Ni Ujumbe uliopo kwenye hicho kitabu mada ya Mwisho inayoelekeza namna ya kuingia Shambani au kuanza huduma;
Kumekuwa na tatizo kubwa sana kwa watumishi wengi wa leo, wanazitaka ishara na miujiza, pamoja na vitu vya mwilini kabla hawajaenda kuanza huduma.
Wanasahau maandiko husema kuwa ishara hizo zitaambatana na hao waaminio, ikiwa na maana kitu cha kwanza ni wao kuingia shambani, ndiposha ishara, na miujiza na mafanikio au vitendea kazi vya mwilini kama vyombo, majengo na hata mwanamke mjane wa sarepta hutokea kazini.
Siku moja wakati Roho ananifudisha jambo hili, alinipa mfano wa ajabu sana, aliniambia; Si unawaona madereva na magaria ya dalala, na makondakta wake, nami nilijibu ndiyo.
Ingekuwaje kama wangekaa nyumbani, au walipopaki magari yao, na kuanza kupiga debe wakiwa hapo, wangepata abiria?
Nalijibu hapana! Yenye alama ya mshangao, ndipo aliponiambia na watu wangu huwa katika mfano huo, wanapiga debe, ya kwamba gari lao linaelekea mahali fulani, lakini hawapo tayari kuliendesha na kuingia barabarani, yaani huanza kutafuta abiria, wakiwa au gari likiwa ndani, limeifadhiwa, bila kuliwasha na kuanza kazi barabarani.
Lakini madereva wa dunia hii, hulitoa gari lilipohifadhiwa wakiwa hawana abiria, ila wanapofika njiani au kituoni huanza kupiga debe na hatimaye kupata abiria, ikifika jioni, wana hesabu ya tajiri au ya gari, na wao wana riziki zao.
Watu wangu wasiowasha gari na kuanza kazi, nao ikifika jioni wanataka riziki zao, angali hawana hesabu ya tajiri, au ya gari.
Kwa hiyo hawana budi kuingia barabarani, maana huduma tayari nimeshawapa, ambayo ni gari.
Mpendwa jambo hili ni kubwa, nalo ni pana, lina hitaji kulifahamu, maana ni kweli hata anayeuza duka, anapofungua asubui hajui atakayemuuzia, lakini wateja huja, na wewe huna budi kuanza huduma, wateja yaani washirika watakuja, na vitu kama vyombo, vya matangazo, na usafiri, vitakufuata tu.
Swali: Kuna abiria anayelipa nauli bila kuona gari? Sasa mbona wewe unataka vya mwilini bila kuingia shambani?
Kama Mungu akikujalia kukupa kabla, ni vyema, ila usimpangiye, ifanye kazi yake, kwa kutumia kipengele kile cha kuwa tayari kutumika popote, na ukumbuke Mwana wa Adamu hana pa kukilaza kichwa chake, ikiwa na maana ya kwamba, mazingira yoyote yasikuzuiliye kuifanya kazi ya Mungu.
Marko 16:17 Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya.
Biblia ya mafafnuzi, imetumia lugha nyepesi kidoko katika zitafutana;
(17Na ishara hizi zitaandamana na wale wanaoamini: kwa jina langu watatoa pepo na watasema
kwa lugha mpya.)
Ya Basic English imetumia neno ishara hizo zitakuwa nao hao wenye imani na jina langu;
(Mark 16:17 And these signs will be with those who have faith: in my name they will send out evil
spirits; and they will make use of new languages;)
Na ya King James Version, Imetumia neno, zitawafwata, maana yake, waende, alafu zije;
(17 And these signs shall follow them that believe; In my name shall they cast out devils; they shall speak with new tongues;)
Sasa chukua neno, Zita-wafwata, Zitakuwa nao, kuandana, na kufuatana, maana yake, ili kuvipata hivyo, unapaswa kwenda, navyo vije, usipofungua duka, na wateja wasipokuja, usilaumu wateja au muajiri wako, bali jilaumu wewe maana unapaswa kulifungua hilo duka, ndipo waone bidhaa, hakuna mtu ananunua mbuzi aliyepo kwenye gunia au kiroba, ni shariti aonekane kwanza.
Alafu pia hilo andiko linasema waaminio, au wanaoliamini jina la Yesu, nawe unapaswa kuwa na imani ya kwamba Yesu atakutokea tu, huko uendako, yupo kunguru atakayekutunza, wala usihofiye vya mwilini ya kwamba vitakuwaje.
Hakuna vyombo, hubiri bila vyombo, vitakuja tu, maana hata Yesu hakutembea na punda siku zote alizokuwa akiingia Yerusalemu, ila ipo siku aliingia na punda.
Sio kila mahali Yesu alihubiri juu ya jukwaa, ni mara chache sana alipata ofa za mitumbwi/boti na kuitumia kuingai ndani yake, na wakati mwingine alikuwa akikwepa makutano waliokuwa wakimsonga sana, pia na ili aweze kufikisha ujumbe vyema maana akiwa majini upepo wa mawimbi husafirisha sauti, nawe kuna siku utakutana na mtuimbwi wa wakina petro na kuupanda, yaani utapata jukwaa tu, wala usiwe na shaka.
KITABU KIKITOKA USIKIKOSE
Kama hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU, ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
Na Huduma ya UKOMBOZI GOSPEL, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigospel@gmail.com Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigospel.blogspot.com
Pia #Like #Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata habari hizi kwa haraka, zaidi. @ugukombozi Gospel
PAGE: https://www.facebook.com/ugukombozigospel/
Kikundi: https://www.facebook.com/groups/2268418230050621/
Pia kwenye mtando Mpya wakitanzania wa
2 DAY SKY: https://www.2daysky.com/ukombozigospel
Pia TAZAMA VIDEO ZETU HAPA https://www.youtube.com/channel/UCv1tghnugOSpbmb5h6ebJtA (Ukombozi Gospel)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni