Jumapili, 24 Aprili 2022

NI KWA NINI MUNGU ANAKUTAKA UMKABITHI NJIA ZAKO

Na Mwalimu Oscar Samba (Tafadhali #Share na kwa wengine ili nao Wanufaike)

Utangulizi wa kitabu chetu cha NI KWA NINI MUNGU ANAKUTAKA UMKABITHI NJIA ZAKO

Nilifanikiwa kuzungumza na mtu mmoja aliyeokoka ambaye Mungu amebariki kiuchumi, naye alinipa maneno magumu ambayo yalinifanya kufikiri sana. Aliniambia kuwa alisikia msukumo wa kunipigia simu na gafula akijikuta akiniuliza maswali kadhaa kuhusu mipango yangu ya kihuduma na kieleimu. 

Kisha alinipa maneno ambayo yalinifanya kufikiri sana na kuona hapa kuna kitu ambacho walimu wengi wa somo la maono hatukitendei haki. Aliniambi; Kuwa na maono sio kazi, Mungu anaweza kukupa maono, hata wewe unawea kutengeneza maono. Ila kazi na tatizo ni njia. Kuzijua njia za Mungu na kuzikubali hapo ndipo kazi ilipo.

Alisema watu wengi wana maono, ila tatizo ni njia za Mungu. Aliniambia kuwa njia za Mungu ni ngumu sana. Yusufu kutupwa kwenye shimo, ilikuwa ni njia ya kutimiza ndoto zake. Kuuzwa kwake na kuwekwa gerezani pia. 

Akaniuliza ni nani angezikubali hizo njia? Akaniambia tena kuwa unaweza kujiona unaenda mbele ila Mungu akakwambia rudi nyuma na ikawa ndio njia ambayo Mungu anaitaka.

Ananiambia haya wakati mimi nipo katika mapito magumu na mazito. Kikawaida ni mahali ambapo mtu huoni mbele wala nyuma. Ni sawa na kuwa kwenye kisiwa kile cha Patimo katika majira mbayo bado hujamuona Malaika wa Bwana ili akupe maono yale. Ukigeuka unasikia tu ngurumo za simba, ukijilaza nakutana na michirizi ya chatu, ukijikaza kufunga macho unahisi mitambao ya nyoka, ukigeuka tembo wapo kwenye misafara.

Nilimuelewa sana huyu maana mimi binafsi huwa ninamuheshimu sana mtu aliyeokoka ambaye ndani yake kafanikiwa kiuchumi kihali yaani kwa kumtegemea Mungu na hadi wakati huo bado moto wa wokovu ndani yake haujazimika. Huyu ninamuheshimu sana. Kwanza kufika hapo; lazima kuna mahali kapitia: pili wengi tunawaombea ila wakichanua tu kijinga kinazimika. 

Mtu kama huyu huwa na kanuni. Aliniambi kuwa mtu kuwa na maono sio kazi, wengi wana maono. Ila tatizo njia za Mungu. Akaniambi unajua ni kwa nini maandiko hukutaka umepea Bwana moyo wako ili macho yako yapendezwe na njia zake! Mithali 23:26 Mwanangu, nipe moyo wako; Macho yako yapendezwe na njia zangu.

 Alinipeleka kwa Musa kwenye Kutoka ile 33:13. Ambapo Musa namwambia Mungu ikiwa amepata kibali machoni pake, basi Mungu amuonyeshe njia zake ili nini? Ili apate kumjua kisha aweze kupata neema mbele za Mungu.

Nakuelezaukweli unayesoma kitabu hiki kuwa wengi tunataka kupata neema mbele za Mungu ila hatutaki kujua njia zake kwanza. Hili ni kosa kubwa sana ambalo hulifanya. 

Ndiposa nimeonelea ni vyema kukuletea kitabu hiki ili tuweze kunufaika vilivyyo na jambo hili. Tujifunze kumtumaini Mungu, na kumkabithi njia/kazi zetu ili mawazo yetu yaweze kuthibitika. 

Kitabu kikitoka kitafute tafadhali...

Kama hujaokoka nikutie moyo kufanya hivyo tafadhali. Maana maisha ya dhambi hayampendezi Mungu. Wanaokufa kwenye dhambi mshahara wao ni moto, ila wanaokufa katika neema ya wokovu ni kuishi na Mungu milele. Tafadhali usiseme leo sijajiandaa, ama kesho, au kesho kuta, siku nyingine sio jibu sahihi. Hujui siku wala saa ya kuondoka kwako hapa ulimwenguni. Wapo wanaokufa kwa kugongwa na gari, kuugua ghafula na hata kufia usingizini. Alilala vizuri ila ndo hakuamka tena, alipoaga usiku mwema, kumbe alimaanisha usiku mwingine! Nani ajuaye wako! Huna hakikisho la kuishi milele na hujui siku wala saa, huwa inakuja ghafula.

Sasa fuatisha kwa imani Sala hii ya Toba pamoja nami: Sema, MUNGU BABA, NINAKUJA MBELE ZAKO, NIMETAMBUA KUWA MIMI NI MWENYE DHAMBI, NISAMEHE, NIOSHE, NITAKASE KWA ILE DAMU YAKO, FUTA JINA LANGU KWENYE KITABU CHA HUKUMU, LIANDIKE SASA KWENYE KITABU CHA UZIMA WA MILELE; Amen.

Hongera kwa kuokoka, na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo. 

Kwa maombezi, Maswali, Ushauri na hata Sadaka yako kwa Mpesa, Usisite kuwasilaina nasi. 

Mawasiliano; Simu au WhatApp: +255759859287 Baruapepe: ukombozigospel@gmail.com au tembelea pia YouTube Channel yetu ya Ukombozi Gospel au Ug Tv , www.ukombozigospel.blogspot.com Asante.

Jumapili, 17 Aprili 2022

FAIDA ZA USHINDI WA MATESO NA KIFO CHA YESU KATIKA SURA YA PITO LAKO

 Na Mwalimu Oscar Samba (Tafadhali #Share na kwa wengine ili nao Wanufaike)

Sehemu nyingine (3) ya Kitabu chetu cha MUONE MUNGU NYUMA YA PITO AU JARIBU LAKO. Ni katika mada yetu ya kwanza ya ; 1. Jinsi Mungu Anavyoweza Kuwa Nyuma ya Jambo Gumu Linalokusonga. Na katika pwenti ya mwisho ya mada hii: 

. Mfano wa Mateso ya Yesu na Msalabani: Nawiwa kukuhitimishia mada hii kwa mfano wa Yesu katika mauti ya msalaba. Leo sisi tunaweza kulielewa jambo hili maana faida zake kwetu zi dhairi ila kwa wanafunzi wake na jamii ile halikuwa jambo jepesi. Ndio mana ukisoma kisa kile katika Luka 24 cha wananchi wale waliokuwa wakielekea Emau utaelewa kiupana sana. Kuna mitazamo walikuwa nayo kuhusu ujio wa Yesu. Walimtazama kama mfalme na mkombozi wa dunia ile au kwa Wayahudi kwa jinsi ya kisiasa na kibinadamu.

Maana taifa hili lilikuwa chini ya utawala wa dola ya Kirumi. Kipindi cha nyuma walipokuwa chini ya tawala kama hizo kuna namna kuliibuka watu maalumu waliowakomboa; mfano walipokuwa chini ya Wafilisti Mungu alimuinua Samsoni na kuwakomboa: Waamuzi 13 na kuendelea. Walipokuwa chini wa Wamidiani waliibuka Gideoni na kuwatoa utumwani kwa mkono wa Bwana; soma Waamuzi sita utajionea pale.

Alhamisi, 14 Aprili 2022

FAIDA ZA KUSHINDA JARIBU AU PITO ( Majaribu ni Mtaji)

 Na Mwalimu Oscar Samba (Tafadhali #Share na kwa wengine ilia nao Wanufaikae)

Sehemu nyingine ya Kitabu chetu cha MUONE MUNGU NYUMA YA PITO AU JARIBU LAKO. Ni katika mada yetu ya kwanza ya ; 1. Jinsi Mungu Anavyoweza Kuwa Nyuma ya Jambo Gumu Linalokusonga. Na pwenti ya kwanza pia ya mada hiyo: 

 1. Mfano wa Shadraka, na Meshaki, na Abednego. Napenda sana sentensi yao hii muhimu katika pito, na kwa wale wasomaji wa kitabu cha CHAKUFANYA UNAPOKUWA NJIA PANDA; wanaweza kunielewa kwa upana. Vijana hawa walimnenea mfalme kuwa hata kama Mungu hatawaokoka bado hawawezi kumuacha.

Kwamba kuwaokoa ni jambo jema, na ndilo wanalolisubiria, la hata asipofanya hivyo bado hawawezi kumuacha. Wasomaji wa kitabu cha Waebrania hususani ile sura ya 11 wanaweza kuelewa kuwa kuna aina mbili ya imani tajwa pale. Ya kwanza ni ile iliyoleta wokovu na ya pili ni ile iliyowawezesha kufa katika Bwana yaani bila wokovu kwa jinsi ya mwilini. Hawa nao ni mashujaa japo hawakuokoka katika mateso bali waliyafia mateso;

35….Lakini wengine waliumizwa vibaya hata kuuawa, wasikubali ukombozi, ili wapate ufufuo ulio bora; 36 wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa mafungo, na kwa kutiwa gerezani; 

Jumanne, 12 Aprili 2022

JIFUNZE KUMUONA MUNGU NYUMA YA PITO AU JARIBU LAKO

 Ujumbe huu ni Utangulizi wa kitabu chetu cha MUONE MUNGU NYUMA YA PITO AU JARIBU LAKO

Na Mwalimu Oscar Samba (#Share ujumbe huu kwa Wengine ili Tuvuke pamoja nao)

Kimwili tunaweza kuwaona adui zako kuwa ndio waliokusukumiza kwenye hilo shimo, ndugu zako, wapendwa na hata mchungaji wako. Kumbe Mungu yupo nyuma ya tatizo hilo ili akufanye kuwa waziri mkuu kwenye nchi ya Misri.

Unaweza ukawa na kila sababu za kuwalaumu viongozi waliokuwa wakimzunguka mfalme Nebukadreza ama Dario kwa kutengeneza sheria batili na kisha kumfanya mfalme kukutupa kwenye tundu la simba ama lile tanuru la moto! Kumbe nyuma yake Yesu yupo ili ajitukuze kwa mfalme, dunia yote na kisha kukuokoa ukiwa mshindi na mwenye kuinuliwa kicheo.

Jifunze kumuona Yesu kwenye kila nyuma ya pito au tatizo, ama nyakati ngumu unazokuwa unazipitia. Hii itakupa kunufaika vilivyo na nyakati hizo. Kuna tatizo limenikuta kipindi hiki; limetumika sana kunisukumia kwenye kusudi lake.

Jumanne, 5 Aprili 2022

Elewa ni Kwa nini Ndoa ni Zaidi ya Ulendo

 #VIJANA_NISIKILIZENI_Haya_Nayo_Ni_Maneno_ya_Mwenye_Hekima


Moyo Unaweza Kumpenda Mtu Bila Kuwa na Sababu Yoyote ya Msingi ila Usikubali Kuoana na Mtu Asiyetosheleza Vigezo Vya Ndoa kwa Viwango Fulani.

Moyo wa mwanadamu kuna muda unavutiwa na mtu bila hata kukupa sababu zenye mashiko kwanini umempenda. Utamsikia mtu akisema basi nimepanda tu! Ni kweli ni jambo jema, na hatuwezi kuweka sababu kwa kila mtu au maamuzi ya moyo kupenda.

Ndiposa wengine wakasema mapenzi ni upofu, ikiwa na maana kwamba kuna mambo ya msingi mtu anaweza  kuya_overloock ama kuyapuuza ifikapo swala la kupenda. Hapa napo sina shinda napo.