Jumapili, 1 Novemba 2020

MATESO, MAPITO SIO ISHARA YA KUPUNGUA, KUFIFIA AU KUTOKUWEPO KWA PENDO LA KRITO PAMOJA NAWE.

Na Mwalimu Oscar Samba.

Ujumbe huu ni sehemu ya kitabu chetu cha MUNGU ANAKUPENDA, chenye mukutadha wa kukujulisha hata katika taabu yako pendo lake lingali lipo hapo!

Wiki hii, (wakati mada hii inaandikwa) nilimuliza Mwalimu anayetufundisha kitabu cha Matendo ya Mitume swali gumu sana, ambalo lilisadifu ujumbe huu ambao ninauleta mbele yako siku ya leo!

Nilimuliza ama nalitaka kujua kuwa kweli ni Mungu huyu huyu liyejifunua kwa Stefano wakati anapiga mawe! Stefano anasema anamuona mwana wa Adamu au wa Mungu katika mkono wa kuume, tena tunaambiwa alikuwa amejaa Roho, kwa hiyo utatu mtakatifu ulikwepo ukimtazama au uwepo wake ulikwepo pamoja naye!

 

Mungu Baba alionekana na Yesu pembeni yake, na Roho ndani yake! Lakini cha ajabu hawakumuokoa na kupigwa kwa mawe! Hawakuzuia mawe yasirushwe, wala Roho hakumtetea kama alivyojifunua kwa Yesu wakati wakubatiza kwake wakionekana akishuka kutoka juu mbinguni na kila mwenye mwili kumuona, huku Mungu Baba akimtetea kwa sauti kusikika kutoka juu ikiwataka wamtii kwa kumsikilia Yeye.

 

Kwa Meshaki, Shedraki na Abrinego, aliposhuka kama mtu wa nne kwenye moto tulimuona akiwatetea na kuwapigania, kwa Daniel alipokua kwenye tanuru la simba wale wakali alionekana akimzulia na kifo!

 

Ila kwa Stefano tunamuona akiwepo tna katika Utatu Mtakatifu na bado Stefano anapigwa hadi kufa! Hoja yangu ililenga kujua kama kweli ndie Yesu au Mungu huyu huyu!

 

Unajua kama hujapitia hapa huwezi kuelewa! Huwa najiuliza sana ninapotazama maisha ya wenzangu hapa chuoni! Ni Mungu yule yule aliyetuita wote kwa pamoja ila kuna ambao wanakosa hata sabuni, kuna ambao ada kwao ni shida, kuna ambao wasipokula chakula cha chuo hawawezi kubadilisha hata tunda kwenye genge au hata kununua andazi jirani.

 

Na aliyewaita ni mmoja, aliyewaleta hapa ni mmoja! Lakini maisha yapo tofauti sana! Ni rahisi kuwa na jibu la kwamba kila jambo lina wakati wake, ila kuna jibu zaidi ya hili, japo na hilo ni muhimu sana kulijua!

 

Kwenye huduma wengine wana mpenyo wa haraka, ila wengine hata kwa ugumu hawauoni, Yesu alikaa mjini akila na kunywa, ila Yohana mbatizaji alikaa nyikani, mavazi yake ni ngozi, wala hakuwa na mavazi mororo kama Yesu alivyokuwa akidhibitisha, alipowahoji kilichowapeleka nyikani, Yohana alikula nzige na asali, Yesu na wakina Petro walikula mikate na divai!

 

Nilijikuta nalazimika kusimulia hata mapito ambayo nimewahi kuyapitia kiutumishi, ambapo wasomaji wa kitabu chetu cha USIFEI JANGWANI, wanafahamu katika utangulizi kuwa nimelingamua hilo, kuna wakati ilikuwa nikimuomba Mungu fedha ya huduma ninapata, nikiomba kwa ajili ya mkutano inapatika, ila ya chakula haiji, ya mahitaji yangu haiji, na maisha yalikuwa magumu sana, hadi kufikia kuhisi kufa njaa, nilijiuliza sana ni kwa nini!

 

Turudi kwa Stefano! Anapigwa mawe, anapata maumivu makubwa, na Yesu anamtokea ila hamuokoi na maumivu ya mawe, badala yake anaitwaa Roho yake! Najiuliza sana; nalimuiliza Mwalimu na wenzangu kuchangia mada darasani ni Mungu huyu huyu ambaye anajidhirisha kwake na kuacha kumuokoa na mateso au maumivu yakel!

 

Tunaweza kutarajia kuona kuwa Mungu akiwakemea, na kutuma malaika wake na kuwaadhibu na kuachilia onyo kali kama ilivyo kwetu tunapopitia katika mambo magumu tukifikia hata hatua ya kuwamabia watu na kuwatisha kuwa hawamjui Mungu tunayemtumikia na ngoja wataona watakavyopigwa na Bwana, na haiji kutokea, badala yake anatwa roho au napokea roho yako kama kwa Stefano, ama wengine wanatarajia kuokolewa kutoka taabuni bana badala yake shida ndo kwanza inaongezeka, na kwa bahati mbaya sana tukifika hapo humuona Mungu ametuacha, na hatujui kuwa kiroho Mwana wa Mungu ameketi mkono wa kuume, na Baba yu pamoja naye, huku tukiwa Tumejaa Roho!

 

Katika mada hii na kitabu hiki cha MUNGU ANAKUPENDA, ni kukutaka kufahamu kwamba haijalishi unapitia wapi, unapitia nini, unaona nini mbele yako, unahisi na kuamini nini kwa wakati huu, ila juwa ana fahamu sana jambo moja kwamba Mungu anakupenda! Na upendo wake haupimwi kwa hali inayojidhiirisha kwa nje na kwa ndani, ila fahamu hata katika hilo anakupenda!

 

Alafu kupita sio kupoa kiroho Stefano alikuwa akihubiri, tena injili nzito sana, na alikumbwa na mapito na mateso, na Mungu hakuwa amemuacha ndiposa akayapitia hayo, maana ile huduma ikiwa ngumu, hakuna mpenyo na ni vita kila mahali, jibu rahisi sana ni kuona Mungu amekuacha, hivyo sio sahihi, hayo ni makosa tena makubwa mnoo, Muone Stefano! Tunasoma kutoka katika Matendo ya Mitume 7:54-60. Tuone;

….. Basi waliposikia maneno haya, wakachomwa mioyo, wakamsagia meno. Lakini yeye akijaa Roho Mtakatifu, akakaza macho yake, akitazama mbinguni, akauona utukufu wa Mungu, na Yesu akisimama upande wa mkono wa kuume wa Mungu.

 Akasema, Tazama! Naona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adamu amesimama mkono wa kuume wa Mungu. Wakapiga kelele kwa sauti kuu, wakaziba masikio yao, wakamrukia kwa nia moja, wakamtoa nje ya mji, wakampiga kwa mawe. Nao mashahidi wakaweka nguo zao miguuni pa kijana mmoja aliyeitwa Sauli. Wakampiga kwa mawe Stefano, naye akiomba, akisema, Bwana Yesu, pokea roho yangu.  Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu, Bwana, usiwahesabie dhambi hii. Akiisha kusema haya akalala. Na Sauli alikuwa akiona vema kwa kuuawa kwake.

 

 

Kuna kanuni moja muhimu hapa, katika wazo hili kuu ya kwamba mateso au kuwa katika dhiki, sio ishara wala dalili ya kwamba Mungu amekuacha, akupendi au umepoa ama kurudi nyuma kiroho, na ni makosa pia kuwaza kwa haraka kuwa huenda unaadhibiwa na Mungu, Zaburi husema kuwa aliwaza kwa haraka,,, na kwake ikahesabiwa kuwa ni kosa au dhambi, kanuni hiyo ni hii:

Stefano katika hali yote hiyo, hakuacha kumtazama Bwana, (..akitazama mbinguni, akauona utukufu wa Mungu.)

 

 

Alitazama mbinguni, na wewe nikutie moyo kutazama mbinguni! Ila si mateso, taabu, wala usitafakari matatizo, mtakafakari Mungu, aliyemwanzilishi wa safari yetu, na mkamilishaji, na wewe kupitia hapo sio adhabu, mwenzako Stefano alipitia hapo na bado yalikuwa ni mapenzi ya Mungu, kuna mahali humu kitabuni nimekwambia kuwa unafundishwa kuogolea ndio maana napitishwa kwenye maji!

 

 

Kuna kanuni nyingine ambayo siyo nyepesi, na unatakiwa kuielewa kwa upana kidogo! Anaomba akisema, “naye akiomba, akisema, Bwana Yesu, pokea roho yangu,” alitabua kuwa kitu ambacho Mungu anatafuta au kusudio la Mungu kuruhusu jambo lile, ama mlango wa kutoka katika pito lile na jaribu lile ni kumuona Baba, kwa hiyo aliomba akimtaka Mungu apokee roho yake, sina maana kwamba na wewe uombe hivyo, la! Ila tambua kwa nini unapitia hapo!

 

 

Miongoni mwa majibu ya mchango kuoka kwa wenzangu darsani yaliyopigwa muhuri na mwalimu ilikuwa ni kuhusu jambo kama hili!

 

 

Mramba alishuhudia akisema kuwa katika kipindi hicho kulikuwa na mchungaji mmoja ambaye alikuwa na maisa ya shida sana, ndoa yake iikuwa hatarini kuvunjika kutokana na ugumu wa maisha, watu walimkimbia alikosa hata mdhamini wa ndoa maana walimuita maskini na kumtenga, ila sasa ana maisha mazuri na Mungu amemwinua, anasema alipitishwa ili ajue kuwasaidia wahitaji, ikitajwa shida ajue shida huwa inafananaje!

 

 

Katika kitabu chetu cha NAMNA YA KUISHI WAKATI WA MAJARIBU AU MAPITO, swala hili limefafanuliwa kidogo, ni muhimu kujua ni kwa nini Mungu hajakuokoa na jaribu ilo kama ilivyokuwa kwa Meshaki, Shedraki na Aberinego! Ama Danieli!

Mungu aliyeruhusu Yohana Mbatiaji akatwe kichwa, tena ambaye maandiko humuita nabii muhimu au mkuu, maana katika waliozaliwa na mwanamke hakuna mfano wake, Mungu aliyeruhusu mashujaa wake kupigwa kwa mawe na kuwa, na wengine kukatwa kwa misemeno kama Waebrania 11 isemavyo, uwe na hakika ndie yule yule aliyemtoa Yeremia kwenye shimo kama gereza japo kuwa wenzake wa kipindi hicho aliuawa!

 

 

Epuka sana fikra kama za yule aliyekuwa akimsulubisha Yesu na kumwambia kuwa aliokoa wengine ila hakuweza kujiokoa mwenyewe!

 

 

Nani amekwambia kuwa ili awe Mungu ni lazima akutowe kwenye hilo jaribu! Nani aliyekwambia ili awe Mungu na iwe anakupenda ni lazima ajibu maombi yako!

Uwe makini usije ukawa kama yule mtumishi wa zamani zile aliyefufua wafu wengi sana, na kuweka historia katika hilo jambo, ila mke wake alipokufa na kumuombea na kuona haponi aliamua kwenda baa na kunywa pombe, kisha mlevi akammrushia chupa  ikampata na kumua!

 

 

Kuna  mtumishi mmoja aliyekuwa akifanya mkutano wa injili mahali, na siku hiyo kulikuwa na dalili ya mvua, nawe wajua kuwa mkutano wa nje mvua ni kipingamizi kikubwa sana, alimsihi Mungu sana kuwa mvua isinyeshe, ila haikuwa hiyo, alifika mbali zaidi na kumwambia Mungu kuwa kama mvua itanyesha basi ataenda baa iliyopo jirani na mkutano na kunywa pombo hapo! Haya ni baada ya kuona maombi ni magumu kujibiwa kama yalivyokuwa.

 

 

Punde si punde mvua ilinyesha, naye kweli alienda baa na kuagiza bia, au pombe, akiwa kabla hajaifungua ingali mezani, alikuja mama mmoja na kumpigia magoti alimtaka amuongoze sala ya toba!

 

 

Mkutano haujafanyika ila kuna mtu anataka kuokoka! Natumai naye alishangaa maana kwanza anamfuata baa, anamfuata katika hali ambayo ilipaswa kumuona kama aliyeasi, akiifuata njia mbaya maana aliyenuia kuwaongoza katika wema ameonekana kuikana, mama huyu alimueleza muhubiri kuwa kinachomfanya kuokoka, ni hiki, alianza na neno au maneno kuwa una bahati sana, ama Mungu wake ni mkubwa!

 

Mungu anatukuzwa na mvua imenyesha na maombi ya muhubiri hayajajibiwa! Alimwambia kuwa pale uwanjani walikuwa wamechimbia dawa yao ya kichawi, na shariti lake halikupaswa kuloana na mvua, au maji, sasa mvua imenyesha dawa imeshaharibika!

 

 

Unaona kitu hapo! Ukitaka kujua kuwa mvua hii ni ya Mungu, ona hofu iliyokuwa ndani ya mchawi ambaye alikusudia jambo kinyume na Mungu! Hofu hiyo ilimsukuma kutubu, maana yake nafsi yake iliona adhabu kama hatatubu, iliona ukuu wa Mungu!

 

 

Stefano alikuwa ameshamaliza muda wake, hilo halina ubishi, wakati wa muona Baba ulishafika, ndio maana kwa Paulo hata walipodhania ameshakufa haikuwa hivyo! Kuna jambo zaidi ya unavyotazama wewe kwenye mambo ambayo yanaonekana kuwa ni magumu kwako!

 

 

Ukipata muda na ukifanikwia kupata shuhuda zangu za kimaisha ikwemo ndoa, uchumi, na kihuduma unaweza kupata funzo kubwa sana hapa!

 

 

Fahamu sana kuwa kupitia haimaanishi kuwa Mungu amekuacha, upendo umepungua, wala sio lazima akuokoe, au akuponye ndipo awe Mungu!

 

 

Upendo haujapungua kwako, maandiko yanasema kuwa Elisha nabii alikufa kwa ugonjwa wake! Unajua maana yake! Ni kwamba alikuwa na tatizo la afya la muda refu! Neema yangu ya kutosha, ndilo jibu alilopewa Paulo, sijui wewe ila mimi nina mwiba wangu ambao kwa kweli ni miaka na inakaribia miongo sasa, lakini najua kuwa kupitia huo ninapata nafasi ya kumkimbilia na kumlingana Bwana zaidi!

 

 

Kutokupona kwako, kujibiwa kwako haina maana kuwa upako umepungua, la! Tena ni hapana! Elisha hakupona, ila haina maana kuwa upako haukwepo! La ulikwepo! Vitaamba vya Paulo au vilivyotoka kwake viliponya watu! Kwa hiyo nguo zake zingetosha kuachilia upako katika hilo pito! Ila ihakuwa hivyo!

 

 

Uwe makini usije ukawa kama wale wa YESU, kuwa aliokoa wengine ila yeye hawezi kujiokoa! Wamesahau kuwa aliyekatwa sikio alirejeshewa, walipotaka kumkamata walianguka mara kadhaa! Yesu alikuwa na uwezo wa kuagiza majeshi ya mbinguni ili kumpigania ila hakufanya hivyo, maana aliyajua mapenzi ya Mungu pale!

 

 

Ninajaribu kuikifiri tu kama wewe na mimi uwezo huu ungekwepo mikononi mwetu hakika tungeagiza ili tu tumtete Mungu, tukifikiri kuwa kama tukiokoka katika mikono ya wanaotusulubisha ndipo Mungu tu atatuwazwa! Mtazamo ambao sio wa kibiblia kabsa, Maana utukufu uliojidhiirisha kwa Yesu baada ya kufa na kukufuka ulikuwa ni mkubwa zaidi hata kuliko kama angeokoka mikononi mwa wale watu! Kuna wakati mwingine kifo chako ni sehemu ya utukufu, wala sina maana kuwa utamani au utake kufa, nina maana pana zaidi ya hiyo!

 

 

Kumbuka kuwa Elisha aliyetumika kuponya na kuokoa wengi hautumika kujiponya mwenywe, na haikuwa ishara ya kuishiwa kiroho au Mungu kumuacha, kumbuka na jambo hili ni la ajabu sana lifahamu kwamba, Yule ambaye upako haukumponya aliokuwa nao, ulikuja kutumika kumfufua mtu! Tena mifupa yake, wala sio maiti, bali ni mifupa!

 

 

Ikiwa na maana kuwa hata nyama hazikwepo, huo mwili ulishaoza, hauna hata dalili ya kuwa huu ni mwii wa Elisha, ila upako haukuoza, ulisalia hapo, uka kumfufua aliyekufa, japo haukumfufua mwenye upako, na mifupa iliendelea kuoza, lakini limfufua mwingine!

 

 

Sijui naongea na nani, ila ninajua kuna mtumishi ambae anatumiwa sana na Mungu kuombea ndoa za wengine, nazo zinapokea uponyaji ila ndoa yake bado! Akibandika mikono matumbo ya wa mama wengine, wanapata uzao, ila kiukweli kwake bado, maana mkewe ni mgumba!

 

 

Akiombea wengine wanapona ila yeye ana ugonjwa ambao umechukua muda sasa!

Najua hutakufa kwa huo ugonjwa kama Elisha, ila ninachotaka kukwambia ni kwamba upendo wa Mungu kwako haujapungua, wala usijaribu kutafuta dambi uliyotenda, badala yake mshukuru Mungu, mpe sifa na utukufu, siku yako inakuja, wala usifikirie kuzira kumtumikia Mungu kwa kigezo kwamba wewe hujajibiwa! (Kuhani Zakaria alijibiwa alipokuwa akimtumikia Mungu! Malaika alimtokea akiwa katika utumishi!)

 

 

Maana mkataba wako na Mungu wa utumishi haujafungwa katika kipengele cha shariti kuwa ni lazima akutendee ndipo nawe umtumikie! Akikutendea ni vyema, ila fika mahali uiambie nafsi yako kuwa hata Mungu asipojibu bado Yeye ni Mungu! Ukiijua hii kanuni utafanikiwa sana!

 

 

Kuna mahali nilipita na hata sasa ningali nikipitia, na nilimwambia Mungu kuwa hata asipotenda, asipojibu, yeye bado ni Mungu, huu ni ujasiri kubwa sana kwa mtu anayetaka kudumsha uhusiano wake na Mungu! Akijibu, vyema, ila hata asipojibu mimi sitavunjika moyo!

 

 

Baba yangu kiroho Mwakasege aliwahi kusema katika msiba wa muimbaji Sedekia kuwa , Mungu ni Mungu hata kama hajajibu kama ulivoomba!

 

 

Hii ni matokeo ya wengine kuvunjika moyo sana, wakisema nilifunga na kuomba siku saba ila alikufa! Mungu ni Mungu hata kama mgonjwa hajapona! Hata kama ulifukuzwa kazi, umeachika! Hiyo haimbadilishi kuwa Mungu! Wala haijaondoa upendo wake kwako, yeye ni Mungu, na atabaki kuwa MUNGU!

 

 

Mungu ni Mungu hata kama Stefano amekufa! Mungu awi Mungu kwa kuwa aliwatoa wakina Meshaki na Aberinego na Daniel kwenye lile teso! La! Mungu ni Mungu hata kama hajakujibu hitaji lako!

 

Mungu ni Mungu hata kama hujaolewa, wala huoni dalili ya wewe kuolewa! Mungu ni Mungu hata kama huna mwana! Mungu ni Mungu hata kama mtoto wa Daudi amekufa Daudi akiwa katika maombi ya siku 40!

 

 

Maana wapo wanaodhani kuwa maombi ni njia ya kumlazimisha Mungu kujibu! Niliomba lakini Mungu hakusikia! Uwe makini mpendwa!

Alisikia maombi ya Stefano ipokee roho yangu; uwe na hakika kuwa Stefano angeomba Mungu tuma malaika wako hayo yasingejibiwa! Usibishe maana kama aliweza kumgomea Yesu pale bustanini hadi alipogeuza maombi ya kuwa sio kama atakavyo Yeye bali mapenzi yake Yeye yatimie, uwe na hakika na kwako huwa hajibugi!

 

 

Japo sina maana kuwa kutokujibwa kwako ni matokeo ya kutokuomba vyema! Ibrahimu alikuwa na hitaji sahihi, na aliomba vyema, lakini muda ulikuwa bado, na nje ya muda kuna funzo alikuwa akipotea, imani ilikuwa ni somo kubwa sana hapo!

 

 

Endelea kuomba, ila ukiambiwa neema yangu ya kutosha, usife moyo, na pia usijijengee fikra kuwa Mungu lazima ajibu ili ajitukuze! Fahamu kuwa hata kufa kwa Stefano kulimpa MUNGU utukufu, kufa kwa Yesu pia ndivyo!

 

 

Ukiijua hii siri hutakuwa na zile fikra za kusubiria Mungu akutendee mema ili adui zako wajue kuwa unaye Mungu! sipotenda je!

Kanuni ya kutendewa kwa Ayubu, na kurejeshewa haikutumika kwa Stefano, na kwa wengineo! Umakini ni muhimu sana hapa.

 

 

 Nikirejea swali langu pale awali; Ukweli ni kwamba, Mungu ni yule yule ambae mchungji huyu anamiliki gari, Helikopta, au Ndege ama Meli, lakini mwingine hata baskel hana, anafunga na kuomba Mungu ampe Pikipiki! Wala swala au jibu la muda huwa aliingia kila mahali, maana kuna wengine watakufa hawajamiliki hata hiyo baisikeli, na sio kwamba wamepungua viwango vya kiroho jibu ni la!

 

 

Maana usishangae mbinguni wanataji kubwa kuliko wa helikopta na ndege! Aliyemchagua Yuda ili kumpitishia Daudi ni huyu huyu ambaye hauoni sana makabila mengine yakitajwa kiundani kama ilivyokuwa kwa Walawi na Yuda na uzao wa Yusufu, ama Yusufu mwenyewe, kuwa mtumishi maarufu na mwenye vipawa haimfanyi kuwa Mungu mwenye upendeleo kwa ambae haonekani kama wewe!

Wala sio kwamba unaomba sana, kuna ambao ni waombaji kuliko wewe.

 

 

Twafahamu tu kuwa kuna washirika ambao ni waombaji kuliko wewe, au mchangaji wao, ila haina maana kuwa mtumishi ni mkuu sana, uwe na hakika kuwa ni neema tu! Na kupungukia kwa kitu fulani haimaaniishi kuwa Mungu amekuacha, au amekuchukia, au upendo wake kwake umefifia, ni La!

 

Lazaro alikufa maskini! Haina maana kuwa Mungu hakumpenda kam ilibvyokuwa kwa Ibrahimu ambae alikufa akiwa ni tajiri!

 

 

Mungu ni yeye yule leo, na hata mimilele! Ukifanikiwa kusoma, haina maana kuwa wewe ni bora kuliko ambao hawajafika hapo! Unakifamu kuwa hata darasani kuna ambao walikuzidi uwezo! Lakini ulichaguliwa wewe! Na wewe ambaye hujafanikiwa katika hili, na lile, haina maana kuwa MUNGU HAKUPENDI, LA! ANAYAJUA MAWAZO ANAYOKUWAZIA!

 

Usife moyo Mpendwa, Maana mipango yake sio mipango yako, na kadhalika macho yake hayawezi kuwa kama yako! La muhimu ni wewe kuamini tu! Na la kwanza ni kuamini kuwa Anakupenda, na anakuwazia yaliyo mema, Yeye ni Mungu wa haki na muokoaji, atakuoke na kukutoa katika hiyo hali punde! Nakusihi kuokoka kama bado hujaokoka mpendwa, ili uwepo wa mapenzi yako kwako yatimie vyema.

 

Hongera kwa kusoma ujumbe huu, nakutia moyo kuzidi kumtazama Mungu, na pia uwenda hujaokoka, yaani Yesu sio Bwana na mwokozi wa maisha yako! Nakutia moyo tena kuokoka sasa! Yamkini ni uchumi, fedha, hazipatikani, unazingirwa na nuksi na mikosi, kila unalofanya haliendi, unakabwa na mapepo, ! Wewe njoo kwa Yesu na hayo yote yatapita kabisa ! Sasa natumi u tayari!

 

Sema; MUNGU BABA, NINAKUPENDA, ASANTE KWA KUNIPENDA KWANZA, LEO NIMETAMBUA KUWA MIMI NI MWENYE DHAMBI, NA NIPO TAYARI KUOKOKA, TAFADHALI INGIA NDANI YANGU, SAMEHE DHAMBI ZANGU, NA FUTA JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKU, NA ULIANDIKE SASA KATIKA KITABU CHA UZIMA WA MILELE, Ameni.

 

Kwa kufanya hiyo umekwisha kuokoka sasa, na tafadhali tafuta kanisa la watu waliokoka lililopo karibu nawe ukasali, hapo, waambie kuwa umeokoa hivi karibuni, ili wakulee vyema kiroho.

 

Mawasiliano yetu, kwa M-Pesa au Simu: +255 759 859 287, barua pepe: ukombozigospel@gmail.com

pia temnbelea: www.ukombozigospel.blogspot.com . AU www.mwalimuoscarvitabu.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni