By Mwl Oscar Samba
Ni sehemu ya Ujumbe katika Kitabu cha #NAFASI YA MAMA MCHUNGAJI KATIKA HUDUMA YA MUMEWE
Kitabu kipo katika hatua za Mwisho. Na hapa ni katika pointi ya Beba Udhaifu wa Mumeo; Mfichie Aibu. Jukumu kubwa la nguo ni kuusitiri mwili. Hili ni jukumu la mwanzo na muhimu kuliko yote. Ni kweli nguo ina kazi nyingine kama vile ya urembo au kufanyika pambo, ila la kwanza kabisa ni kuufunika utupu. Aliyevaa nguo na ikaonyesha utupu, ni anajaribu kutuambia ya kuwa hajavaa nguo. Anapaswa kurudi katika Mwanzo sura ile ya tatu, ambapo Adamu na mkewe walipogundu waa uchi walilazimika kutafuta sitara.
Ambapo sitara hiyo ya vazi la majani haikuweza kukidhi hitaji, Mungu akawapatia vazi la ngozi. Sasa kama Mungu aliliondoa vazi ambalo bado lingeonyesha utupu na kuwapatia zuri zaidi. Uwe na hakika anayekataa zuri zaidi na kuvaa lenye kuonyesha utupu kuna shida kichwani; na shida hii itakuwa imeanzia moyoni. Huwa nasema hivi; nguo haina dhambi, ila nguo huwakilisha moyo wa dhambi au moyo mbovu.
Nguo haina dhambi kweli; ila nguo huuwakilisha moyo wa dhambi. Uvaaji ni ishara ya ndani. Sisemei uvaaji uliofunikwa na utamaduni, mfano ndugu zetu za makabila kadhaa; nina maanisha uvaaji uliadhiriwa na mazingira ya dhambi. Nguo ya bafuni, ikivaliwa bafuni ni sawa. Ila ya bafuni inapovaliwa sokoni; uwe na hakika moyo mbovu upo sokoni!
Mke ni nguo, mke ni kama vazi la sitara kwa mumewe. Kama vile Mungu alivyomuona mwanadamu aliyeanguka dhambini ya kuwa hajakamilika kwa vazi la majani. Na akalazimika kumpatia vazi la ngozi, ndivyo vivyo alivyomuona Adamu asiye na mke alivyokuwa hajakamilika. Akampatia mke ili kufunika madhaifu.
Madhaifu haya yapo katika maeneo mbalimbali ambayo hata wewe unayajua. Ukitaka kuhakiki tazama chakula kilichopikwa na mwanaume! Ni chapu-chapu, lakini ufanisi mdogo. Labla kiwe cha hotelini maana sasa pana dhima ya kuwa kazini, ila inapofika swala la nyumbani; wanaume ni kama wanalipua majukumu yao. Tazama katika kudeki, kuosha vyombo na kadhalika. Mtoto mdogo ni mzuri kwa Baba, ila akishajichafua au kujisaidia anatupiwa mama kwa haraka! Na huwezi kulaumu maana ndivyo tulivyo!
Lakini udhaifu mwingine ni huu ulionisukuma kukuandikia pointi hii. Ambao ninakutaka uutazame kwa sura muhimu sana. Mke analo jukumu la kuhakikisha ya kwamba anakabiliana na madhaifu ya mumewe kama yake. Anawajibu wa kumfichia aibu na kumsitiri.
Wepesi wa kusambaza, kufurahia au kuchekelea aibu ya mume au mchungaji ni kupungukiwa busara na ufahamu pia. Kazi ya mama mchungaji ni kufanyika sitara. Maneno kama muache uone atakavyopigwa na Mungu, ni maneno ya mawakala wa kuzimu. Ambao ni maadui wa ufalme wa mbinguni. Wewe kama mjezi wa huu ufalme unapaswa kuwa na fikra chanya za ujenzi. Lakini pia kama mke wa mchungaji huyo, unapaswa kuwa na mawazo mbadaya ya kutatua tatizo na sio kusubiria madhara hasi yatokee ili ajifunze.
Sipora mke wa Musa ni somo kubwa sana kwetu. Alipogundua kosa au udhaifu wa mumewe katika kutimiza agizo la Mungu, alilazimika kuingilia kati na kulitimiza. Unapogundua udhaifu wa mumeo katika kuganga majeraha ya washirika wewe kama mama mchungaji hupaswi kumchongea kwao na kusema ndo Mchungaji wenu huyo, ndivyo alivyo. Na waliopungukiwa ufahamu kabisa huanza kwa kukoleza na kusema ndo mjue jinsi na mimi ndani ninavyoteseka!
Mwenye kujitambua na kutambua nafasi yake, huchukua jukumu la kumganga muhusika kwa kumtia moyo. Kumfariji na kadhalika. Unapogundua udhaifu wa mumeo katika kauli, wewe fanyika kinywa kilichokolea munyu. Kwa maana kwamba, kile washirika wanachokikosa kwa mchungaji wanapaswa kukipata kwako. Kama sivyo kusingekuwa na haja ya wewe kuwepo hapo. Hasi na chanya katika betri zinajukumu la kukamilisha hitajio la kiumeme kwa kifaa husika. Hasi ikijiona ni bora kuliko chanya au chanya ikajiona sio sehemu ya betri, uwe na hakika hitajio halitatimia.
Unapaswa kujitambua na kutambua kilichokufanya kuwa hapo. Kazi ya nguo sio kuinuka, kuvuka au kudondoka ili kumuaibisha mvaaji, bali ni kujisitiri vyema zaidi. Ndio maana tukaiwekea vifungo au zipu. Ni ili kuifanya ibane vizuri kwa kupitia pia na mpira wa kwenye kiuno. Na kisha tunaiongezea na mkanda.
Tumuone Sipora; Kutoka 4:24 Ilikuwa walipokuwa njiani mahali pa kulala, BWANA akakutana naye akataka kumwua (Musa). 25 Ndipo Sipora (mke wa Musa/mama Mchungaji Musa) akashika jiwe gumu na kuikata govi ya zunga la mwanawe, na kuibwaga miguuni pake akasema. Hakika wewe u bwana arusi wa damu kwangu mimi. (Maneno ya mwisho yansema kwake yeye.) Nani Sipora. Kwa hiyo, jukumu lile lili himarisha uhusiano wao, na kuufanya muwa wa kiagano, tena agano lenye damu.
Kwanza ione hasira ya Mungu, tazama matomeo ya tukio. Matokeo sio katika uhusiano wao na Mungu tu kuimarika bali hata mahusiano ya kindoa! Inatufundisha nini hapa! Ni kwamba kutenda vyema katika utumishi kwamo kama mke. Kunamfanya Mungu kuimarisha uhusiano huo zaidi kiagano.
Kwa maana kwamba kutokutenda vyema kunaimungungua au kunaibomoa ndoa kiagano. Unapojitenda na utumishi, ni uanitenga si tu na baraka za Mungu kindoa kiagano, bali ni unafungulia mlqngo wa vita vya Shetani vinavyokuja katika mkakati wa kiagano.
Ukitaka kuamini, tazama ndoa za kitumishi zilizokosa uimara, kisha utafute moyo wa mke wa mchungaji katika kutumika pamoja na mumewe, lazima utakutana na nyufa. Ninaamini ni asilimia kubwa ndivyo.
Biblia ya kingereza imetumia neno husband, badala ya bwana lilotumika katika Biblia ya kiswahili. Hii ikupe kuepuka kufikiria ya kuwa bwana/Bwana anayenenwa pale sio mume. Tazama; Then Zipporah took a sharp stone, and cut off the foreskin of her son, and cast it at his feet, and said, Surely a bloody *husband* art thou to me.
Kitabu Kikitoka Kitafute:
Mawasiliano:
Tutembele ama Wasiliana Nasi
http://www.ukombozigospel.blogspot.com
Tumeunda Channel ya WhatApp, Tufolo;
https://whatsapp.com/channel/0029Va827LBJENy9u6Enke1h
Kundi letu la WhatsApp https://chat.whatsapp.com/E0eD0xegh1eIGMjRykPyRD
Telegram https://t.me/+fft3GHXC9xIzYjhk
Subscribe YouTube yetu: https://www.youtube.com/@ukombozigospeltv
Kwa Maombi +255759859287, Email: ukombozigospel@gmail.com
Usiache Kutembelea na Ku-Like Page Yetu Ya Mafundisho ya Neno la Mungu Facebook:
https://www.facebook.com/MafundishoyanenolaMungunamwalimuoscarsamba?mibextid=ZbWKwL
Tuandikie pia Maoni Yako; mwalimuoscarvitabu@gmail.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni