Ijumaa, 28 Agosti 2020

Utangulizi wa Kitabu chetu cha UTUMISHI NA MTUMISHI

Mwalimu Oscar Samba

Luka 10:20 Lakini, msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.
Ni kweli kabisa maandiko yanasema kuwa mtawatambua kwa matunda yao! Na mti mbaya au mwovu hauwezi kuzaa matunda mema, kwani tini huzaa tini wala zabibu haiwezi kuzaa michongoma, au kwa lugha nyingine huwezi kuchuma embe kwenye mti wa mchongoma au mchicha katika mbigili!
Lakini ukweli na uhalisia ni kwamba andiko hilo lina mukutadha wake na undani wake! Wengi wamekuwa wakiyatumia ili kuficha uhalisia wao bila kujua kuwa hawamdanganyi Mungu bali ni wanadamu wenzao, na hawa ni wale wasiojali sana hatima zao, yaani kwao maisha baada ya kufa sio kipaumbele chao kikuuu!
Kitabu hiki mpendwa kimebeba nia na kusudi la kuwasaidia watumishi, ili wasije kubweteka na utumishi walio nao, au wakifikiria kuwa utumishi ni tiketi au kibali cha kuwapeleka mbinguni, ni vyema kufahamu kuwa pasipo huo utakatifu haiwezekani kumuona Mungu!
Utumishi na Mtumishi maana yake ni kwamba hakuna uhusiano kati ya utumishi ulionao na wewe kumuona Mungu! Kuingia mbinguni kigezo kikubwa ni utakatifu au wokovu na sio jinsi gani unatumiwa na Mungu! Na kitabu hiki pia kitawasaidia wale watu ambao wanateseka na kuumia na kujiuliza maswali yasiyo na majibu kuwa inakuaje mtu anatumiwa na Mungu kwa ishara na miujuza, au kwa neno ambalo linawasaidia wengine na wengi kuokoka ama kufunguliwa lakini maisha yake mwenyewe binafsi ni machafu!
Sikatai kuwa kuna mapungufu, ambayo mtu huzidi kukamilishwa, au kuna kuanguka au kukosea kama Daudi alipolala na mke wa mtu, na kumua mumewe, au jinsi Musa na Haruni walivyokorofishana na Mungu, ama mapungufu kadha wa kadha ambayo pia tunayona kwa Petro!
Hapa ninanena habari za watu walioharibika mioyo kabisa, au ambao wapo katika kuharibika lakini kwa kuwa Mungu anajithiirisha kwao au kwa kuwa bado wamejaa Roho basi wanabweteka na hali hiyo, na kudhania kuwa Mungu hachukizwi na kosa au mwenendo wao!
Kuna muda utakatifu unaenda pamoja na utumishi! Ila kuna muda utumishi au mapenzi (kusudi maalumu) ya Mungu hutimizwa hata na chombo ambacho sio kisafi! Tutajionea kwa Balaamu, mtu mchawi aliyetumiwa kiunabii na kukamilisha makusudi ya Mungu, ila alikuwa mchawi na utumishi haukubadili maisha yake, lakini pia tutajionea kwa watu kama yule mganga wa kienyeji alivyo mpandisha Samweli nabii kutoka Ahera au kifuani mwa Ibrahimu, (Paradiso) lakini alikuwa ni mpunga pepe!
Nakutaka sana kuhakikisha kama kweli unataka kwenda mbingunbi basi unjitahidi kuulinda utakatifu! Na hii ilikuwa ni shabaha kubwa sana ya Paulo mtume, kuwa alilinda asije akawa wa kuwahubiria wengine na kisha yeye kuachwa! Nawe uwe makini, pepo kutoka sio kigezo cha wewe kuiona mbingu!
Ndio maaana furaha ya wanafunzi wa Yesu kuhusu ishara na ambao yaliyotokea haikuwa kipimo au kigezo chawao kuiona mbingu, bali furaha yao iliyopaswa kupimwa ni kwa kuwa majina yao yameandikwa mbinguni! Kuupata ulimwengu wote, kujaaa karama na kutenda miujiza hakuna faida kwako kama utapata hasara ya nafsi yako! Mathayo 16: Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? 27 Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
Kilio chako kikubwa, na haja yako kubwa isiwe ni huduma yenye miujiza, ishara na umaarufu wa kiutumishi, bali utakatifu kwanza! Tafuta kumpendezesha Mungu kwanza!
Nayanena haya maana tumekuwa na watumishi ambao wapo tayari hata kutumia ushirikina ili tu wahakikishe wanapata nafasi fulani kwenye dini au dhehebu lake! Wapo ambao hutumia rushwa, na hata kampeni chafu ili tu kupata vyeo, wapo ambao hutumia hila wakifanya miujiza bandia ili tu wapate umaarufu na kadhalika!
Utakatifu kwanza, kisha vingine baadae! Tumekuwa na watumishi ambao hukandamiza vipawa au huduma za wengine kwa hofu ya kupinduliwa kiutumishi, na hata kuwatengenezea tuhuma au hila mabaya ili tu kuwachafua wengine kwa nia ya kulinda mkate!
Wapo ambao huhakikisha wanawaaribia wengine kwa lengo la kuchua nafasi walizo nazo! Wengine hutimia vibaya mahusioano yao na waangalizi, maaskofu au watu wenye dhamana husika ili kuwataka wamuondoshe ama wampe uhamisho mtumishi fulani kwa lengo la wao kukaa kwenye hiyo nafasi! Hii ni dhambi kama nyingine! Fahamu sana kuwa haki ni tabia ya Mungu, kutenda haki ni sehemu ya utakatifi!
Wapo viongozi ambao huonea wengine, wakikosewa au wakiona hawajatendewa sawa hata kama muhusika yupo sahihi basi kinachofuata ni wao kumuadhibu kwa kumuamisha au kumuondoa kwenbye vyeo fulani fulani! Huyu naye hatambua kwamba anapaswa kuhakikisha jina lake li mbinguni kwa kuwa mtu wa haki!
Mshirika! Kitabu hiki ni muhimu kwako pia! Maana unapaswa kuhakikisha kuwa unazingatia mambo ya adili au maadili ya kiroho kwanza na sio vinginevyo! Maana Yesu alisema kuwa napenda adili kwanza! Na katika Agano la Kale akasema anataka rehema kwanza! Kwa maana kwamba kuna vitu vya msingi ambavyo Mungu anavitazama, ili kukuhesabia haki!
Epuka sana mambo fulani fulani yakaonekana mema ila wewe ukakataliwa! Mungu alimkubali Habili, na sadaka yake, kwa hiyo angeweza kuikubali sadaka ya Habili, ila asimkubali Habili! Kwa Korinerio aliikubali sadaka yake/zake na kumkataa Korinerio! Kisha akahakikisha anamtuma Petro ili sasa sio sadaka tu zikubalike bali na kiroho cha Korinerio kikamilishwe! Sasa kwa Kornerio ilikuwa ni kesi tofauti! Kwako wewe uliyeijua kweli yote, ukiteleza/haribika hakika utakuwa kama Kaini, ambaye sadaka yake ilikuwa mbovu, ikakataliwa, na maisha yake yalikuwa mabaya pia nayo yakakataliwa! Sasa wewe usiishilie tu kuwa na sadaka njema, kuwa mfanya usafi mzuri kanisani, kumjali mchungaji wako na kusahau roho yako ! Ambapo hayo yatakubalika! Bali hakikisha na kiroho chako kipo vyema! Kwa hiyo kwa moyo mkunjufu ninakukaribisha humu kitabuni!
Kitabu kikitoka kitafute!
Hongera kwa kusoma ujumbe huu, nakutia moyo kuzidi kumtazama Mungu, na pia uwenda hujaokoka, yaani Yesu sio Bwana na mwokozi wa maisha yako! Nakutia moyo pia kuokoka sasa! Yamkini ni uchumi, fedha, hazipatikani, unazingirwa na nuksi na mikosi, kila unalofanya haliendi, unakabwa na mapepo, ! Wewe njoo kwa Yesu na hayo yote yatapita kabisa ! Sasa natumi u tayari!
Sema; MUNGU BABA, NINAKUPENDA, ASANTE KWA KUNIPENDA KWANZA, LEO NIMETAMBUA KUWA MIMI NI MWENYE DHAMBI, NA NIPO TAYARI KUOKOOKA, TAFADHALI INGIA NDANI YANGU, SAMEHE DHAMBI ZANGU, NA FUTA JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKU, NA ULIANDIKE SASA KATIKA KITABU CHA UZIMA WA MILELE, Ameni.
Kwa kufanya hiyo umekwisha kuokoka sasa, na tafadhali tafuta kanisa la watu waliokoka lililopo karibu nawe ukasali, hapo, waambie kuwa umeokoa hivi karibuni, ili wakulee vyema kiroho.
Mawasiliano yetu, kwa M-Pesa au Simu: +255 759 859 287, barua pepe: ukombozigospel@gmail.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni