Alhamisi, 2 Mei 2019

Muimbaji Faustin Munishi na Kilio cha Kushuka kwa au Kupoa kwa Moto wa Uinjilisti leo

Pichani NI MAKAMANDA WA YESU WALIOITIKISA TZ KWA INJILI.
  Ev Daudi Kuselya | Ev Emmanuel Lazaro | Ev Moses Kulola.

Ameyaeleza katika Mtandao wake wa kijamii wa Face book, unishi Muimbaji ameyasema haya ambayo kwangu leo ni changamoto, "NAKUMBUKA TULIKUWA DODOMA MWAKA 1982 KWENYE MKUTANO WA INJILI KANISA LA TAG LILILOKUWA LINAONGOZWA NA MCHUNGAJI MHINA

KABLA YA MKUTANO JIONI, NILIMWOMBA ASKOFU MOSES KULOLA WAKATI HUO MWINJILISTI WA TAIFA TAG TWENDE STUDIO TUCHUKULIWE PICHA HII.

Kushoto ni Mimi Mtumishi Faustin Munishi, Katikati ni Askofu Moses Kulola na kulia ni Aliyekuwa msaidizi wa Mwinjilisti Kulola wakati huo Mwinjilisti Emmanuel Mwasota Ambaye sasa ana Kanisa Dar.

Tulikuwa na ratiba iliyojaa kuzunguka Tanzania yote tukihubiri Injili.


Baada ya Mkutano huo tulienda Tabora, Shinyanga na Mwanza kabla ya kuekekea Temeke Dar Kwa mchungaji Masalu ambaye naye ni marehemu kwa sasa.

Arusha uwanja wa NMC haikuwa imesahaulika kwenye ratiba yetu kwa mchungaji Mwizarubi.

AJABU NI KWAMBA WOTE TULIKUWA HATUMILIKI GARI WALA PIKIPIKI NA HATA BAISKELI TULIKUWA HATUNA, LAKINI INJILI TULIIPELEKA KILA KONA YA TANZANIA.

Leo hii tuna magari na kasi ya kupeleka Injili kwa maoni yangu naona imepungua.

Na wachungaji tunaonyeshana magari kuliko kupeleka Injili.

Mungu atusaidie ili magari na Helicopter tulizo nazo leo zitusaidie kupeleka Injili na siyo kufunga barabara na kuwatisha watu watoke kutupisha tupite kwenda wapi?"

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni