Ijumaa, 20 Novemba 2026
USIWE NA MSIBA WAKO TENA
Na Mwl Oscar Samba
Yesu akamwambia yule mwanamke aliyetokwa na damu kwa muda wa miaka 12, mfululizo ya kwamba: Imani yako imekuponya, Uwe Mzima; Usiwe na Msiba Wako Tena!
Na iwe vivyo kwako hivi sasa, ya kwamba usiwe ama usiendelee kuwa na msiba wako tena. Msiba kwa tafsiri kuu ya kiswahili ni tatizo lililokupata ambalo limekuacha na masononeko, ama maombolezo au majonzi makuu. Ni mlima uliokushinda kuukwea. Nathani ndio sababu kifo kikaitwa pia msiba, ni kutokana na maumivu kinachoacha kwa wapendwa wa karibu wa marehemu.
Tazama Andiko; Marko 5:34 Akamwambia, Binti, imani yako imekuponya, enenda zako kwa amani, uwe mzima, usiwe na msiba wako tena.
Yesu anakutangazia vivyo hivyo siku ya leo, haijalishi umeteseka na huo ugonjwa kwa muda wa miaka mingapi, umetumia ghrama kubwa kiasi gani! Ama umeteswa na hiyo ndoa ama na watesi wako kwa kiwango kikubwa kiasi gani, ila ninachojua mimi ni kwamba haupaswi kuendelea kuwa na huo msiba wako tena. Pokea uzima, pokea uponyaji, pokea kukombolewa kwa damu ya Yesu.
Mungu aliyesikia kilio cha wengi katika Biblia amesikia na chako pia. Umekuwa ukisikia tu na kusoma tu shuhuda za wengine, leo ni siku yako ya kuwa na ushuhuda wako binafsi.
Usihesabu muda, wala miaka uliyoka na hilo tatizo. Mungu wetu afungwi na muda. Muda kwake sio kikwazo. Kama aliweza kumponya yule kiwete wa mlango mzuri katika Matendo ya Mitume 3, aliyekaa kwa muda wa miaka 40, hawezi kushindwa kutenda kwako hivi leo.
Mama aliyetokwa na damu kwa muda wa miaka 12, alipokutana na Yesu, alipokea muujiza wake. Je, wewe? Umeshasumbuka miaka 12? Je, tatizo lako limeshachukua miaka 40 kama yule kiwete?
Hata kama jibu ni ndiyo, uwe na hakika yule Yesu mponyaji wa kwenye Biblia leo tunaye. Nimekuletea huyu Yesu...
Nami ni maombi yangu hivi sasa kukutaka kupatana naye kwanza..
Yamkini hujaokoka, au uliwahi kuokoka ukarudi nyuma, nawiwa kukutia moyo kuhusu kupatana naye kwanza. Katika kupatana naye ndipo utakapofanikiwa kurejesha mahusiano yako na Yeye. Na hapo utamfungulia mlango wa Yeye kukuponya. Sauti za kukata tamaa nazinyamazisha ndani yako kwa damu ya Yesu.
Fuatisha maneno haya sasa kwa imani, ili uweze kupokea wokovu.
*Sema* ; Ewe Mungu Baba, mimi ni mwenye dhambi, ninakuomba unisamehe, nisamehe dhambi zangu zote. Amina.
Hongera kwa kuokoka, tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
Maombi ya Uponyaji:
Baba Katika jina la Yesu Kristo, ninaachilia uponyaji katika afya yake sasa, watoto ama ndugu yake huyo, ninatangaza kuanzia sasa asiwe na msiba wake tena. Kila mlima mrefu na mpana mbele yake ninatangaza kuondoa sasa. Mlima wa kukosa kazi, mlima wa kukataliwa, mlima wa ugumu kimaisha, mlima wa kukosa mpenyo kiuchumi, katika jina la Yesu Kristo ukaondoke sasa; Amina.
(Unaweza kurudia rudia maombi haya, hadi usikie wepesi moyoni..Amina)
Tuandikie muujiza (Ushuhuda) hapa
+255759859287
Jina ni Oscar Samba
Tafadhali Endelea Kutufuatilia
Follow the Mwalimu Oscar Samba Mafundisho Ya Neno La Mungu channel on WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029Va827LBJENy9u6Enke1h
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni