Jumatano, 29 Septemba 2021

KWETU NI MBINGUNI



Waebrania 13:14 Maana hapa hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao.

Sijui wewe! Ila nijualo ni kwamba Sisi Tuliokoka, ama Tuliomuamini Bwana Yesu kwetu ni Mbinguni hapa Duniani sio kwetu!

Ni sawa na kituo cha Mabasi cha Ubungo ama kile cha Mbezi, ni sawa na stendi ya Daladala au Matatu! 

Hapa Duniani ni sawa na Njiani..mimi sijafika wala wewe hujafika, bali tunapaswa kukaza mwendo, huku tukiwa na taraja ama shabaha yetu ikiwa ni kuvikwa taji ama kupata Thawabu ile isiyoharibuka..

Kwa hiyo huna haja ya kujitaabisha na mateso na shida ama manyanyaso ya dunia hii..

Jumanne, 28 Septemba 2021

Mtazame Yesu Sio Wimbi

 

MTAZAME YESU NA SIO WIMBI

Mathayo 14:29 Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu.

30 Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe.

Sijui umekwamia wapi..? Nina chojua ni kwamba ulianza au ulipokea wazo hilo la biashara katika imani kubwa, na moyoni mwako ulisema huyu ni Mungu ndie aliyenipatia wazo hili, kazi hii, mke au mume huyu..ila mara baada ya kuanza kumeanza kuinuka vikwazo naq ghafula ukajikuta unaanza kukata tamaa kiasi cha kuyumbisha imani yako sio katika hilo jambo tu bali hata kwa Mungu kama kweli ulimsikia sawasawa ama kama kweli bado yu pamoja nawe..


Alhamisi, 16 Septemba 2021

KARAMA YA KUONYA

Bwana Yesu asifiwe ndugu yangu katika Bwana. Hapana shaka u mzima tena buheri wa afya? Kama sivyo basi Bwana Yesu akupe amani na furaha tele, huku ukimtwika Yeye yale yaliyokulemea na iruhusu furaha yake itawale maisha yako.

Leo Bwana amenipaka mafuta kukuletea ujumbe huu muhimu sana. Sio mara kwa mara utasikia ukifundishwa japo ni kitu ambacho hutakiwa kukifanya kila sehemu. Mashuleni kuna maonyo, kazini, njiani, kwenye vyombo vyetu vya usafiri utasikia nako wakionyana, kwenye makusanyiko mbalimbali hili nalo lipo. Nyumbani na hata makanisani twapaswa kuonyana.

Nawiwa kukueleza kwa upana wake namna ambavyo tunapaswa kuonyana, na jinsi ambavyo karama hii hutakiwa kuwa na vitu muhimu ambatanishi aidha iwe tabia au roho fulani au karama saidizi kwayo. Haijalishi ni karama zinazojitegemea ila hapa zinapaswa kuambatana na hii, alikadhalika tabia ama tunda la Roho.

MSINGI WA KARAMA KIUJUMLA

1 Wakorintho kinaeleza kiupana kuhusu aina 9 za karama, na mbele yake kuna huduma tano zinatajwa. Lengo la karama na huduma ni kujenga mwili wa Kristo kama Waefeso inavyotanabaisha;