Jumatano, 30 Oktoba 2019

NGUVU YA KUWA NA UTULIVU MOYONI UNAPOKUWA KATIKA MAZINGIRA MAGUMU.

Ujumbe huu ni sehemu ya kitabu chetu cha Mungu yu Pamoja Nawe, pwenti ya nne, karibu: Na Mwalimu Oscar Samba.
4. Uwe na Utulivu Nafsini Mwako, kukosa utulivu maana yake ni kuwa na mahangaiko moyoni, ni kuwa na wasiwasi au mashaka, ni hali ya kujisumbukia au kuhaha.

Hali hii ni mlango wa dhambi, maana ni adui wa imani, humuondolea mtu uwezo wa kumtegemea Bwana, maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari liwezalo kupelekwa huku na kule na upepo !

Kukosa utulivu ni kukosa raha, ni kupungukiwa kwa kiasi kikubwa na amani, ambayo hiyo amani ni njia ya Mungu kuongea, maana maandiko husema kuwa na amani ya Kristo iamuwe mioyoni mwenu, kwa hiyo hayo mazingira humzuilia Mungu kuamua ndani yako, lakini pia amani ni njia ya Mungu kukuongoza, sasa ikipotea maana yake hutaiona njia, ndio maana dalili kubwa ya mtu aliyekosa utulivu na matokeo yake ni kuwa kama mtu aliyeko njia panda asiyejua njia ya kuiendea !

Jumatatu, 14 Oktoba 2019

HISTORIA YA WOKOVU, AMA SIMULIZI ya Uamsho wa MASAMA MUDIO. Sehemu ya 6, Zamani Enzi za Askofu Imanueli Lazaro

Utapatapia Unabii wa Askofu kuhusu kufa kwa zao la Kawaha, na Pigo kwa Uchumi wa wanaume na kuhamia kwa Wanawake.
.
Kulia ni Mwandishi wa Makala hii Mwalimu Oscar Samba akiwa na Msimulizi wetu Mch. Theofilo
Inasimuliwa na Mzee na Mchungaji Mstaafu wa TAG huko Masama, THEOFILO BARTOMAYO KIMARO, huyu ni pacha au ndugu na Mchungaji Wilsoni Kimaro.
Tuanze simulizi yetu; Niliokoka mwaka wa 1962 January na Mungu kuniita mwaka huo huo, niliunganika na kanisa huko Mbuguni, ambako kanisa nililikuwa halijaanza huko, (la wokovu) nilipokoka tukaanza kushuhudia nyumba kwa nyumba kama vijana.

Nakumbuka kuna mama mmoja kipindi hicho alishikwa na kansa, huyu mama sikuwahi kumuona kanisani maana alikuwa mgonjwa na alikuwa amekonda sana,

Jumatano, 2 Oktoba 2019

UJUZO WA HISTORIA YA UAMSHO WA MASAMA KAMA INAVYOSIMULIWA NA Afuraeli Munisi, Sehemu ya 5.

Anasema kuwa sio kwamba kanisa la TAG lilianzia hapa, lilikuwa limeshaanza huko Mbea hapa lilifika huo mwaka 1959, walianza kuokoka huko ni Askofu Lazaro na Jakobo Ringo ni mpare kutoka Same, walikutana na Askofu huko Arusha na mmeshenari Paulo Brutoni. ( Kama tulivyojionea hapo awali !)

Sikumbuki tarehe wala mwezi ila ni mwaka huo baada ya wao kuanza kushuhudia huko Arusha kidogo,hapo awali alikuwa ni mshirika wa KKT, na mama yake na baba yake pia, baba alikuwa ni mzee wa kanisa mtunza hazina wa hiyo dini, anaendelea kusimulia Mzee Munisi ! ( Ambae kwa sasa ni mzee wa miaka 83 na mke wake ni 72, aitwae Anarabi Afuraeli Munisi, ambao kwa kweli wamezeeka na mzee hapa huongea kwa utulivu maana pia sio buheri sana wa afya.)
Tunaendelea !


Walipokuja ndo walikuja