Saburi ilipungua ! Ni kweli ilikwepo
Alhamisi, 27 Juni 2019
Alhamisi, 13 Juni 2019
Mngoje Bwana
| Mngoje Bwana, Jipe moyo, Usife Moyo |
Unajua mwanadamu haaminiki kwa asilimia zote, huweza kukwambia ningoje hapa, nisubirie hapa, na kisha asije kutokea, au akakwambia nilikwama, nilipitiwa, ila sio Mungu wetu, huyu Mungu ni mwaminifu, ni wa dhati na kweli.
Kuna heri, au ipo baraka kwa wanaomngoja Bwana ! Mithali 8:34 Ana heri mtu yule anisikilizaye, Akisubiri sikuzote malangoni pangu, Akingoja penye vizingiti vya milango yangu.
Hasemi siku moja, mbili, au tatu ! Hasemi mwezi mmoja, wala miaka miwili, bali husema siku zote !
Hili ni jibu kwa wenye swali la ningoje hadi lini ? Na kufuatiwa na maelezo kama kungoja kwa kweli nimengoja sana, nimesubiri sana, ila sijibiwi ! Ni hadi haki yako ichomoze kama mwangaza, na kufanywa sifa, na unapaswa kufanya hivyo siku zote, na ungoje kwenye vizingiti vya milango yake !
Jifunze Kuongeza au Ombea Imani yako ya Kupokelea Majibu
| Aina za Imani katika Kuomba, na Mwalimu Oscar Samba |
Wakati unaomba, unatakiwa kutokuwa na shaka, na uamini kile unachokihitaji, au kukiamrisha kiwe, kitakuwa, ama itakuwa kama vile ulivyokusudia au kunuia moyoni mwako. Ukisema ugonjwa huu toka, pona, uwe na hakika unachokihitaji kitakuwa, na ugonjwa utatoka. ( Hii ni imani inayotumika muda wa kuomba.)
Sasa ukishaomba, inakuja imani au inatakiwa iwepo imani ya kupokelea majibu, nikiwa na maana kwamba yale uyaombayo, au uliyokwisha kuyaomba, unatakiwa kuamini kuwa yamekwisha kuwa yako, pia imani hii itakusaidia kuendelea kushikilia wingu la maombi, na kukusaidia mara kwa mara kurejea katika imani ya kuomba, na kukuwezesha kuomba bila kukoma, ikiwa ni sehemu ya uhusiano uliopo kati ya aina ya kwanza na ya pili, na fahamu ya pili haiwezi kuja bila ya kwanza kufanya kazi yake.
Na sababu kubwa
Jumatatu, 10 Juni 2019
Upako ni Kulipa Gharama
Nimeandika hivi, katika kitabu chetu cha NGUVU YA KUOMBA BILA KUKOMA !
Najifunza kitu kisichochepesi kwa Elisha ! Natumai unajiuliza ni kipi tena hicho Mwalimu ! Ni hiki ! Elisha alikuwa na msimamo sana, maana Elia licha ya kumpa upinzani mzito ili kuuhakikisha moyo wake kama kweli umekusudia, kuna mthihani mwingine alimpa mara baada ya kuomba ombi lile !
2 Wafalme 2:10 Akasema, Umeomba neno gumu; lakini, ukiniona nitakapoondolewa kwako, utalipata; la hukuniona, hulipati.
Ni baada ya kuomba upako mara dufu, sasa Elia anampa shariti, kuwa akimuona saa anaondoka, atapokea, la hakumuona, hatapokea !
Huu ulikuwa ni mtihani muhimu sana, na kwa

Endelea Kumkumbusha Mungu, Kamwe Usiwe Kimya, Kaza Kuomba Bila Kukoma !
Kukaa kwako kimya kutamfanya Mungu nae kunyamaza, ila kuendelea kumzongazonga kwa maombi yako na sadaka ndiko kutakakomfanya kutokutulia, na kisha kukupatia majibu yako upesi !
Amejiaidia mwenye hapa ! Isaya 62:1 Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza, na kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia, hata haki yake itakapotokea kama mwangaza, na wokovu wake kama taa iwakayo.
:2 Na mataifa wataiona haki yako, na wafalme wote watauona utukufu wako; nawe utaitwa jina jipya, litakalotajwa na kinywa cha Bwana.
Daudi anatuambia kuwa katika taabu yake alimlilia Bwana, kisha naye akasikia kilio chake ! Sijui wewe katika taabu yako huwa unafanyaje ?

Alhamisi, 6 Juni 2019
Muhesabu Mungu kuwa ni Mwaminifu, ni katika kitabu cha NGUVU YA KUOMBA BILA KUKOMA.
| Muhesabu Mungu kuwa ni Mwaminifu, ni katika kitabu cha NGUVU YA KUOMBA BILA KUKOMA. |
Yamkini umeliombea jambo hilo kwa muda sasa, na imefika mahali limegeuka na kuwa jaribu ! Nikimaanisha sio hitaji la kawaida, maana limeanza kukuweka njia panda na kukufanya uanze kufikiri kwa upya kuhusu uhusiano wako na Mungu, au kuhusu uendelee kumngoja Bwana kwa saburi au umngoje katika hali ambayo akitenda sawa na asipotenda pia ni sawa, ili mradi wewe unachojua ukitwaliwa leo ni mbinguni mengine hutaki tena kuyajua !
Jumanne, 4 Juni 2019
Usiogope Adui MTAZAME MUNGU, NA TENDA KWA AKILI . Na Mwalimu Oscar Samba.
Aliinuka Sauli mfalme enzi za Biblia na kujaribu kupigana na shauri la Bwana akimuwinda Daudi aliyekuwa mfalme mtarajiwa kila kona lakini mwisho wake alijikuta akiishilia kwa mganga wa kienyeji na hatimae shauri la Bwana kushinda ndani ya Daudi !
Yamkini huyo anayepigana nawe hana hata cheo cha ubalozi wa nyumba kumi, na uwenda hakuwahi kuwa hata kiranja alipokuwa shule !
Sasa kwa nini uogope ! Ni kwa nini ukubali kutishwa na mwenye mwili wakati yupo awezae kuuzima kwa dakika ama sekunde moja na hata nusu sekunde !
Enzi za wakina Petro ama kanisa la kwanza aliinuka mtu mkoja aliyeitwa Herode, na kujipiga kifua mbele za Mungu wetu ila mwisho wake aliishilia kutafunwa na mdudu hadi kufa !
Farao alijifanya kupigana na taifa teule na mwisho wak
Jumatatu, 3 Juni 2019
Mtumaini Bwana Bila Wasiwasi !
![]() |
| Zaburi 26:1. |
Ni muhimu sana kufahamu sana kuwa imetupasa kumuomba Mungu bila kukata tamaa, hii iwe ndio dira yetu peke maana Mungu hujibu kwa wakati wake, na inatupasa kumuomba siku zote bila kuvunjika moyo, maana sisi wenye kumkumbusha Bwana twaambiwa tusiwe na kimya, anasema ameweka walinzi juu ya kuta zako, ambao hawatanyamaza usiku wala mchana , walinzi mpendwa ni aina ya waombaji !
Kwa hiyo Bwana amekusimamishia watu
Jumapili, 2 Juni 2019
HAWA NI WATU WALIOMDHIHAKI MUNGU NA KUPATWA NA SHIDA
1. JOHN LENNON (MUIMBAJI)
Wakati alipokuwa akihojiwa na mwandishi wa habari wa gazeti la American alinukuliwa akisema hivi "Ukristo utakufa na kutoweka duniani, siwezi kuwa na wasiwasi na hilo kwa kuwa nina uhakika nalo. Mafundisho ya Yesu yalikuwa sahihi na wala sipingi hilo ila mafundisho yale yalikuwa mepesi sana ambayo mtu yeyote anaweza kuyafundisha. Hebu angalia leo, tumekuwa maarufu hata zaidi yake (Hapo alilitaja kundi lake la The Bettle). Ilikuwa mwaka 1966. Wiki moja baada ya kutamba kwamba yeye na kundi lake lilikuwa maarufu hata zaidi ya Yesu, akapigwa risasi sita na kufariki.
2. TANCREDO NEVES (RAIS WA BRAZIL)
Jumatano, 29 Mei 2019
Usifadhaike, Mungu anajua Unayohotaji.
![]() |
| Mathayo 6:8. |
Huna sababu ya kukosa usingizi, kushindwa kula, wala kukosa amani kisa una ukata, au ukwasi
Jumanne, 28 Mei 2019
WAPOLE WATAIRITHI NCHI.( Upole, Unyenyekevu kama Silaha ya Kivita.)
Na Mwalimu Oscar Samba
WAPOLE WATAIRITHI NCHI.( Upole, Unyenyekevu kama Silaha ya Kivita.)
Ijumbe huu utaupata katika kitabu chetu cha #TEKATAWALANAUMILIKI
. Fahamu: Wapole Watairithi Nchi; Upole ama Unyenyekevu ni miongoni mwa silaha muhimu sana ya kivita, (fahamu sana kuwa upole unaotajwa kwenye maandiko sio wenye maana ya ule unaokuwa rathi kupokonywa haki yako, au kukosa ujasiri wa kujitetea, ama uzubaifu, la ! Ni upole kama tunda la Roho au kama tabia ya Rohoni, maana hata Yesu aliwahi kupinduapindua meza, kuvuruga gulio pale hekaluni akiitetea kweli ya Mungu, lakini bado alikuwa mpole, aliwahi pia kuwaambia nendeni kamwambie yule mbweha, akimlenga Herode aliyekuwa mtawala, pia aliwahi kumkaripia Petro vikali akimwambia rudi nyuma yangu Shetani, na kadhalika ila bado alikuwa mpole, twajifunza pia kwa Musa, alikuwa mpole lakini ifikapo swala la uhusiano na Mungu wake kuna namna upole ule haukuwa kikwazo maana ulikuwa ni tunda la Roho na sio hulika ya kawaida ya kibinadamu, au ule upole ambao ni matokeo ya "slow mindi" ama ufahamu uliopumbazika.

| Mathayo 5:5 |
Alhamisi, 2 Mei 2019
SI MAPENZI YA MUNGU TUWE MASIKINI Na Mwalimu CHRISTOPHER MWAKASEGE
Utangulizi: (Namna ya mkristo kuishi katika hali ngumu ya uchumi bila kumkosea Mungu).
Kati ya mambo yaliyotabiriwa kutokea katika siku hizi za mwisho ni dhiki katika mataifa, pamoja na hali ngumu ya uchumi. Soma mwenyewe katika Luka 21:25-26 na Ufunuo wa Yohana 6:5-6.
Pia, tunasoma kutoka katika biblia ya kuwa biashara na uweza wa kuuza na kununua utafuata mfumo fulani uliojaa dhuluma, ambao utatawaliwa na kundi fulani ulimwenguni. Watu hawatauza wala kununua bila ya kupatana na watu wa kundi hilo, na hasa kiongozi wao. Na asomaye na afahamu. Soma kitabu cha Ufunuo wa Yohana sura yote ya 13.
Si hivyo tu, bali biblia inaeleza wazi kabisa kuwa katika siku hizi za mwisho kutakuwa na uhusiano mkubwa sana kati ya utajiri na uasherati na pia kati ya biashara na uasherati. Soma kitabu cha Ufunuo wa Yohana sura za 17 na 18. Lakini pia unaweza kuwa na utajiri na ukafanya biashara bila kujihusisha na uasherati na mambo mengine yaliyo kinyume na maadili ya Mungu.
Muimbaji Faustin Munishi na Kilio cha Kushuka kwa au Kupoa kwa Moto wa Uinjilisti leo
![]() | |||
| Pichani NI MAKAMANDA WA YESU WALIOITIKISA TZ KWA INJILI. | Ev Daudi Kuselya | Ev Emmanuel Lazaro | Ev Moses Kulola. |
Ameyaeleza katika Mtandao wake wa kijamii wa Face book, unishi Muimbaji ameyasema haya ambayo kwangu leo ni changamoto, "NAKUMBUKA TULIKUWA DODOMA MWAKA 1982 KWENYE MKUTANO WA INJILI KANISA LA TAG LILILOKUWA LINAONGOZWA NA MCHUNGAJI MHINA
KABLA YA MKUTANO JIONI, NILIMWOMBA ASKOFU MOSES KULOLA WAKATI HUO MWINJILISTI WA TAIFA TAG TWENDE STUDIO TUCHUKULIWE PICHA HII.
![]() |
| Kushoto ni Mimi Mtumishi Faustin Munishi, Katikati ni Askofu Moses Kulola na kulia ni Aliyekuwa msaidizi wa Mwinjilisti Kulola wakati huo Mwinjilisti Emmanuel Mwasota Ambaye sasa ana Kanisa Dar. |
Tulikuwa na ratiba iliyojaa kuzunguka Tanzania yote tukihubiri Injili.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)