Na Mwl Oscar Samba,
Lengo: Kukujengea Kiu ya
KuhakikihaMiujiza na Ishara na Matendo ya Mungu ya Ajabu Yanatendeka kwenye
Huduma yajo kama Ilivyokuwa Kipindi ca Baba, na Mababu Zetu Kiimani.
Utangulizi
Mungu wa ma
Mtendo ya Mitume ndie Mungu wetu! Wala hajawahi kubadilika, na jambo hili halitarajiwi
wala kutazamiwa kuwa ipo siku itakuwa vivi, maana imenenwa hivi; Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na
hata milele. Waebrania 13:8.
Ile ishara za Mungu hazijawa halisi kwako haina maana kwamba Mungu amebadilika, kaishiwa nguvu, ama amebadili utendaji na hata kufikiri kwamba ilikuwa ni kwa kipindi kile tu na kwa sasa haiwezekani, au inaonekana kwama Mungu hajaamua kufanya au kutenda kama hapo kale pia ni makosa tena mazito!
Ni kwambie ukweli ni kwamba tatizo lipo kwetu! Yeye ni Yeye Yule,
jana leo hata milele, habadiliki, fahamu sana kuwa kama mvua ina nyesha na wewe
hujaloana usijaribu kugombana na mvua, ila utupe mwamvuli uliojifunikia, toka
chini ya paa la nyumba linalokuzuilia, na kama upo chini ya mti wewe toka hapo
maana unyeshewaji wako utakuwa tofauti n ambaye hajafunikwa na matawi au majani
ya mti!
Wala usijaribu kufikiri kugombana na mti, au kung’o mti, ama
kuezua paa la nyumba, ila wewe tafuta mlango ulipo na utoke! Usigombane na dini
yako, wala dhehebu lako au Mchungaji wako ambaye haamini katika Roho Mtakatifu,
dini au dehebu ama huduma ambayo inasema kwamba Roho alikujaga na hataka aje
tena, ama waliojazwa na kutumiwa na Roho ni wale tu wa kansia la kwanza, ama
wale wasemao kuwa utendaji wa Mungu wa kipindi kile sio kama wa leo! Hao usifanye
nao vita, bali wewe jitenge kati yao na utafute kundi sahihi kwako, huu sio wa
kati wa kukumbatia dini na kuacahana na wingu la utendaji wa kazi za Mungu.
Ninakwambia hivi kwa maana kwamba kitabu hiki hakijaja kwa
bahati mbaya, na japo na hakijaja ili kukutenga na dini yako, ila kimekuja ili
kukusaidia kufuatana na wingu hili, Kifu
Barthomayo, na yule wa Yohana 9, wote hawa walikuwa na dini zao, alikuwa dini
ya Mafarisayo na yamkni pia Masaduayo, ila alipo au walipomuona Yesu anapita moja
kwa moja walipaza sauti zao! Walitambua kuwa kuna wingu linapita ambalo lina
mujiza wangu hawakukubali kamba ya dini iwazuilie, waliruka ukuta wa dini! Ninaamini
hata mlangoni hawakutokea, yaani hawakwenda kuaga ka wakuu wao wa dini bali
walichomoka! Unaju ukitaka kuwa huru, hutatafuta pa kutokea, maana ukigundua au
hata hapa dirishani ninaweza kuchomaka, basi utachomoka! Maana hata Daudi aipokuwa
akiwindwa na Sauli, mkewe Mika, alimtolea au alimuwezesha kutoroka kwa kuptia
dirisha!
Yule wa Yohaa 9, Mafarisayo walinuka kweli kweli ili kupinga
jambo hilo, ila hakukubali kukwamishwa nao, ndio maana alidiriki kufika mahali
na kusema kuwa mimi sijui kama ni mwenye dhambi yaani Yesu, ila ninachojua ni kwamba
nilikuwa sioni na sasa ninaona, ni kwa nini ninakujuza haya? Jambo la kutaka
kuziona ishara za Mungu zinakuwa dhairi kwako ni vita! Na kama ni vita inakupasa
ujue namna ya kukubaliana navyo, na uwe tayari! Dini isikuzuilie kumjua Mungu zaidi!
Hata wakina Petro na wengine walikuwa na dini zao, ila walihakikisha
wanalifuatilia au wanafuta wingu sahihi!
Kwani Yesu alimwambiaje Nathanaeli! Nathanaeli akamjibu, Rabi, wewe u Mwana
wa Mungu, ndiwe Mfalme wa Israeli. Yesu akajibu, akamwambia, Kwa sababu
nilikuambia, Nilikuona chini ya mtini, waamini? Utaona mambo makubwa kuliko
haya. Ni Yhana 1:49-50.
Unaonaje kama angegoma kumfuata au angezembea, ama angeendelea
kusema kama wengine wanavyosema leo kuwa nina dini yangu, hata huku kwetu
tunamuamini Mungu! Hakika ambayo alikuja kuyashuhudia isingaliwezekana kwake!
Kumbe kuna vitu ambavyo huweza kutuzuilia kutenda ishara na
miujiza! Ni kweli kabisa Mwalimu Oscar, natumai kuwa hilo ndilo jibu lako!
Unajua Paulo Mtume angeweza kuendelea kusema kuwa Yesu wewe unajua
kuwa mimi nina dini yangu, na kuongezea kuwa hii dini ndiyo ile tuliyoachiwa na
Musa, sisi ni watu wa Torati, kwa hiyo hata huku ninaweza kumtumikia Mungu, na
kadhalika! Uwe na hakika yale aliyoyatend asingeweza kuyateda kabisa!
Wala mimi sina
lengo au nia ya kukutoa humo kwenye dini au kusanyiko lako kama nilivyokujuza hapo
awali, ila nataka kukufikirisha kiupana zaidi kama dini, au kusanyiko lako ni
kizuizi cha Mungu kutembea na wewe uwe na hakika kuwa ile kiu, na shahuku iliyo
ndani yako haiwezi kamwe kutimia, Gideoni alikuwa na maswali kama yako, kuwa yupo
wapi Mungu wa Baba zao, Yule ambaye amesikia matendo yake, na yamkini alipita
kule ambako wana wa Reubeni, na Nusu ya Kabila ya Manase na wagadi walipoweka
alama, madhabahu ambayo ilikua na nia ya kuja kuonyesha watoto au wajukuu au vizazi
vijavyo kuwa yupo Mungu aliyewatoa utumwani na kuwafikisha hapo, kama Yoshua 22
isemavyo, lakini pia Yoshua aliweka alama ya mawe au nguzo ikiwa na maana kwamba
uzao ujao ukiyaona au kuona wajue kuwa yupo Mungu, na maswali hayo yalikuwa
magumu sana kwake! Lakini fahamus sana
kuwa, katika hali hiyo utendaji wa Mungu haukuwa umeisha nguvu zake!
Na kuna mambo huyu Gideoni litatikana
kuyatenda na alipoyatenda Mungu yule yule wa Baba zake ndipo alipokuja na
kujidhiirisha, na wewe kuna mambo muhimu unatatikana kuyatenda ili kunufaika na
utendaji wake kwenye huduma yako! Fahamu sana umuhimu wa kumfuata Yesu kama
Nathanaeli! Ukikwama hapa, hakika utakwama na kwenye miujiza na ishara,
haijalsihi dini yako inamtajaje Yesu, maana hata Torati ya Pauo ilimtaja, maana
Yesu alitabiriwa katika Torati, Zaburi na Manabii ila haikumuwezesha Paulo
kunufaia na alichobeba Yesu, na wewe maamuzi haya ni kwa ajili yako leo na
huduma yako!
Tafathali
kitabu kiitoka kitafut, pia tumeanza kuuza kwa njia ya
‘Soft
Copy’ bathi ya vitabu vyetu.
Hongera kwa
kusoma ujumbe huu, nakutia moyo kuzidi kumtazama Mungu, na pia uwenda
hujaokoka, yaani Yesu sio Bwana na mwokozi wa maisha yako! Nakutia moyo tena
kuokoka sasa! Yamkini ni uchumi, fedha, hazipatikani, unazingirwa na nuksi na
mikosi, kila unalofanya haliendi, unakabwa na mapepo, ! Wewe njoo kwa Yesu na
hayo yote yatapita kabisa ! Sasa natumi u
tayari!
Sema; MUNGU
BABA, NINAKUPENDA, ASANTE KWA KUNIPENDA KWANZA, LEO NIMETAMBUA KUWA MIMI NI MWENYE
DHAMBI, NA NIPO TAYARI KUOKOKA, TAFADHALI INGIA NDANI YANGU, SAMEHE DHAMBI
ZANGU, NA FUTA JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKU, NA ULIANDIKE SASA KATIKA
KITABU CHA UZIMA WA MILELE, Ameni.
Kwa kufanya
hiyo umekwisha kuokoka sasa, na tafadhali tafuta kanisa la watu waliokoka
lililopo karibu nawe ukasali, hapo, waambie kuwa umeokoa hivi karibuni, ili
wakulee vyema kiroho.
Mawasiliano
yetu, kwa M-Pesa au Simu: +255 759 859 287, barua pepe:
ukombozigospel@gmail.com
pia
temnbelea: www.ukombozigospel.blogspot.com
. AU www.mwalimuoscarvitabu.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni