Jumatatu, 12 Februari 2024

Ni Sehemu ya Kitabu Chetu Tarajiwa cha IMANI SAHIHI, Katika Mada ya Misingi na Tabia za Imani Sahihi.

 


Mwalimu Oscar:

Mwl OSCAR SAMBA ( #NasahazaMwlOscar )
#FaidayaJaribu: #Usiogope
 Lengo la kitabu hiki ni kukuwezesha kuijua au kuitambua imani ya kweli, na kuzifahamu hila za adui Shetani katika imani potofu; ikiwemo namna ya kuzitofautisha na ile ya kweli na jinsi ya kuzishinda.

Misingi na Tabia za Imani Sahihi
Maana ya Imani. Katika Biblia na hata maisha yetu ya kawaida, neno imani limegawanyika katika maana zaidi ya moja, na huweza kuwa na maana kuu mbili. Mosi ni ile imani kama kuwa na hakika ya jambo unalolitarajia ambalo bado hujalipata ama kuliona ila unamatumaini nalo. Waebrania 11:1 Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
Unganisha na hili andiko; Warumi 8:24 Kwa maana tuliokolewa kwa taraja; lakini kitu kilichotarajiwa kikionekana, hakuna taraja tena. Kwa maana ni nani anayekitarajia kile akionacho?

Maana ya Pili ya Neno Imani: Ni mfumo au "settings" ya mambo muhimu yenye kunuia kuunda aina fulani ya njia ya mtu; kimtazamo, fikra na hatimaye kimatendo, (kiimani "faith:") yenye kufuma namna ya kuabudu kwake, kusali, miiko fulani na maadili muhimu ya kuishi hapa ulimwenguni; sanjari na nini kitatokea kama miiko au maadili hayo yatavunjwa au kuheshimiwa: yaani adhabu na dhawabu kwa maisha ya sasa na baada ya kifo. (Imani nyingi zina hatima fulani au maisha fulani baaada ya kifo, ambayo hutokana na jinsi muhusika alivyoishi humu ulimwenguni.)
Kwa ujumla imani au "belief" tuna weza kuiita ni dini. Neno dini kiswahili ni neno la Kiarabu lenye maana ya njia. Kwa hiyo ni njia inayosadikika (neno kusadikika limewekwa ili kujumuisha imani mbalimbali) kumuamini Mwenyezi Mungu, pamoja na kutembea katika njia zake.

Mfano wa imani au dini hizi ni Uislamu, dini zenye kuabudu mizimu au zile za asili kwa baadhi ya jamii, Ukristo katika Wokovu (Wapentekoste), Ukristo katika Romani Catholic, Ukristo katika Usabato, Ukristo katika Lutheran, Ukristo katika Anglikana, na Ukristo katika madhehebu mbalimbali. Pia kumeibuka kundi jingine ambalo leo hii baadhi ya Wanatheolojia huliita "New Pentecostal Group." Yaani kundi jipya la kipentekoste. Hawa ndio wale ambao wamekuja na mifumo mipya ya ibada ikiwemo matumizi ya chumvi, maji, mafuta, na kadhalika. Japo nami binafsi jina hilo sikubaliani nalo maana hatuna upentekoste mpya, kwani kama kuna mpya basi wazamani u wapi?
Nakundi hili halikubali kuwa wa zamani maana hao ndio halisi. Labla liitwe chipukizi jipya la kipentekoste.
Hapo juu nilipoorodhesha hizo dini, hususani katika eneo la Kikristo, kama dhehebu lako halijatajwa usikwazike, na utajaji huo ni kwa mujibu wa uchambuzi wangu. Japo ndio ulio sahihi, maana huwezi kuutaja Ukristo kama dini kwa sura ya kutaka madhehebu yote yanayotumia Biblia yawe ni njia moja la! Maana humo ndani kiuhalisia njia zao zinatofautiana sana. Wapo wanaokubaliana na kufanana kwa sehemu, hao huweza kukaa kundi moja. Lakini la muhimu la kufahamu ni kwamba Yesu hakuanzisha dini bali alianzisha Ukristo. Na mkristo siye yule wenye jina la Kikristo kwa jinsi ya mwilini au kujulikana kwake, wala anayeshiriki ibada katika kanisa linalojulikana linatumia Biblia, bali ni yule ambaye anamuamini YESU Kristo na kuyaishi maisha yake. Yaani ni mfuasi wa Kristo Yesu. Hapa wokovu haukwepeki.

Maana ya Misingi
Msingi maana yake ni mambo muhimu au vitu muhimu vinavyotoa sababu ya uwepo wa kitu, au vinavyoshikilia maisha ya kitu ama vinavyobeba uimara au uwepo wake. Nyumba ya nguzo nne ukiondoa moja ni umedhuru uimara wa uwepo wake. Nyumba ukigusa msingi wake kwa kudhuru mawe ya msingi ni umetishia uhai au uimara wake.

Taasisi yenye malengo matano, ukigusa moja ni umedhuru sababu za uanzishwaji wake. Kiini cha uwepo wake.
Alikadhalika katika imani yoyote ile kuna mambo muhimu yanayotoa sababu za udhabiti wake. Kwenye Ukristo ule halisia ulioasisiwa na Yesu Kristo kuna mambo muhimu yanayoitwa msingi. Ni misingi ya imani hii ya wokovu.

Mfano katika Uislamu kuna nguzo kuu 5, hizo huufanya Uislamu uwe Uislamu. Ikiwemo zaka, kuhiji Maka, Mfungo kipindi cha mwezi Ramadhani na kadhalika. Kwetu Wokovu, Ubatizo, Uungu wa Yesu Kristo, Biblia kuwa ni Neno la Mungu, Yesu ni Mwana wa Mungu, Kujazwa Roho Mtakatifu ni miongoni mwa Misingi muhimu.
Nasi kuna mambo muhimu ukiyaona unafahamu fika hii ni imani sahihi ya Kipentekoste au wokovu. Ndiyo imani ambayo Biblia inamaanisha inapofika swala la kumuabudu Mungu katika Roho na Kweli.

Tafadhaali funga mkanda sasa maana kama ni ndege inakaribia kuanza kupaa, kqmq ni "Bus" basi safari ndo inaanza. Tunaanza sasa uchqmbuzi wa kitabu chetu, tuanze na Imani katika mada hii ya kwanza, na kisha Misingi.
1. Imani Katika Utatu Mtakatifu
2.
3.


Dalili na Tabia, au Viashiria vya Imani Potofu
Namna ya Kujiepusha na Imani Potofu

. Ombea Macho Yako ya  Ndani....yatiwe nuru
Kitabu kikitoka Kitafute
http://www.ukombozigospel.blogspot.com
Tumeunda Channel ya WhatApp, Tufolo; https://whatsapp.com/channel/0029Va827LBJENy9u6Enke1h
Kundi letu la WhatsApp https://chat.whatsapp.com/E0eD0xegh1eIGMjRykPyRD
Telegram https://t.me/+fft3GHXC9xIzYjhk
Subscribe YouTube yetu: https://www.youtube.com/@ukombozigospeltv
Kwa Maombi +255759859287
Usiache Kutembelea na Ku-Like Page Yetu Ya Mafundisho ya Neno la Mungu Facebook: https://www.facebook.com/MafundishoyanenolaMungunamwalimuoscarsamba?mibextid=ZbWKwL

Nikutakie Siku Njema

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni