Jumatano, 25 Novemba 2026
FURAHIA MAJARIBU
Na Mwl Oscar Samba
Sii Rahisi Kuelewa, ila Ukweli ni Kwamba, Changamoto au Jaribu Ni Jambo la Kufurahiwa. Kuna Fursa Usingaliweza Kuipata Kama Usingekumbana na Vikwazo Kadhaa Unayokutana Navyo.
Miaka ile ya 1990's, kulikuwa na mtu mmoja alienda kuomba kazi katika shirika au ofisi fulani huko ughaibuni, aliulizwa kama ana baruapepe. Jibu lake lilikuwa ni hapana; (kipindi hicho haikuwa rahisi kumiliki baruapepe). Akakosa kazi kwa kukosa baruapepe.
Alikuwa na fedha kiasia kama shilingi elfu 2 za Kitanzania, kwa hasira na masikitiko akanunua "Ice Cream" za fedha hizo, zilikuwa kama ishirini hivi. Akaketi barabarani akijiadhibu azile zote. (Kumbe ndio chanzo cha utajiri wake!)
Wakapita wanafunzi wa shule, wakamuliza unauza? Naye kwa haraka akachangamkia fursa; akajibu ndio: na kuwauzia.
Mtu huyu alikuja kutajirika sana, baada ya muda kidogo... aliwahi kuingia katika orodha ya matajiri bora 10 duniani. Katika shuhuda zake, anasema asante Mungu kwa kuwa sikuwa na baruapepe pepe (Email).
Wakati nafurumushwa kazini, mwaka jana 25 December; kijana mmoja alinipa simulizi hii. Ya kwamba kulikuwa na mtu aliyelazimika kupunguzwa kazini kutokana na kampuni yao kushindwa kuendelea kumudu kuwa na idadi kubwa ya wafanyakazi kwa sababu ya mdororo wa uchumi wa dunia.
Mtu huyu alianza "kubumba," glasi, (ni neno la kisukuma lenye maana ya kuunda kwa kufinyanga kwa mkono). Ghafla akajikuta vyombo vyake vina pata soko kubwa; baada ya muda kitambo tu alijikuta ni miongoni mwa watu waliopata au kujizolea umaarufu mkubwa duniani kutokana na ubunifu huo. Umaarufu wa ubunifu duniani ulimwangukia. Akisimulia haachi kuonesha kufuraishwa na hali ya kuondolewa kazini; ingawaje awali haikuwa rahisi. Napo mimi nalijifunza kitu.
Vivyo hivyo ndivyo ilivyo katika Biblia, tunapaswa kufurahia majaribu.
Tazama Andiko; Yakobo 1:2 Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali;
Kibiblia kila jaribu lililokusudiwa na Mungu nyuma yake lina faida. Kukamatwa, kuteswa, na kusulubiwa kwa Yesu kwetu ni ukombozi tosha.
Mateso kwa kanisa la kwanza, huko Yerusalem; ndiyo yaliyofungua mlango kwa injili kuenea kote kama Yesu alivyowaagiza. Kwa hiyo bila mateso hayo kuruhusiwa, Samaria wasingeipata injili.
Tazama; Matendo ya Mitume 8:4 Lakini wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilihubiri neno.
5 Filipo akatelemka akaingia mji wa Samaria, akawahubiri Kristo.
Ukisoma muktadha wa andiko hilo la Yakobo 2, utafahamu jinsi ambavyo majaribu hunuia kutuimarisha.
Asante kwaKuwa Pamoja Nami, Nikutake Sasa Kuhakikisha ya Kwamba, Unayastahimili Majaribu...Unavumilia, huku Ukijua Wazi ya Kwamba Ipo Faida, Hata Kama Kwa Jinsi ya Mwilini Inaonekana ni Jambo Gumu, na Lenye Kuogofya; Ila Kila Amtumainie BWANA hata tahayarika. Bali huimarishwa...Hutakufa, Hata Ujapo aibika ni kwa Muda Kitambo Tu...Yesu Aliaibika kwa Siku 3 tu! Mara baada ya hapo simulizi za ushindi wake zilitapakaa Yerusalem yote, na hata miisho ya nchi.
Mungu Akubari:
Ningefurahi Kupata Shuhuda Zako
+255759859287
Uwe na Ushindi katika Kristo Yesu
Tafadhali Endelea Kutufuatilia
Follow the Mwalimu Oscar Samba Mafundisho Ya Neno La Mungu channel on WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029Va827LBJENy9u6Enke1h
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni