Na Mwalimu Oscar Samba #UgMinistry #SHARE #SAMBAZA Ili
kueneza injili hii Zaidi.
Ujumbe
huu ni sehemu ya kitabu changu cha SABABU ZA DAMU YA YESU KUWA NA NGUVU ILIYO
NAYO.
Kama uliwai kuua mtu, kwa kukusudia au
bila kudhamiria, kwa njia ya ajli, au kutumia silaha, kutoa mimba, ukiwa kama
mama wa mtoto, baba, dakitari, au kushiriki kiushauri ama kiuwezeshaji ama kwa
njia yoyote ile.
Pia hata kama ulihusika
katika mauaji ya mtu au watu, kwa njia yoyote, ikiwemo ya ushauri, kupanga
mipango, au unafahamu fika na bayana kuwa damu ya mtu fulani ipo juu yenu, au
juu yako, au katika eneo unaloishi njia hii itafanyika msaada kwako au kwenu
Lakini pia hata kama wewe ni asikari, au mwanajeshi, na uliwai kumwaga damu,
haijalisha uliona ina hatia au la, ila ujue ukweli wa hatia hiyo na uhalali wa
mauaji hayo anayefahamu ni Mungu mwenyewe, Shetani na damu husika , kwa hiyo
nawe yafanye haya maombi, ukijaribu kujihesabia haki kuwa ulikuwa ukitimiza
wajibu wako sawa, au uliwajibika kufanya hivyo na haoni kosa lako, “it’s ok,”
ila kwa ushauri wangu na waimizo la Roho Mtakatifu ndani yangu, huna budi
kufanya hivyo:
Hakikisha unainyamazisha
hiyo damu, ili isiendelee kunena mabaya au kulia kisasi au malipizi kwenye
ulimwengu wa roho. Lakini kanuni ya kwanza;
1. Omba Rehema, tubia tukio hilo,
muombe Mungu akusamehe, wala usijihesesabie haki, kwa namna yoyote ile. Tumia
Damu ya Yesu katika kutubia hilo kosa, ombea rehema kutokana na umwajikaji wa
Damu ya Yesu kwa ajili ya ondole la dhambi, Mathayo 26:28. Omba hadi upate mani
ya kiungu moyoni mwako.
2. Inyamazishe hiyo damu. Katika
maandiko tunaambiwa kuwa damu ya Habili ilinena, ukienda katika Mwanzo 4: 10 Akasema,
Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka
katika ardhi. Tunaona hapo kuwa hii
damu ililia, ukiendelea mbele yake, unaona Mungu akiachilia adhabu, ikiwa na
mantiki kuwa kilio kile kilihitaji ulipizaji wa kisasi, kwani baada ya kisasi
hatuinoni ikilia tena.
Kwa kuwa wewe umeshaomba
Rehema, ni fika kuwa Mungu amesha kusamehe, au kufuta hilo tukio kiroho, kwa
hiyo unao uhalali wa kutumia Damu ya Yesu ili kunyamazisha hiyo damu
iliyomwagwa.
Tamka kuinyamazisha kwa
kumwaga Damu ya Yesu juu yake na kuitaka inene mema, tumia andiko la Waebrania
12:24 linalosema kuwa Damu ya Yesu inanena mema kuliko ile ya Habili.
Omba hivi, kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth, natumia
Damu ya Yesu kuinyamazisha hiyo damu iliyomwagika, “kama unamjua mtaje jina,”
namwaga Damu ya Yesu kwenye hiyo aridhi, kwa Damu ya Yesu Kristo, ewe
damu nyamaza kimya, milele, ninakuamrisha nyamza kimya, namwaga Damu ya Yesu
ile ya Agano jipya, sawasawa na Luka 20:22, na Matayo 26:28, ninakunyazamazisha
ewe damu ya fulani, pia ninaitaka Damu ya Yesu kunena mema ili kubatilisha
sauti za kisasi na maneno ya malipizi kutoka kwenye hiyo damu ya fulani.
Fanya hayo maombi kwa
imani, huku ukimnyima Shetani kukuhukumu moyoni kuwa uliua, fahamu toba
uliyoifanya tayari Mungu alishakusamehe, kwa hiyo hatia yako haipo tena mbele
za Mungu na Mungu akishasamehe huwa anasahau kabisa. Kwa hiyo hukumu ya kipepo
ipinge kwani inalenga kukuondolea ujasiri mbele za Mungu, na fahamu kwa mujibu
wa Waebrania, tunaambiwa tukisogele kiti cha Neema kwa Ujasiri ili tupate
Rehema, kwa hiyo hakikisha unapingana na Ibilisi katika hili jambo pili nafsi
yako pia isi-kuhukumu, na muombe Mungu ama Roho Mtakatifu aiwezeshe kujisamehe.
3. Futa Madhara Yote yaliyopenya na
yaliyokusudiwa, kunapotokea mauaji au umwajikaji wa damu isiyo na hatia,
kwenye ulimwengu wa roho Shetani hutumia jambo hilo kama lango la kupenyeza
madhara, au matatizo fulani, lakini pia, hata Mungu huachilia adhabu, ukitaka
kuamini vyema, nenda kwa Kaini nawe hapo utajionea haya mambo vyema.
Kwa hiyo nyunyiza Damu
ya Yesu huku ukitamka kufuta hayo madhara, na kuyachomoa, yaweza kuwa ni
magonjwa, roho ya kukataliwa, mauti kwenye uchumi, mauti kwenye ndoa na
kadhalika.
Chimbuko la ujumbe huu,
ni pale mwanamke mmoja aliyenifuata siku chache zilizopita, akiniambia kuwa
uchumi wa mume wake upo mahali pa gumu, na kubainisha kuwa kazini kwao,
kuna mfanya kazi mwenzao, alisababisha ajali, na aliyegongwa alifariki.
Mara baada ya ajali hiyo
uchumi wa kiwanda umekuwa mahali pa gumu hadi kufikia hatua ya mishahara ya
wafanya kazi kusumbua.
Mimi nilielewa kwa
haraka kuwa damu ya mauti iliyomwagika ilisababisha hayo madhara, na iliachilia
mauti kwenye uchumi wa kiwanda.
Kwa hiyo ilinibidi
kuomba rehema kisha kuinyamazisha ile damu kwa Damu ya Yesu, na kuitaka Damu ya
Yesu inene, mema, nikiwa na maana kuwa ile ya aliyegongwa ilinena au kulia au
kuhitaji mauti kwenye uchumi wa kiwanda sasa hii ya Yesu itafuta yale maneno,
na kunena Baraka, na mafanikio katika kiwanda.
Kama upo makini,
umeshaelewa umuhimu wakutubia hata matukio yaliyofanywa na wengine, kwani yana
matokeo makubwa kwako, kieneo, kihuduma, na hata kikazi kama yapo mafungamano,
pia hata kindugu kama upo uhusiano, kwani mtoto wa Kaini, na mke wake,
wanashiriki matokeo ya adhabu ya baba yao, au mumewe.
Kwa hiyo, tamka kuondoa
hayo madhara kwenye ulimwengu wa roho, hata kama huja yajua, Roho Mtakatifu
atakusaidia kuomba vyema au kukufahamisha pia zuia yaliyokusudiwa yasitokee.
4. Itisha Urejesho,
Upatanisho na Matengenezo,
Jambo hili liliharibu kasa maisha ya Kaini, na kwa kiwango fulani maisha ya
Mfalme Daudi pale alipomua yule mume wa mke aliye mtwaa, yaani Uria.
Kwa hiyo, maadamu Mungu
ameshakusamehe, au kumsamehe muhusika, au rehema yake ipo juu yenu au juu ya
eneo husika taasisi na hata kampuni, ni fika unaweza sasa kumuomba Mungu afanye
urejesho kama kuna vitu vilivyo haribika, au kupotea, au kufa kabisa, kama
uchumi, afya kusumbua na hata migogoro, unaweza fanya urejesho kupitia damu ya
Yesu.
Fanya pia matengenezo,
kweye vitu vivyo haribiwa, maana mauti hufanya mauti na uharibifu mwingi kwenye
mengi, kwa Daudi kulitokea mauaji kwa wanae, Amnoni kuuawa na Absalom, wake au
masuri wake, kutezwa na mwanaye, ufalme wake kutaka kupinduliwa, hata yeye
kuvunjiwa heshima, “ingawaje kulikuwa na makosa mawili, yaani la kulala na mke
wa mtu, lakini pia la mauji ya mume wa mtu, lilichangia mno.”
Pia itisha upatanisho,
kama ulikuwa nami vyema katika kitabu hiki utafahamu kuwa Damu ya Yesu inafanya
upatanisho nami nimekujuza toka hapo awali kuwa kupitia shuhuli za kikuhani,
hapo zamani za Agano la Kale, kuwa ipo dhima ya Upatanisho.
Tatizo hili la mauaji,
lina tabia ya kuleta mafarakano kwenye ulimwengu wa roho, na hata kujidhiirisha
mwilini, kama ni kwenye kampuni, imetokea ajali au mauaji fulani, au kwenye
taifa, kabila na kabila wanapouana, kinachofuata ni watu hao kuwa na uhasama,
au kuchukiana, kitu ambacho ni hatari na kinazuia upatikana wa amani sana,
maana hali hii huenda kizazi hadi kizazi.
Kwa hiyo jipatanishe na
patanisha jamii husika, kupitia Damu ya Yesu, kwa mujibu wa maandiko
tuliyoyaona hapo awali kwenye pwenti zilizotangulia humu kitabuni, Damu hii ina
uwezo mkuwa, na ukizingatia ni Damu ya kuhani mkuu, na kama tunavyo fahamu
kuhani ana dhima ya kufanya upatanisho, wa Agano la Kale walitumia damu za
wanyma na hata za ndege, ila huyu Yesu alijidhamini kwa Damu yale mwenyewe, kwa
mantikii hiyo nguvu yake ni kubwa mno.
5.Futa Alama ya damu ya
Mauti na Adhabu, damu inapomwagika bila
hatia, huwa inaacha alama mahali husika kwenye ulimwengu wa roho, kwa hiyo
ifute kwa Damu ya Yesu, sio katika aridhi tu, bali hata katika taasisi,
kampuni, serikali, na hata, familia au kazi fulani, au mtu binafsi, kanisa na
kadhalika.
Lakini pia, kuna kuwa na
Alama, ya Adhabu, jambo hili utaliona vyema kwa Kaini;
Mwanzo
4: 15 Bwana
akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara
saba. Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga.
Unaweza usilielewe jambo
hilo kama utachambua hilo andiko kimwili, maana utaona tu, kuwa alama hiyo ni
matokeo ya maombi ya Kaini ya kwa Mungu au kama kinga ili asidhuriwe.
Lakini licha ya jambo
hilo ambalo kweli lipo, na lipo dhairi, ila ukweli ni kwamba, umwagaji damu,
huachilia alama fulani ya kiadhabu, ambayo pia hufanyika kama lango la
haribifu.
Ukisoma hapo katika hilo
andiko, utafahamu kuwa hiyo alama inanenewa, kuwa kila atakayemua, Kaini,
atalipizwa mara 7, kwa hiyo alama yake, ilibeba au ilikuwa na mukutadha wa
mauti, uliyotoka na mauti, ambapo tena, una maudhui ya kimauti kwa
atakayesababisha mauti.
6. Funga hilo Lango la Uharibifu,
Fanya maombi ya Malango, kama huyafahamu tafuta kitabu changu cha MALANGO
KWENYE ULIMWENGU WA ROHO.
Kwa kifupi, damu isiyo
na hatia ya mauti ni lango la Uharibifu, lilisababisha uharibifu kwa Kaini, kwa
Daudi, kwa Yoabu, na wenzake, (1 Wafalme 2: 5 Na zaidi ya hayo,
umejua alivyonitenda Yoabu, mwana wa Seruya, yaani, alivyowatenda majemadari
wawili wa majeshi ya Israeli, Abneri, mwana wa Neri, na Amasa, mwana wa
Yetheri, ambao aliwaua, na kuimwaga damu ya vita wakati
wa amani, akautia damu ya vita mshipi uliokuwa viunoni mwake,
na viatu vilivyokuwa miguuni mwake.)
Kwa hiyo nyunyiza Damu
ya Yesu kwenye hilo lango, na tamka kulifunga wakati unanyunyiza, fanya maombi
haya mfumo wa maombi ya vita.
Pia kama ni mauti au
maujia ya kikabla, jamii na jamii, au vuta vya wenyewe kwa wenyewe, huna budi
kuhakikisha unayafanya kwa mzigo zaidi, na ukisha maliza achilia amani ya Bwana
kwenye eneo, jamii, kampuni, mtu au sehemu husika.
Mwisho, Mshukuru
Mungu kwa uponyaji wake, na msamaha, lakini pia nyunyiza, Damu ya YESU, kama
ulinzi, juu yako, au katika eneo ulilokuwa ukiliombea, na ifunge kabisha hiyo
roho ya mauti isirejee tena, au kuendelea kukaa hilo eneo.
Na kama uliyemuombea,
yupo mahabusu, futa kesi kwa Damu ya Yesu, kwani rehema imesamuondolea hatia
rohoni, na kama mmekata rufa, tengua hukumu husika kimaombi.
Pia kama yupo
gerezani yaani amehukumiwa tayari, na haijalishi amehukumiwa kunyongwa au la!
Na hataka kama ni kifungo cha maisha au miaka mingi gerezani, wewe tamka
kufunguliwa kwake, maana hii Damu ya Yesu, ina huo uwezo, na jambo hili lipo
wazi kimaandiko;
Zekaria
9: 11 Na kwa habari zako wewe, kwa sababu ya damu ya agano
lako, nimewatoa wafungwa wako katika shimo lile
lisilo na maji.
Cha msingi ni wewe kuwa
na imani ya kutosha, kuhusu matumizi ya hii Damu ya Yesu.
Tumia pia Andiko la
Isaya 61:1, ili kutangaza uhuru wake, au kujitangazia uhuru wako, kama ni wewe
unajiombea;
Isaya
61: 1 Roho
ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri
wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia
mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.
Dalili au ishara zitakazokujulisha kuwa damu iliomwagika ingali
juu yako:
Na Suluhu la kuepukana
na mambo haya ni kufuata hatua za kanuni iliyotangulia hapo juu, kama
umeshaifutua, rudia tena kufanya hayo maombi, na ukimaliza, fanya maombi ya
vita dhidi za hizo roho za mauti la lango lake, na lango la ndoto za mauti
ulifunge.
1. Hofu ya Mauti, Ukiona kila ukikaa mwenyewe, au ikifika usiku,
au ukilala, ukitembea, ama ukikumbuka hilo tukio, unaingiwa na hofu kubwa,
fahamu fika roho ya mauti inakufuatilia, na inatumia lango la hiyo damu.
Ukisoma katika 1 Wafalme 2, utajione mwenyewe kuwa
Yoabu, aliingiwa na hofu kama hii, na kukimbilia madhabahuni, ila aliuawa hapo
hapo.
Ikiwa na maana hofu
inayokuja, inalenga kudai ulipizwaji wa kisasi, kwa hiyo ni vyema kushuhulikia
jambo hilo, maana njia kuu ya mauti ni hofu, na dalili kuu pia ni mtu kuwa na
hofu, woga, ukiona mtu anyeumwa, nakwambia anasikia kufakufa au ana hofu kubwa
sana, jua Mauti imekaribia, kama ni muombaji msaidie.
2. Kuota Ndoto za Mauti, Hali ya kuota upo msibani, makaburini, eneo
lenye maiti, ni dalili ya kwamba lipo lango la mauti linalokufuatilia, na ndoto
hizo huweza kuua, uchumi, ndoa, kazi, na hata kuleta mauti ya kimwili.
Lakini pia wengine
hutokewa katika ndoto na marehemu, na wapo ambao sio katika ndoto bali wazi
wazi, huweza kuwa mchana, au usiku, wapo ambao pia huona kivuli chake, kumbuka
sio yeye, bali ni mizimu, au mapepo ya mauti yanatumia lango la mauti yake.
Lakini, wengine hufika
mahali pa kupiga kelele, hali ambayo inaweza kuwafanya kuonekana kama vile
wamerukwa na akili au kuchanganyikiwa, mfano utamsikia akisema, “hao, wanakuja
kunichukuwa, hao, hao, nisaidieni, wanakuja,” anaweza kuwataja na majina yao,
au kujikuta kitaja aliowahi kuwaua, wachawi wanateseka sana na kifungo kama
hiki.
Wasio jua huenda kwa
waganga ili kupa msaada, ambapo hatapata suluhu, ila watazituliza, au kupunga
hayo mapepo yaliyokaa kwenye hilo lango la mauti ya damu isiyo na hati, lakini
madhara yako palepale, na udhibitisho ni kwamba baada ya muda hali hiyo
hujirudia tena.
Lakini baya zaidi
mashariti ya mganga huweza kudai agano au kafara ya damu, halia ambayo
italifanya tatozo kupanuka, na kuwa kubwa zaidi kwani umwagaji wa damu nyingi
utaliimarisha tatizo, na kuongeza ukubwa wake, na kuikaza hiyo nira, na
kuongeza idadi ya mapepo.
Ila wanao jua,
wataitumia njia nilizo zitaja humu kitabuni ili kujiepusha na hili tatizo, wala
hawataangaika kutumia sindano za usingizi au kuamini muhusika amerukwa na akili
au kalewa kwa pombe na hata kulogwa ama kutupia majini, bali ni mapepo ya
mauti, katika lango la mauti la damu isiyo na hatia.
Bali wakati madakitari
wanadunga sindano za usingizi, yeye anapabana na tatizo kiroho.
3. Kujiwa na Kumbukumbu
za hilo Tukio, kwa wengine wanapo
pita eneo husika, au kila inapofika muda fulani, kumbukumbu hizo humjilia, na
wengine husikia maumivu kama ya moyo kuuma, ila ni katika eneo la kulia la
mwili wake, ukiona hivyo fahamu ni ishara ya roho ya mauti kutumia hilo lango.
4. Uchungu wa Mauti, wapo wanaoua, na wao kujiua, au kutamani kufa,
au kuwa na uchungu iliopitiza au huzuni ya mauti.
Yuda Iskariote
alipomsaliti Yesu alitamka bayana kuwa ameisaliti damu isiyo na hatia, matokeo
yake, ni yeye kumbilia kitanzi;
Mathayo
27:3 Kisha Yuda, yule mwenye kumsaliti, alipoona ya kuwa amekwisha
kuhukumiwa, alijuta, akawarudishia wakuu wa makuhani na wazee vile vipande
thelathini vya fedha, akasema, Nalikosa nilipoisaliti damu isiyo na
hatia.
Kilichofuata ni yeye
kujinyonga, kwa nini? Uchungu wa mauti na huzuni yake;
I
Wakorintho 15:56 Uchungu wa mauti ni dhambi, na
nguvu za dhambi ni torati.
2
Wakorntho 7:10 Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba
liletalo wokovu lisilo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanya mauti.
(Kama wewe ndie uliyeua,
ninakutaka kuomba rehema na sio kujidhuru)
Pia kama tatizo hili
lipo kwenye eneo, au nyumba unayoishi au kufanyia kazi, basi kila ukiishi hapo,
au kufika hapo, utasikia uchungu huu wa mauti, na dawa yake ni kumwaga Damu ya
Yesu kwenye hilo eneo, ukiomba Rehema, kuinyamazisha na kufuta uhalali wake, na
kuitaka ile ye Yesu inene mema.
Kama kuna mtu aliwi
kuua, au kuuawa, na anawatokea mara kwa mara, bila kujali, ni ndugu yenu
alihusika au la, wewe tumia Damu ya Yesu ya Agano Jipya kumwaga juu ya kaburi
lake, au mauti yake, na ukifanya hiyo kwa imani, hatawatokea tena milele,
nimelifanya hili na nimeona matokeao yake, kwa hiyo sikufundishi nadharia bali
ni jambo ambalo ni bayana na hakika.
5. Kuota Ndota ukiwa
unakula nae chakula, au kula na watu
waliokufa, hii ni ishara kwamba, unaishi chini ya agano la mauti, yaani kuna
mtu amekuingiza, au kuliingiza eneo unaloishi chini ya hilo agano au lipo agano
ulilowai kuingia lenye mauti ndani yake, yaani lilosababisha damu ya mtu asiye
na hatia kumwagika.
Kumbuka unapoenda au mtu
anapoenda kwa mganga, na kuhitaji utajiri, kisha kupewa mashariti ya kumchukuwa
mtu msukule au kafara ya damu, ni bayana jambo hilo huwa ni agano la mauti au
la damu.
Sasa kama umeajiriwa, au
kufanya kazi kwenye kampuni kama hiyo, ninakutaka kujitenga na hilo agano, kwa
maombi ya Damu ya Yesu, lakini kama umerithishwa au kuinunua hiyo kampuni, ni
fika hilo agano unapaswa kulifuta, kwa maombi ya rehema, na yakulifuta kwa Damu
ya Yesu, tubia ufanyikaji wake kiundani katika kuomba rehema, na yafanye hayo
maombi kwa kuugua.
Kumbuka kama unafanya
kazi kwenye hiyo kampuni, au biashara au ni muajiriwa hapo, na kufahamu lipo
agano la damu, sija kwambia, ulivunje, ni elewe, wala usijifanye wa kiroho kuko
mimi au Roho Mtakatifu, nimekwambia jitenge, ila kama kampuni umeinunua wewe,
au kuirithi, hapo unapaswa kulivunja.
Na ukimuona mtu kama
huyu, kama ni muajiriwa, mtenge na hili agano kimaombi, kama ni nyumba uliyo
panga kitenge chumba chako au eneo unaloishi kwa Damu ya Yesu.
Udhibitisho wa kuwa
ndoto kama hizo, za kuota unakula chakula ni ishara ya uwepo wa agano la mauti,
upo katika kitabu kile cha Mathayo 26, na Luka 22, katika karamu ya Yesu, Yesu
alimega mkate, kumpa kila mwanfunzi wake na mzao wa mzabibu, akisema jambo hilo
ni ushirika wa kiagabo, na yale maji ya mzabibu, katika Luka 22:20, na Matahyo
26:28 tunaambiwa ni Agano jipya, lakini ukitazamwilini ni chakula na shurubati
au “juice” kwa kingereza.
Lakini pia yawezekana ni
agano lilofungwa na babu zako, au baba zako, au jamii ya kwenu, cha muhimu ni
wakina nani unaowaota, na mahali gani au moyoni mwako unashudiwa kuwa ni wakina
nani.
Usijaribu kupuzi mambo
haya, maana yasiposababisha mauti ya kimwili, huweza kuwa ile ya kiuchumi, na
hata kiroho, au kiafya ama kihuduma.
Kuna watu wakisha ota
hivyo, gafla hali ya kuhudumu au utayari wa kufanya huduma unapotea, au kufifia
na hata kufa, au anapoteza ile ladha ya kusoma biblia, kufanya maombi au
utumishi fulani, na Roho Mtakatifu ananiambia hata ushirika na wapendwa wenzake
huadhirika pia, akiwaona atwakwepa, atakwua mziato kuchangamana nao, na huweza
hata kuondoka nyumbani akijua atakuja, cha ajabu hana hata sababu ya msingi
uzito tu unakuja moyoni na nafsi mwake na ni hatari zaidi ukiingia hadi rohoni.
Ukisoma vyema hayo
maandiko ya karamu ya Yesu utabaini kwamba, jambo lile lililenga kuwa na
ushirika pamoja na Kristo, ndio maana hata leoa, tunatakiwa kufanya hivyo,
yaani kushiriki meza ya Bwana.
Licha ya hivyo, katika
Yohana 6. Tunataarifiwa, ili tuweze kuurithi uzima wa mielele, ni lazima tuule
mwili,wake , na kunywa Damu yake.
Kama kwa Yesu lililenga
kutupa ushirika pamoja naye, ni bayana hata kwa Shetani linanuia kumfanya huyu
mtu kuwa na ushirika na mizimu, au roho za kuua huduma, kiroho ukisha ingizwa
kwenye ushirika na nguvu za giza ni dhairi kuwa hali yako ya ushirika na Kristo
Yesu, itafifia.
Ndio maana kulitoa pepo
lililoingia ndani ya mtu kwa njia ya chakula, au akiota ndoto anakula au kunywa
na watu, huwa linasumbua sana, na ukitaka hauweni ya haraka, mnyeweshe huyo mtu
Damu ya Yesu ile ya Agano Jipya.
(Lakini pia fahamu sio
kila ndoto ya kuota unakula, ni ya kipepo, nyingine huwa na ujumbe wa Mungu,
zaidi tafuta kitabu changu cha NGUVU YA NDOTO KWENYE ULIMWENGU WA ROHO.)
NB: Ukigundua eneo au aridhi uliyonunua, kuwa ina
Damu ya Mauti juu yake, yaani iliyomwagika bila hatia, ama kitu ulichonunua, au
biashara uliyo nayo, gari ulilorithi na hata nyumba, huna budi kuhakikisha
kuwa, utafuata hizo kanuni za kujinasua na hilo dhara, kwani hata kwa kiwanja
au eneo lilonunulia kwa fedha za usaliti wa Yesu alizopewa Yuda, lilitwa konde
la damu;
Matendo
ya Mitume 1:18 Basi mtu huyu
alinunua konde kwa ijara ya udhalimu; akaanguka kwa kasi akapasuka matumbo yake
yote yakatoka.
1.19 Ikajulikana na watu wote wakaao Yerusalemu; hata konde lile
likaitwa kwa lugha yao Akeldama, maana yake, konde la damu.
Unaonaje kama wewe ukija
kununu kiwanja cha konde la damu na kuishi hapo bila kushulikia hilo tatizo?
Utashanga roho za mauti
haziachi kubisha hodi kwenu, nyumba nyingi zenye matatizo, ambazo hazikaliki au
zenye mauza-uza, au majini, zina hili tatizo.
Kama hujaokoka na
unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na BWANA kwa
upya leo, tafadhali fuatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA YESU,
NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU, ULIKUFA NA
KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA
YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa kuokoka na
tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
Na Huduma ya UKOMBOZI
GOSPEL, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka wasiliana nasi,
Barua pepe: ukombozigospel@gmail.com Simu: +255 759 859 287 pia
waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigospel.blogspot.com
Pia #Like #Penda
Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata habari hizi
kwa haraka, zaidi. @ugukombozi Gospel
Pia kwenye mtando Mpya
wakitanzania wa
2 DAY SKY: https://www.2daysky.com/ukombozigospel
Pia TAZAMA VIDEO
ZETU HAPA https://www.youtube.com/channel/UCv1tghnugOSpbmb5h6ebJtA (Ukombozi Gospel)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni