Jumanne, 13 Desemba 2022
Bibi Kikongwe katika Mkutano wa Injili
Huyu Bibi Alinifuraisha na kunitia Moyo sana, Aliudhuria mkutano wangu wote wa Ubaa Posta ya Zamani au Mahakama ya Mwanzo Rombo siku zote. Alikuwa anakaa migombani na kiti chake. Siku nyingine namkuta kashanitangulia.
Siku moja akaniambia kwamba yale maneno niliyoyasema, (kuyahubiri) ameyasikia na atayafanyia kazi!
Katika stori niligundua pia anakumbukumbu sana maana anakumbuka hadi tarehe ya Arusi yake. Alisema ni 1957, Mwezi wa 2 tarehe 22.
Kwangu huyu ni hazina. Nilimuhaidi kumtembelea siku moja (japo naye alinialika nyumba) ili kufahamiana zaidi.
Kwangu hii ni furaha moja wapo inayonifanya kuhubiri. Maana hadi vikongwe nao wanamkimbilia Yesu.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni