Jumanne, 14 Februari 2023

kitabu chetu cha: CHAKUFANYA UNAPOLEMEWA NA MZIGO MZITO AMBAPO MUNGU, BADO ANATAKA UENDELEE KUUBEBA.

Ujumbe huu ni sehemu ya kitabu chetu cha: CHAKUFANYA UNAPOLEMEWA NA MZIGO MZITO AMBAPO MUNGU, BADO ANATAKA UENDELEE KUUBEBA.

Hiki sii kitabu cha kawaida wala si somo tu bali ni ujumbe. Najua kila ujumbe ni somo katika mukutadha wa mafundisho na ufundishaji. Japo sio kila somo ni ujumbe.

Ujumbe huu ni matokeo ya mahali ninapopapitia ambapo mwaka jana palinipatia vitabu kama viwili hivi. Mosi ni kile cha  HAKUFANYA UNAPOKUWA NJIA PANDA. Na pili ni kile cha MUONE MUNGU NYUMA YA PITO LAKO.

Kwa lugha nyingine unaweza kusema kuwa sii jumbe za kawaida. Bali ni maelekezo. Mfano wa ujumbe kibiblia ni pale mfalme Nebukaddeza alipoota ile ndoto na kisha kujikuta hana tafsiri yake na kuomba msaada kwa Danieli nabii wa Mungu. Tukiachana na yote pale, yale maneno, "Danieli 4:27 Kwa sababu hiyo, Ee mfalme, shauri langu lipate kibali kwako; ukaache dhambi zako kwa kutenda haki, ukaache maovu yako kwa kuwahurumia maskini; huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za kukaa raha."


Kwa hiyo, kama Mungu amekupa kukisoma kitabu hiki, moja kwa moja fikra zako zielekeze kwenye ujumbe uliopo ndani yake. Ambao unanuia kumsaidia kwa kumpa mtu husika maelekezo muhimu ya kufanya ili kuendelea mbele na pito au jaribu analolipitia.

Ni matoke ya mimi katika jana ya leo, baada ya kuzungumza na kiongozi wangu mmoja juu ya pito ninalolipitia na majibu ya Mungu juu yangu. Majibu hayo yalinitaka niendelee kuvumilia. Na aliniambia hadi nimalize masomo. Nikauliza je nikimaliza Mungu ndo atanijibu?

Akaniambia hata yeye hajui kama atanijibu au la, ila alichoambiwa ni kwamba kwa wakati huu usijaribu kubeba mambo mawili. Kwa mujibu wa mukutadha wa hekima ile ni kwamba inaonekana maamuzi yangu dhidi ya pito husika nyuma yake hayana mapenzi makamilifu ya Mungu. 

Na ili kuvuka hapa sinabudi kuhakikisha nina kuwa na uvumilivu.
Sii kila aliyekwama alitaka kukwama. Hakuna kitu kibaya kama kukata tamaa. Aliyekata tamaa yupo tayari kuasi. Maana ni aliyezimia moyo. Wana wa Israel jangwani sio kwamba walitoka Misri na mioyo mibovu, La Hasha! Bali maandiko hutuambia kuwa wakafa moyo kwa sababu ya njia ile! 

Tazama kichofuata! Ni kumlalamikia Musa na Mungu. Na Mungu hakuwaacha hewani bali aliwatumia nyoka wa moyo. Akawapiga kwa pigo lililo kuu mno. Waliotaka kurudi Misri, sio kwamba walikuwa wamejipanga hapo awali kurudi. La, bali ni matokeo ya kuchoka kiroho! Ukisoma kwa utulivu utagundua kuwa mara baada ya habari mbaya walioipata ndipo wazo la kurudi Misri likazaliwa.

Hata katika ile Hesabu 16, utagundua kuwa ule uasi wa Kora ni matokeo pia ya watu kuchoka. Watu kushindwa kumuelewa MUNGU pamoja na Musa wake. Ndio maana wakafikia walipofikia. Kila utakapokutana na malalamiko ya wana wa Israel kule jangwani, tazama mukutadha wake. Utakutana ni wa wao kukata tamaa au kuchoka kiroho. 

Maneno kama vile, je huko Misri hakukuwa na makaburi ndiposa ukatuleta huku jangwani ili tuje kufia huku au yale  tumeyakumbuka masufuria ya nyama, matango na vitungu vya Misri ni matokeo ya hali kama hii. 

Hata yale maneno ya Musa kwenye Hesabu 11 dhidi ya Mungu ni matokeo ya hali kama hii. Sijui hadi sasa umeshajifunza nini? 

Ni kwamba kila penye kuchoka kiroho, au kulemewa na mzigo; kuna mbegu ya uasi huwa inanuiwa kupandwa na adui Shetani. Wasomaji wa vitabu tajwa hapo juu wananielewa nilichokigusia hapo. 

Kwa hiyo, tunapewa fikra za kuwa makini sana, dhidi ya maamuzi yetu pindi tunapokuwa kwenye hali nhumu.

Ninakumbuka maneno ya Mtumishi wa Mungu Mwalimu Christopher Mwakasege kipindi cha msiba wa muimbaji Sedekia kuwa; "Mungu ni Mungu hata kama hajajibu maombi yako." Mungu kutokujibu kama ulivyoomba hakumfanyi kutokuendele kuwa Mungu. 

Mtumishi huyu katika mazungumzo yake na mimi hapo jana ya leo ya uanzaji wa uandishi wa kitabu hiki alinijulisha mambo kadhaa. Ya kwanza ni hili, ni katika mfano wa MWINJILISTI MWENYE MKE MLEVI. Aliniambia kuwa, kulikuwa na Mwinjilisti mmoja ambaye Mungu alimtumia katika viwango vikubwa sana vya kiroho. Alifanya miujiza na maajabu katika uweza wa Kiungu.

Ila alikuwa na mke mlevi. Aliliombea jaribu hilo kwa muda wa kutosha. Siku moja akiwa sasa katika hali ya kuchoka na kufa moyo, akamwambia Mungu nakupa siku 30, usipojibu ....kitatokea... Akiazimia kuwa mlevi kama mkewe. 

Aliingia kwenye maombi ya hizo siku 30, hadi siku ya mwisho Mungu hakuwa amemjibu. Kilichofuata ni yeye kumwambia mkewe, leo twende wote. Mke akashituka na kuanza kuuliza wapi? Akamjibu huko unakokendaga. Akimaanisha baa, mke akamwambia mtumishi wa Mungu kama wewe hutakiwi kwenda.

Hatimaye akaenda, alipofika akajionea jinsi watu wanavyomnunulia pombe mke wake nakumfanyia yasiyofaa, ndipo uzalendo ukamshinda kama wasemavyo vijana akajikuta anapigana. Aliishilia kupigwa na chupa moja na kufa pale pale!

Usiniulize inakuwaje, ila rejea pale kwa awali kuwa Mungu atabakia Mungu hata kama hajibu maombi yako.

Ni rahisi kumcheka, ila elewa tabia ya moyo uliochoka kama nilivyokujulisha hapo awali! Na kama hujawahi pitia hapa uwezi nielewa, mimi nimepitia, ninaelewa kwa haraka na kwa wepesi, ndio maana lile andiko la Zaburi la ya kwamba machozi yamekuwa chakula changu, ...ninaliloanisha godoro kwa kulia kwangu...huwa nalielewa sana.

Jaribu kufikiri, umetoka kwenye mkutano, na maajabu yametendeka, njia nzima unapita ukiwa unaimba pambio la nimeuona mkono wa Bwana, na yamkini na vijana wako kihuduma wamekusindikiza huku mkijawa na sifa tele; kisha unafika nyumbani na kupokelewa na mke akiwa amelewa! Anakupokea na matusi huku akiwa anapepesuka, na yamkini wanaume wamemshikili huku na huku.

 Kwa huku akidondoka mbele yako, huku nawe ukipaswa kumshika mkono umpeleke chumbani. Nguo zimejawa tope unapaswa kuzibadilisha!
Mwenzako alivumilia kwa mida wa kutosha, ikafika mahali akamwambia Mungu, mimi naombea wengine wanapona, ninakuona kwenye mikutano, akafu nakuomba na mke wangu habadiliki! Haiwezekani.

Unaweza kujikuta unaongea kwa ujinga kwa kujisemea kuwa bora mume mlevi kuliko mke mlevi. Rafki, jaribu ni jaribu. Wala usiseme kwamba lakini kulikuwa na neema yake. Kwa hiyo alipaswa kuvumilia. Mbona wewe mkeo ama mumeo sii wala mlevi ni hasira tu au ni udhaifu fulani tu mdogo lakini umekuchosha?
Kwa hiyo kwako hakuna neema kwake ndo kuna neema? "BytheWay"  sio neema inayopita, bali ni wewe. Neema ipo palepale kukusaidia.

 Ndio maana umaskini unahitajika sana. Maana tabia moja wapo ya neema ni wewe kujifunza kunyenyekea kama 1 Petro 5; inavyotufundisha. Na kunyenyekea hapa maana yangu ni wewe kufuata kanuni muhimu za Kiungu dhidi ya hilo pito.

Na kumbuka sana andiko hili; Mithali 24:10 Ukizimia siku ya taabu, Nguvu zako ni chache.
Mwingine, alinipa pia mfano wa MCHUNGAJI MWENYE MKE MZIZI. Aliniambi kuna mchungaji mmoja huko Tanga, ambaye ndiye aliyekuwa mchungaji wake, alikuwa na mke mzizi. Unajua ndugu yangu haya mambo unaweza jikuta unatamka kwa ujinga kuwa atakuwa alikosea kuoa. Hayakuwa mapenzi ya Mungu. Ni rahisi sana kuwaza kwa upumbavu hivyo. Nashawishika kusema kuwa hayajakukuta! Yakikukuta utaelewa kuwa njia za Mungu ni ngumu sana.

Ni kama vile aliliacha ili akiingiza shuleni. Na Mungu akitaka kukufunza, hakuchagulii somo. Kwa maana kwamba hakuonei huruma kwa vile utakavyopitia, anachotazama ni utukufu wa njia ile. Hata kama ni ya aibu. Maana mwisho wa Ayubu ulijawa na shangwe.

Tuendelee na kisa cha MCHUNGAJI MWENYE MKE MZIZI. Mke huyu alikuwa sugu katika hali hii. Unaambiwa mtumishi huyu alikuwa na kipawa cha ajabu sana. Alikuwa na karama ambapo upo Tanga, na yeye yupo Dar es Salam. Ila anakupigia simu na kukwambia acha hiki na hiki. Na ni hali ambayo upo nayo muda huo! Mungu alimtumia  sana. 

Ila kuna wakati anatoka kwenye mkutano, vilema wametembea, na miujiza mingi kutendeka, ila mke wake kazini. Mke huyu pia amemuwekea sumu mara kadhaa, ila mume hakufa. Kuna wakati anakula chakula na akikimaliza ndipo anajulishwa au anafahamu rohoni kuwa kilikuwa na sumu na kuamua kumuliza mkewe. Mke alimjibu kuwa kufa ili niolewe! Najua usipokuwa makini unaweza rusha ngumi.

Baba huyu alivumilia vya kutosha. Ikafika mahali huyu MCHUNGAJI MWENYE MKE MZIZI akasema sasa Mungu inatosha. 
Aliamua kuiacha nyumba, akaondoka kabisa Tanga na kuhamishia makazi yake mkoa mwingine, huku mke wake akiendelea kuwa na wanaume wengine, hadi leo; ila baya kwa mtumishi ni kwamba aliamua kuoa mke mwingine. Alizunguka kwenye mkanisa mbalimbali akitaka kumsaidia kufunga hiyo ndoa yake, ila walimgomea. Akaona isiwe shida, akaamua kuoa kiholela zaidi.

Sasa, kilichomkuta ni kwamba, huku alimkimbia MKE MZIZI, na huko (Shetani alivyomwaminifu katika utendaji wake) akampa mke "Freemason". Uliwahi kukimbia siafu ukakutana na nyoka? Baya zaidi huku neema ya kupita kwenye jaribu ambayo kule ilikwepo huku haipo!

Aliishi naye kwa muda mfupi na baada ya hapo alijikuta wanashindwana. Akaona isiwe taabu, akaamua kuingia mahusiano mengine.
Sasa unaweza kunielewa kuwa moyo unapochoka, Mungu huwa anakuja akiwa na sindano, vidonge, lita ya maji, pamoja na "tripu" ili akutie nguvu kama Elia kwenye 1Wafalme 19 ambapo aliletewa na chakula akala na kisha kutiwa nguvu. Kula na kunywa kulimvusha Elia.
Lakini pia Shetani huja na mbegu ya uasi! Ambapo akipata nafasi huwa anaipanda. Na kuimwagilia kwa haraka sana. 

Sasa, natumai sasa utanielewa kwa haraka ni kwa nini Musa, Haruni kisha na Kalebu na Yoshua waliwaambia au waliwataka wale watu wasimwasi Bwana! Ni kwa sabau walitambua fika katika hali hii, adui  mwake kabeba mbegu ya uasi! Na anataka kuipanda.

Hesabu 14:9 Lakini msimwasi Bwana, wala msiwaogope wale wenyeji wa nchi, maana wao ni chakula kwetu; uvuli uliokuwa juu yao umeondolewa, naye Bwana yu pamoja nasi; msiwaogope.

Mimi sina shida sana na hali ya kuchoka, hali ya kutamani kufa, hali ya kuona ni bora turudi Misri kama hawa watu. Ila kinachonipa shida ni kufikia hatua ya mtu kutokusikia maelekezo au ujumbe wa kunuia kumsaidia napopitia!

Elia alipoambiwa kwanza amka, kisha ule na kunywa, alitii maelekezo. Japo alifikia hatua ya kutaka kufa. Na aliomba hayo maombi. Nakujuza hili ili usiwe mwepesi wa kuwalaumu na kuona watu waliofikia hatua hii ni kama tayati sasa wamekwisha kuasi. 

Narudia tena, kinachonipa shida hapa ni hali ya kugoma kumsikia Mungu anapokujilia ili kukusaidia. Watu hawa ilifikia hatua ya kutamani kuwapiga kwa mawe waliokuwa wakinuia kuwasaidia.

Cha ajabu katika hali hii napo  yupo karibu ili kukusaidia lakini ukigoma hakuna namna utasaidika. Tazama; Hesabu 14:10 Lakini mkutano wote wakaamuru wapigwe kwa mawe. Ndipo utukufu wa Bwana ukaonekana katika hema ya kukutania, mbele ya wana wa Israeli wote.

Kumbuka tena kuwa Mungu ni Mungu hata kama hajajibu maombi yako, akijibu au hata asipojibu, hiyo haimfanyi yeye kutokuwa MUNGU. Yeye ni Mungu sio kwa sababu huwa anajibugi maombi, ni kwa sababu ni Mungu. Lazaro alikuwa mcha Mungu, lakini aliishi na hatimaye kufa maskini. Na bado Mungu alitukuzwa katika hilo. Sina maana kwamba na wewe hali hiyo utadumu nayo mielele la! Ila nataka ujue kuwa Mungu ni Mungu hata kama hujapona, maana hata Elisha alikufa kwa ugonjwa wake.

Ikimaanisha japo alikuwa na upako, na hata mifupa yake kufufua mtu, ila bado alikufa na ugonjwa wake. Paulo anaelezea mwiba wake, na anatupa faida zake, na katika Wagalatia anaeleza jinsi ambavyo watu walitamani hata kung'oa macho yao ili kumsaidia. Ikitupa kufahamu yamkini halikuwa na shida ya macho. 

Usijaribu kuziba masikio unapokuwa umekata yamaa na tayti mkuo wako umekwisha kuazimia kuasi. Bibyi mmoja aksema, Mchungaji, nimesubkri vya kutosha, sasa liwalo na liwe, akija hata evi, au mwisilamu mimi nitaolewa naye. 

Ukianza kumsaidia na kuona moyo haubadiliko, uwe na hakika ameziba masikio. Atukuzwe Mungu wengine tumewasidia na sasa wan watoto.
Ninakumbuka maneno ya wimbo wa Ambwene kuhusu yule mwanamke aliyefiwa na mume wake, kisha watoto wa tano kuwa, "Mwanangu usijaribu kumuacha Mungu hata kama amekuumiza." 

Haijalishi aliyekuumiza au kukujeruhi ni Mungu, ila Mungu ni Mungu. Gharama ya kuamuacha ni kubwa mno. 

Njia ya mwenye haki ni ngumu sana. Kuna watumishi unawaona au kuwasikia leo, na ni msada mkubwa sana kwako, ila hujui walipopita au kutoka. Kadhalika kwako ndivyo ilivyo.

Inuka ule, ukatawale na kumiliki hata milele. Mbingu sio ya walioshindwa, bali ni ya walioshinda.

Kumbuka; Penye kuchoka, adui ana mbegu ya uasi, ukengeufu, na anguko...na Mungu ana sindano ya kukutibu, "bandeji" ya kukufunga majeraha sanjari na mkate kwa maziwa kama ilivyo kitabu hiki ambacho ni mana ya kiroho ili akutie nguvu.

Mwenye maamuzi ni wewe! Kula usonge mbele, au ukwame uishiliye kwenye anguko. 
Nilifika hapa ninaumia sana, napo pananipa kumuheshimu Mungu. Musa alipendwa sana na Mungu, ila alipochoshwa na wana wa Israel kama wewe ulivyochoshwa na huduma au ndoa, alifanya kosa ambalo lilimpelekea kutokuingia Kanani.

Sijui kama wewe umefikia viwanvo vya Musa! Ila kwenye Agano la Kale nje ya Ibrahimu, Musa ni miongoni mwa watumishi waliotembea na Mungu kipekee sana. Hakuna aliyewahi kumuona Mungu kwa aina yake kama Musa. Ila alikwama mahali! 

Tafadhali kitabu kikitoka kitafute:

Kama Hujaokoka, na umesikia ujumbe huu na moyoni mwako kumeingia msukumo wa Mungu wa kutengeneza naye! Nikutie moyo kuitii sauti hiyo. Kwa hiyo kwa imani fuatisha pamoja nami maneno haya;

Sema; EE MUNGU BABA, NINAKUJA KWAKO, NIKIJUA MIMI NI MWENYE DHAMBI, NAKUSIHI UNISAMEHE, NA ULIFUTE JINA LANGU KWENYE KIATABU CHA HUKUMU, NA LIANDIKE SASA KWENYE KITABU CHA UZIMA WA MILELEL.

 Mawasiliano +255759859287 Baruapepe: ukombozigospel@gmail.com 

Jiunge pia na Kundi Letu la Mafundisho ya Neno la Mungu la WhatApp:
 https://chat.whatsapp.com/DHu25ZssUrEDJSzn4Iv2d5

Hapa utapata na Mafundisho ya Mikutano na Semina za Mwl. Telegraph: https://t.me/+fft3GHXC9xIzYjhk

Tazama Channel Yetu ya Youtube, kuba mahubiri pia Subcribe ili uweze kupata matangazo yetu kwa haraka.
https://www.youtube.com/@ukombozigospeltv

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni