Na Mwalimu Oscar Samba
Neno Kiungu huwakilisha kutoka kwa Mungu au Shetani,
ujumbe huu ni sehemu ya hiki kitabu chenye mada na pwenti kadhaa, ila hapa
nimezicha,bua mbili tu; #Corona #Covd19 #Tsunam #Majanga #Kimbunga #magonjwayamlipuko #tanzania
1. Lifanye Eneo Unloishi kuwa Ghosheni yako. 2. Ijue
na Uitumie Damu ya Yesu ya Pasaka; 3. Mulize Mungu kama Daudi; 4. Litengenezee
Kusudi la Mungu Kisafina kama Musa, ama Nuhu; 5. Jifunze Jambo kwa Mke wa Lutu;
6. Sadaka kama Ulinzi; 7. Sadaka kama Sehemu ya
Rehema, Mfano ile ya Daudi kipindi cha adhabu ya Tauni, 8. Taka Kujua pigo Hilo
au Adhabu hiyo Inataka nini ili Ujisalimishe kwa Bwana, Mfano Rahabu, na Epuka
kosa la Farao.
9. Yajue na
Uyaombe Maombi ya Musa ya Kulitengeneza Boma, 10. Mtafute na Umuondoe Akani, 11.
Jitenge na Kusanyiko, au Kiunganishi cha Kusanyiko ama Waadhibiwa, ondoa jina
lako kwenye watu wanaotakiwa kupewa hiyo Adhabu kwa Damu ya Yesu.
12. Tafuta Maelekezo Maalumu ya Mungu juu yako, kama
Isaka dhidi ya Janga la Njaa na Wazazi wa Yesu. 13. Unapoisikia Hofu Usiipuzie,
Taaka Kujua ni Aina gani ya Hofu ala Uikabili..
14. Tafuta Kukumbuka kama Mungu Aliwahi Kukujuza
hapo Awali na Hukumsikia Vyema au Hukumbuki. (Amosi 3:7 Hakika Bwana MUNGU
hatafanya neno lolote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.)
Sijui sana ni kwa nini kanisa la leo lina uzito kwenye hili, nijualo ni kwamba uwezo wa kusoma alama za
nyakati, au majira umekuwa ni adimu sana kwa kizazi cha leo! Nafahamu kuwa hali
ya kupuzia ndoto, kutokutambua jinsi Mungu anavyoongea, na mafundisho manyonge
kuhusu uhusiano wetu na Roho Mtakatifu ni miongoni mwa sababu ambatanishi.
Kama kuna mahali Shetani amefanikiwa leo ni kuondoa,
ama kuzimisha kama sio kufifisha karama ya unabii, na huduma ya nabii, pamoja
na neno la maarifa!
Na anatumia njia kuu kama mbili hivi, moja ni
kuhakikisha kanisa linapoteza imani na manabii au wanaotumiwa na karama hizi,
kwa kujiwekekea manabii wa uongo, ili kuwakatisha watu tamaa na kuwafanya wa
waone hata wale wa Mungu nao ni kama hao wengine!
Pili analitumia kanisa lenyewe, kwa kufikia hatua ya
kupinga, na kukataa, na kuzimisha huduma na karama hizi, na sababu zao ni
nyingi ila hazina hoja timilifu kibiblia, maana kama kuna wimbi la mafundisho
na huduma potofu, suluhu bado sio kuzima na kukataa ile ya kweli, bali wafunze
watu namna ya kutambua kweli na uongo. Mchele ukiwa na chuya, dawa sio kukataza
nyumbani wasipike tena mchele bali ni kuwafunza kuzitoa, na kama ni mcahanga
basi watake kuwa makini kuchambua maana mawe mengine ni yale meupe, kwa hiyo
yanafanana kwa karibu na mchele, lakini pia kama ni vigumu, wafunze kupembua au
kuuchambua wakati wanauosha na maji, njia ambayo ni salama zaidi.
Maharage yakiwa na mchanga au mawe, hayamwagwi, bali
huchambuliwa! Na wewe ukiona dosari katika hudumka na karama hizi, hakikisha
unazikabili!
Maandiki yako wazi kabisa katika biblia kuwa
tunatakiwa kujifunza na kuhakikisha kuwa tunasoma alama za nyakati, au tunajua
mabadiliko kwa kuzitambua dalili zake, mkulima asipojua kusoma uso wa nchi,
hakika atakuwa akipitwa na maamuzi dhabiti katika majira husika, wakati wengine wanandaa mashamba yeye atashindwa kufanya hivyo, ama atajikuta
akiwacheka wengine, maana kwa wengine ili walime ni hadi waone mvua imenyesha bila
kujua kwa kufanya hivyo ni gharama zaidi maana aridhi husumbua kwani kulima
kwenye tope ni kugumu zaidi! Pia ipo hatari ya kushindwa kufanya vyema maana
kuna uwezekano wa kunyeshewa! Kuna kuchelewa pia kupanda, maana wakati wa
kuotesha wewe ndo kwanza unakwatua udongo.
Hosea hufananisha jambo la kuukwatua udongo sawa na
kuomba, maana husema tumtafute Mungu, akitangulia na kututaka kuukwatua udongo
wa mashamba yetu! Kiroho kuna vipindi kama hivi! Kuna kipindi cha kumtafuta
Mungu kabla ya adahabu haijaja! Ukichelewa gharama yake ni kubwa sana! Unaweza
kujikuta umeshapoteza ndugu wengi, ama hasara kubwa imeshatokea!
Mama yangu wakati ugonjwa huu unaingia au umeanza
kushamiri, ndipo aliponitaarifu kuhusu ndoto aliyowahi kuiota! Japo hakuwa
ameielewa kipindi hicho! Ila nataka ufahamu kuwa Mungu alikuwa ameshaongea
naye!
Elimu na ufahamu wa kuzijua nyakati ni muhimu sana,
na ni kiroho kabisa, jihakikishie kwa watu hawa, ambapo hata leo makanisani
wapo, na kama hawajafungwa