Mwalimu Oscar Samba
Ijumaa, 28 Agosti 2020
Utangulizi wa Kitabu chetu cha UTUMISHI NA MTUMISHI
PENDO LA KRISTO JUU YAKO NI LA MAFANIKIO
Mpendwa nikutie tu moyo kuwa Yesu anakupenda, anakuwazia mawazo yaliyo mema, ni Mawazo ya Amani, Furaha, ana mipango mizuri juu yako, ni Mipango ya Kuinuliwa, Kufanikiwa, kama ilivyo nia yake katika 1 Yohana 3:2, kuwa anataka ufanikiwe kimwili au kifya na katika kila eneo la maisha yako ikiwemo uchumi, ndoa, huduma na kadhalika kama vile roho au nafsi yako ifanikiwavyo:
YESU ANAKUPENDA!
Na Mwalimu Oscar Samba
Sijui kama unajua kuwa Yesu anakupenda! Ni hatari kujaribu kusema kuwa mbona ninateseka, mbona maisha ni magumu, sasa inawezekanaje Yesu anipende wakati huu ni mwaka wa .. sijapona?
Ukweli ni
kwamba Yesu anakupenda, na kuteseka kwako ni wewe tu bado hujatambua unachotakiwa
kufanya ili kukubaliana na pendo hili! Unajua ndugu yangu acha nikwambie ukweli
huu, nikuweke wazi katika viwango hivi vya uwazi! Mungu ili afanye kazi kwenye
maisha yako ni lazima wewe umpe nafasi!
Mungu ni
tofauti sana na Shetani, Shetani huweza kulazimisha, anaweza kutumia hila na
mbinu batili ili kufanya jambo kwenye maisha yako, ila ili Mungu akusaidie wewe
unapaswa kumruhusu!
Mfano, kuna
mama mmoja alitokwa na damu kwa muda wa miaka 12; kwenye biblia tunajuzwa hili
jambo, muda wote huo alikuwa akiwaendea waganga wa kienyeji na matatibu wa dunia
hii! Ila siku alipoamua na kudhamiria moyoni mwake kwa kulishika pindo la vazi
la Yesu hapo hapo alipokea uponyaji, wake!
Sasa jionee!
Ni kwamba kupona kwake, kulitokea pale ambapo aliamua, alidhamiria kumuendea
Yesu; Luka 8:43 Na mwanamke mmoja,
ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, [aliyekuwa amegharimiwa
mali zake zote kwa kuwapa waganga] asipate kuponywa na mtu ye yote, 44 alikwenda nyuma yake, akaugusa upindo wa vazi
lake; na mara hiyo kutoka damu kwake kulikoma.
Hapo pendo la
Kristo linadhibitika ndani yake! Uponyaji unatokea, lakini sio kwamba Yesu
alianza kumpenda alipomponya la! Upendo ulikwepo ila huyu mama alipoamua
kukubaliana na pendo hilo ndipo alipopona!
Yesu
alitupenda na alimpenda huyu mama hata kabla hajavaa mwili yaani hajaja humu
ulimwenguni, na pendo hili linadhibitishwa na Uungu wote; Yohana 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda
ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali
awe na uzima wa milele.
Dhambi
ilipoingia ulimwenguni pendo la namna hii ililijidhiirisha mara! Halikuanzia
katika kuzaliwa kwa Yesu, bali hata Agano la mlima Sinai ni ishara ya hili
pendo, Mungu alipochinja mnyama na kuwavika wakina Adamu nguo ilikuwa ni sehemu
ya utendaji wa hili pendo! Mahali pengine kwenye biblia hujulikana kama neema,
unapoona neema, uwe na hakika huwakilisha pendo la Kristo, tumeokolewa kwa
neema tu, ama tumeitwa kwa neema tu, uwe na uhakika ni pendo lake!
Pendo hili haliwezi
kujifunua kwako wakati ukiwa na shida unaenda kwa waganga wa kienyeji, ukiwa na
mahitaji humulezi Yesu unawaeleza watu tu na kuishia hapo! Hutaki kwenda
kanisani, maana huyu mama alimfuata Yesu kwenye kusanyiko, na penye kusanyiko
maana yake ni penye uwepo wa Mungu, sasa kwenye ibada ndipo alipo Kristo!
Usiende
kanisa ni kanisa, usiende kusanyiko ni kusanyiko, maana siku hizi watumishi
wengi wa uongo wameibuka, tafuta kanisa la watu walio hai kiroho, mahali ambapo
kiukweli hata akili na ufahamu wako wa kawaida unatambua hapo Mungu yupo, epuka
mbwe mbwe za Shetani, na misisimko isiyo na Mungu ndani yake.
Yawe ni
maombi yako na ni maombi yangu pia kuwa Mungu afunguwe macho yako ya ndani ili
uweze kujua sehemu sahihi itakayokuwezesha kukutana na Yesu wa kweli, maana siku
hizi kuna ma-yesu wengi wa uongo, hawamuhubiri Yesu mwenye kukemea dhambi, kwao
dhambi ni sehemu ya ibada, hapo kimbia!
Ukiona huduma
isiyokemea dhambi, hiyo imepotoka, ukiona huduma ambayo wazinzi na walevi wamo
humo humo na ni watumishi, hapo kimbia wala usiage! Ukiona mtumishi anawataka
washirika wake kimapenzi ujue huyo ni “ajenti” ama wakala wa kuzimu, na
ukimkubalia atakuunganisha na kuzimu moja kwa moja, kwani mashariti yao moja
wapo ya kuwaunganisha ni kulala na watu! Hususani wenye nyota ambazo
zitawasaidia kuvuta watu makanisani! Epuka na kimbia hili!
Unajua kuna
watu wanaenda kanisani ili kuirithisha nafsi yao kuwa nao wapo kanisani! Hii ni
hatari sana, ni sawa na kunywa maji machafu ili tu uwe umekunywa maji! Ni sawa
na kula mkapi au vyakula vibovu ili tu kukidhi hitajio la kula! Ukifikia hapo
upo mahali pagumu sana!
Maana baada
ya muda afya yako itakongoroka tu! Wengine huabudu kwa kufuata mkumbo! Yaani ni
mtumishi yupi anawika sana mjini siku za leo, akipoa au akiona ushabiki
umempungua basi hufikiri kuhama hapo! Akiibuka mwingine mjini, humfuata!
Watoto
hata! Shetani huwa naye anahubiri, tena ni muhubiri mzuri tu! Ukipinga muendee
Yesu kwenye Mathayo na Luka 4, utamuona Yesu akihubiriwa na Shetani pale, na maandiko
anamsomea, kuwa akiwa ndie Mwana w aAdamu ageuze jiwe kuwa mkate, na
alimuonyesha hata utajiri alionao akimpa na kanuni kuwa akimsujudia atampatia!
Sasa
usitishike na injili za mafanikio, maana hawakuanza wao alianza Shetani, na
kupata fedha au mafanikio kutoka kwao sio jambo la kigeni, maana hata Yesu angemsujudia
hakika angepewa, maana ni muhimu kujua nao huwa wanamsujudia nani!
Kusoma maandiko
na kuyafafanua siyo kipimo, kwani hata Shetani alimsomea Yesu, maana ni kweli
yapo kwenye biblia! La muhimu na jambo zuri kuliko yote ni wewe kuhakikisha
kuwa ndani yako unapata amani ya Kristo, maana wapo ambao Mungu anawakosesha amani
na mtu husika ila kwa ushabiki huzidi kugandamana naye! Huku ni kupotea!
Injili ambazo
jina la Yesu limewekwa kando, msisitizo wa maombezi sio katika jina la Yesu na
Damu yake kwenye uhalisia, ama nguvu za Roho Mtakatifu, bali ni katika
viambatanishi, au visaidizi, kama mafuta ambayo yamesingiziwa kuwa ya upako, na
wengi hawataki kujua kama ni upako upi unaotajwa hapo, maji ya upako au maji ya
baraka, wengine wanagawa hadi bangili za upako, pete za upako, nasikia siku
hizi kuna keki za upako, hii ni hatari
sana!
Najua wana
wa upotevuni ni wepesi sana kukinzana na ukweli huu, na wana hoja nyingi sana
wakitumia maanadiko, ila mioyoni mwao wanaujua ukweli, maana sifa zipo kwenye
mafuta na maji yakaniponya, Yesu amekuwa kama ni msaidizi!
Nisikilize,
ukitaka kuliona pendo la Kristo likikusaidia maishani mwako ni muhimu sana
kuhakisha kuwa unaambatana na Yesu kama alivyo, waepuke wanaokupa maji machafu,
katika Yohana 7:38-39 Yesu anaita akiwataka wale wenye kiu waje au waende kwake
ili awape maji!
Maji yake ni
safi, alimwambia yule mama kwenye kisima cha Yakobo katika Yohana 4 kuwa
kiyanywa hayo maji ya Yesu hataona kiu tena! Sasa wamekupa Yesu na bado kiu ya
ulevi ipo, wamekupa Yesu na bado una kiu ya kuiba waume za watu! Ukimuona mume
wa mtu mate yanakutoka kama fisi na mfupa! Wamekupa Yesu angali bado una kiu ya
dogo-dogo, ukimuona kijana “handsame” ama binti mrembo, hata kama ni umri wa mwanao
jicho linakutoka kama vile fundi simu aliyedondosha nati, maana nati zake ni
ndogo kwa hiyo asipotoa macho hawezi kuziona kirahisi, huu akiwa na hofu
usikute imepotea!
Unasema eti
umeokoka, au unamependa na una Yesu, sawa sikataii! Lakini mbona hajaondoa kiu
ya dhambi nadani yako! Bado ni mwizi, unazini kwa siri, nyumba ndogo kuacha
umeshindwa! Hakika huna Yesu aliyehai una yesu marehemu! Wala usinikunjie
ndita, ila ukweli ndio huo!
Anasema hivi;
Yohana 4:13 Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji
haya ataona kiu tena.
Yesu
akiingia nadani yako, na kiu ya mambo ya dunia ispoondoka, uwe makini, rejea msalabani
upya!
Neno la
Mungu ni maji, sasa injili kama inahubiriwa haibadilishi maisha yako, kuna mambo
mawili hapo makuu, wewe mwenyewe u na moyo mbovu, ama injili unayopewa ni maji
machafu, ni maji yasiyo na uwezo wa kukausha kiu ya dhambi, na tamaa zake,
swala la upinzani wa Shetani hili ni la maombi tu! Ila hatuwezi au maombi hayawezi
kukusaidia sana kama wewe mwenyewe hujakaa eneo salama, maana pepo mchafu
amtokapo mtu na akipata mwanya mwingine hurejea, maandiko husema mmekuwa safi
kwa lile neno, neno hukuweka kuwa safi, na mapepo hayakai maeneo ambayo
yamesafishwa kwa Damu ya Yesu!
Huwa nasema
kuna yesu aliyekufa, na kuna Yesu aliye hai, unaposema nataka kumuona Yesu,
nina haja na Yesu, uwe makini maana wakina Pilato wapo hapo kukupa yesu
aliyekufa kama Yusufu wa arimathayo, huyu alipewa Yesu/yesu ila mfu,
aliyempatia alihakikisha kuwa amekwisha kufa! Na aina hii ya Yesu hawezi kuleta
mabadiliko kwenye maisha yako!
Unasema una
Yesu lakini hatuoni badiliko la ndani; ndani yako, una sema una Yesu lakini
hatuoni matokeo ya wewe kuhuishwa hata kidogo! Yesu aliye hai, hukushindia
dhambi, huhuisha utu mpya na kuua ule utu wa kale, hawezi kuchangamana na
dhambi! Ukiona unajiita una Yesu lakini hakuna badiliko la dhambi au la kiroho
ndani yako uwe na hakika kuwa kuna shida ipo mahali, utakuwa wamekupa yesu
aliyekufa siyo Yesu aliye hai kama Yule aliyefufuka siku ya tatu, maana kuna
dini zina yesu sawa, ila ni yesu marehemu!
Wanahubiri
habari za Yesu, Lakini wao wenyewe ni wazinzi, ni walevi, hawawezi kusimama
madhabahuni bila kunywa pombe kidogo, hawawezi kukaa bila kutongoza washirika!
Ni mzee wa kanisa ila sigara anavutia chooni!
Ona hapa; Marko
15:44 Lakini Pilato akastaajabu, kwamba
amekwisha kufa. Akamwita yule akida, akamwuliza kwamba amekufa kitambo. 45 Hata alipokwisha kupata hakika kwa yule
akida, alimpa Yusufu yule maiti.
Kuna dini,
zimehakikisha kuwa yesu waliye naye amekwisha kufa, ndio maana wamekupa wewe!
Maji yao siyo yale halisi yenye uwezo wa kuondoa kiu ya dhambi, ndio maana
wamekupa wewe!
Huwa
ninaweka sana angalizo hili, kuwa unapokuwa na kiu ya kutaka kumjua Yesu,
unapokuwa na kiu ya kutaka kukoka, unapaswa kuwa makini tena mno, maana ukisema
nina kiu, moja kwa moja uwe na hakika kuwa wapo watu ambao hawaachi kukuletea
maji, ambayo kwa kweli siyo sahihi, ndio maanaYesu kwenye ile Yohana akapaza
sauti aksema kila mwene kiu na aje kwangu, aje anywe, hakusema na aje achote
maji ila alisema na aje kwangu, kwa hiyo jifunze kumtafuta Yesu kwanza, na sio
maji kwanza , kama wengi wafanyanvyo! (Maana ukiwa na Yesu, atakwambia haya
maji uliyopewa siyo yangu.)
Najifunza
sana kwa Yesu mwenyewe, alipokuwa pale msalabani na alipopatwa na kiu, alisema
naona kiu, na badala ya kumletea maji walimletea siki! Uwe na hakika na wewe
ukisema nina kiu, wapo na watu ambao nao watakuletea siki ama maji machafu!
Ukisema
nataka kuokoka, ninamtaka Yesu watakwambia usiondoke kwenye dini yetu maana na
huku pia watu wanaokoka, kuna vikundi huku nako vya uaomsho, uwe na hakika ni
uamsho bandia, maana kuna na moto bandia, ambao hufananishwa na ule wa Roho
Mtakatifu!
Namtaka
Yesu, wanakuletea Yesu ambaye amekufa, hawezi kuondoa dhambi! Ndio maana adui
ameweka utitiri wa madhehebu na makanisa mapya na watumishi wengi, ni ili kuwapoteza
watu, maana ma-yesu wafu wamejaa sana humu duniani! Umakini unahitajika sana!
Asante kwa
kunisikiliza (nafsini mwako), ama kunifuatilia kwa njia ya usomaji huu wa hii
makala, nina amini kuwa kuna kitu umekipata hapa, Yesu anakupenda, ila kama
hujakutana na pendo lake uwe na hakika kuna dosari ipo mahali, chukua hatua
mapema mnoo!
Pia anasema
kwamba mtu akimpenda atazishia amri zake, kwa hiyo kama kweli umedhamiria,
mpende kwa kuzishika amri zake, epuka michanganyo, epuka kuuzoelea wokovu,
asante na Mungu akubariki mno; Yohana 14:23
Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba
yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake. 24 Mtu
asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu,
ila ni lake Baba aliyenipeleka.
Hongera kwa
kusoma ujumbe huu, nakutia moyo kuzidi kumtazama Mungu, na pia uwenda
hujaokoka, yaani Yesu sio Bwana na mwokozi wa maisha yako! Nakutia moyo tena
kuokoka sasa! Yamkini ni uchumi, fedha, hazipatikani, unazingirwa na nuksi na
mikosi, kila unalofanya haliendi, unakabwa na mapepo, ! Wewe njoo kwa Yesu na
hayo yote yatapita kabisa ! Sasa natumi u
tayari!
Sema; MUNGU
BABA, NINAKUPENDA, ASANTE KWA KUNIPENDA KWANZA, LEO NIMETAMBUA KUWA MIMI NI
MWENYE DHAMBI, NA NIPO TAYARI KUOKOOKA, TAFADHALI INGIA NDANI YANGU, SAMEHE
DHAMBI ZANGU, NA FUTA JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKU, NA ULIANDIKE SASA
KATIKA KITABU CHA UZIMA WA MILELE, Ameni.
Kwa kufanya
hiyo umekwisha kuokoka sasa, na tafadhali tafuta kanisa la watu waliokoka
lililopo karibu nawe ukasali, hapo, waambie kuwa umeokoa hivi karibuni, ili
wakulee vyema kiroho.
Mawasiliano
yetu, kwa M-Pesa au Simu: +255 759 859 287, barua pepe:
ukombozigospel@gmail.com
pia
temnbelea: www.ukombozigospel.blogspot.com
.