Jumanne, 17 Novemba 2026

Jipe Moyo

Na Mwl Oscar Samba Y
esu Anatutaka Tujipe Moyo, Kwa Maana Yeye Ameushinda Ulimwengu. Kuna siri gani kati ya kushinda kwake, na sisi kujipa moyo! Ni muhimu sana kulifahamu jambo hili, ili imani yako iweze kujengeka na hatimaye uweze kunufaika na rai hii. Tusome Wote: Yohana 16:33 Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; *lakini jipeni moyo* ; mimi nimeushinda ulimwengu. Anatutaka tuwe na Amani, anasisitiza ya kwamba Yeye ameushinda ulimwengu...kwa hiyo kwa kuushinda kwake, na sisi tunapaswa kuushinda...kwa nini? Biblia inamtaja Yesu kama mtangulizi, mzaliwa wa kwanza kati ya ndugu wengi. Ndugu wapi? Mimi na wewe ndio hao ndugu. Lakini pia ni mrekebishaji wa kosa la Adamu. Yesu anaitwa Adamu wa Pili, akirekebisha kosa la Adamu wa kwanza mumewe na Hawa. Marekebisho hayo yalimpa ushindi dhidi ya dhambi, dhidi ya mfumo wa dhambi na dhidi ya Shetani na nguvu zake za utendaji kazi, (mauti). Waebrania 2:14 imefafanua. Katika Mwili Wake, Alichukua Masikitiko Yetu, Magonjwa Yetu, Maumivu Yetu, Kukataliwa Kwetu, Kudharauliwa Kwetu, na Kadhalika, na Kadhalika. Kwa hiyo, kama unasumbuliwa na magonjwa, uwe na hakika Kwa kupigwa kwa Yeye wewe ni mzima...ndio maana anakwambia Jipe Moyo maana AMESHINDA.Isaya 53 inafafanua hilo, utaliona hapa pia: 1 Petro (1Pe) 2:21 Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake. 22 Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake. 23 Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki. 24 Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa. Mstari wa 21 unabainisha ya kuwa, alituachia kielelezo ili tufuate nyayo zake! Ndio maana anasema Yeye Ameushinda Ulimwengu. Akijua kwa ushindi wake sisi tunapo pahala pa kukanyaga. Lakini katika huo mstati wa 24 anaelezea jinsi alivyochukua dhambi zetu! Kwa hiyo, kama unasumbuliwa na dhambi unapaswa kufahamu wazi kabisa ya kwamba unapaswa KUJIPA MOYO ya kwamba ushindi na suluhisho limepatikana, lipo katika msalaba wake Kristo Yesu. Jipe Moyo Maana Yeye Mungu Ametushindia. Ndiyo, Yesu ni Mungu...alikuja kutupatia ushindi kwa njia ya kanuni ambazo zilimlazimu kuzifuata mara baada ya dhambi kuingia ulimwenguni. Anaposema ameushinda ulimwengu, tafadhali ifahamike ya kwamba anamaanisha mfumo wa utawala wa Shetani uliopata kibali na malaka katika Bustani ya Edeni kutokana na lile kosa. Ndiposa, mara baada ya hapo, alitutoa ulimwenguni na kutufanya kuwa wana wa ufalme, ili nini? Sababu ni ili mfumo wa dhambi (ulimwengu) usiwe na nguvu, au mamlaka dhidi yetu. Kwa hiyo Yesu alishatutangazia ushindi hata kabla ya mapambano. Kwa maombi haya ya Yesu, mimi nikitakie tu Ushindi Mwema, huku ukijipiga piga kifua na kujisemesha ya kwamba, SASA NAJIPA MOYO...MIMI NI MSHINDI....(weka jina lako). Jiambie Mimi.....NI MSHINDI...Sitaogopa Tena. Yohana 17:14 Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. 15 Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu. 16 Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. Kwa Mafundisho Zaidi Tafadhali Tufuatilie Katika Chaneli Yetu.. Follow the Mwalimu Oscar Samba Mafundisho Ya Neno La Mungu channel on WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029Va827LBJENy9u6Enke1h

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni