Jumatatu, 25 Februari 2019

Mwalimu Oscar Samba:Ujumbe kwa Waimbaji: Nisehemu ya kitabu changu cha TUNU YA TUNDA LA ROHO, ni kipingele katika Tunda la Furaha, pwenti ya tano:


5. Humuwezesha Mtu Kumuimbia Bwana kwa Furaha, Changamko la moyo ni miongoni mwa vitu munimu sana wakati wa kumuimbia Bwana, iwe ni kusifu au kuabudu, mtu mwenye hili Tunda haijalishi yupo taabuni au la! Ikifika wakati wa kumsifu na kumuabudu au kumuimbia Bwana Mungu wake furaha na bashasha na mashamushamu huufunika uso wake kama moshi ufunikavyo nyumba ipikiayo kuni, ama wingu liufunikavyo mlima na msitu wakati wa baridi, na kipupwe.

Ninakupa maandiko ambayo hudhiirisha uso huu wa furaha nayakati za kumuimbia Bwana, na kwa waimbaji au viongozi wa uimbaji, ni munimu jambo hili kuwa kwao, maana chakula cha Mungu ni moyo uliochangamka mbele zake, huzuni na masononeko unatakiwa kuvisahau inapofika swala la kusogea patakatifu pa Bwana;

Tulione kwanza agizo :1 Mambo ya Nyakati 15:16 Kisha Daudi akamwambia mkuu wa Walawi, kwamba awaagize ndugu zao waimbaji, pamoja na vyombo vyao vya kupigia ngoma, vinanda, na vinubi, na matoazi, wavipige na kupaza sauti kwa furaha.

Kisha tujionee vitendo:
1 Mambo ya Nyakati 16:10 Jisifuni kwa jina lake takatifu; Na ufurahi moyo wao wamtafutao Bwana.
27 Heshima na adhama ziko mbele zake; Nguvu na furaha zipo mahali pake.
31 Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie; Na waseme katika mataifa, Bwana ametamalaki;
32 Bahari na ivume na vyote viijazavyo; Mashamba na yashangilie na vyote vilivyomo;
1 Mambo ya Nyakati 16:33 Ndipo miti yote ya mwituni iimbe kwa furaha,

Kumbuka au fahamu kwamba mnapomuimbia Mungu, kushangilia ambako hakuja beba furaha ya ndani, ni maigizo, hakuna kelele za shangwe ambazo hazina furaha ndani yake, upigaji wa makofi na miluzi na "mbinja" nje ya furaha ya dhati, ni kuigiza, unajua maji au chai hata uiweka kwenye chupa ya soda haiwezi kuwa soda!

Sieti-ee? Lakini ki-ukweli vimo kwenye chupa ya soda, ila ni maji au chai, hasilani abadani haviwezi kugeuka na kuwa soda kwa sababu tu! vimo chupani.

Alikadhalika ndivyo ilivyo makofu, na miluzi na vigelegele bila kuchanganywa na furaha ya Roho Mtakatifu ambayo hudhiirika hata usoni kwa anayemuimbia Bwana.

Jambo kama hili au dhima kama hii ya uimbaji utaiona tena kwenye kitabu changu maalumu cha wimbaji kiitwacho:

IJUWE HUDUMA YA UIMBAJI, Tafadhali vitabu vikitoka vitafute.

Pia kama hujaokoka na ungependa kuoka tafadhali fuatisha maneno haya;
Sema, BWANA YESU, MIMI NI MKOSAJI, NISAMEHE,NIOKOWE, NINAKUAMINI NA KUKUPOKEA MOYONI MWANGU KAMA MUNGU NA BWANA NA MWOKOZI WANGU, NI KWELI ULIKUFA NA KUZIKWA, NA KUFUFUKA, AMENI.

Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la walokole lilokaribu yako ukaabudu hapo, mawasilino yangu, +2557 598 592 87.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni