Ijumaa, 16 Desemba 2022

Mngoje Bwana kwa Saburi

rr*MNGOJE BWANA KWA UVUMILIVU* Zaburi 40:1 Nalimngoja Bwana kwa saburi, Akaniinamia akakisikia kilio changu. (Anatuambia kuwa alimnyonga Bwana kwa saburi naye akamuinamia! Kumuinamia maana yake ni kumsikiliza, ni kuweka umakini katika kumsikiliza. Kumuinamia ni sawa na mtu mrefu anapoongeleswa na mfupi, au mtu mzima kwa mtoto mdogo hulazimika kuinama kidogo ili sikio lake lifikile kimo cha kinywa chake.) Endelea na maandiko mengine kisha nitakujuza ninalotamani kukufahamisha hapa: "kichwani weka neno Saburi akiba" :2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu. :3 Akatia wimbo mpya kinywani mwangu, Ndio sifa zake Mungu wetu. Wengi wataona na kuogopa, Nao watamtumaini Bwana :4 Heri aliyemfanya Bwana kuwa tumaini lake, Wala hakuwaelekea wenye kiburi, Wala hao wanaogeukia uongo. Heri aliyemfanya Bwana kuwa tumaini lake! Neno tumaini jumlisha na saburi. Natumai unakumbuka kuwa nilikutaka kuweka akiba akilini neno "Saburi"! Katika mstari ule anatuambia kuwa alimngoja Bwana kwa saburi naye akamuinamia. Yaani anamshinikiza ama kumjibu. Nataka uone neno kumngoja Bwana..kisha neno kwa linatupa kufahamu ni njia ipi au kanuni ipi ilitumika hapa...ni saburi.. Saburi ni nini basi? ... Saburi ni aina ya uvumilivu ambao ndani yake una unyenyekevu, utulivu, amani ya Roho ni pamoja na tumaini katika Bwana kuwa siku moja atamjibu. Nataka kukwambia nini? Haijalishi unapitia mahali pagumu kiasi gani, wewe jifunze kumngoja Bwana kwa saburi..uwe na uvumilivu ambao ndani yake umebeba tumaini thabiti kuwa ipo siku Mungu atakujibu...haijalishi leo kuna ukimya mgumu kiasi gani ila siku moja najua yaja nitajibiwa tu. Nikutie moyo kuwa mngoje Bwana kwa saburi naye atakujibu tu....siku moja yaja, nawe utapokea majibu yako. Na Yamkini haujaokoka, nawe umeguswa na ujumbe huu na unatamani kuokoka (kumbuka wokovu maana yake ni kumkataa Shetani na mateso yake, dhambi na taabu zake na kumkubali Yesu na Uzima ama mbingu)... Kama ndivyo basi nikutie moyo kufuatisha Sala hii ya Toba kwa imani, Sema; EWE MUNGU BABA, MIMI NI MWENYE DHAMBI, NIMEGUNDUA MAKOSA YANGU, NISAMEHE YESU, FUTA MAJINA YANGU KWENYE KITABU CHA HUKUMU, NIANDIKE KWENYE KITABU CHA UZIMA WA MILELE, Amen. Hongera kwa Kuokoka na tafadhali tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo, Ameni. ... Zaidi tembelea www.ukombozigospel.blogspot.com Tazama na Sikiliza Mahubiri na Mafundisho Yetu hapa, Usisahau Ku-Subcribe ili uyapate kwa haraka zaidi; https://www.youtube.com/@ukombozigospeltv Jiunge nasi pia kwenye WhatsApp group letu la mafundisho ya neno la hapa: https://chat.whatsapp.com/E0eD0xegh1eIGMjRykPyRD Kundi letu la Telegram https://t.me/+fft3GHXC9xIzYjhk (Hapa utapata Mahubiri/Mafundisho Yetu kwa Haraka) Namba ya Telegram au Mawasiliano: +255759859287 inatumika pia kwenye WhatsApp na M-Pesa. Ukiguswa kuachilia Sadaka yako tafadhali usisite kufanya hivyo. Jina ni Oscar Samba. Usisite Kututembelea pia kwenye Ukurasa (Page) wa Facebook na "Ku-like" https://www.facebook.com/MafundishoyanenolaMungunamwalimuoscarsamba?mibextid=ZbWKwL Ama tuandikie email (Baruapepe) ukombozigospel.@gmail.com

Jumanne, 13 Desemba 2022

Bibi Kikongwe katika Mkutano wa Injili

Huyu Bibi Alinifuraisha na kunitia Moyo sana, Aliudhuria mkutano wangu wote wa Ubaa Posta ya Zamani au Mahakama ya Mwanzo Rombo siku zote. Alikuwa anakaa migombani na kiti chake. Siku nyingine namkuta kashanitangulia. Siku moja akaniambia kwamba yale maneno niliyoyasema, (kuyahubiri) ameyasikia na atayafanyia kazi! Katika stori niligundua pia anakumbukumbu sana maana anakumbuka hadi tarehe ya Arusi yake. Alisema ni 1957, Mwezi wa 2 tarehe 22. Kwangu huyu ni hazina. Nilimuhaidi kumtembelea siku moja (japo naye alinialika nyumba) ili kufahamiana zaidi. Kwangu hii ni furaha moja wapo inayonifanya kuhubiri. Maana hadi vikongwe nao wanamkimbilia Yesu.

Alhamisi, 8 Desemba 2022

Mkutano Ubaa Posta ya Zamani au Mahakama ya Mwanzo Rombo

Jana Ndivyo Tulivyoanza Mkutano wetu wa 20 hapa Ubaa Posta ya Zamani au Mahakama ya Mwanzo Rombo. Hakika Sijawahi kuona mkutano wenye mwitikio mkubwa km huu! Watu wa Ubaa Hongereni. Nitajitahidi kuhifadhi matukio vyema km nitajaliwa. #Pia_tafadhali_Endelea_Kutuombea

Jumapili, 4 Desemba 2022

Mabadiliko Machache RATIBA ZA MIKUTANO YETU (iliyosalia)

Hadi sasa tangu mwezi wa 7/2022 tupo kwenye mkutano wa 19 18. Kitasha Kakfua (Chekechea) 23-27/11/2022 19. Kitasha; Shule ya Msingi Roya, (umeandaliwa na Kanisa la PSMA) 30/Nov -4/Dec /2022 20. Ubaa, Ushiri. 7-11/12/2022 21. Sio Makalema tena, (badala ya Yamerejea Mamsera ktk Kanisa la Kingdom kwa Mch Daniel.) 14-18/12/2022 22. Himo, 21-25/12/2022 (Moshi Vjjn) 23. Kinyauli, Kerio Mashati. 2-8/1/2022 Mingine Rombo Klnjaro. Na Mwl. O. Samba

Neno la Leo Jumapili

Neno la Leo
Zaburi 127:5 Heri mtu yule Aliyelijaza podo lake hivyo. Naam, hawataona aibu Wanaposema na adui langoni. Maana yake Heri au Amebarikiwa mtu yule ambaye podo lake limewekwa mishale kwa ajili ya vita ama silaha Hataogopa adui zake inapofika majira ya msimu mpya (langoni) au anapohitahi mpenyo fulani au kuvuka ktk eneo fulani

Alhamisi, 1 Desemba 2022

Habari Picha za Mkutano Kitasha Rombo

Kulia ni Mchungaji Maziko wa Kanisa la PSMA Kitasha Rombo (Mch Mwenyeji) akishika na mkono na Mwl Oscar Samba ikiwa ni Ishara ya kumkaribisha ili shubiri.



Na Picha tatu zilizotangulia ni waudhuriaji wa mkutano huo
Pichani ni Mwl Oscar Samba akihubiri



 

Ndivyo Tulivyo Anza Jana #Kitasha hapa PSMA

Ujumbe unaitwa: KWA NINI SWALA LA UWOKOVU NI LA MUHIMU . Luka 19:10 Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.

Kama ukijua huu umuhimu, ni dhahiri utakubali kuokoka maana Yesu alikuja kutafuta wewe ambaye bado hujaokoka.

Na Yamkini haujaokoka, nawe umeguswa na ujumbe huu na unatamani kuokoka (kumbuka wokovu maana yake ni kumkataa Shetani na mateso yake, dhambi na taabu zake na kumkubali Yesu na Uzima ama mbingu)...
Kama ndivyo basi nikutie moyo kufuatisha Sala hii ya Toba kwa imani, Sema; EWE MUNGU BABA, MIMI NI MWENYE DHAMBI, NIMEGUNDUA MAKOSA YANGU, NISAMEHE YESU, FUTA MAJINA YANGU KWENYE KITABU CHA HUKUMU, NIANDIKE KWENYE KITABU CHA UZIMA WA MILELE, Amen.
Hongera kwa Kuokoka na tafadhali tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo, Ameni.
... Zaidi tembelea
www.ukombozigospel.blogspot.com
Tazama na Sikiliza Mahubiri na Mafundisho Yetu hapa, Usisahau Ku-Subcribe ili uyapate kwa haraka zaidi; https://www.youtube.com/@ukombozigospeltv

Jiunge nasi pia kwenye WhatsApp group letu la mafundisho ya neno la hapa: https://chat.whatsapp.com/E0eD0xegh1eIGMjRykPyRD

Kundi letu la Telegram https://t.me/+fft3GHXC9xIzYjhk (Hapa utapata Mahubiri/Mafundisho Yetu kwa Haraka)

Namba ya Telegram au Mawasiliano: +255759859287 inatumika pia kwenye WhatsApp na M-Pesa. Ukiguswa kuachilia Sadaka yako tafadhali usisite kufanya hivyo. Jina ni Oscar Samba.
Usisite Kututembelea pia kwenye Ukurasa (Page) wa Facebook na "Ku-like" https://www.facebook.com/MafundishoyanenolaMungunamwalimuoscarsamba?mibextid=ZbWKwL
Ama tuandikie email (Baruapepe) ukombozigospel.@gmail.com