Alhamisi, 13 Februari 2025

Follow the Mwalimu Oscar Samba Mafundisho Ya Neno La Mungu channel on WhatsApp

 Follow the Mwalimu Oscar Samba Mafundisho Ya Neno La Mungu channel on WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029Va827LBJENy9u6Enke1h 

CHUNGA MNASEMA NINI MBELE YA FAMILIA NA WASHIRIKA.


Ujumbe huu ni Sehemu ya Kitabu cha NAFASI YA MAMA MCHUNGAJI; KATIKA HUDUMA YA MUMEWE, Toleo la Pili.

Na Mwalimu Oscar Samba
Katika hii pointi ya Chunga Mnasema Nini Mbele ya Familia, Uzao Wako, Washirika au Kanisa Kuhusu Dhehebu, Viongozi Wako wa Kiroho Dhidi ya Wito Wenu au Utumishi.

Unachopanda Kinaota. Linda Sana Unapanda nini katika fikra na mioyo yao. Watoto ndio kanisa la sasa na kesho. Washirika ndio watumishi wanaoandaliwa. Unaandaa watumishi wa aina gani?

Kumbuka, Upandacho Ndicho Uvunacho. Au Upandacho, Ndicho Tuvunacho!
Iwe ni wewe au mmeo, ama mtumishi mwingine katika madhabahu mliyopewa na Bwana, huna budi kuhakikisha udhaifu huo unaondoka miongoni mwenu. Mbegu nyingi za uasi zinapandwa mioyoni mwa washirika, au watoto kama sehemu ya manung'uniko kutoka kwa wazazi au watumishi wao. Wataponda dhehebu lao, watachambua kila madhaifu, lakini wao hawatoki; wanakuja kushangaa baadae wana watoto au washirika wasiopenda dhehbu la wazazi wao! Wanaanza kutafuta na kujaribu kuwarudisha bila mafanikio!

Hakuna sehemu isiyokuwa na madhaifu, hakuna viongozi waliokamilika. Sema tu, unafanya nini kukabiliana na hayo madhaifu ya wengine hapo ndipo swali lilipo. Malalamiko ya kwamba katika dini hii mchungaji binafsi huwezi kuendelea, michango ni mingi, mara mimi mchungaji nikifa leo mke wangu hatathaminiwa, ni miongoni mwa mambo ya kulinda sana. Mioyo ya watoto huumia wanaposhirikishwa maumivu ya wazazi, na tena huumia zaidi. Wanaanza kukua na "mentality" ya kwamba dini hii inawanyanyasa wazazi wangu. Fikra hizi zinakuja kuamia kwenye mioyo yao.

Machozi unayolizwa na viongozi yalilie bafuni, ili ukimaliza kulia maji unayoogea yaweze kuyasafirisha machozi yote; na lisisalie hata moja. Daudi hakuruhusu ubaya wa Sauli mfalme kuendelea kwenye moyo wa Sulemani mwanaye. Lazima hekima ya namna hii tuwe nayo. Ni hatari tukampa adui Shetani nafasi ya kutufanya kuandaa kizazi chenye "elements" au chembechembe za uasi ndani yake. Na uasi unaotokana na maumivu ni mbaya sana. Magumu unayoyapitia mengine umeandikiwa na Mungu ili baadae ukijakuwa kiongozi uweze kuja kuwa mtu sahihi kwa watu wako.

Nimeshuhudia mtoto wa mchungaji mmoja toka akiwa shule ya msingi na kisha sekondari akijisemea ya kuwa: siku nikiwa mkubwa sitafungua kanisa TAG, Kisa maneno ya malalamiko kutoka kwa wazazi wake. Wenzangu niliokuwa nao wengi walihama dini, kisa mbegu kama hizi. Baadae wanakuja kugundua ya kuwa walifanya maamuzi yasiyo sahihi!

Chunga sana, unalalamika nini kuhusu dhehebu, viongozi wako wa kidini, au utumishi ulio nao mbele ya watoto, uzao wako, mwenza wako na hata kanisa kwa ujumla! Kile unachokifanya kinapandwa ndani yao kama mbegu. Kuotesha mchongoma ni kazi ndogo sana, ila kuung'oa ni kubwa mno.

Baya zaidi, wengine wanachambua madhaifu kama haya, hata mbele ya watumishi ambao wapo chini yao, au ambao tayari anawaanda kabisa kuwa watumishi. Hili ni tatizo kubwa sana. Ni sawa na kubandua vipande vya boti vilivyowekwa kwenye nyufa au maungio ya mbao ya boti mliyoipanda.

Muungwana hutafuta na gundi ili kuziba vizuri kwa nia ya kupaimarisha zaidi. Ni lazima fikra zetu zifikie mahali pa kukua na kukomaa vizuri kabisa katika hili.

Kitabu Kikitoka Kitafute:
Mawasiliano:
Tutembele ama Wasiliana Nasi

http://www.ukombozigospel.blogspot.com

Tumeunda Channel ya WhatApp, Tufolo;

https://whatsapp.com/channel/0029Va827LBJENy9u6Enke1h

Kundi letu la WhatsApp https://chat.whatsapp.com/E0eD0xegh1eIGMjRykPyRD

Telegram https://t.me/+fft3GHXC9xIzYjhk

Subscribe YouTube yetu: https://www.youtube.com/@ukombozigospeltv

Kwa Maombi +255759859287, Email: ukombozigospel@gmail.com

Usiache Kutembelea na Ku-Like Page Yetu Ya Mafundisho ya Neno la Mungu Facebook:

https://www.facebook.com/MafundishoyanenolaMungunamwalimuoscarsamba?mibextid=ZbW

KwL

Tuandikie pia Maoni Yako; mwalimuoscarvitabu@gmail.com

Jumanne, 11 Februari 2025

Jumatatu, 3 Februari 2025

Nukuu ya Mwalimu Oscar Samba: Ufunguo wa Uamsho

 


Kumtafuta Mungu Kuna Maana Kuu Mbili
Mosi; Kuna Kitu Kimepotea au Unakitaka, na pili Nia Dhabiti ya Mtafutaji ni Hadi Akipate anachokitaka.
 Huu Ndio Ufunguo wa Uamsho.

By Mwalimu Oscar Samba 
Zaidi Endelea Kutembelea: www.ukombozigospel.blogspot.com 

#Uamsho
#nukuu

Alhamisi, 30 Januari 2025

Jumatatu, 13 Januari 2025

Alhamisi, 2 Januari 2025

Neno la Leo

Habakuki 3:19 YEHOVA, aliye BWANA, ni nguvu zangu, Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu, Naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka


Visti www.ukombozigospel.blogspot.com

Jumatano, 1 Januari 2025

Kalamu ya Historia na Nukuu ya Mwalimu Oscar Samba

Kalamu ya Kuandika Historia, Ina Wino Mwingi Sana. Kwa Hiyo, Usigonge Kichwa cha Kalamu.

By Mwalimu Oscar Samba 

Unapaswa Kuvumilia Hadi Wino Uishe. .. _Ukigonga Kichwa Itagoma Kuandika na Utajidanganya Wino Umeisha_ ....

For More Keep In Visiting

www.ukombozigospel.blogspot.com

 

Jumanne, 31 Desemba 2024

Mama Mchungaji: MUNGU AMEKUPA KIWANGO FULANI CHA BUSARA AU HEKIMA AMA AKILI.

B Mwl Oscar Samba

Ni sehemu ya Kitabu chetu cha NAFASI YA MAMA MCHUNGAJI; KATIKA HUDUMA YA MUMEWE. Kitabu kipo katika hatua ya mwisho. 

10. Mungu Amekupa Kiwango Fulani cha Busara au Hekima ama Akili. Nachelea kusema kuliko mwanaume: maana hili pia utaliona kwa wenza wakiume ambao wake zao ni wachungaji. Na wao (wachungaji wa kike) wanapaswa kujifunza sana kuwaheshimu, kwa kutanguliwa na utambuzi wa nafasi za waume zao katika hili eneo la utumishi wao. Unatakiwa uijue hiyo nafasi ya umakamo kuwa huwa inaambatana na hekima au busara au akili za namna hii; ili uzitumie kutatua migogoro.


 Mama mchungaji epuka sana kuwa mtu wa kukoleza chumvi inapofika swala la tatizo au mzozo fulani. Epuka  pia tabia ya kutaka kuwa upande wa mumeo ili tu kupata kibali kwake, angali unajua yeye ana makosa, au uamuzi wake sio sahihi.


Msuluishaji yeyote yule lazima awe na tabia na maarifa ya kuwa katika mizani ya haki na usawa. Usitafute kupata kibali, tafuta kutatua mgogoro. Mke wa Hamani inaonekana alijua ukweli, alifahamu mumewe hayupo sahihi, lakini hakumuonya. Hadi mambo yalipoelekea mrama au kwenda kombo, ndipo alipomueleza wazi wazi; ya kwamba huyu Modekai uliyeanza kuanguka mbele yake....., hili ni kosa.

Mke wa Hamani laiti kama angejua mapema ya kuwa, anguko la Hamani mumewe, ni anguko lake; basi angalichukuwa taadhari mapema. Hamani alipotundikwa, na mkewe na watoto nao waliuawa, wakapokonywa na nyumba yao. 

Una neema ya ajabu sana, itambue na uitumie vizuri (msisitizo upo katika kuitambua na kuitumia vizuri). Mama mchungaji wangu aliyenilea Arusha, siku moja alichungulia dafutari la mchungaji la matangazo, akaona tangazo la kuivunja kwaya. Alitumia hekima kuinusuru, alimuomba kuwa atazungumza nao. Na kweli alifanikisha jambo lile. Unaonaje kama angekoleza chumvi? 

Jumatatu, 30 Desemba 2024

#BEBA MADHAIFU YA MUMEO; MFICHIE AIBU.

By Mwl Oscar Samba

Ni sehemu ya Ujumbe katika Kitabu cha #NAFASI YA MAMA MCHUNGAJI KATIKA HUDUMA YA MUMEWE

Kitabu kipo katika hatua za Mwisho. Na hapa ni katika pointi ya Beba Udhaifu wa Mumeo; Mfichie Aibu. Jukumu kubwa la nguo ni kuusitiri mwili. Hili ni jukumu la mwanzo na muhimu kuliko yote. Ni kweli nguo ina kazi nyingine kama vile ya urembo au kufanyika pambo, ila la kwanza kabisa ni kuufunika utupu. Aliyevaa nguo na ikaonyesha utupu, ni anajaribu kutuambia ya kuwa hajavaa nguo. Anapaswa kurudi katika Mwanzo sura ile ya tatu, ambapo Adamu na mkewe walipogundu waa uchi walilazimika kutafuta sitara.

Ambapo sitara hiyo ya vazi la majani haikuweza kukidhi hitaji, Mungu akawapatia vazi la ngozi. Sasa kama Mungu aliliondoa vazi ambalo bado lingeonyesha utupu na kuwapatia zuri zaidi. Uwe na hakika anayekataa zuri zaidi na kuvaa lenye kuonyesha utupu kuna shida kichwani; na shida hii itakuwa imeanzia moyoni. Huwa nasema hivi; nguo haina dhambi, ila nguo huwakilisha moyo wa dhambi au moyo mbovu.

Ijumaa, 20 Desemba 2024

Kuliko Nafasi Ishindwe Kulinda Haki, Bora Ife; Kwangu Nafasi Kazi Yake ni Kutoa Haki.

By Mwalimu Oscar Samba

 Follow Channel Yetu https://whatsapp.com/channel/0029Va827LBJENy9u6Enke1h/161


Jumamosi, 30 Novemba 2024

Nukuu ya Mwalimu Oscar Samba, Adui Wanaokuzunguka

 Kuwa Makini, Unapozungukwa na Watu Waliobeba Tochi Inayomulika Ulipokanyaga (Wakitafuta Makosa); Na Sio Wakumulikie Ili Usikosee Kukanyaga.


By Mwalimu Oscar Samba

Jumatano, 13 Novemba 2024

Nukuu ya Mwalimu Oscar Samba, Taa


Sii Kila Wakati Unahitaji Taa; Kuna Nyakati Unahitaji Macho Yenye Taa. 

Jifunze kwa Wanyama Waonao Usiku!


Mwenye Taa, Akikimbia Nayo; Unabaki na Macho Yako: Usiku na Mchana Utaweza Kutembea.

UTOFAUTI KATI YA MSAADA NA SADAKA, na hata Mchango

*UTOFAUTI KATI YA MSAADA NA SADAKA* 


Nimejibu swali la Mpendwa aliyetaka kujua huo utofauti


1.Msaada unatoa chochote....Sadaka Unatoa Ulichoguswa moyoni


2. Sadaka Unatoa ukiwa na Imani Kuna kitu nitapata kutoka kwa Mungu...Msaada unatoa ili kukidhi tu hitajio


3. Sadaka Unatoa kama kwa Bwana,....Msaada Unatoa kwa kumlenga muhusika


4. Sadaka Ukiitoa kwa Mazoea ina Adhabu kwa Mungu, Kuna kukataliwa kama Kaini au watu wa Kitabu cha Malaki moja na mbili...ila Msaada Sivyo


5. Baraka za Sadaka ni Kubwa kuliko Msaada.


6. Utoaji wa Sadaka Hukukutanisha na Mungu...Mfano Kornerio ktk Mtd. 10, na Mfalme Sulemani; 1 Wafalme 3. .....ila msaada utakutana tu na shukurani za wapokeaji...


NB: (a). Unaweza Kugeuza Msaada Kuwa Sadaka kwa Kuliombea jambo hili ili utoaji wako uwe na mguso wa Kiungu.


(b). Pia Kusikia Moyoni Mwako Roho Anakusukuma Kutoa nini? 


(c) Toa Kwa Imani...yaani tarajia kitu kutoka kwa Mungu.

 Muhimu : Kama ndivyo basi, likija changizo lolote, ikiwemo la harusi au kanisani...usiwe mwepesi kutoa kiwango kile kile kilichoainishwa au kuombwa kwenye kadi au kile cha desturi.


Badala yake tenga muda wa kutaka mapenzi ya Kiungu hapo. Sii vibaya ukavuka lengo lao au mazoea, kusikia kutoka moyoni na kutii ndiko kutakakobadili utoaji huo kutoka kwenye mchango au changizo la kawaida na kuwa Sadaka. 


Maana Warumi 10:17 hutuambia imani chanzo chake ni kusikia, na kusikia huko huja kutokana na Neno la Kristo na neno ni Kristo Mwenyewe...na utoaji wa kiimani ndiyo huitwa Sadaka.


Ukichunguza kwa umakini ujumbe huu...utagundua ya kuwa hata makanisani muda ule wa sadaka wengi wetu hatutoi Sadaka bali ni kama msaada.


Tunatoa kwa sababu bila hivyo mchungaji ataishiwa chakula, tunatoa kwa sababu jirani yangu hapa atanionaje nimekuja kanisani bila Sadaka! Ama ninaona aibu wenzangu wote wamesimama kutoa na mimi sijatoa!


Tunachangia kwa sababu bila hivyo kengo halitajengwa...! Ni kweli ni wajibu...lakini badili wajibu kuwa Imani..


Ndiyo maana watu wengi ni wagumu kutoa kwenye ujenzi wa kanisa jingine, tena kama ni dhehebu tofauti basi ndipo huwa wagumu zaidi.


Sababu kubwa ni imani kukosekana katika hili. Moyo wowote wa utoaji, lazima daraja lake liwe ni imani. Licha ya imani kutarajia kutoka kwa Mungu...lakini kitu kimoja wapo kikubwa inafanya ni kuyataka mapenzi ya Mungu katika hilo jambo...Kumsikia Yeye na Kumtii.


Maandiko yanaposema kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, hunuia kutusaidia katika kusudio lililozaliwa na imani. Ndiposa anatukumbusha kuwa akitoa haba au kidogo atapata kidogo, na baraka zipo kwa anayetoa kwa moyo wa ukarimu...huu sio ukarimu wa kawaida ni ukarimu ambao ndani yake una nasaba za Kiungu....


 Note : Kilio kikubwa cha kutoa sana na kutokuziona baraka...kinatokana na imani kutokuwa daraja la utoaji....utoaji ukiunganishwa na daraja la mazoea, msaada, changizo na hata lile la ninaona aibu wenzangu wanatoa mimi sijatoa; uwe na hakika baraka zake ni haba au hafifu.


Mungu anaposema atoaye haba atapata haba, ni makosa kulitazama hili andiko kwa kuangalia kiwango cha utoaji tu...Mungu hakuwa analenga tu kiwango cha utoaji...maana yule mwanamke alitoa kidogo kwa jinsi ya kipimo, ila kwa Mungu hakikuwa haba.


Imani ni kitu muhimu sana kinachopimwa hapo...utaiona kwa yule mwanamke wa kipindi cha Yesu, imani ilimsukuma kutoa vyote!


Huwezi kutoa vyote kama huna tarajio na humuamini aliyekutaka kutoa ya kwamba hatima ya maisha yako yote anayo yeye!


Ni rahisi kutoa ziada, au kumi ya 100 kati ya vile ulivyo navyo, maana una uhakika jioni asilimia 90 iliyosalia itakulisha, italipa yamkini na ada pia na hata rejesho la VICOBA!

Ila kutoa vyote, yaani asilimia 100 yote, ni imani kubwa sana maana umemuachia Mungu chakula cha jioni, ada na rejesho.


Sikuimizi kufanya hivyo! 

Maana pia kama hujasikia kutoka moyoni bado itakuwa sio imani ni msisimko! 


Na hapa ndipo wengi wanakwama...wanatoa kwa msisimko na wanashangaa hawajapokea hadi leo!


Imani lazima izaliwe katika kusikia ndani!

Tatizo wengine ni viziwi wa kiroho, masikio yao kwenye utoaji yamezibwa...hata Roho Mtakatifu akisema hawasikii....unapaswa kutatua hili tatizo...

Jumamosi, 2 Novemba 2024

Nukuu ya Mwalimu Oscar Samba, Wokovu, Maisha, Usikate Tamaa, Usivunjike Moyo, Jipe Moyo


Maisha ya Wokovu: Kuna Wakati Hata Kama Huoni mbele; Muamini Aliyekutangulia, yaani Kristo. Kwa hiyo usitumie Nguvu Nyingi Sana Kutazama Mbele, Bali Tazama Alipokanyaga ili Na Wewe Ukanyage.

By Mwalimu Oscar Samba