Jumatatu, 16 Novemba 2026
USIOGOPE
Mungu Anakwambia ya Kwamba Usiogope. Kwa nini Anatupa Ujumbe Huu Muhimu Namna Hii?
Ukilisoma hili andiko, kuna vitu kadha wa kadha utaviona hapo..
Isaya (Isa) 41:10 usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.
Mosi, anasema kwa maana Yeye Mungu yu Pamoja Nawe,....Sasa kama Mungu yuko upande wako, ni jambo gani linaloweza kusimama kinyume chako na likakushinda! Hapana shaka kabisa hakuna, maana Yeye ni muweza wa yote.
2. Anajinadidi Kabisa ya kwamba... "usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako;" Mungu anapojitambulisha kama Mungu wako wewe hofu kwako na mfadhaiko ni ya nini sasa! Embu simama kiume huku ukijua wazi ya kwamba Mungu ni Mungu wako...
3. Nguvu..anaendelea kusema ya kwamba.. "nitakutia nguvu,"..kumbe sio swala la kujisemea ya kwamba umechoka, umeishiwa nguvu, unajisikia kukata tamaa...la! Hasha. Mungu anasema yeye mwenyewe ya kwamba atakutia nguvu...huna budi kuwa na ujasiri wa namna hii maana nguvu zipo... Yeye mwenyewe kasema atakutia nguvu....kwa hiyo, USIOGOPE wala Usifadhaike...kufadhaika ni kuwa na masikitiko au maumivu au moyo wako kuwa na hali ya kuugua...
4. Utasaidiwa... "naam, nitakusaidia,"... Hivi ukisaidiwa na Mungu, ni nani awezaye kushindana nawe! Ni jambo gani ambalo Mungu litamshinda mbalo kwako kiukweli huwezi ila Yeye akikusaidia hataweza? Jibu lipo wazi tu ya kwamba Mungu wetu anaweza yote...ana nguvu na uweza wote...humuita "Ommipotaince"
5. Utashikwa Mkono Wewe.. tazama.."naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu." Sio mkono ili mradi mkono, bali ni mkono wa kuume, yaani wenye nguvu.
Je unajua maana yake? Ni kwamba usiogope kujaribu, wewe thubutu. Kwa maana kwamba hata ukianguka, Yeye Mungu atakushika mkono wake wenye nguvu, wewe jaribu tu, hata ukikwama atakusaidia. Wewe anza tu na wala usifadhaike maana Yeye yupo ili akutie nguvu..... USIOGOPE.
Jisemee Moyoni Siku ya Leo ya Kwamba, Sitaogopa...Mimi Siogopi...Nitathubutu na Hata Nikikwama Amehaidi Kunishika Mkono...
Tafadhali Endelea Kutufuatilia...
Follow the Mwalimu Oscar Samba Mafundisho Ya Neno La Mungu channel on WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029Va827LBJENy9u6Enke1h
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni