7⃣SOMO:JIEPUSHE NA MAKOSA YAFUATAYO UKITAKA KUVUKA KWA USHINDI MWAKA HUU
Hili ni eneo ambalo unahitaji kulielewa sana kwa sababu si kila mtu atapita mahali ambako pako shwari.
Kila mtu anapita kwenye dhoruba yake na si kila dhoruba ni mbaya.
Warumi 8:28.
28 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.
Simama kwenye kusudi la Mungu shetani hawezi kukuzamisha atajaribu kila namna lakini atashangaa ukisimama kwa upya.
Kuna matatizo mengine Mungu anayaruhusu kwa ajili ya kukujengea msuli wako kwa ajili ya mambo yaliyopo mbele yako.
Yesu aliomba “kikombe hiki kiniepuke” alikuwa anajua kabisa angeweza kuamuru jeshi la malaika kumtetea na kumpigania, angeweza kuwatoroka, lakini Biblia inasema mbigu zilinyamaza kwa sababu Mungu hakuwa na mpango wa kumwondolea msalaba,kwa sababu msalaba ungeondolewa hakuna mahala tungekombolewa.
Mungu akinyamaza usikasirike, endelea tu kuomba kwa sababu inawezekana ni jambo bado majira yake.
Tatizo tunambea katika majira ambayo tunahisi tunapopata matatizo tunahisi tumepungukiwa imani lakini kumbe hatujajua ni sehemu ya safari au sehemu ya maisha.
Hakuna mtu hapa Duniani atayekuambia matatizo ni mazuri. Lakini tunapotembea hapa Duniani hakuna mtu yeyote ambaye hatakutana na matatizo, kwa hiyo usijaribu kuishi na mawazo kwamba hautakutana na matatizo.
Hata Yesu anazungumza juu watu ambao wanamsikiliza kwamba nyumba zao zitapigwa na dhoruba lakini yule anayelisikiza Neno la Bwana na kulitenda ni kwamba dhoruba itakuja na kuipiga nyumba lakini haitaanguka, kwa sababu alifuatilia maelekezo ambayo alikuwa amepewa.
Wenzake na Daniel yaani Meshack, Shadrack na Abedinego wakiwa Babeli walipotakiwa kuisujudia ile sanamu walikataa wakaendelea kumwabudu Mungu wao. Wakashitakiwa wakapelekwa mbele ya mfalme,wakamwambia mfalme hujui uhusiano tulionao na Mungu wetu. Wakasema sisi tuko tayari kufa kwenye hili tanuru la moto hata Mungu akitunyamazia kwenye hili tanuru tuko tayari kufa kwa ajili yake waliingizwa kwenye tanuru la moto
Walimkuta mtu anasura kama ya Mwana wa Adamu na kumbe ni Yesu alikuwa anawasubiri ndani ya tanuru la moto. Kwanini asiwasaidie nje hadi kawasubiri waingie ndani ya tanuru la moto? Jibu ni watu wengine watajuaje ya kuwa yupo Mungu ambaye anaweza waokoa watu hata katika shida kubwa namna hiyo!
Ni rahisi sana kumziria Mungu unapopita kwenye matatizo na hakusaidii.Lazima kuna sababu fulani wewe endelea kuomba, usichoke,wala usikate tamaa, lakini endelea kufuata maelekezo anayokuelekeza katikati ya dhiki hiyo.Ndio maana wakati mwingine anakupitisha kwenye bonde la uvuli wa mauti, ila hakuondoi , anahakikisha unapita.
Wale wanafunzi walifadhaika kwa sababu Yesu alitembea juu ya dhoruba na mawimbi hakuyatuliza. Kwa sababu waliwahi kumwona akituliza dhoruba, lakini leo anawaona wanahangaika hawasaidii. Walifikiri angetuliza dhoruba ila yeye anatembea juu ya ile ile dhoruba
Walifadhaika kwa sababu walimzoea Yesu anayewaondolea matatizo si Yesu anayewapitisha kwenye matatizo.
Yesu anaweza kuja kwenye maisha yako na akatembea katikati ya matatizo yako,ili kukupitisha.Shida ni kuwa kila tatizo unamwona shetani na shetani anaweza kutumia hayo mazingira akakuvuruga kweli.Lakini unaweza ukaamua katikati ya shida ukamwona Yesu,kwa sababu yupo hapo hapo. Anasema “niite katikati ya matatizo nami nitakuokoa” lakini anapokuja anatembea juu ya majaribu.
Hapa ndio mwisho wa hili somo.Hakikisha somo hili unaliweka kwenye matendo. ubarikiwe sana. Nakutakia mwaka wa baraka maishani wako uweza wa Mungu uwe juu yako na ufanikiwe katika kila ulifanyalo.
Mungu akufanikishe mwaka huu.🙏🙏🤝👋👋
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni