Jumamosi, 2 Agosti 2025
Jumanne, 29 Julai 2025
AKILI ZILIZO MACHO KATIKA UFALME WA MBINGUNI Mathayo 24:45
Ujumbee huu ni Sehemu ya Kitabu Chetu Kipya Cha: KILI ZILIZO MACHO KATIKA UFALME WA MBINGUNI
Mathayo 24:45
Na Mwalimu Oscar Samba
Hiyo ni picha muhimu unayopaswa kuwa nayo, wakati huu unapoelekea kukisoma kitabu hiki. Ni muhimu sana kufahamu ya kuwa maana moja wapo ya Yesu ya kututaka tusilale usingizi yaani tuwe macho; ama tukeshe ililenga eneo la akili zetu.
Tazama mfano ule wa Wana Wali watano wenye Busara na watano Wapumbavu. Ndipo utakapotambua ya kuwa upumbavu unaotajwa pale, ni unaotokana na hali ya kutokujua ni nini cha kufanya katika nyakati kama hizi.
Malengo ya Kitabu:
1. Kuyafumbua Macho ya Aliyefumbwa, Kuziamsha Akili za Asinziaye ili Aweze Kuwa na Utayari wa Kutumika Kiusahihi (kama impasavyo), Katika Kulielekea Kusudi Aliloitiwa Kinyakati.
2. Kumpatia Ufahamu, Utakaotumika Vyema na Akili Zake, ili Kujua Ni Nini Kimpasacho Kukifanya Katika Majira Husika.
1 Mambo ya Nyakati 12:32 Na wa wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao walikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao.
3. Kumjengea Fikra za Kumuwezesha Kuzitambua Hila za Adui Shetani; Katika Mpango wa Kumnyamazisha au Kutaka Kumpoozesha Kiroho na Kiutumishi, (au Kiutumishi/Kiroho.) 2 Wakorintho 2:11 Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikra zake.
4....
Lengo Kuu: Kukujengea Fikra za Kiuamsho, Ili Kuibua Hari na Kuamsha .... Kukuumbia Nia ya Kiuamsho Ndani Yako. (Penye Nia, Pana Utayari).
.....,....
1. Maonevu na Migogoro Katika Kanisa, Ama Baina ya Watumishi, au Washirika: Ni Ishara ya Kujisahau Kiroho. Watu waliopoteza kusudi, au kulisahau ama walioshindwa kujitambua ndio pekee huweza kuanza kuumana. Unapoona
Jumamosi, 19 Julai 2025
ROHO MTAKATIFU KAMA MSAADA, KATIKA GHARAMA ZA KULIPA ILI KULETA UAMSHO
Na Mwl Oscar Samba
Matendo ya Mitume 1:8 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.
Lengo la Somo:
Kukuwezesha, au Kukujengea Fikra za Kuhitaji Msaada Wa Roho Mtakatifu; Ili Awe Mwezeshaji Wako Mkuu, Katika Kulipa Gharama kwa Ajili ya Uamsho.
Taswira ya Ujumbe: Imejikita katika kufahamu umuhimu wa kumpata Roho Mtakatifu kipindi cha maandalizi ya kiroho kwa ajili ya uamsho. Hapa nilipo nalenga aina ya upako unao hitajika, ili kulipa gharama ya kuleta Uamsho. Ni sawa na kipindi kile cha mwanafunzi kusoma kabla ya kazi. Uamsho ni kipindi cha kazi, lakini kabla ya kazi kilipita kipindi aidha cha chuo au shule.
Askari kabla ya kuingia vitani, au kuwa askari kuna kipindi cha mafunzo au cha maandalizi ya vita. Sasa kipindi hiki katika swala la Uamsho, ndicho hukiita kipindi cha kulipa gharama kwa ajili ya Uamsho.
Kati ya eneo kubwa na muhimu watu wengi hawalijui wala kulizingatia, ni lile la maandalizi au la kulipa gharama. Mfano, Uamsho wa huduma ya Yesu, ulilipwa gharama na watu wengi. Akiwemo Yohana Mbatizaji, aliyekaa nyikani akila asali ya mwitu na nzige. Akivaa mavazi kama ya Elia, yaliyo ya ngozi na kadhalika. Maana huyu alikuwa ni mtangulizi.
Jumamosi, 5 Julai 2025
Nukuu ya Mwalimu Oscar Samba, Kuishi na Watu Kwa Akili ili kumshinda Shetani
Shetani Hutumia Watu Ili Kufanya Vita na Wewe; Kwa Hiyo Ukifanikiwa Kuishi na Watu Kwa Akili: Ni Umemshinda Shetani Kwa Viwango Vikubwa.
By Mwalimu Oscar Samba
Jumatatu, 23 Juni 2025
Roho Mtakatifu Anaweza Kubadilisha Tabia Zisizofaa Maishani Mwetu. Jifunze Kumpa Nafasi.
Shalom Mtu wa Mungu, Karibu katika Makala hii, ikiwa ni Sehemu ya Kitabu Chetu Kipya cha JIFUNZE KUMUAMINI ROHO MTAKATIFU KATIKA HILO ENEO*..
Na Mwl Oscar Samba
Katika Badiliko la Tabia
. Unageuzwa/Hutugeuza Na Kutupa Maisha Mapya . Dhambi ilipoingia ulimwenguni ilitupatia mwili wenye tabia au vinasaba vya chembechembe za dhambi. Ile mauti iliyonenwa, iliua sehemu kubwa ya asili au ya tabia ama ya vinasaba vya Kiungu katika maisha yetu. Na badala yake, tukatwa asili ya Shetani. Ndiposa kuna kitu Paulo hukiita utu wa kale, pia tabia za mwilini ama mwili huu wa tamaa ama tamaa za mwili. Ndiposa suluhu hutajwa ni kuokoka, ili uwe au uusulubishe mwili wako pamoja na Kristo pale msalabani. Waruni 5-8, na Wagalatia 5 inatusaidia sana katika hili.
Paulo anatufundisha sana kuwa, Yesu alipokuwa anakufa, aliufia mwili wa dhambi. Yaani mauti yake, ilikuwa inauwa asili ya Shetani katika miili yetu; japo kwa lugha ya Kibiblia neno nguvu ya mauti, au utawala wa mauti katika miili yetu linaonekana kutumika zaidi. Kwa lugha nyingine tunasema mfumo wa dhambi. Lile andiko la tulio wa Kristo hatutendi dhambi (1 Yohana 3:6, 8, 9; "ukisoma utakuna na neno mbegu, tafakari kwa kina neno hilo" wa 10, 'unakupa matokeo:') maana yake, tuliookoka hatupo au hatutawaliwi na mfumo au utawala wa dhambi. Ikimaanisha nguvu ya mauti, au mauti twajua ni nguvu ya Shetani kupenyeza dhambi.
Soma; Waebrania 2:14 Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi,
Ijumaa, 20 Juni 2025
Mada ya Ushuhuda, Uliyochimbuko la Kitabu hiki chaJifunze Kumuamini Roho Mtakatifu Katika Eneo Hilo ...
Mada ya Kwanza Katika Kitabu Chetu Kipya cha Jifunze Kumuamini Roho Mtakatifu Katika Eneo Hilo...
Na Mwl. Oscar Samba
1.Ushuhuda
Chimbiko kuu la kitabu hiki ni tukio binafsi lililonikuta, ambalo moja kwa moja Roho Mtakatifu alilitumia kama somo ili kunivusha mahali lakini pia kwa nia ya kupangua baadhi ya mienendo isiyo sahihi katika njia zangu. Iwe ni za kihuduma au kimaisha kama vile uchumi, kijamii na kadhalika.
Somo hili nimelipata katika mradi ninaoufanya wa kutotolesha vifaranga vya kuku na ufugaji. Siku ya 21 ilipofika, vifaranga vikaanza kuanguliwa; kikanuni ni hadi kitoke kwenye kasha lake, kikauke ndipo ukitoe kwenye mashine.
Mimi vilipoanza tu kutoboa kasha, (eneo la kichwa) nililazimisha kumenya kasha zima. Hali iliyovipelekea kufa maana nilikuja kugundua ya kuwa eneo la kichwa ndilo hutangulia, na maeneo mengine hufuatia kwa kuendelea kukomaa au kukauka au kujiunda na humalizikia mkiani. Sasa ukikimenya pale mwanzoni, unakifanya kife maana maeneo hayo mengine yanakuwa bado hayajafikia muda wake wa kukamilika.
Baya zaidi, yale mayai ambayo yameshaanza kumenyeka au kupasuka eneo la kichwa, niliyachukua baadhi (yaliyoelekea sana) na kuyapeleka eneo la kukuzia vifaranga. Hapo nikaja na kukuta vyote vimekufa kwa kuzidiwa na joto! Lo! Nikajifunza kitu.
Kati ya funzo moja wapo la Kibaolojia ni kwamba, elimu ya kifizikia iliyotumika kutengeneza mashine ya kuatamieshia, imeundwa katika mfumo wa joto lililopangwa (mfano kwa vifaranga kwangu naweka 37.8) kuwa na uwezo wa kutoongezeka. Yaani halipandi kiasi cha kuadhiri mayai au vifaranga. Kwanza kuna feni na kuna hali ya unyevunyevu, pamoja na vifaa vilivyotumika kutokupata joto.
Alhamisi, 19 Juni 2025
Jifunze Kumuamini Roho Mtakatifu Katika Eneo Hilo
Utangulizi wa Kitabu Chetu Kipya Cha_ Jifunze Kumuamini Roho Mtakatifu Katika Eneo Hilo ....
Na Mwl. Oscar Samba
Utangulizi
Tumekuwa na utamaduni mkubwa sana wa kutegemea akili zetu bila kufahamu umuhimu wa kumtegemea Roho Mtakatifu. Ni kweli akili na fahamu zetu ni kiungo muhimu katika kuyaendesha maisha yetu. Ila Kibiblia mwanadamu hakuumbwa kuzitegemea, badala yake aliumbwa kumtegemea Mungu, ingawaje aliumbwa kuzitumia akili; tena Paulo mtume anamtaka azitumie ipasavyo. Kwake sio kuzitumia tu, bali ni ipasavyo. Utafiti mmoja rasmi uliwahi kuonyesha kuwa, bara fulani ulimwenguni watu wake tunatumia asilimia tano tu ya ubongo wetu. Natumai hii ni sehemu au chachu kubwa ya hali duni ya maisha tuliyonayo.
Lakini tena na tena, yote katika yote; ni kwamba akili za mwanadamu ziliumbwa zifanye kazi kwa msaada wa Kiungu. Ni dhambi tu ilivuruga eneo hili, na kumfanya mwanadamu kuishi kana kwamba
Jumatano, 18 Juni 2025
KUMSIFU NA KUMUABUDU MUNGU, KULIKO HALISI
Na Mwl Oscar Samba
Ujumbe huu ni Sehemu ya Kitabu Chetu Kipya cha MOTO WA UAMSHO KATIKA BIBLIA, Tunachambua kila Tukio Muhimu la Kiuamsho Katika Biblia.
Somo la .... SIFA NA KUABUDU KATIKA KWELI; Maneno Yenye Uhalisia Katika Kumuabudu au Kumsifu Mungu.
Licha ya umuhimu wa hali ya kiroho ya mtu anayemsifu au kumuabudu Mungu, ambapo tunaongozwa na lile andiko la Zaburi linalotutaka tuwe na moyo safi ( Zaburi 33:1 Mpigieni BWANA vigelegele, enyi wenye haki, Kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo. Rejoice in the LORD, O ye righteous: for praise is comely/inatoka for the upright.); lakini pia uteuzi wa maneno na muundo wa sentesi zetu katika kumuimbia Mungu: lazima visadifu uhalisia.
Lazima yataje aidha ukuu wa Mungu, uweza wake au utukufu na utakatifu wake. Tabia zake na utendaji wake uliotukuka vinapaswa kuwa ni sehemu ya maneno yaliyoteuliwa na mtunzi sanjari na muimbishaji wa wimbo.
Tuna nyimbo nyingi leo zinaitwa za kuabudu ni kwa sababu tu zinaimbaa katika hali ya utulivu. Na zile za kusifu ni kwa sababu zinaimbwa kanisani na katika hali ya kuchangamka. Hatusifu kwa kuwa wimbo unamsifu Mungu, bali ni kwa kuwa muimbishaji katuambia tusiamame tumsifu Mungu. Ni kwa kuwa mpigaji kapiga mapigo yakutuchangamsha.
Ijumaa, 13 Juni 2025
FIKRA SAHIHI KATIKA LANGO LAKO LA MSIMU MPYA.
Na Mwalimu Oscar Samba
Ujumbe huu ni Sehemu ya Kitabu Chetu Kipya cha MOTO WA UAMSHO KATIKA BIBLIA
Tunachambua kila Tukio Muhimu Katika Biblia Nzima, hususani lile lenye Ujumbe wa Kiuamsho Ndani Yake.
Kitabu cha Kutoka, Sura ya 13 na 14
Somo la .... KUVUKA BAHARI YA SHAMU: Ushindi Katika Mlango wa Msimu Mpya Kihuduma au Kimaisha.
Msimu Mpya maana yake ni mabadiliko au hatua nyingine mpya ya kimaisha, na hata kihuduma yaani kiroho. Mabadiliko haya huanzia rohoni kweli, ila huwa na matokeo katika maisha ya uhalisia ya mwilini. Kabla ya kuingia msimu huo mpya, unahitaji kupita katika lango la msimu. Hapa ndipo huwa na upinzani mkubwa sana. Mwanafunzi yeyote lazima awe makini na kipindi chake cha mitihani. Na kuna wengine kipindi hicho huwa katika mashambulizi sana. Ni kwa nini? Ni kwa sababu kuingia kwake katika hatua nyingine, kunategemea kuvuka kwake katika mtihani huo.
Wana wa Israel walikuwa wanaingia katika msimu wa maisha mapya. Kiuchumi tungeuita sekta isiyo rasmi. Maana ile ya jangwani tunaiita ni sekta ya umma. Walilishwa na serikali, na kuhudumiwa na wao. Jangwani wanajiandaa kuishi maisha ya ndege wa angani, yaani sekta isiyo rasmi. Hapo wanalishwa na MUNGU mwenyewe kwa njia ya muujiza.
Jumanne, 29 Aprili 2025
Pasaka ya Kweli: UKOMBOZI SAHIHI KATIKA MSAMAHA WA DHAMBI.
Ujumbe huu ni Sehemu ya Kitabu Chetu Kipya cha MOTO WA UAMSHO KATIKA BIBLIA. Ni kitabu kinachochambua kila Tukio la KiUamsho Ndani ya Biblia nzima.
Na Mwl Oscar Samba
Kitabu cha Kutoka. Sura ya 12 ...
Somo la...... UKOMBOZI KWA NJIA YA DAMU: Kristo Yesu Ndiye Pasaka.
1 Wakorintho 5:7 Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo;
8 basi na tuifanye karamu, si kwa chachu ya kale, wala kwa chachu ya uovu na ubaya, bali kwa yasiyochachika, ndio weupe wa moyo na kweli.
Tunajulishwa ya kuwa Kristo ndiye Pasaka wetu, na ili kumuenzi au kuyaishi maisha yake basi tunapaswa kuwa na mwenendo au moyo safi ama weupe wa moyo. Tuifanye karamu hii katika hali au kusudio lililokusudiwa pale msalabani ambalo ni la ukombozi wa kutoka dhambini. Tumaanishe katika wokovu, kwa lugha nyingine Ukristo sio dini tu, bali kunabeba maana pana ya kuyaishi yale aliyoyaishi Yesu Kristo.
Kuyaacha mambo ya kale, maisha ya Misri yako, maisha yenye michanganyiko na chachu za dhambi, uzinzi, masengenyo, biashara za magendo na kadhalika. Ukristo ni Kuokoka, hakuna utofauti kati ya wokovu na Ukristo. Anayejiita Mkristo na hajaokoka huyo ni mpagani mwenye dini. Lazima uiondoe chachu inayokufanya kuwa donge lisilofaa, uwe na maisha safi, maisha bila chachu.
Miongoni mwa imizo kubwa la Mungu katika siku hii ya Pasaka kule Misri ilikuwa ni kula mikate isiyotiwa chachu kwa muda uliopangwa. Lengo lilikuwa ni mkazo wa kiroho katika picha ya maisha ya wokovu, ambapo ni maisha bila mawaa. Sijui unakisoma kitabu hiki ukiwa wapi, na ni lipi dhehebu lako; na inawezekana linasherekea na Pasaka, na yamkini huamini kuhusu wokovu! Pole ni nyingi kwako, maana karamu hiyo unaifanya kwa hasara. Paulo anatutaka kuifanya kwa faida. Bila chachu ndani yake; 1 Wakorintho 5:8 basi na tuifanye karamu, si kwa chachu ya kale, wala kwa chachu ya uovu na ubaya, bali kwa yasiyochachika, ndio weupe wa moyo na kweli.
Jumatatu, 28 Aprili 2025
Pambano la Nguvu, Ni Vita Dhidi ya Ufalme wa Giza, Mawakala na Wajumbe wa Kuzimu "Maajenti."
Ujumbe huu ni Sehemu ya Kitabu Chetu Kipya cha MOTO WA UAMSHO KATIKA BIBLIA. Katika Pointi ya Pambano la Nguvu (Ni kitabu kinachogusa Matukio na Mambo Muhimu Katika, Biblia Nzuma.)
Na Mwl Oscar Samba
Kitabu cha Kutoka. Sura ya 7:..
Somo la .... : PAMBANO LA NGUVU; Pigano la Ushindi Dhidi ya Wakala au Mwakilishi ama Mjumbe wa Ibilisi yaani mfalme wa Ufalme wa Giza.
Ni wasaa mwingine mzuri, tunaendelea kujifunza kuhusu Moto wa Uamsho Ndani ya Biblia. Kama nilivyokujuza hapo awali kuhusu pambano la nguvu dhidi ya ufalme wa giza kwa Musa, basi sasa nawiwa kukupanulia swala hili kiupana zaidi. Hapa tutatazama hadi tukio la namna hii la Paulo mtume dhidi ya yule mchawi, pamoja na Daudi na Goliathi. Karibu:
Musa na Fimbo ya Haruni kwa Farao
Mungu alimpatia Musa ishara ya fimbo yenye kugeuka nyoka. Fimbo huwakilisha mamlaka, utawala, uchungaji, pigo na hata heshima kwa mtu wa aina fulani. Mfano, kuna makabila ambayo kijana akifikia umri fulani hukabidhiwa fimbo, au huruhusiwa kutembea na fimbo. Rungu na fimbo, huwa na muktadha unaofanana sana kwa baadhi ya jamii. Kumbuka pia fimbo ni silaha ya ulinzi, makabila yenye utamaduni wa ufugaji, au kuishi porini hili wanalifahamu sana. Pia fimbo, ni ishara ya kuwa nipo tayari kwa safari. Jamii za kale zililijua sana hili; ndiposa katika Kutoka 12 wana wa Israeli walipaswa kula nyama ya Pasaka wakiwa na fimbo mikononi mwao. Ili nini? Ilikuwa ni sehemu ya ishara kwao ya kuwa, wamekaa mkao wa kisafari. Viatu miguuni, mshipi kiunoni, viliwakilisha pia.
Inapogeuka na kuwa nyoka, ni swala la ishara yenye miujiza ndani yake. (Ishara ni kiwakilishi, maana yake ni kwamba, ukiona alama au jambo hili, fahamu kuna hiki nyuma yake. Kuna alama mtu akiionyesha maana yake ni kwaheri au anakuaga. Nyingine ni anakuita, au anakwambia subiri. Alikadhalika, kuna vitu kama ishara vikitokea, hukujulisha kuwa Mungu yupo hapa. Ama ni MUNGU mkuu ndiye aliyelifa ya hili, na kadhalika.)
Ijumaa, 25 Aprili 2025
Ishara na Miujiza Kwa Mkono wa Musa: MIUJIZA HUITAMBULISHA HUDUMA.
Ujumbe huu ni Sehemu ya Kitabu Chetu Kipya cha MOTO WA UAMSHO KATIKA BIBLIA (Tunachambua kila Kila Tukio Lenye Uamsho ktk Biblia Nzima).
Na Mwl Oscar Samba
Kitabu cha Kutoka ... na Yoshua Sura ya 3 na 4, pia Yohana 2:7-11.
Somo la ....: Ishara na Miujiza Kwa Mkono wa Musa: MIUJIZA HUITAMBULISHA HUDUMA.
Shalom mtu wa Mungu, tumekutana tena katika somo jingine. Hapa kwa pamoja tunaangazia nafasi ya ishara na miujiza katika kuitambulisha huduma au mtumishi husika.
Tukiwa tungali katika wito wa Musa kwenye kitabu hiki cha Kutoka; Musa alipoitwa, na kukabidhiwa majukumu kadhaa, alionyesha hali ya kutokukubalika. Alikuwa na mashaka au wasiwasi kama atapata kibali kutoka kwa watu. Jibu la Mungu lilikuwa ni jepesi tu kwake, Mungu alimpatia ishara kadha wa kadha. Na kumwambia ya kuwa, watamuamini kwa kupitia hizo.
Jumatatu, 7 Aprili 2025
Nukuu ya Mwalimu Oscar Samba, Uhuru wa Maoni na Kukosoa. Quote of Teacher Oscar Samba, Freedom of Option and Criticizing
Alhamisi, 3 Aprili 2025
Moto wa Uamsho Katika Biblia
Jumamosi, 29 Machi 2025
Alhamisi, 27 Machi 2025
Amani na Umoja ni Nguvu, na Ni Ishara ya Upako
*Ujumbe wa Leo*
Chumvi Ndani Yetu (Roho Mtakatifu/Ushuhuda wa Kristo/Utakatifu/Utu Wema
Hutuwezesha Kukaa Kwa Amani Baina Yetu (Sisi kwa Sisi)
Kwa hiyo, Tukipoteza Umoja, Mapendano Baina ya Ndugu, ni ishara ya kwamba Hatuna Chumvi. Au Magomvi Baina Yetu, Hutuondolea Chumvi.
Marko 9:50 Chumvi ni njema; lakini chumvi ikiwa si chumvi tena, mtaitia nini ikolee? Mwe na chumvi ndani yenu, mkakae kwa *amani ninyi kwa ninyi.*
Salt is good: but if the salt have lost his saltness, wherewith will ye season it? Have salt in yourselves, and have peace one with another.
By Mwalimu Oscar Samba
Zaidi Soma: https://ukombozigospel.blogspot.com/?m=1
Jumamosi, 22 Machi 2025
Kitabu cha CHAKUFANYA UKIWA NJIA PANDA, Kitakufikia Punde.
Ni kwa Njia ya PDF free. Zidi Kutuombea
Utakipata kwa Namba hizi hapa kwa WhatsApp +255759859287
Andika Neno Vitabu
Utatumiwa na Vitabu Vinginevyo Vingi vya Mwl. Oscar Samba
Jumatano, 19 Machi 2025
Quote of Teacher Oscar Samba in Learning and Teaching
Any Good Preacher Should Remember This: We Are Still Learning, We Are Still Teaching.
It will help us from too much self condemnation.
By Mwalimu Oscar Samba
Zaidi Tembelea:
https://ukombozigospel.blogspot.com/?m=1
#quote #t #teaching #learning #Oscarsambaquotes #preacher
Jumanne, 18 Machi 2025
Nukuu ya Mwalimu Oscar Samba MAOMBI DHIDI YA JARIBU
Usipotumia Nguvu Nyingi Katika Maombi, ili Kuyashinda Majaribu: Utalazimika Kutumia Jitihada Nyingi Katika Kuyavumilia na Kukabiliana Nayo.
By Mwalimu Oscar Samba
Zaidi Tembelea: https://ukombozigospel.blogspot.com/?m=1
Jumamosi, 15 Machi 2025
Mwl Oscar Samba Nukuu ya Watoto au Kijana ama Vijana Chipukizi na Utumishi
"Tusiwasukumie Watoto Wetu Kwenye Utumishi ili Wamjue Mungu. Bali Tuwasaidie Kwanza Kumjua Mungu Ndipo Wamtumikie."
By Mwalimu Oscar Samba
Utaukuta Kwenye Kiatabu Chetu cha
UMUHIMU WA KUMJUA NA KUMPENDA MUNGU KAMA MTOTO AU KIJANA CHOPUKIZI.
Zaidi Tembelea: www.ukombozigospel.blogspot.com
Mwalimu Oscar Samba Nukuu, KUKATALIWA NA KUKUBALIWA
Dunia Ina Makundi Mawili ya Ndugu: Ana Akili Sana, Tumtenge, Tumchukie, Tumnyime Nafasi Asije Akapata Kibali Kuliko Sisi. Ana Akili Nyingi, Tumpe Nafasi Atatusaidia Miaka Saba ya Njaa.
Mara Nyingi Kundi la Kwanza Huwa Linatangulia. Usikubali Likakuvunja Moyo; Wape Muda Tu, Na Kundi la Pili Litakuja.
By Mwalimu Oscar Samba
Alhamisi, 13 Machi 2025
Andiko Muhimu Katika Biblia
Utakutana na Ujumbe huu kwenye Kitabu Chetu Kipya Kinachoandikwa Hivi Sasa cha UMUHIMU WA KUMPENDA NA KUMJUA MUNGU KWA MTOTO AU KIJANA CHIPUKIZI
NA Mwl Oscar Samba
Andiko hili linagusa nyanya zote muhimu kwako wewe kama mtumishi wa Mungu. Mosi ni eneo la kifamilia yaani baba mama na watoto au ndugu zako wengine. Pili eneo la kiserikali, anaposema muheshimu mfalme, hapo pia pana gusa viongozi wako wa kikanisa, viongozi wa kiroho na hata wakitaasisi au kampuni. Kwa ujumla ni kuheshimu utawala.
Anatupa dhima ya kumcha Mungu, kumpa Mungu heshima yake. Nasi twajua habari za kumcha Mungu! Ya kwamba ni kumuhofu, kuukataa na kuuchukia ovu. Yusufu akasema nitendeje uovu huu ni mkose Mungu? Linaanza na kukutaka kutoa heshima kwa watu wote. Bila kubagua umri, dini, ama kabila na kadhalika. Anasema katika watu wote.
1 Petro 2:17 Waheshimuni watu wote. Wapendeni ndugu. Mcheni Mungu. Mpeni heshima mfalme.
Zaidi Soma: www.ukombozigospel.blogspot.com
Jumanne, 4 Machi 2025
Kwenye Jina Tanzania Kuna Dini Fulani Imejumuishwa Hapo
The Ahmadiyya is an Islamic reform movement that originated in British India in 1889. Its members believe that Mirza Ghulam Ahmad (1835-1908) was the promised Messiah and Mahdi.
Ijumaa, 28 Februari 2025
Nukuu za Mwalimu Oscar Samba KUISHI TUNAYOYAHUBIRI
Tusipoishi Tunayo Yahubiri; Kuna Siku Tutaishi Tunayo Yatenda.
Zaidi Endelea Kutembelea www.ukombozigospel.blogspot.com
Jumatatu, 24 Februari 2025
#Ushuhuda Ni wa Kiongozi wa CASFETA Baada ya Kusoma Kitabu Changu cha KESHO YAKO NI BORA KULIKO LEO YAKO
"Ubarikiwe sana mwalim Oscar Samba, kwa kitabu hiki, kimenitia moyo sana kwa hali ninayopitia saiv chuoni, Siku sita nyuma nimekuwa mtu wa kuchoka, kuwa na mawazo mengi na kuhuzunika sana na kukata tamaa, nimekosa amani kulingana na Nafsi niliyonayo katika huduma ya Yesu kristo. Ila jana usiku roho inalisii na kunisisitiza kusoma kitabu hiki, nimekisoma hadi sa nane usk asubuhi nimekimaliza, kweli Mungu akubariki kwa huduma hii, niliwaza hadi kuachia nafasi niliyonayo ya huduma ili nipambane na masomo, ila najikuta nina nguvu za kusimama kuwaongoza tena watu ambao Mungu amenipa kuwaongoza, nimengi sana ya kusema Ahsante sana Mungu kwa neema ya kunikutanisha na Mwalimu Oscar Samba, Mungu akubariki na kukuinua kwa kazi hii.
Tuzidi kuombeana
Kesho yangu ni bora kuliko leo yangu, sitakubari kuzimia Moyo, Licha ya changamoto ninazopitia"
Ukikihitaji Kitabu Niandikie Ujumbe huu Wasapu +255759859287
Jumatano, 19 Februari 2025
Yesu Hata Kuacha
Hakuna Aliyewahi Kuja Kwa Yesu Akamtupa
Haijalishi Unapitia Mahali Pagumu Kiasi Gani, Huna Budi Kuhakikisha ya Kwamba Unaamua Kuokoka
Wokovu Utampa Yesu Nafasi ya Kuyapigania Maisha yako...Anasema Hata Kutupa Kamwe....Hili Ni Andiko la Ajabu Kabisa Katika Biblia.
Jumatatu, 17 Februari 2025
Mama Mchungaji: ISHINDE HOFU YA MAISHA YA BAADAE.
Na Mwl Oscar Samba
Ujumbe huu ni Sehemu ya Toleo la Pili la Kitabu Chetu cha NAFASI YA MAMA MCHUNGAJI; KATIKA HUDUMA YA MUMEWE.
Kwenye Pointi ya . Ishinde Hofu ya Kesho Kimkakati, (Maisha Baada ya Huduma au Uwepo wa Mume Wako). Kuna maisha baada au nje ya wito ama Utumishi. Umri ni kigezo muhimu cha kuweza kuwaondoa katika utumishi wa madhabahuni. Kifo pia ni njia ya jambo hili.
Ni kweli kabisa kumekwepo na maisha magumu, na hata manyanyaso mara baada ya mchungaji kufariki, kuondoshwa katika utumishi ama kustaafu. Mke na watoto au familia hujikuta wakiwa katika maisha yasiyo mepesi. Machozi ya uchungu na huzuni uwaandama. Malalmo na majeraha huwa sehemu ya maisha yao.
Hali hii imepelekea hofu kubwa katika nyumba nyingi za kitumishi. Watoto kwa mama wachungaji wamejikuta wakizungukwa na tatizo hili. Na hii
Alhamisi, 13 Februari 2025
Follow the Mwalimu Oscar Samba Mafundisho Ya Neno La Mungu channel on WhatsApp
Follow the Mwalimu Oscar Samba Mafundisho Ya Neno La Mungu channel on WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029Va827LBJENy9u6Enke1h
CHUNGA MNASEMA NINI MBELE YA FAMILIA NA WASHIRIKA.
Ujumbe huu ni Sehemu ya Kitabu cha NAFASI YA MAMA MCHUNGAJI; KATIKA HUDUMA YA MUMEWE, Toleo la Pili.
Na Mwalimu Oscar Samba
Katika hii pointi ya Chunga Mnasema Nini Mbele ya Familia, Uzao Wako, Washirika au Kanisa Kuhusu Dhehebu, Viongozi Wako wa Kiroho Dhidi ya Wito Wenu au Utumishi.
Unachopanda Kinaota. Linda Sana Unapanda nini katika fikra na mioyo yao. Watoto ndio kanisa la sasa na kesho. Washirika ndio watumishi wanaoandaliwa. Unaandaa watumishi wa aina gani?
Kumbuka, Upandacho Ndicho Uvunacho. Au Upandacho, Ndicho Tuvunacho!
Iwe ni wewe au mmeo, ama mtumishi mwingine katika madhabahu mliyopewa na Bwana, huna budi kuhakikisha udhaifu huo unaondoka miongoni mwenu. Mbegu nyingi za uasi zinapandwa mioyoni mwa washirika, au watoto kama sehemu ya manung'uniko kutoka kwa wazazi au watumishi wao. Wataponda dhehebu lao, watachambua kila madhaifu, lakini wao hawatoki; wanakuja kushangaa baadae wana watoto au washirika wasiopenda dhehbu la wazazi wao! Wanaanza kutafuta na kujaribu kuwarudisha bila mafanikio!
Hakuna sehemu isiyokuwa na madhaifu, hakuna viongozi waliokamilika. Sema tu, unafanya nini kukabiliana na hayo madhaifu ya wengine hapo ndipo swali lilipo. Malalamiko ya kwamba katika dini hii mchungaji binafsi huwezi kuendelea, michango ni mingi, mara mimi mchungaji nikifa leo mke wangu hatathaminiwa, ni miongoni mwa mambo ya kulinda sana. Mioyo ya watoto huumia wanaposhirikishwa maumivu ya wazazi, na tena huumia zaidi. Wanaanza kukua na "mentality" ya kwamba dini hii inawanyanyasa wazazi wangu. Fikra hizi zinakuja kuamia kwenye mioyo yao.
Machozi unayolizwa na viongozi yalilie bafuni, ili ukimaliza kulia maji unayoogea yaweze kuyasafirisha machozi yote; na lisisalie hata moja. Daudi hakuruhusu ubaya wa Sauli mfalme kuendelea kwenye moyo wa Sulemani mwanaye. Lazima hekima ya namna hii tuwe nayo. Ni hatari tukampa adui Shetani nafasi ya kutufanya kuandaa kizazi chenye "elements" au chembechembe za uasi ndani yake. Na uasi unaotokana na maumivu ni mbaya sana. Magumu unayoyapitia mengine umeandikiwa na Mungu ili baadae ukijakuwa kiongozi uweze kuja kuwa mtu sahihi kwa watu wako.
Nimeshuhudia mtoto wa mchungaji mmoja toka akiwa shule ya msingi na kisha sekondari akijisemea ya kuwa: siku nikiwa mkubwa sitafungua kanisa TAG, Kisa maneno ya malalamiko kutoka kwa wazazi wake. Wenzangu niliokuwa nao wengi walihama dini, kisa mbegu kama hizi. Baadae wanakuja kugundua ya kuwa walifanya maamuzi yasiyo sahihi!
Chunga sana, unalalamika nini kuhusu dhehebu, viongozi wako wa kidini, au utumishi ulio nao mbele ya watoto, uzao wako, mwenza wako na hata kanisa kwa ujumla! Kile unachokifanya kinapandwa ndani yao kama mbegu. Kuotesha mchongoma ni kazi ndogo sana, ila kuung'oa ni kubwa mno.
Baya zaidi, wengine wanachambua madhaifu kama haya, hata mbele ya watumishi ambao wapo chini yao, au ambao tayari anawaanda kabisa kuwa watumishi. Hili ni tatizo kubwa sana. Ni sawa na kubandua vipande vya boti vilivyowekwa kwenye nyufa au maungio ya mbao ya boti mliyoipanda.
Muungwana hutafuta na gundi ili kuziba vizuri kwa nia ya kupaimarisha zaidi. Ni lazima fikra zetu zifikie mahali pa kukua na kukomaa vizuri kabisa katika hili.
Kitabu Kikitoka Kitafute:
Mawasiliano:
Tutembele ama Wasiliana Nasi
http://www.ukombozigospel.blogspot.com
Tumeunda Channel ya WhatApp, Tufolo;
https://whatsapp.com/channel/0029Va827LBJENy9u6Enke1h
Kundi letu la WhatsApp https://chat.whatsapp.com/E0eD0xegh1eIGMjRykPyRD
Telegram https://t.me/+fft3GHXC9xIzYjhk
Subscribe YouTube yetu: https://www.youtube.com/@ukombozigospeltv
Kwa Maombi +255759859287, Email: ukombozigospel@gmail.com
Usiache Kutembelea na Ku-Like Page Yetu Ya Mafundisho ya Neno la Mungu Facebook:
https://www.facebook.com/MafundishoyanenolaMungunamwalimuoscarsamba?mibextid=ZbW
KwL
Tuandikie pia Maoni Yako; mwalimuoscarvitabu@gmail.com
Jumanne, 11 Februari 2025
Jumatatu, 3 Februari 2025
Nukuu ya Mwalimu Oscar Samba: Ufunguo wa Uamsho
Alhamisi, 30 Januari 2025
Nukuu ya Mwalimu Oscar Samba KUMSIKIA MUNGU UNAPOKUWA KATIKA PITO AU MAUMIVU MAKALI.
Jumanne, 21 Januari 2025
Nukuu ya Mwalimu Oscar Samba KALAMU YA HISTORIA
Usiongeze, Wala Kupunguza Wino Kwenye Kalamu ya Historia ya Maisha Yako. Uliopo Unatosha.
By Mwalimu Oscar Samba
Jumatatu, 13 Januari 2025
Karibu Katika Channeli Yetu ya Whatsapp ya MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU
https://whatsapp.com/channel/0029Va827LBJENy9u6Enke1h
Nukuu ya Mwalimu Oscar Samba CHANGAMOTO DHIDI YA MTAZAMO WA ADUI NA MUHUSIKA
Nukuu ya Mwl Oscar Samba: Hekima Katika Majaribu au Changamoto za Kimaisha
Kuna Mlima wa Kuing'oa na Kuutupa Baharini, na Kuna Mlima wa Kuuzunguka Upite.
Tunza Hili Daima...sio Kila Tatizo Lazima Liondoke...Mengine Yakwepe.
By Mwalimu Oscar Samba
Alhamisi, 2 Januari 2025
Neno la Leo
Habakuki 3:19 YEHOVA, aliye BWANA, ni nguvu zangu, Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu, Naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka .
Visti www.ukombozigospel.blogspot.com
Jumatano, 1 Januari 2025
Kalamu ya Historia na Nukuu ya Mwalimu Oscar Samba
Kalamu ya Kuandika Historia, Ina Wino Mwingi Sana. Kwa Hiyo, Usigonge Kichwa cha Kalamu.
By Mwalimu Oscar Samba
Unapaswa Kuvumilia Hadi Wino Uishe. .. _Ukigonga Kichwa Itagoma Kuandika na Utajidanganya Wino Umeisha_ ....
For More Keep In Visiting
www.ukombozigospel.blogspot.com