*UTOFAUTI KATI YA MSAADA NA SADAKA*
Nimejibu swali la Mpendwa aliyetaka kujua huo utofauti
1.Msaada unatoa chochote....Sadaka Unatoa Ulichoguswa moyoni
2. Sadaka Unatoa ukiwa na Imani Kuna kitu nitapata kutoka kwa Mungu...Msaada unatoa ili kukidhi tu hitajio
3. Sadaka Unatoa kama kwa Bwana,....Msaada Unatoa kwa kumlenga muhusika
4. Sadaka Ukiitoa kwa Mazoea ina Adhabu kwa Mungu, Kuna kukataliwa kama Kaini au watu wa Kitabu cha Malaki moja na mbili...ila Msaada Sivyo
5. Baraka za Sadaka ni Kubwa kuliko Msaada.
6. Utoaji wa Sadaka Hukukutanisha na Mungu...Mfano Kornerio ktk Mtd. 10, na Mfalme Sulemani; 1 Wafalme 3. .....ila msaada utakutana tu na shukurani za wapokeaji...
NB: (a). Unaweza Kugeuza Msaada Kuwa Sadaka kwa Kuliombea jambo hili ili utoaji wako uwe na mguso wa Kiungu.
(b). Pia Kusikia Moyoni Mwako Roho Anakusukuma Kutoa nini?
(c) Toa Kwa Imani...yaani tarajia kitu kutoka kwa Mungu.
Muhimu : Kama ndivyo basi, likija changizo lolote, ikiwemo la harusi au kanisani...usiwe mwepesi kutoa kiwango kile kile kilichoainishwa au kuombwa kwenye kadi au kile cha desturi.
Badala yake tenga muda wa kutaka mapenzi ya Kiungu hapo. Sii vibaya ukavuka lengo lao au mazoea, kusikia kutoka moyoni na kutii ndiko kutakakobadili utoaji huo kutoka kwenye mchango au changizo la kawaida na kuwa Sadaka.
Maana Warumi 10:17 hutuambia imani chanzo chake ni kusikia, na kusikia huko huja kutokana na Neno la Kristo na neno ni Kristo Mwenyewe...na utoaji wa kiimani ndiyo huitwa Sadaka.
Ukichunguza kwa umakini ujumbe huu...utagundua ya kuwa hata makanisani muda ule wa sadaka wengi wetu hatutoi Sadaka bali ni kama msaada.
Tunatoa kwa sababu bila hivyo mchungaji ataishiwa chakula, tunatoa kwa sababu jirani yangu hapa atanionaje nimekuja kanisani bila Sadaka! Ama ninaona aibu wenzangu wote wamesimama kutoa na mimi sijatoa!
Tunachangia kwa sababu bila hivyo kengo halitajengwa...! Ni kweli ni wajibu...lakini badili wajibu kuwa Imani..
Ndiyo maana watu wengi ni wagumu kutoa kwenye ujenzi wa kanisa jingine, tena kama ni dhehebu tofauti basi ndipo huwa wagumu zaidi.
Sababu kubwa ni imani kukosekana katika hili. Moyo wowote wa utoaji, lazima daraja lake liwe ni imani. Licha ya imani kutarajia kutoka kwa Mungu...lakini kitu kimoja wapo kikubwa inafanya ni kuyataka mapenzi ya Mungu katika hilo jambo...Kumsikia Yeye na Kumtii.
Maandiko yanaposema kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, hunuia kutusaidia katika kusudio lililozaliwa na imani. Ndiposa anatukumbusha kuwa akitoa haba au kidogo atapata kidogo, na baraka zipo kwa anayetoa kwa moyo wa ukarimu...huu sio ukarimu wa kawaida ni ukarimu ambao ndani yake una nasaba za Kiungu....
Note : Kilio kikubwa cha kutoa sana na kutokuziona baraka...kinatokana na imani kutokuwa daraja la utoaji....utoaji ukiunganishwa na daraja la mazoea, msaada, changizo na hata lile la ninaona aibu wenzangu wanatoa mimi sijatoa; uwe na hakika baraka zake ni haba au hafifu.
Mungu anaposema atoaye haba atapata haba, ni makosa kulitazama hili andiko kwa kuangalia kiwango cha utoaji tu...Mungu hakuwa analenga tu kiwango cha utoaji...maana yule mwanamke alitoa kidogo kwa jinsi ya kipimo, ila kwa Mungu hakikuwa haba.
Imani ni kitu muhimu sana kinachopimwa hapo...utaiona kwa yule mwanamke wa kipindi cha Yesu, imani ilimsukuma kutoa vyote!
Huwezi kutoa vyote kama huna tarajio na humuamini aliyekutaka kutoa ya kwamba hatima ya maisha yako yote anayo yeye!
Ni rahisi kutoa ziada, au kumi ya 100 kati ya vile ulivyo navyo, maana una uhakika jioni asilimia 90 iliyosalia itakulisha, italipa yamkini na ada pia na hata rejesho la VICOBA!
Ila kutoa vyote, yaani asilimia 100 yote, ni imani kubwa sana maana umemuachia Mungu chakula cha jioni, ada na rejesho.
Sikuimizi kufanya hivyo!
Maana pia kama hujasikia kutoka moyoni bado itakuwa sio imani ni msisimko!
Na hapa ndipo wengi wanakwama...wanatoa kwa msisimko na wanashangaa hawajapokea hadi leo!
Imani lazima izaliwe katika kusikia ndani!
Tatizo wengine ni viziwi wa kiroho, masikio yao kwenye utoaji yamezibwa...hata Roho Mtakatifu akisema hawasikii....unapaswa kutatua hili tatizo...
Watu wengi wanaombea uwezo wa kusoma Biblia, watakuomba Mchungaji uwaombee wajawe na nguvu za maombi...wajazwe Roho Mtakatifu...lakini ni wachache sana utakaowakuta wakiwa na ajenda ya kumtaka Mungu awape uwezo wa kumsikia inapofika eneo la utoaji...ndio maana kuna watu sasa ni mwaka wa 10 ikifika eneo la utoaji, bado anatoa 1000 Tsh.
Ikifika muda wa ibada, yeye hiyo ndiyo fedha yake ya karibu kuitoa!
Hakuna siku anatulia na kuruhusu kusikia kutoka moyoni!
Zaidi kitabu changu cha SADAKA ILIYOTUKUKA MBELE ZA MUNGU, Kikitoka kitafute ukisome.
www.ukombozigospel.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni