Jumanne, 15 Agosti 2023

BWANA ANA HAJA NAWE


Na Mwl Oscar Samba 

Duniani hatukuja kwa bahati mbaya, lipo kusudio la kuumbwa kwetu. Kama vile mtu anavyomuajiri mfanyakazi na kisha kuwa na malengo naye katika eneo analohitaji asaidiwe kazi, ndivyo na Mungu wetu alivyotuumba akiwa na kusudio maalumu la uumbaji wake kwetu.

Nimfano wa mtu aliyenunua chombo chake cha usafiri! Hapana shaka huyu mtu huwa na malengo katika matumizi fulani ya hicho chombo. Mimi na wewe ni chombo cha Mungu. Mungu hakutuumba kwa bahati mbaya, wala hukuzaliwa kwa bahati yoyote kama vile wengineo huweza kuzania. Kila mtu amezaliwa kwa kusudi la Mungu lililo kamili kabisa.

Wasomaji wa kitabu kile cha Zekaria wanajuwa kuna unabii ulitolewa kuhusu punda ambaye Yesu alikuja kumtumia miaka kadhaa mbele katika Agano Jipya. Najuwa kuna jinsi jambo kama hili huweza kuonekana kuwa ni dogo, lakini lilishatabiriwa au kuangaziwa toka miaka mingi yenye oroda ya mamia ya miaka ama mlolongo wa karne nyingi.

Usipojuwa unaweza kuliona hili tukio kuwa ni la kawaida ila kiuhalisia lilishaandaliwa; Marko 11:2 akawaambia, Nendeni mpaka kile kijiji kinachowakabili; na katika kuingia ndani yake, mara mtaona mwana-punda amefungwa, asiyepandwa na mtu bado; mfungueni, kamleteni.

3 Na mtu akiwaambia, Mbona mnafanya hivi? Semeni, Bwana anamhitaji na mara atamrudisha tena hapa.

Luka 19.33 Na walipokuwa wakimfungua mwana-punda, wenyewe waliwaambia, Mbona mnamfungua mwana-punda? 34 Wakasema, Bwana ana haja naye.

Sasa jaribu kufikiia kama punda anaandaliwa hivi kwa ajili ya tuko la siku moja tu! Je, wewe sii Zaidi? Ambaye unatarajiwa kutumika miaka na miaka! 

Ugumu wa maisha unayoishi leo, hali ya kukataliwa inayokugubika leo, matatizo kadha wa kadha yanayokukuta leo, sio ishara ya kwamba Mungu amekuchoka au hakuhitaji, wala sio jibu la kwamba hukuzaliwa kwa makusudi kamili ya Mungu bali ulizaliwa bahati mbaya ndio maana huku duniani unaona kama vile huna makao maalumu, ni  kama vile nafasi yako ya kukaa haipo. Na ndivyo walivyo baadhi ya watu, ni kwamba wamekutana na mambo magumu huku ulimwenguni kiasi cha kuona nafasi yao ya kuishi au kukaa haipo kabisa, ni kama vile wamekosa “siti” huku ulimwenguni.

Maana kila mahali nahisi kukataliwa, kubaguliwa, kutengwa na hata kudharauliwa. Nisikilize, Yusufu mwana waYakobo yaliwahi kumkuta hayo, ndugu zake wamemkataa, na hata huko alikouzwa nako wamemkataa vivyo; akajikuta yupo jela. Napo pia aliyemtafsiria ndoto naye amemsahau. Inawezekana hata uliowasaidia wakaja wakafanikiwa kuliko wewe nao pia wamekusahau! 

Sikiliza neno la Bwana…Bwana nasema hajakusahau ndio maana anakwambia kwamba “”Ana Haja Nawe.” Anakuhitaji..maana wewe kwake ni chombo kiteule chake. Wakati Ananiya anamuona Paulo kama muuaji Mungu alimuona kuwa ni chombo chake kiteule, Anania alikuwa bado anatembea na picha mbaya ya maisha ya Paulo hakujuwa Mungu anatembea na picha mpya ya Mtumishi wae. Ni hatari naye Paulo kama angekubali kujiona kama wengine walivyokuwa wamesalia kumuona.


Wakati wanafunzi ama Mitume wanamuona bado kama muuaji, Mungu alimuinulia Barnaba aliyemtambulisha rasimi na kueleza jinsi Paulo alivyobadilika. Mungu nawe atakuinulia Barnaba wako, na nikueleze kuwa mimi ndiye. Ninakutia moyo ya kwamba wewe u chombo chake kiteule, usitazame mchungaji wako au wapendwa wenzako wanakuonaje, bali tazama Mungu anakuonaje wewe!

Eliabu alimuona Daudi kama ni mwenye kiburi, na mtu asiyeweza kupigana na Goliathi, na ndivyo mfalme Sauli alivyomuona,; akimuona kama ni kijana mdogo tu. Asiye na uzoefu na vita wala asiyeweza kumkabili Goliathi. Lakini ashukuriwe Mungu kuwa Daudi alijiona ni mwenye uwezo huo.

Usikubai kujiona duni mbele za watu na Mungu wako. Maisha unayoshi hayawezi kusadifu ulichobeba…Unaiuliza Mwalimu Oscar inakuaje? Nenda kasome Wamuzi 6, utakutana na mtu anatwa Gedion, utastaajabia ninachokwambia. Alikuwa ni mtu aliyewaogopa Wamidiani, na alikuwa amejificha kwenye pango lilojirani na mti wa mwaloni akiwa anapeta ngano huko. Maana aliwaogopa watampora mazao yake. 

Cha ajabu, katikati ya hofu kubwa kama hiyo Mungu anamtoke n kumwambia asiogpe, kisha anamuita shujaa na anamtaka akawaokowe watu wake. Lilikuwa jambo la jabu sana hata kwake mwenyewe, kwamba anaitwa shujaa, na kinachomshangaza zaidi eti Mungu yupamoja naye! Anakuwaje pamoja naye na wakati wanatawaliwa na muda huo amejificha kwenye pango? Lakini kiukweli Bwana alikuwa pamoja nao kweli, ndio maana Mungu aliwaokoa dhidi ya yale mateso na alimtumia huyu huyu.

Ndiposa ninapokwambia kuwa Mungu yu pamoja nawe kwenye hiyo shida nielewe, maana hata maandiko husema Yusufu alipotupwa gerezani, Bwana alikuwa pamoja naye, alipoingia kwa Potifa na kuwa mfanyakazi wa ndani huko nako Bwana alikuwa pamoja naye. Bwana kuwa pamoja nawe, haimaanishi kuwa hutapitia magumu, wala hutakataliwa, kwani hata Yusufu na mashujaa wengine walikataliwa na kupitia pagumu na bado Bwana alikua pamoja nao.

Na wewe ikutie moyo kuwa Bwana yu nawe simama sasa na ujikubali..Amua sasa   kakutumie..kama aliyoagiza punda afunguliwe na akampanda mgongoni akielekea Yerusalemu, na wewe kubali leo kutumika. 

Kumbuka msisitizo mkubwa wa ujumbe huu sio kukutia moyo tu, bali ni kukutaka ufahamu kuwa Bwana anakuhitaji, anakutaka utumike. Anakutaka umtumikie.

Pia wewe ambaye hujaokoka, fahamu Bwana anahaja nawe kama alivyokuwa na haja na yule punda..huna budi kuokoka sasa ili uweze kutimiza kusudio la kuumbwa kwako… 

kama hujaokoka na umeusoma ujumbe huu na kufahamu jinsi pendo la Kristo lilivyokubwa kwako, na unataka kumpa Yesu maisha yako, basi nikupongeze na hongera kwa hatua hiyo, nakutaka kufuatisha nami maneno haya ya sala hii ya toba kwa imani, na baada ya hapo utakuwa umeokoka:

sema, MUNGU BABA, NINAKUPENDA, NINAKUTAKA UINGIA NDANI YANGU, ILI UFANYIKE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINAAMINI KUWA YESU NI MUNGU, ALIKUFA NA KUFUFUKA, TAFADHALI FUTA JINA LANGU KWENYE KITABU CHA HUKUMU, NA ULIANDIKE SASA KWENYE KITABU CHA UZIMA WA MILELE, Amen.

Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo, kwa maombezi, ushauri na mahuburi au maswali wasiliana nasi kwa Simu namba: +255759859287, Emaili: ukombozigospel@gmail.com au tembelea www.ukombozigospel.blogspot.com


Kundi letu la WhatsApp:  https://chat.whatsapp.com/E0eD0xegh1eIGMjRykPyRD

Telegram:  https://t.me/+fft3GHXC9xIzYjhk

Neno la Leo ( #NasahazaMwlOscar )

http://www.ukombozigospel.blogspot.com

Kundi letu la WhatsApp https://chat.whatsapp.com/E0eD0xegh1eIGMjRykPyRD

Telegram https://t.me/+fft3GHXC9xIzYjhk

Subscribe YouTube yetu: https://www.youtube.com/@ukombozigospeltv

Kwa Maombi +255759859287 


Nikutakie Siku Njema

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni