Jumanne, 29 Agosti 2023

Faida ya Jaribu na Dhima ya Utoaji au Kumtunza Mtumishi wa Mungu ( soma sura yote ya Wafilipi 4 )


 Neno la Leo ( #NasahazaMwlOscar )

#FaidayaJaribu:

Wafilipi 4:8 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo.

:9 Mambo mliyojifunza kwangu na kuyapokea, na kuyasikia na kuyaona kwangu, yatendeni hayo; na Mungu wa amani atakuwa pamoja nanyi.

:10 Nalifurahi sana katika Bwana, kwa kuwa sasa mwisho mmehuisha tena fikira zenu kwa ajili yangu, kama vile mlivyokuwa mkinifikiri hali yangu lakini hamkupata nafasi.


:19 Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.

(Baraka Hizi za Paulo Zinakuja Baada ya Hawa Watu Kusimama Kwenye Nafasi Yao)

http://www.ukombozigospel.blogspot.com

Kundi letu la WhatsApp https://chat.whatsapp.com/E0eD0xegh1eIGMjRykPyRD

Telegram https://t.me/+fft3GHXC9xIzYjhk

Subscribe YouTube yetu: https://www.youtube.com/@ukombozigospeltv

Jumanne, 22 Agosti 2023

Faida ya Majaribu au Mapito ( Mtazame Yesu )


 Neno la Leo ( #NasahazaMwlOscar )








 Faida ya Jaribu :

Waebrania 12:3 Maana mtafakarini sana yeye aliyeyastahimili mapingamizi makuu namna hii ya watendao dhambi juu ya nafsi zao, msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu.


:4 Hamjafanya vita hata kumwagika damu, mkishindana na dhambi;


Tunapewa Nasaha za Kumtazama Yesu Aliyestahimili Mambo Magumu kwa Ajili Yetu, Hata Akautoa Uhai wake..Mimi Na wewe Hatujafikia Kipimo Hicho cha Kuimwaga Damu...Nasi Hatuna Budi Kuyastahimili kama Yeye Alivyofanya kwa Ajili Yetu..Nasi Tufanye kwa Ajili Yake..


http://www.ukombozigospel.blogspot.com

Kundi letu la WhatsApp https://chat.whatsapp.com/E0eD0xegh1eIGMjRykPyRD


Telegram https://t.me/+fft3GHXC9xIzYjhk


Subscribe YouTube yetu: https://www.youtube.com/@ukombozigospeltv

Kwa Maombi +255759859287 


Nikutakie Siku Njema

Jumatano, 16 Agosti 2023

SEMINA KKKT MWANZA 2016. NA MWL CHRISTOPHER MWAKASEGE KOSA LA SABA. 7.YESU AKIAMUA KUTOITULIZA DHORUBA USIMKASIRIKIE BALI ENDELEA KUOMBA NA KUFUATA MAELEKEZO YAKE.

 7⃣SOMO:JIEPUSHE NA MAKOSA YAFUATAYO UKITAKA KUVUKA KWA USHINDI MWAKA HUU


Hili ni eneo ambalo unahitaji kulielewa sana kwa sababu si kila mtu atapita mahali ambako pako shwari.

Kila mtu anapita kwenye dhoruba yake na si kila dhoruba ni mbaya.

Warumi 8:28.
28 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.

Simama kwenye kusudi la Mungu shetani hawezi kukuzamisha atajaribu kila namna lakini atashangaa ukisimama kwa upya.

Kuna matatizo mengine Mungu anayaruhusu kwa ajili ya kukujengea msuli wako kwa ajili ya mambo yaliyopo mbele yako.

Yesu aliomba “kikombe hiki kiniepuke” alikuwa anajua kabisa angeweza kuamuru jeshi la malaika kumtetea na kumpigania, angeweza kuwatoroka, lakini Biblia inasema mbigu zilinyamaza kwa sababu Mungu hakuwa na mpango wa kumwondolea msalaba,kwa sababu msalaba ungeondolewa hakuna mahala tungekombolewa.

Mungu akinyamaza usikasirike, endelea tu kuomba kwa sababu inawezekana ni jambo bado majira yake.

Tatizo tunambea katika majira ambayo tunahisi tunapopata matatizo tunahisi tumepungukiwa imani lakini kumbe hatujajua ni sehemu ya safari au sehemu ya maisha.

Hakuna mtu hapa Duniani atayekuambia matatizo ni mazuri. Lakini tunapotembea hapa Duniani hakuna mtu yeyote ambaye hatakutana na matatizo, kwa hiyo usijaribu kuishi na mawazo kwamba hautakutana na matatizo.


 Neno la Leo ( #NasahazaMwlOscar )


Yakobo 5:10 Ndugu, watwaeni manabii walionena kwa jina la Bwana, wawe mfano wa kustahimili mabaya, na wa uvumilivu.

:11 Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma.

http://www.ukombozigospel.blogspot.com

Kundi letu la WhatsApp https://chat.whatsapp.com/E0eD0xegh1eIGMjRykPyRD

Telegram https://t.me/+fft3GHXC9xIzYjhk

Subscribe YouTube yetu: https://www.youtube.com/@ukombozigospeltv
Kwa Maombi +255759859287

Nikutakie Siku Njema

Jumanne, 15 Agosti 2023

BWANA ANA HAJA NAWE


Na Mwl Oscar Samba 

Duniani hatukuja kwa bahati mbaya, lipo kusudio la kuumbwa kwetu. Kama vile mtu anavyomuajiri mfanyakazi na kisha kuwa na malengo naye katika eneo analohitaji asaidiwe kazi, ndivyo na Mungu wetu alivyotuumba akiwa na kusudio maalumu la uumbaji wake kwetu.

Nimfano wa mtu aliyenunua chombo chake cha usafiri! Hapana shaka huyu mtu huwa na malengo katika matumizi fulani ya hicho chombo. Mimi na wewe ni chombo cha Mungu. Mungu hakutuumba kwa bahati mbaya, wala hukuzaliwa kwa bahati yoyote kama vile wengineo huweza kuzania. Kila mtu amezaliwa kwa kusudi la Mungu lililo kamili kabisa.

Wasomaji wa kitabu kile cha Zekaria wanajuwa kuna unabii ulitolewa kuhusu punda ambaye Yesu alikuja kumtumia miaka kadhaa mbele katika Agano Jipya. Najuwa kuna jinsi jambo kama hili huweza kuonekana kuwa ni dogo, lakini lilishatabiriwa au kuangaziwa toka miaka mingi yenye oroda ya mamia ya miaka ama mlolongo wa karne nyingi.

Usipojuwa unaweza kuliona hili tukio kuwa ni la kawaida ila kiuhalisia lilishaandaliwa; Marko 11:2 akawaambia, Nendeni mpaka kile kijiji kinachowakabili; na katika kuingia ndani yake, mara mtaona mwana-punda amefungwa, asiyepandwa na mtu bado; mfungueni, kamleteni.

3 Na mtu akiwaambia, Mbona mnafanya hivi? Semeni, Bwana anamhitaji na mara atamrudisha tena hapa.

Luka 19.33 Na walipokuwa wakimfungua mwana-punda, wenyewe waliwaambia, Mbona mnamfungua mwana-punda? 34 Wakasema, Bwana ana haja naye.

Sasa jaribu kufikiia kama punda anaandaliwa hivi kwa ajili ya tuko la siku moja tu! Je, wewe sii Zaidi? Ambaye unatarajiwa kutumika miaka na miaka! 

Jumatano, 9 Agosti 2023

Neno la Leo, Kufurahia Pito au Majatibu, kwa Ajili ya Injili au Kristo

 

Neno la Leo (Nasaha za Mwl Oscar)

Mathayo 5:11 Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu.

:12 Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.

*Kesho nitakupa Mfano wa Watu Waliofurahia Mateso na Dhiki ikiwemo Kupigwa kwa Ajili ya Yesu au Injili..Unapaswa Kufurahia Kufukuzwa Kazi, Kuonewa na Hata Kubaguliwa ama Kuchukiwa kwa Ajili tu Wewe Umeokoka...Kila Dhaa kwa Ajili ya Imani Yako, Kwako Lifurahie Maana Malipo Yake ni Mkaubwa Mbinguni... Maana Bila Hayo Taji Yako ni Ndogo* ...

www.ukombozigospel.blogspot.com

Jiunge na Kundi Letu la Telegram

https://t.me/+fft3GHXC9xIzYjhk
Kwa Maombi: +255759859287

Uwe na Siku Njema


Jumatano, 2 Agosti 2023

Neno la Leo, Amani na Maendeleo

 

Neno la Leo (Nasaha za Mwalimu Oscar)

Maombolezo 3:17 Umeniweka nafsi yangu mbali na amani; Nikasahau kufanikiwa.

*Kumbe Amani Ikitoweka na Mafanikio nayo Hupotea au Huwa Adimu..! Kwa hiyo; Hakikisha Amani Haipotei Moyoni Mwako ili Kulinda au Kuchunga na Kudumisha Mafanikio...Tazama Toka Uchungu, Hasira na Msongo wa Mawazo Vilipokukabili..Utakuta na Kasi ya Mafanikio Imepungua na Hata Mambo ya Msingi km Ujenzi na Biashara Kukwama* ..

www.ukombozigospel.blogspot.com

Kundi Letu la Telegram

https://t.me/+fft3GHXC9xIzYjhk

Nikutakie Siku Njema