Mathayo 6:8. |
Huna sababu ya kukosa usingizi, kushindwa kula, wala kukosa amani kisa una ukata, au ukwasi
wa fedha unakuandamia, ama kisa kuna ugonjwa una kusumbua, ama ni muda sasa hujauolewa, au ndoa ina migogoro,yamkini pia ni kazini hakuna amani ama uchumi ni mgumu ! Wewe jua tu ! " Mungu wako anajua unayoyahitaji" na jukumu lako ni kuomba bila kukoma, na wewe mwenye kumkumbusha Bwana usiwe na kimya kama maandiko yasemavyo, Luka 18 inatoa imizo kubwa sana, ni hakika wakati wa Bwana umekaribia, kwa hiyo usizimie moyo, maana Bwana yu malangoni !
Upako uliokuwa juu ya Daudi alipokuwa akimkabili Goliathi u juu yangu sasa, na ninakuhakikishia kuwa, ni majira ya kutoka katika hiyo adha sasa ! 1 Samweli 17:32 Daudi akamwambia Sauli, Asizimie moyo mtu ye yote kwa ajili ya huyu; mimi mtumishi wako nitakwenda kupigana na Mfilisti huyu.
Nami ni maombi yangu kwa Bwana sasa, huyo adui ama hilo jambo lililosimama mbele yako, nalingoa katika jina la Yesu Kristo aliye hai ! Natumai umesema Ameni, sasa tembea kama mshindi, zungumza kama mshindi, inuka ule na ushibe huna sababu ya kuwa na hofu maana mtetezi wako yu kazini ! Na vita ni vywa Bwana sio vyako, kazi yako ni kujiandaa tu kuteka nyara kama wale wa zama zile za mfalme Yehoshefathi, lakini kumbuka, walikuwa wakimuimbia Bwana, sio wakiogopa, kwa hiyo nawe anza kumuimbia Bwana, na weka hofu kando !
Zaidi kipo kitabu chetu kiitwacho NGUVU YA KUOMBA BILA KUKOMA, ( huu pia ni Msaada kwa Waliopoteza Uwezo wa Kuomba, au Kuombea Jambo Fulani, ama Waliomba na kuona Majibu yao yamechelewa, au Wenye Maombi ya Muda Ambayo Hayaja jibiwa Bado !)
Na kama hujaokoka na unataka kufanya hivyo sasa tafadhli kwa imani kubwa nakuu kabisa fuatisha pamoja nami maneno haya, au sala hii ya toba ili uweze kuokoka, Sema;
BWANA YESU, NIMETAMBUA KUWA MIMI NI MWENYE DHAMBI, NATUBU MBELE ZAKO LEO, NISAMEHE NA NINAKUOMBA UFUTE JINA LANGU KWENYE KITABU CHA HUKUMU, TAFADHALI LIANDDIKE KWENYE KITABU CHA UZIMA, NINAKUKIRII NA KUKUPOKEA MOYONI MWANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, HAKIKA WEWE NI MUNGU NA ULIFUFUKA KATIKA WAFU, Amen.
Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo, kwa maombi, sadaka kwa njia ya M-Pesa, kupiga simu au Wasats App, ni +25559859287. Tupo Arusha Tanzania.
Kwa undani wa Mafundisho au Habari zetu tembelea; www.ukombozigospel.blogspot.com .
#MwalimuOscarSamba #UgMinistry #UkomboziGospel #MwalimuOscarVitabu #Neno #Biblia #Zaburi #Pic #Picha #Tanzania #Afrika
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni