Alhamisi, 27 Julai 2023

Neno la Leo, Amani Moyoni

 

Neno la Leo

Zaburi 119:165 Wana amani nyingi waipendao sheria yako, Wala hawana la kuwakwaza.

*Jifunze Kupendezwa na Sheria au Neno au Maelekezo Yenye Kukutaka Kutokutenda.. ama Kutenda yaliyo ya Mungu. Ukifanya hivyo ndipo Amani Yake Itakukalia...Kwa hiyo; Ukiona Unafanya Jambo na huna Amani, jitazame km Moyoni Mwako Umependezwa nayo..*

www.ukombozigospel.blogspot.com

Nikitakie Siku Yenye Baraka na Amani Nafsini..


Jumanne, 25 Julai 2023

Neno la Leo AMANI NA FURAHA KATIKA MAGUMU Zaburi 4:7, 8.

 

Neno la Leo

Zaburi 4:7 Umenitia furaha moyoni mwangu, Kupita yao wanapozidishiwa nafaka na divai.

:8 Katika *amani* nitajilaza na kupata usingizi mara, Maana Wewe, Bwana, peke yako, Ndiwe unijaliaye kukaa salama.

*Katika Yote Hakikisha Una Amanj ya Kristo, Usitazame wingi wa Vita na ukubwa wa Maadui, bali Tazama Amani ya Kristo ndani yako..ilinde hiyo..Amani yake ni Ishara ya Uwepo wake...Kujibizana na Maadui na Manung'uniko huondoa Amani.. Amani Huleta Utulivu..*

Uwe na Siku Njema


Jumamosi, 15 Julai 2023

Neno la Leo Ujira waKahaba au Fedhaa ya Sadaka Isiyo Halali

 Neno la LEO


Kumbukumbu la Torati 23:18 Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya Bwana, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yo yote; kwani haya ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako, yote mawili.


 *Sadaka Ambayo Mapato Yake Siyo Halali Haikubaliki Mbele za BWANA na ni Machukizo*


Nikutakie Umakini ktk Utoaji


Pia na Siku Njema