Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Ninakukaribisha ndugu msomaji wangu katika safu hii ya mafundisho ya Neno la Mungu kupitia
makala zetu, leo tunamalizia kulitazama kabila la Yuda.
Mstari unaofwata una mantiki ya aina yake katika hii
Nguvu ya Kiagano,
12 Macho yake yatakuwa mekundu kwa mvinyo, Na meno yake yatakuwa meupe kwa maziwa.
12 Macho yake yatakuwa mekundu kwa mvinyo, Na meno yake yatakuwa meupe kwa maziwa.
Wekundu wa macho unawakilisha Ghadhabu na Mvinyo kulevia,
weupe wa meno ni umaridadi wa maneno yake ama hotuba zake. Tukimtazama Yesu
alikuwa ni mwenye hekima kinywani mwake na aliyekubalika kwa maneno yake.
Kwa uapnde wa Mvinyo ama kulevia na Ghadhabu wasomaji wa
maandiko wanafahamu fika ya kwamba ipo silaha ya ajabu sana ya kupigania vita
kwenye ulimwengu wa roho itwayo kikombe cha ghadhabu, kikombe hiki hulevia
kisha huaribu na kuangamiza. Mimi binafsi hukitumia sana kikombe hiki
ninapokuwa nikipigana vita vya kimaagano na mizimu. Maana hutambua silaha hii
ina nguvu ya ziada katika hivyo vita.