Alhamisi, 25 Juni 2020

UWE HODARI, SHUJAA NA MOYO MKUU.



Na Mwalimu Osacar Samba
Kuna kipindi nilipitia mahali pa gumu sana, na kutamani kufa, ama kujiua, ilifika mahali nikiwa napita mjini nilitamani kujirusha mbele ya gari ili nife! Moyo wangu ulipoteza matumaini kwa kiwango kikubwa sana! Ila kila nikitaka kufanya hivyo mbele yangu kwenye ulimwengu wa roho na kwenye mawazo yangu au nafsini mwangu nilikuwa nikiletewa picha ya watu ambao wamekwama mahali na kisha sauti kuniambia kuwa hao watu wananitegemea au wananingojea mimi! Nikikwama na wao watakwama!

Wakati namsimulia mshirika au kijana wangu mmoja aliniambia kuwa, “sasa mchungaji hauoni kuwa hao watu ndio mimi! Kama ungejiua leo ningepata wapi huu msaada!” nilifikiri kwa kina na kulitia jambo lile moyoni mwangu!


Sasa leo asubuhi (siku ya mwanzo ya uandishi) nikiwa hapa darasani, wakati naongoza maombi nilisukumwa kusoma andiko la kitabu cha Yoshua, 1:6-8; ambapo Roho alinifunza kitu kigumu kiidogo, kwamba ni Yoshua ndiye aliyepewa jukumu la kuhakikisha wana wa Israeli wanavuka salama!

Jumamosi, 20 Juni 2020

Usizike Ndoto Zako.



Na Mwalimu Oscar Samba
Utangulizi
Ninamshukuru Mungu kwa kibali na upendeleo alionipa kuhusu kitabu hiki, ni kweli nimeandika vitabu vingi ila hiki kinaupekee wa aina yake! Vipo vingi kweli vyenye kutia moyo watu, ila hiki nacho kina kitu chake cha upekee.

Kitabu hiki kinaitwa USIZIKE NDOTO ZAKO, haikuwa jambo la akili zangu kukipata, nilikuwa najisomea darasani muda wa usiku, na ghafula nikasikia Roho Mtakatifu anaugua, nilijitahidi kuhakikisha kuwa ninamaliza kwa haraka ratiba yangu ya kuhakikisha nasoma biblia kabla ya kwenda kulala maana niligundua moyoni kuwa muda wangu wa kukaaa darasani umeniishia!

Lakini haikuwa rahisis kukubaliana na wazo hili la Roho Mtakatifu maaana nilitakiwa au nilihitajika kusoma zaidi kwa mujibu wa ratiba yangu, natumai ndio maana aliamua kutumia njia ya kuugua ili kunishindikiza!

Alhamisi, 4 Juni 2020

NGUVU YA MAOMBI YA KUOMBA BILA KUKOMA


Na Mwalimu Oscar Samba:
“Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa.” Luka 18:1.
Nina kusalimu ndugu yangu kupitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo! Ni yangu matumaini ya kuwa u mzima tena buheri wa afya tele, na kama sivyo basi Bwana wetu Yesu Kristo aipatie nafsi yako amani, na faraja tele. Na kama ni uponyaji au haja fulani, ipokee kwa imani sasa!
Siku ya leo hapa mtandaoni nimekuandalia ujumbe huu muhimu sana, wenye mukutadha ama sura ya kukutaka kuona umuhimu wa maombi ya nayoombwa bila kukoma, au kukata tamaa!