Na Mwalimu Oscar Samba
Ujumbe huu ni Sehemu ya #Kitabu Chetu cha CHAKUFANYA UNAPOLEMEWA NA MZIGO MZITO AMBAPO MUNGU, BADO ANATAKA UENDELEE KUUBEBA. Tunaendelea kidogo plae tulipoishia katika Makala iliyopita, kisha ttutatazama jambo la Kwanza; Karibu:
Ikifika mahali ukiona msisitizo uliopo ndani yako sio kumtwisha tu Mungu mzigo wako, sio Mungu tu kukutia nguvu. Bali swali lako ni kwamba sawa nitavumilia, ila Mungu atanijibu lini? Uwe na hakika kuwa unahitaji msaada mkubwa zaidi.
Maana kuna mambo mawili hapo. Mosi ni la kuchoka na pili ni la kuhoji uaminifu wa Mungu kwamo?
Kwamba huna shaka, hata sasa ukimuita akutie nguvu anweza, ila hoja ni kamba huu ni mwaka wa tano sasa, kumi au miaka naho inaenda, unakaribia 40 na hata 50 sasa ila bado hajakutokea. Ndio maana ukinielewa hapa hutaacha kuyaelewa maandiknya Zabuti kuhusu uaminifu. MUNGUkuna.mahali unasoma na unaona jinsi mtunga Zabuti anavyopitia sehemu ngumu, kisha anataja uaminifu wa Mungu.
KANUNI
1. Fahamu ni Kwanini Mungu Anataka Bado Uendelee Kuubeba au Uendelee Kupitia. Waliowahi kusoma kitabu kile cha Isaya 55 utabaini kuwa watu wale kuna namna walikuwa wamepishana na mipango ya Mungu maishani mwao. Ndio maana Mungu anafika hatua ya kuwaambia kuwa mawazo yenu sio mawazo yangu, wala njia zenu sio njia zangu. Anawapa na kipimo husika, kwamba kama vile mbingu zilivyo mbali na aridhi; ndivyo mimi nanyi tunavyopishana.
Najua unajua kuwa Mungu ana akili kuliko wewe. Ufahamu wake ni mkubwa kukuzidi. (Ikupe kujiuliza kwa nini kakuacha.) Na kubwa zaidi ni kwamba anakupenda kuliko unavyo mpenda. Na kile kitabu chetu cha MUONE MUNGU NYUMA YA PITO LAKO kinafunza kiunagaubaga kuhusu kusudi la Mungu kukupitisha hapo.
Nataka kukujulisha nini? Kuna wakati Mungu anatupitisha mahali, akiwa na nia ya kutuepusha na mambo kadha wa kadha. Sasa kama anayotuepusha nayo bado hayajapita, maana yake ni kwamba; tukilazimisha kutoka, hakika tutakuwa tunakimbilia matatizo ambayo Mungu ananuia kutuepushia.
Uliwahi kusikia au kuambiwa na Polisi kuwa ni kweli mtuhumiwa hana kosa au hatia kisheria ila tunamshikilia kwa ajili ya usalama wake!
Polisi wanajua, hana kosa la mauaji. Lakini hataki kumuachia mapema maana hasira ya wananchi ni kali.
Kwa maana kwamba, kuna watu leo wapo kwenye vifungo fulani, au mapito fulani, sio kwamba wamekosea la! Nj kwa sababu adui kama Simba angurumaye bado anazunguzunguka kwenye mji wao ili aweze kummeza.
Hivi unajua kuwa Nuhu alilazimika kukaa kwenye Safina muda mrefu sio kwa sababu mvua inanyesha au bado inaendelea kunyesha bali ni kwa sababu maji hayajakauka? Wasomaji wa kitabu chetu cha NAFASI YA VIUNGO AU MWILI WA MWANADAMU KWA MUNGU, huweza kunielewa kwa haraka zaidi. Nilipofikia eneo la mguu, nilikutaka kutokukanyaga mahali ambapo maji hayajakauka. Maana utazama, ili ukanyage au utoke kwenye Safina, hakikisha kwanza maji yamekauka.
Ni kweli unaona mvua imekoma, hainyeshi tena, ila ukweli ni kwamba aridhi haijakauka. Ndio maana alimtuma kunguru kwanza, naye hakupata pa kutua. Hakuishia hali alimtuma njiwa, naye hakupata pakutua bali alirejea na tawi la mti bichi. Napo akagundua aridhi bado haijakauka. Aliendelea kuwa na subira. Kisha akamtuma tena, ndipo alipoona harudi naye alifahamu kuwa nchi imekwisha kauka sasa ni salama kwake.
Aliamua kutoka kwenye Safina. Kwa hiyo muda aliuokaa humo ilibidi uwe mkubwa sio kwa sababu Nuhu aliyapenda yale mazingira. Sio kwa sababu MUNGU hakutaka kumtoa huko. Sio kwa sababu Safina haikuwa na mlango. Bali ni kwa sababu nchi ilikuwa haijakauka.
Hii ikupe kutokulazimisha kutoka kwenye pito. Hapa unapata pia na somo la Saburi, ikiwa na maana ya uvumilivu ulio na tumaini mbele za Mungu. Sio kuvumilia tu kwa sababu hakuna njia nyingine ya kufanya. Bali ni kuvumilia huku ukijua kuna siku Mungu atafanya.
Ile Mungu anakutaka bado upitie hapo, au ubaki hapo, basi hakikisha na wewe unakubaliana na nia ya Mungu. Uchungu wa maumivu ya jeraha, kulemewa na mzigo au kuchoka kuendelea kusubiri kusije kukufanya kutaka kumlazimisha Mungu au kukubali kukata tamaa.
Unaonaje mtuhumiwa kama huyu ambaye hasira kali ya wanachi ipo juu yake, naye akatamani au kulazimisha kutoka gerezani! Uwe na uhakika kuwa hatabaki salama. Na askari wakimpenda uwe na uhakika watamlinda hata kwa nguvu ili tu asitoroke. Na wewe Mungu anakupenda ndio maana bado anataka uendelee kuubeba huo mzigo.
Unaonaje kama Nuhu angetoroka au angelazimisha kutoka kwenye Safina? Ninachojua ni kwamba hata kunguru hakutolewa mlangoni bali ni dirishani? Hakutaka hata kufungua mlango, na dirisha lenyewe ni lile la juu.
(a) Mungu Anataka Uendelee Kubakia Kwenye Hilo Pito Kwa Saabau Anayajua Mawazo Anayokuwazia. Uwe na hakika kabisa kuwa kuna Mawazo Mungu anakuwazia ambayo ninya amani, ushindi, wala sio ya kukuumiza wala kukuzalilisha kama uwezavyo kuwaza au kufikiri.
Mungu sio adui, wala sio mkatili. Ni sawa na askari aliyekuifadhi kituoni ili usiuawe na maadui wanaowinda uhai wako. Inawezekana kabisa Nuhu alichoshwa na maisha ya kwenye Safina. Maana ni sawa na kukaa ndani bila kutoka nje kwa muda mrefu, jua inabidi utegee dirishani ili uweze kuliota. Uwashaji wa moto ni mgumu maana unaweza unguza Safina.
Chakula unachokula sio "fresh" maana mboga za majani kama unazila basi ni zile zilizokaushwa. Matunda yenyewe hupati. Humo ni fujo tele maana kila mnyama na vurugu na ustaarabu wake.
Furaha ya mbweha, mbwa, fisi na wengineo ni kelele zao. Jogoo hana raha asipowika. Kasuku humo ni kuiga kila sauti hata ile ya fisi na ya komba. Hapakuwa sehemu yenye raha kwake. Ila alilazimika kuhakikisha Tunda la Uvumilivu halipunguki kwake hadi avuke.
Alihakikisha anakuwa na utulivu hadi mazingira yakae sawa. Ukiwa wewe ni Nuhu wa leo, njia pekee ya kisaikolojia hapo sio kukubali kukwazwa na mazingira, bali ni kuhakikisha unayageuza mazingira hayo kuwa kama kituo cha utalii.
Kelele zao hao wanyama zisiwe kero kwako, bali ziwe sehemu ya utalii. Hii itakusaidia sana kuvuka salama. Hakuna kipindi nimeandika vitabu kama hiki cha hili pito langu. Mwaka jana ulikuwa mgumu sana kwangu, kwa matukio makubwa kama mawili hivi. Lakini licha ya kunipatia vitabu tajwa hapo awali pamoja na kile cha VUMILIA WAMJUE MUNGU WAKO, hakuna kipindi nimepiga kazi kwa muda mfupi kama hicho. Ndani ya miezi 7 mikutano kama 23 sio jambo jepesi.
Ukienda mbinguni nenda kamuulize Paulo Mtume jinsi alivyonufaika na kufungwa kwake jela! Utagundua kuwa vitabu kadhaa vilivyoko kwenye Biblia ni matokeo ya kufungwa kwake.
Hapa unapaswa kujifunza kuwa na utulivu unapokuwa jela. Maana hapo napo kuna nyaraka muhimu sana, Waefeso, Wafilipi, Wakolosai na Filomoni vinategemea sana utulivu wako hapo jela. Ukiishilia kuwa malalamikaji uwe na uhakika kuna watu wataingia jela pamoja na wewe japo wapo uraiani.
Kwa maana kwamba kuna watu wanaosubiria nyaraka zako, ambao watakwama kutokana na wewe kukwama. Kuna watu wapo urainani ila kuvuka kwao kunategemea neno lako la faraja lako wewe uliopo jela.
Hukuwai kuwa na shida ya ndoa, alafu ukatumika kuiponya ndoa ya mtu mwingine! Hadi mwenyewe ukawa unashangaa mbona mimi nina tatizo hili na lile lakini watu wanakuja kwangu, kwani hajui yangu imenishinda?
Ni hatati ukagoma kuwasaidia, na utakuwa hujui maana ya wewe kupitia hapo. Pito linaleta upako. Inawezekana huja ielewa, tukutane kwenye kipengele kinachofuata.
(b) Ili Kukupatia Nguvu, Ufahamu na Upako wa Kiroho. Ni hatari kuitoa ndoo boombani ambayo haijaja bado. Njiani utaishiwa maji. Ile Mungu anakupitisha bado, anajua kiwango cha upako, au nguvu unayoihitaji kwa ajili ya safari yako ya mbele.
Elia alipaswa kula kwa kipimo cha Mungu, ili kupata nguvu za kumsaidia kwa safari yake. Alipokula kidogo, aliambia kipimo hiki hakitakufikisha mwisho. Na wewe Mungu ile anataka bado uendelee kukaa hapo, uwe na hakika kuna kitu hakijakamilika bado. Kipimo hakijajaa.
1 Wafalme 19:6 Akatazama, kumbe! Pana mkate umeokwa juu ya makaa, na gudulia la maji, kichwani pake. Akala, akanywa, akajinyosha tena.
7 Malaika wa Bwana akamwendea mara ya pili, akamgusa, akasema, Inuka, ule; maana safari hii ni kubwa mno kwako. (Wengi wanaishia hapa, kwamba "nimevumilia vya kutosha, sasa Bwana nitoe.." Mungu akikuangalia anajisemea, inuka ule tena akijua kiwango cha upako ulionao kitaponya tu vipofu 10 na kumbe mbele yako wapo 17, kwa hiyo saba watasalia na shida zao.
1 Wafalme 19:8 Akainuka, akala, akanywa, akaenda katika nguvu za chakula hicho siku arobaini mchana na usiku hata akafika Horebu, mlima wa Mungu.
Pito ni chakula cha nafsi na roho. Najua mwili wako utapiga makelele maana unateseka ndio maana unahiji kutoka hapo.
(c) ...
(d) Anakupenda....
Na Yamkini haujaokoka, nawe umeguswa na ujumbe huu na unatamani kuokoka (kumbuka wokovu maana yake ni kumkataa Shetani na mateso yake, dhambi na taabu zake na kumkubali Yesu na Uzima ama mbingu)...
Kama ndivyo basi nikutie moyo kufuatisha Sala hii ya Toba kwa imani, Sema;
EWE MUNGU BABA, MIMI NI MWENYE DHAMBI, NIMEGUNDUA MAKOSA YANGU, NISAMEHE YESU, FUTA MAJINA YANGU KWENYE KITABU CHA HUKUMU, NIANDIKE KWENYE KITABU CHA UZIMA WA MILELE, Amen.
Hongera kwa Kuokoka na tafadhali tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo, Ameni.
... Zaidi tembelea
www.ukombozigospel.blogspot.com
Tazama na Sikiliza Mahubiri na Mafundisho Yetu hapa, Usisahau Ku-Subcribe ili uyapate kwa haraka zaidi; https://www.youtube.com/@ukombozigospeltv
Jiunge nasi pia kwenye WhatsApp group letu la mafundisho ya neno la hapa: https://chat.whatsapp.com/E0eD0xegh1eIGMjRykPyRD
Kundi letu la Telegram https://t.me/+fft3GHXC9xIzYjhk (Hapa utapata Mahubiri/Mafundisho Yetu kwa Haraka)
Namba ya Telegram au Mawasiliano: +255759859287 inatumika pia kwenye WhatsApp na M-Pesa. Ukiguswa kuachilia Sadaka yako tafadhali usisite kufanya hivyo. Jina ni Oscar Samba.
Usisite Kututembelea pia kwenye Ukurasa (Page) wa Facebook na "Ku-like" https://www.facebook.com/MafundishoyanenolaMungunamwalimuoscarsamba?mibextid=ZbWKwL
Ama tuandikie email (Baruapepe) ukombozigospel.@gmail.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni