Na Mwalimu
Oscar Samba
Utangulizi
Ninamshukuru
Mungu kwa kibali na upendeleo alionipa kuhusu kitabu hiki, ni kweli nimeandika
vitabu vingi ila hiki kinaupekee wa aina yake! Vipo vingi kweli vyenye kutia
moyo watu, ila hiki nacho kina kitu chake cha upekee.
Kitabu hiki
kinaitwa USIZIKE NDOTO ZAKO, haikuwa jambo la akili zangu kukipata, nilikuwa
najisomea darasani muda wa usiku, na ghafula nikasikia Roho Mtakatifu anaugua,
nilijitahidi kuhakikisha kuwa ninamaliza kwa haraka ratiba yangu ya kuhakikisha
nasoma biblia kabla ya kwenda kulala maana niligundua moyoni kuwa muda wangu wa
kukaaa darasani umeniishia!
Lakini haikuwa
rahisis kukubaliana na wazo hili la Roho Mtakatifu maaana nilitakiwa au
nilihitajika kusoma zaidi kwa mujibu wa ratiba yangu, natumai ndio maana
aliamua kutumia njia ya kuugua ili kunishindikiza!
Wakati nikiwa
natoka kujisomea saa naenda bwenini kulala, naliwaona wanfunzi wenzangu
wakijifanyia mazoezi ya kuhubiri, ghafula nikapata wazo la kuungana nao,
nilijitahidi kulitii maana ni wa darasa jingine, na ngazi ya chini kidogo
kitaaluma, kwa hiyo nilijitia moyo kuwa yamkini nikapata kibali kwao,
walinipokea na kujiungana nao, kisha alisimama Mchungaji mwanafunzi mmoja
aitwae Ben, na kuhubiri ujumbe huu!
Moja kwa
moja, nilifahamu moyoni mwangu kuwa ndicho ambacho Mungu alinuia nikipate,
kwanza kutokana na mahali nilipokuwa ninapapitia, pili niligundua moyoni
mwangu! Ujumbe huu nimepewa niuendeleze kama kitabu!
Maana alipoutaja
tu, nilipewa picha nzima ya anapoelekea na kuanza kufunuliwa kana kwamba
nilikwepo naye wakati anauandaa, alipomtaja mwanamke husika nilipewa picha yote
kabla ya kudadavua zaidi!
Nilimshukuru
Mungu na kuanza kukimungunya kitabu hiki nafsini mwangu (moyoni) mwangu!
Kwa hiyo kitabu
hiki kimenuia kukutia moyo, kwa njia ya kimaarifa, ambayo yanakutaka
kutokufanya makosa au maamuzi ambayo moja kwa moja yatazika ndoto, mipango,
maono, au mambo uliyonuia kuyafanya au mahali ulipotaka ama unapotamani
kupafikia!
Msingi mkubwa
wa kitabu hiki upo katika kisa kile cha mwanamke yule tajiri wa Shunami, mama
huyu alikuwa hana mwana, na alipopata mwana alifariki, lakini mtoto alipofariki
hakumzika, bali alimwendea Elisha, na wewe yamkini ndoto zako zimekufa, kuna
jambo ambalo umeliona haliwezekani, usikubali kukata tamaa bali muendee Yesu!
Kuna makosa
kadhaa ambayo wengi huyafanya hususani tunapokutwa na tatizo, badala ya
kuchukuwa hatua ya kuliponya, au kulihuisha moja kwa moja huenda kulizika!
Sijui kama
huwa unajifunza kwa mwanmke yule mjane wa mji wa Naini, kuwa mwana wake
alipofariki moja kwa moja alichukuwa hatua za mazishi kama watu wengine! Ila ashukuriwe
Mungu alimuonea huruma na kuzua kuzikwa kwa mtoto!
Sasa usiniulize
mimi ujumbe huu ulipotolewa ulinisaidiaje kutokuzikwa kwa jambo fulani maishani
mwangu ila hapa jitazame wewe maana ya mkini upo kwenye msafara wa mazishi ya
ndoto yako ya kutaka kuja kuwa mwalimu kisa tu umefeli mtihani wa kidato cha
nne, mwingine amejikatia tamaa na kuona kuwa hawezi tena kuwa dakitari kisa na
mkasa ni mara baada ya yeye kushindwa kupata ada ya masomo, wapo walioacha
kabisa ama kufikiri hata kufanya hivyo maana ndoto yao ya kuwa mfanya biashara
aliyefanikiwa ni kama vile haiwezekani tena kwa sababu tu ya hali ya uchumi
kuwa ngumu, na sasa wapo kenye maandalizi ya mazishi ya ndoto zao kama yule mjane
wa mji wa Naini!
Mpendwa! Ingekuwa
hivyo, basi Mungu asingekuwa ni Mungu wa utukufu! Ili atukuzwe ni lazima kuwe
na bahari ya Shamu mbele, na nyuma kuwe na jeshi kubwa la Misri, alafu akiigawa
bahari ya Shamu utukufu uje kwake! Kufa kwa mtoto sio mwisho wa maisha ya mototo!
Inawezekana ndio mwanzo mpya wa maisha yake!
Ni kwamba
Shetani anaweza kuua ndoto, ila wewe ukamsaidia kuizika! Ndoto inaweza kuzimia
lakini wewe ukaisaidia kuimalizia kabisa, na huu ni ukatili mbaya sana ni sawa
na madakitari wanao wadunga wagonjwa sindano za vifo eti kwa kuwahurumia maana
wameteseka sana!
Tutakapokuwa
tukianza uchambuzi wa kisa hiki, utajionea mambo kadhaa ambayo huyu mwanamke
aliyafanya, kwani wengine wangepiga ukunga na kuanza kuandaa mipango ya
mazishi!
Ni sawa na yule
ambaye aliyekosa ada na kuamua kuondoka chuoni mwenyewe bila hata kufukuzwa na
mwalimu husika, na kukata tamaa kabisa na elimu! Ni sawa na mchungaji
aliyekimbia eneo la huduma kisa ni ligumu kiroho, bila kujua kuwa penye mwamba
ndipo Musa alipoamriwa apapige ili maji ya toke! Na hakuna dhahabu
inayochimbuliwa vumbini, bali ni mchangani!
Huduma ikiwa
ngumu, na washirika wote kukukimbia, na kufikia hatua hadi mwenzi wako wa ndoa
kuwa kizuizi, wewe nawe usianze kuisema vibaya, huko ni kuimalizia, kwa maana
kwamba yamkini imezimia sasa kwa maneno yako ni kwamba unaiua!
Na usifikie hatua
pa kuanza kuwa na mipango ya kukimbia, au kuondoka, maana huko ni kumpangia
marehemu mipango ya kumzika, wewe kata rufaa mbele za Mungu, maana kama mifupa
mikavu iliweza kuishi uwe na hakika kuwa huduma yako yaweza fufuka, la muhimu
wewe usiizike ndoto yako, maana ni kweli adui anaweza kuiuwa, ila jambo la
kuzika ni lako, ajali ya barabarani inaweza kuondoa uhai wa mpendwa wako sawa,
ila swala la kuzika ni lako! Sio la ugonjwa wa malaria, au ebola, ama ugonjwa fulani,
bali wazikao ni wanadamu, kwa hiyo usiruhusu na wengine kukuhubiria kushindwa
maana hao ndio wachonga majeneza ama wachimba kaburi wa ndoto zako!
Ukija katika
kitabu kile cha Ezekieli 37, kuna jambo muhimu sana pale najifunza, “Nanyi
mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapoyafunua makaburi yenu, na kuwatoa
ninyi katika makaburi yenu, enyi watu wangu.”
Anazungumza
na watu wake! Lakini wapo makaburini! Sasa hawa sio marehemu kwa jinsi ya
kawaida, maana huwezi kuongea na waliokufa, ninachotaka ukione hapa ni hii
picha ya kiroho kwamba kuna namna matumaini yalikauka ndani yao, kuna namna
waliishiwa kabisa muono wa mbele, sasa na Mungu ananuia kuwatoa kwenye
makaburi, ambayo yalizika ndoto zao! Ni kweli maisha waliyokuwa wakiyaishi yalisadifu
hayo kutokana na ugumu wake maana walimuasi Mungu, ila la muhimu hapa ni wewe
kufahamu kuwa haijalishi upo katika wakati mgumu kiasi gani, ni chini ya adhabu
ya Kiungu, au ni mapito, juwa tu kwamba hutakiwi kuzika ndoto yako, na kama ilishazikwa,
usiwe na shaka; mifupa mikavu ya elimu yako, utumishi wako, ndoa yako, biashra
yako ni lazima vifufuke.
Kwa
hiyo ninawiwa kukukaribisha katika kitabu hiki ambacho kinanuia kukujengea ulinzi
maalumu kimaarifa, ambao utakusaidia kutokuchukuwa maamuzi mabovu, ama ambayo
siyo sahihi punde unapokuwa katika hali ngumu! Elia aliwahi kupitia hapo! Na kufikia
hatua ya kutamani kuzika ndoto zake za utumishi! Alimwambia Mungu amuuwe! Sasa nawe
usifike hapo! Nafasi bado unayo, yakikushinda wewe; wewe yaache msalabani! Karibu:
Kwa hiyo
kitabu kikitoka tafadhali kitafute, na tunavyo vingi vya kutia moyo, pamoja na
vile vyenye kukuwezesha kutimiza ndoto zako, vya kukuza kiroho na kadhalika:
Lakini mpendwa
kuna jambo muhimu sana nataka ulifahamu, sijui kama umeokoka, kama la, nakutia
moyo kuhakikisha ya kwamba unamruhusu Yesu leo aingie katika maisha yako,
kuokoka sio habari ya dini mpya, ni Yesu kuingia ndani yako, na kukuwezesha
kuishi maisha matakatifu, ili ukifa uwe na hakika ya kwenda mbinguni, nje ya
wokovu ni jehanum ya moto milele, moto uunguzao na kuchoma, maandiko husema
kutakuwa na kilio na kusaga meno, jaribu kufikiri hayo ni maumivu makubwa kiasi
gani!
Ila waliookoka
wataishi na Mungu milele, wataishi naye na kukaa naye karibu, watakula raha za
mbinguni! Sasa amuoa leo, wala usiseme kesho! Mapito na maisha ya hapa duniani
ni ya muda mfupi sana, huna uwakika na hiyo kesho au wewe usemaye kuwa ipo
siku, hujui ni lini, fikiri ni wangapi waliopanga kuwepo leo ila hatunao tena! Ni
wangapi ambao hukutarajia kuwa kama wangekufa mapema lakini hatuko nao tena!
Yesu anakupenda, namuona akibisha katika mlango wa moyo wako, ili aingia wewe
sasa mpe nafasi! Anakuita kwa huruma, yu tayari kuikupa faraja ya milele,
kukuponya majeraha ya moyo wako! mruhusu awe Baba yako sasa ili akusaidie
katika mambo ambayo ni magumu kwako, yamkini ni uchumi, fedha, hazipatikani,
unazingirwa na nuksi na mikosi, kila unalofanya haliendi, unakabwa na mapepo, !
Wewe njoo kwa Yesu na hayo yote yatapita kabisa !
Sasa natumi u tayari!
Sema; MUNGU
BABA, NINAKUPENDA, ASANTE KWA KUNIPENDA KWANZA, LEO NIMETAMBUA KUWA MIMI NI
MWENYE DHAMBI, NA NIPO TAYARI KUOKOOKA, TAFADHALI INGIA NDANI YANGU, SAMEHE
DHAMBI ZANGU, NA FUTA JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKU, NA ULIANDIKE SASA
KATIKA KITABU CHA UZIMA WA MILELE, Ameni.
Kwa kufanya
hiyo umekwisha kuokoka sasa, na tafadhali tafuta kanisa la watu waliokoka
lililopo karibu nawe ukasali, hapo, waambie kuwa umeokoa hivi karibuni, ili
wakulee vyema kiroho.
Mawasiliano
yetu, kwa M-Pesa au Simu: +255 759 859 287, barua pepe:
ukombozigospel@gmail.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni