Jumanne, 5 Aprili 2022

Elewa ni Kwa nini Ndoa ni Zaidi ya Ulendo

 #VIJANA_NISIKILIZENI_Haya_Nayo_Ni_Maneno_ya_Mwenye_Hekima


Moyo Unaweza Kumpenda Mtu Bila Kuwa na Sababu Yoyote ya Msingi ila Usikubali Kuoana na Mtu Asiyetosheleza Vigezo Vya Ndoa kwa Viwango Fulani.

Moyo wa mwanadamu kuna muda unavutiwa na mtu bila hata kukupa sababu zenye mashiko kwanini umempenda. Utamsikia mtu akisema basi nimepanda tu! Ni kweli ni jambo jema, na hatuwezi kuweka sababu kwa kila mtu au maamuzi ya moyo kupenda.

Ndiposa wengine wakasema mapenzi ni upofu, ikiwa na maana kwamba kuna mambo ya msingi mtu anaweza  kuya_overloock ama kuyapuuza ifikapo swala la kupenda. Hapa napo sina shinda napo.

Ila msemo huu ndio unaonipa shida; kipendacho roho hula nyama mbichi! Ndugu yangu, nyama mbichi huvimbisha matumbo, huleta kuharisha sanjari na hatari ya magonjwa ya minyoo.

Unaweza kujikaza kuila ila uwe na hakika hapo mbeleni utakabiliwa na madhila tu, maana tumbo la kuhara, na magonjwa ya minyoo vitakuumbua tu!

Kwa maana kwamba sio kila uliyempenda anakufaa kuwa mke, au mume, swala la kuingia kwenye ndoa ni upana zaidi ya "maneno lakini nimempenda!"

"Lakini kanipenda,.. lakini aninampenda," umeshamfumania mara kadha, ukimuonya haonyeki, akizira leo ni hadi Jumanne ijayo, ana kiburi zaidi ya wote! Alafu ukiambiwa huyu kijana hafai kila mtaa ana mwanamke wewe unaishilia kusema lakini tunapendana! Oho... sijui moyo wangu umempenda hivyo hivyo!!

Kwenye kitabu chetu cha NDOA NI ZAIDI YA UPENDO, nimekutaka kuwa unapopenda au kupendwa usiweke akili mfukoni, nikatolea mfano wa kiatu kizuri nilichotaka kukunua pale eneo la Mipango Dodoma lakini hakikuwa kinanikaa.

Ningeweza kulazimisha kukinunua ila uwe na hakika kuwa mbele ya safari kingenichubua mguu na kunisababishia jeraha tu! 

Kiatu kinachobana hata mwendo unabadilika, badala ya kutembea umenyooka unataanza kwenda zigizagi, baya zaidi na speed au Kasi nayo inaathirika.

Kuna watu maisha yao leo yanayumba kama mlevi au machela inayowayawaya kama sio kunesanesa kwa kuchakaa au kuchoka. Maisha yao yamepunguzwa mwendo kwa sababu tu ya kuoana na Watu wasio sahihi. Ambao lakini waliwapenda, lakini walionyesha upendo, ila walikuwa wabovu kitabia, upendo ukawapofusha lakini maisha yakawazaliisha.

Wengine sio hata maisha ya ndoa, ni uchumba tu lakini kajikuta anakosana na kila mtu, biashara na miradi vinazorota, kielimu ama kitaaluma anadidimia kila mara hadi walimu wanajiuliza kuna nini! Nahelewani na kila mtu hadi wazazi! Kawa kama kichaa! Naye anajua kisababishi ni John, Juma ama Fatuma kama sio Jenifer

Huyo aliyekwambia kuwa ukipenda/wa unatakiwa uweke akili mfukoni na kutembea uchi ni nani? Nani kasema kwamba kuwa ukipenda ndo kila kitu kiyumbe kwenye maisha yako! Sasa huo ni uchumba tu hali ipo hivyo, je ndoa!

Mama Samia Rais wa Tanzania angeolewa na mtu ni mtu leo asingefika hapo! Kuna Watu ukiwaona hivi moja kwa moja unaona kaburi la ndoto zako, maana unatamani kuwa mchumi mkubwa, ila mwenzako kazi hataki na kila fedha yako anaipangia matumizi tena ni matumizi ya hovyo!

Hawazii kuwekeza bali ni kula na kuvaa na kujionyesha. Ukimuelekeza anakuwa mkali! Alafu bado unaendelea kubanana naye! Sawa, ila ujiandae kukutana na matokeo ya kula nyama mbichi! Ambayo ni umaskini na kuishilia kuwaomba omba! 

Kwa kifupi, ni ruksa kumpenda kila mtu, ila sio ruksa kuolewa au kuoana na mtu ni mtu!

Swala lake la kiimani ni muhimu, ampende Mungu na ajali utu! Kama mmeokoka kama mimi basi hakikisha haufungwi nira yaani usikubali kuoana na mtu asiyeokokna, hii ni Kibiblia wala haina mjadala.

Pia awe na tabia rafiki kimahusiano, kama kutokuwa na kiburi, akubali kusahihishwa anapokuwa amekosea au anapoonekana kuwa na mwenendo usio mwema. Maana wote tuna mapungufu, ila la muhimu ni unakabilianaje na mapungufu hayo, unaonyesha mrejesho gani unapoambiwa hapo pana kasoro!

Swala la uaminifu wa kimahusiano ni la lazima sana, akiwa sio mwaminifu,  nakushauri kuachana naye kabisa, usijidanganye kuwa mkioana atatulia, atabadilika, kama kashindwa kubadilika kipindi hiki huko mbele ya safari haiwezekani. 

Uwezo na fikra zake kiuchumi, tabia ya matumizi mabaya ya fedha na uzito au uvivu wa kujituma ni mambo ya kuyazingatia. Ukiona mapungufu msaidie, hasaidiki amua moja, kama utaendelea naye basi uwe na mbadala, na kama una uhakika atakuwa akihitaji fedha zako kwa nguvu au utakuwa mzigo mzito fanya maamuzi.

Jambo la kukijua chake cha upeo wa kutambua mambo ni muhimu. Mke sio mfanyakazi wa ndani, wala mume sio kwa ajili tu ya kuzalisha au kuionyesha jamii kuwa nawe umeolewa! Kuna zaidi ya hapo. Kama huna maono makubwa swala hili puzia ili kama ndoto zako ni kubwa hapa panahitaji uangalifu.

Sikutaki kuchagua wenye elimu kubwa, maana wapo waliosoma ila upeo wao ni mdogo.

Yapo mambo mengi ila nilichotaka hapa ni wewe kujifunza kutokuoana na mtu tu kwa sababu unampenda! Moyo unaweza kupenda jambazi! Lazima ujifunze kuuzuilia.

Maana wapo mabinti waliokatazwa na kuonywa na wazazi na jamii ila wakalazimisha baadae wakaja kujutia. 

Pia ukimpenda mtu usijizuilie kufanya uchunguzi kuhusu maisha yake ya zamani na ya sasa, na usizibe masikio unapoletewa habari mbaya kumhusu, zichunguze na ukiona ukweli zikabili. Upendo usikupofushe kiasi cha kupuzia kwa kila jambo. Na kuona wanaokuletea hizo taarifa ni wazushi au wanakuia wivu, ukizichunguza ndo utabaini ukweli.

Ni vyema kuhakikisha kuwa unamuombea, madhaifu mengine ni ya kibinadamu na mtu hapendi ila anayo. Ukiyaombea Mungu atayaondoa. Kubwa zaidi isitegemee akili zako katika mahusiano.

Muombe Mungu naye atakupatia aliyesahihi: Mithali 19:14 Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na Bwana.

Bwana anayetajwa hapo ni Bwana MUNGU. Andiko hilo la Biblia linatupa kuwa na hakika kuwa hatupaswi kumpata mwenzi nje ya mpango wa Mungu. Lakini pia haizuilia akili zako na moyo wako kupenda na kufanya tathimini. Ila elekeze moyo na fikra zako katika mapenzi ya Mungu. Ukimpenda hakikisha Mungu anakuhakikishia kuwa huyu ndie!


By Mwl Oscar Samba +255759859287 au tembelea www.ukombozigospel.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni