Ujumbe huu ni Sehemu ya Kitabu Chetu Kipya cha MOTO WA UAMSHO KATIKA BIBLIA (Tunachambua kila Kila Tukio Lenye Uamsho ktk Biblia Nzima).
Na Mwl Oscar Samba
Kitabu cha Kutoka ... na Yoshua Sura ya 3 na 4, pia Yohana 2:7-11.
Somo la ....: Ishara na Miujiza Kwa Mkono wa Musa: MIUJIZA HUITAMBULISHA HUDUMA.
Shalom mtu wa Mungu, tumekutana tena katika somo jingine. Hapa kwa pamoja tunaangazia nafasi ya ishara na miujiza katika kuitambulisha huduma au mtumishi husika.
Tukiwa tungali katika wito wa Musa kwenye kitabu hiki cha Kutoka; Musa alipoitwa, na kukabidhiwa majukumu kadhaa, alionyesha hali ya kutokukubalika. Alikuwa na mashaka au wasiwasi kama atapata kibali kutoka kwa watu. Jibu la Mungu lilikuwa ni jepesi tu kwake, Mungu alimpatia ishara kadha wa kadha. Na kumwambia ya kuwa, watamuamini kwa kupitia hizo.
Tazama; Kutoka 4:1 Musa akajibu akasema, Lakini, tazama, hawataniamini, wala hawataisikia sauti yangu; maana watasema, BWANA hakukutokea. 2 BWANA akamwambia, Ni nini hiyo uliyo nayo mkononi mwako? Akasema, Ni fimbo.
3 Akamwambia, Itupe chini; akaitupa chini, nayo ikawa nyoka; Musa akakimbia mbele yake.
4 BWANA akamwambia Musa, Nyosha mkono wako, kamshike mkia; (akaunyosha mkono wake akamshika, naye akageuka kuwa fimbo mkononi mwake;)
5 ili kwamba wapate kusadiki ya kwamba BWANA, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amekutokea.
6 BWANA akamwambia tena, Sasa tia mkono wako kifuani mwako. Akautia mkono wake kifuani mwake; naye alipoutoa, kumbe! Mkono wake ulikuwa una ukoma, umekuwa mweupe kama theluji.
7 Akasema, Tia mkono wako kifuani mwako tena. Akautia mkono wake kifuani mwake tena, na alipoutoa kifuani mwake, kumbe! Umerudia hali ya mwili wake. <br><br> And he said, Put thine hand into thy bosom again. And he put his hand into his bosom again; and plucked it out of his bosom, and, behold, it was turned again as his other flesh.
8 Basi itakuwa, wasipokusadiki, wala kuisikiliza sauti ya ishara ya kwanza, wataisikiliza sauti ya ishara ya pili.
Katika mstari wa kwanza, Musa analalamika ya kwamba, sauti yake haitasikika, hawataisadiki. Mungu anamwambia ya kuwa, atafanya ishara nao wataisikia/wataiamini hiyo sauti ya ishara, na wasipoiamini hiyo au kuisikia hiyo; basi ipo ishara nyingine ya kuyafanya maji kama damu katika nchi.
Tazama; Kutoka 4:9 Kisha itakuwa wasipoamini hata ishara hizo mbili, wala kuisikiliza sauti yako, basi, yatwae maji ya mtoni uyamwage juu ya nchi kavu, na yale maji uyatwaayo mtoni yatakuwa damu juu ya nchi kavu.
Msisitizo wangu mkubwa hapa, upo katika sauti ya Musa, inayosaidiana na sauti ya ISHARA. Kumbe, upako wako kama muhubiri, unaweza kutiwa nguvu au unaongezewa kibali zaidi, kutokana na utendaji wa upako katika ishara na maajabu au miujiza!
Kudhibitishwa kwa Yoshua: ISHARA ILIMTAMBULISHA.
Ndivyo Mungu alivyomwambia; BWANA akamwambia Yoshua, Hivi leo nitaanza kukutukuza mbele ya Israeli wote, wapate kujua ya kuwa mimi nitakuwa pamoja na wewe, kama nilivyokuwa pamoja na Musa.
Maneno haya yanakuja, wakati ambao Yoshua amekabidhiwa kijiti cha utawala na Musa, mara baada ya kifo chake. Mungu, anamuhaidia kumtukuza, kwa maneno mengine ni kumtambulisha mbele ya watu. Na tukio linalotarajiwa kufanyika, ni muujiza au ishara katika ajabu la maji ya mto Yordani.
Tazama; Yoshua 3:16 ndipo hayo maji yaliyoshuka kutoka juu yakasimama, yakainuka, yakawa chuguu, mbali sana, huko Adamu, mji ule ulio karibu na Sarethani, na maji yale yaliyotelemkia bahari ya Araba, yaani Bahari ya Chumvi, yakatindika kabisa; watu wakavuka kukabili Yeriko.
Yoshua 3:17 Na hao makuhani waliolichukua sanduku la agano la BWANA wakasimama imara mahali pakavu katikati ya Yordani; Israeli wote wakavuka katika nchi kavu, hata taifa lile lote likaisha kuvuka Yordani.
16 ndipo hayo maji yaliyoshuka kutoka juu yakasimama, yakainuka, yakawa chuguu, mbali sana, huko Adamu, mji ule ulio karibu na Sarethani, na maji yale yaliyotelemkia bahari ya Araba, yaani Bahari ya Chumvi, yakatindika kabisa; watu wakavuka kukabili Yeriko.
17 Na hao makuhani waliolichukua sanduku la agano la BWANA wakasimama imara mahali pakavu katikati ya Yordani; Israeli wote wakavuka katika nchi kavu, hata taifa lile lote likaisha kuvuka Yordani.
Andiko lifuatalo, linatupatia somo la ya kwamba; kitu muhimu au kimoja wapo kilichoamisha kibali cha Musa kwenye mioyo ya wana wa Israeli, ilikuwa ni ishara ya maji ya mto Yordani. Maana kama walivyokuwa na uchaji kwa Musa, ndivyo walivyokuja kufanya kwa Yoshua. Maandiko hukiri wazi ya kwamba, Mungu alimtukiza Yoshua mbele zao.
Tazama; Yoshua 4:14 Siku ile BWANA alimtukuza Yoshua mbele ya macho ya Israeli wote; nao wakamcha, kama walivyokuwa wakimcha Musa, siku zote za maisha yake. (Walimcha Yoshua, kama walivyokuwa wakimcha Musa.)
Tunajifunza nini hapa?
Karama za nguvu, yaani matendo ya miujiza, uponyaji na ile ya imani; ni muhimu katika kipindi hiki cha kuutafuta uamsho. Ni lazima tumatake Bwana na nguvu zake. Ili huduma na utumishi wetu uweze kuvuka mipaka, ni lazima ifike mahali pa kuhitaji utendaji wa namna hii. Maana ukigusa maisha ya watu, ukifanya mambo makubwa kama haya; utapata kibali kwao. Ukuu wa Mungu wako au wetu ukidhihirika, lazima atapata heshima. Na akiheshimika, na wewe utatukuzwa. Nawe ukiinuliwa, maana yake na jina ulilolibeba linakuwa katika utukufu mkuu zaidi.
Kukubalika kwa Huduma ya Yesu Zaidi, Huko Kana ya Galilaya.
Swala hili, lilijitokeza pia kwa Yesu. Maandiko hutujulisha ya kuwa, mara baada ya muujiza ule; wanafunzi wake wakamuamini. Haimaanishi walikuwa hawamuamini hapa awali! Ila kiukweli, ishara ile iliongeza kiwango cha imani dhidi yao.
Mwetu lazima iwe ni funzo, na somo litakalotusukuma zaidi na zaidi katika kuhitaji aina hii ya utendaji. Ni mweli tuna mafundisho mazuri, tuna misingi mizuri ya imani; ila changamoto mubwa inasalia kuwa ni kibali husaninkwa dunia nzima.
Kuna muda tunatamani jumbe tunazohubiri kanisani, zingesikika na taifa zima, na hata bara zima; lakini unajikuta unasimama mbele ya watu wasiozidi mia moja. Nikupe kiu sasa ya kuhitaji aina hii ya utendaji wa Kiungu. Maandiko yana majibu tu, yanakutaka kuzitaka karama za Rohoni; anaposema itakeni karama iliyo kuu; maana yake ni karama ile inayohitajika kwa wakati ule. Kwa mgonjwa ni ya uponyaji, kwa kiwetea au kipofu; ni matendo ya miujiza.
Tumuone Yesu na jinsi wanafunzi wake walivyoongeza kiwango chao cha kumuamini zaidi; Yohana 2:7 Yesu akawaambia, Jalizeni mabalasi maji. Nao wakayajaliza hata juu.
8 Akawaambia, Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa meza. Wakapeleka. 9 Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu wa meza alimwita bwana arusi,
10 akamwambia, Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa.
11 Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini.
Tukirudi katika ishara kwa Musa: Sasa, kama ishara inaongea, au ni sauti ama ni mamlaka katika utumishi, basi sasa hapana shaka utaelewa ni kwa nini waganga nao walifanya ishara, mbele ya Farao katika ya ishara za Musa! Ni kwamba, walikuwa wanajaribu kunyamazisha sauti ya Musa, yaani mamlaka iliyokwamo ndani yake.
Lakini pia, walitaka sauti zao ziwe kubwa kuliko ile ya Musa. Kwa lugha nyingine lilikuwa ni pambano la nguvu. "Power encounter". Hii ikupe kutokuwa na huruma na watu wanaojiinua kinyume na huduma yako. Maana pambano la namna hii ni sharti ulipigane. Hakikisha nyoka wako anameza nyoka zao! Usipofanya hivyo, lazima watakunyamazisha tu.
Jifunze kwa Musa na Haruni (Haruni huwakilisha fimbo au mamlaka ya Kikuhani); Kutoka 7:11 Ndipo Farao naye akawaita wenye akili na wachawi; na hao waganga wa Misri wakafanya vivyo kwa uganga wao.
12 Wakabwaga chini kila mtu fimbo yake, nazo zikawa nyoka; lakini fimbo ya Haruni ikazimeza fimbo zao.
Kitabu Kikitoka Kitafute
Zaidi Endelea Kutembelea https://ukombozigospel.blogspot.com/?m=1
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni