Ijumaa, 28 Agosti 2020

PENDO LA KRISTO JUU YAKO NI LA MAFANIKIO


 Mpendwa nikutie tu moyo kuwa Yesu anakupenda, anakuwazia mawazo yaliyo mema, ni Mawazo ya Amani, Furaha, ana mipango mizuri juu yako, ni Mipango ya Kuinuliwa, Kufanikiwa, kama ilivyo nia yake katika 1 Yohana 3:2, kuwa anataka ufanikiwe kimwili au kifya na katika kila eneo la maisha yako ikiwemo uchumi, ndoa, huduma na kadhalika kama vile roho au nafsi yako ifanikiwavyo:

Hali ya mapito unayokutana nayo leo ni muhimu sana kufahamu kuwa ni ya muda tu! jangwa lipo ili kukufundisha na kukutengenezea mazingira mazuri zaidi kwa ajili ya Kanani yako! wana wa Israeli walipita hapo ili waweze kuishi vyema kwenye nchi ya Maziwa na Asali!
Nawe nchi yako ya maziwa na asali yaja ndiposa u ukipitishwa hapo!
La muhimu ni kuhakikisha imani yako haiyumbi, wana wa Israeli waliofia jangwani ilikuwa ni matokeo ya kutokuchanganya ile ahadi na imani kama maandiko yafunzavyo:
Lakini ukija katika Waebrania 3 na 4 utauona uapo wa Mungu pale kuwa aliwapia hawataingia rahani mwake kwa sababu ya kupungukiwa imani, na katika ile Hesabu 14 Mungu anamwambia Musa kuwa watu hawa watanidharau hadi au hata lini! Ikiwakilisha kuwa jambo la wewe kuogopa adui zako au vitisho katika safari yako ya kiroho kwa Mungu ni kumdharau ni sawa na kutokuliheshimisha jina lake!
Nikutie moyo kuwa kama wakina Yoshua na Kalebu na Musa na Haruni walivyosimama upande wa Mungu na kulitetea jina lake pale wakiwasihi wenzao wasimwasi Mungu wala wasiogope, na wewe hakikisha haumuasi Mungu nami ninakwambia kuwa usiogope maana uvuli uliokuwa juu yao umondolewa!
Jikaze kiume, jikaze viuno kama maandiko yatufunzavyo, kisha songa mbele! Mema yako yapo. majibu yako yapo. Ushindi wako upo, la muhimu ni wewe kujipa moyo!
Fahamu sana kuwa Yesu anakupenda, na anakuwazia yaliyo mema, mapito ni ishara ya upendo huo, wala sio mateso, maana askari mzuri ni yule aliyeandaliwa vyema, na Mungu anataka uwe askari mzuri!
kama hujaokoka na umeusoma ujumbe huu na kufahamu jinsi pendo la Kristo lilovyokubwa kwako, na unataka kumpa Yesu maisha yako, basi nikupongeze na hongera kwa hatua hiyo, nakutaka kufuatisha nami maneno haya ya sala hii ya toba kw aimnai, na badaa ya hapo utakuwa umeokoka:
sema, MUNGU BABA, NINAKUPENDA, NINAKUTAKA UINGIA NDANI YANGU, ILI UFANYIKE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINAAMINI KUWA YESU NI MUNGU, ALIKUFA NA KUFUFUKA, TAFADHALI FUTA JINA LANGU KWENYe KITABU CHA HUKUMU, NA ULIANDIKE SASA KWENYE KITABU CHA UZIMA WA MILELE, Amen.
Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo, kwa maombezi, ushauri na mahuburi au maswali wasiliana nasi kwa Simu namba: +255759859287, Emaili: ukombozigospel@gmail.com au tembelea www.ukombozigospel.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni