Jumamosi, 28 Novemba 2026
POKEA PUMZIKO KWA JINA LA YESU
Na Mwl Oscar Samba
Jana Nilikujulisha Kuhusu Yesu Kama Pumziko, Leo Nakufafanulia Kwa Kina Fulani.
Asili kabisa ya Neno Sabato pumziko. Mungu aliliasisi katika Agano la Kale, LIkiwa na picha ya pumziko katika Kristo Yesu.
Yesu anafafanua kabisa ya kwamba Yeye ndie Bwana wa Sabato.
Katika andiko hili maneno ya kwanza, yanatupa mantiki pana. Yaanza na neno kwa maana...inatupa kufahamu au kutoa jibu pana katika chanzo cha mazungumzo au mabishano au mjadala uliokwepo.
Tazama; Mathayo 12:8 Kwa maana Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato.
Hapa, tunapata tena neno jingine ya kwamba akawaambia, akawaambia maana yake alijidhiirisha kwao.
Tazama Tena; Luka 6:5 Akawaambia, Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato.
Sabato, ni pumziko. Pumziko katika kutuliwa mzigo, kutoka katika taabu au matatizo. Pumziko la dhambi, pumziko la mateso ya dunia hii pamoja na yale ya Shetani muovu.
Ndio maana mbingu mpya na nchi mpya katika Waebrania huitwa Sabato kuu na pia ndio ya mwisho.
Leo, Nataka kukutangazia uzima na uponyaji, Yesu kama Bwana wa Sabato akutuwe mzigo na mizigo yote.
Hii ndiyo sababu za Yesu kuponya ama kutenda miujiza mingi siku ya Sabato. Mafarisayo hawakumuelewa, lakini Yeye alikuwa akitimiza dhima ya Sabato. Ambapo hatima kuu ni katika maisha mapya ya milele yajayo. Yesu anataka akutie mizigo yote. Maana Yeye ndie BWANA wa Sabato.
Endelea katika hiyo Luka, na uwe na hakika muujiza huu unapaswa kuwa wako leo, haijalishi taabu zako, Sabato iko kwako sasa. Yaani pumziko, sina maana ya dini za kisabato leo. Bali nina maana ile halisi ya Biblia ya kisabato. Ambayo ni wewe kupata pumziko la taabu zako zote.
Endelea Kusoma:
6 Ikawa siku ya sabato nyingine aliingia katika sinagogi akafundisha; na mlikuwamo mtu ambaye mkono wake wa kuume umepooza.
7 Na waandishi na Mafarisayo walikuwa wakimvizia, ili waone kwamba ataponya siku ya sabato; kusudi wapate neno la kumshitakia.
8 Lakini yeye akayatambua mawazo yao, akamwambia yule mwenye mkono uliopooza, Ondoka, simama katikati; akaondoka akasimama.
Na wewe katika jina hili la Yesu Kristo ninaaamuru sasa kila kilichokushikilia kikakuachie sasa, katika jina la Yesu Kristo.
Magonjwa, umaskini, laana za kurithi na kutamkiwa. Vikwazo katika biashara, misukosuko katika ndoa na kazi, kukataliwa na ndugu, jamaa, wapendwa na hata katika huduma.
Kila ugonjwa sugu na yale ya kuridhi yakuachie katika jina la YESU Kristo aliye BWANA wa Sabato: Amen.
Hongera kwa uponyaji, amini tu.
Sasa kama hujaoloka, uwe na hakika umebakisha Sabato moja kuu, yaani pumziko muhimu la mzigo na mateso ya dhambi. Nikutie moyo kufanya hivyo sasa, ili siku moja uwe katika pumziko la milele kule mbinguni; uepukane na mateso ya milele katika ziwa la moto.
Sema; MUNGU BABA, HAKIKA MIMI NI MWENYE DHAMBI, NAKUSIHI UNISAMEHE SASA ZOTE , Nakupenda Yesu na Asante kwa Msamaha: Amen.
Tafadhali Tafuta Kanisa la Watu Walio Okoka Ukasali Hapo.
Ni Yangu Furaha Kama Nitapokea Shuhuda Zako
+255759859287
Tafadhali Endelea Kutufuatilia
Follow the Mwalimu Oscar Samba Mafundisho Ya Neno La Mungu channel on WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029Va827LBJENy9u6Enke1h
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni