Ijumaa, 16 Desemba 2022

Mngoje Bwana kwa Saburi

rr*MNGOJE BWANA KWA UVUMILIVU* Zaburi 40:1 Nalimngoja Bwana kwa saburi, Akaniinamia akakisikia kilio changu. (Anatuambia kuwa alimnyonga Bwana kwa saburi naye akamuinamia! Kumuinamia maana yake ni kumsikiliza, ni kuweka umakini katika kumsikiliza. Kumuinamia ni sawa na mtu mrefu anapoongeleswa na mfupi, au mtu mzima kwa mtoto mdogo hulazimika kuinama kidogo ili sikio lake lifikile kimo cha kinywa chake.) Endelea na maandiko mengine kisha nitakujuza ninalotamani kukufahamisha hapa: "kichwani weka neno Saburi akiba" :2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu. :3 Akatia wimbo mpya kinywani mwangu, Ndio sifa zake Mungu wetu. Wengi wataona na kuogopa, Nao watamtumaini Bwana :4 Heri aliyemfanya Bwana kuwa tumaini lake, Wala hakuwaelekea wenye kiburi, Wala hao wanaogeukia uongo. Heri aliyemfanya Bwana kuwa tumaini lake! Neno tumaini jumlisha na saburi. Natumai unakumbuka kuwa nilikutaka kuweka akiba akilini neno "Saburi"! Katika mstari ule anatuambia kuwa alimngoja Bwana kwa saburi naye akamuinamia. Yaani anamshinikiza ama kumjibu. Nataka uone neno kumngoja Bwana..kisha neno kwa linatupa kufahamu ni njia ipi au kanuni ipi ilitumika hapa...ni saburi.. Saburi ni nini basi? ... Saburi ni aina ya uvumilivu ambao ndani yake una unyenyekevu, utulivu, amani ya Roho ni pamoja na tumaini katika Bwana kuwa siku moja atamjibu. Nataka kukwambia nini? Haijalishi unapitia mahali pagumu kiasi gani, wewe jifunze kumngoja Bwana kwa saburi..uwe na uvumilivu ambao ndani yake umebeba tumaini thabiti kuwa ipo siku Mungu atakujibu...haijalishi leo kuna ukimya mgumu kiasi gani ila siku moja najua yaja nitajibiwa tu. Nikutie moyo kuwa mngoje Bwana kwa saburi naye atakujibu tu....siku moja yaja, nawe utapokea majibu yako. Na Yamkini haujaokoka, nawe umeguswa na ujumbe huu na unatamani kuokoka (kumbuka wokovu maana yake ni kumkataa Shetani na mateso yake, dhambi na taabu zake na kumkubali Yesu na Uzima ama mbingu)... Kama ndivyo basi nikutie moyo kufuatisha Sala hii ya Toba kwa imani, Sema; EWE MUNGU BABA, MIMI NI MWENYE DHAMBI, NIMEGUNDUA MAKOSA YANGU, NISAMEHE YESU, FUTA MAJINA YANGU KWENYE KITABU CHA HUKUMU, NIANDIKE KWENYE KITABU CHA UZIMA WA MILELE, Amen. Hongera kwa Kuokoka na tafadhali tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo, Ameni. ... Zaidi tembelea www.ukombozigospel.blogspot.com Tazama na Sikiliza Mahubiri na Mafundisho Yetu hapa, Usisahau Ku-Subcribe ili uyapate kwa haraka zaidi; https://www.youtube.com/@ukombozigospeltv Jiunge nasi pia kwenye WhatsApp group letu la mafundisho ya neno la hapa: https://chat.whatsapp.com/E0eD0xegh1eIGMjRykPyRD Kundi letu la Telegram https://t.me/+fft3GHXC9xIzYjhk (Hapa utapata Mahubiri/Mafundisho Yetu kwa Haraka) Namba ya Telegram au Mawasiliano: +255759859287 inatumika pia kwenye WhatsApp na M-Pesa. Ukiguswa kuachilia Sadaka yako tafadhali usisite kufanya hivyo. Jina ni Oscar Samba. Usisite Kututembelea pia kwenye Ukurasa (Page) wa Facebook na "Ku-like" https://www.facebook.com/MafundishoyanenolaMungunamwalimuoscarsamba?mibextid=ZbWKwL Ama tuandikie email (Baruapepe) ukombozigospel.@gmail.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni