Alhamisi, 20 Aprili 2023

Jana tulianza Mkutano wetu hapa KWA TOKORA katika Kijiji cha MACHAME ALENI Keni Rombo Kilimanjaro Tanzania

 Umenza tarehe 19 hadi 23 (jumatano hadi jumapili) 2023


Ujumbe: UFALME WA MBINGUNI UMEKARBIA. Mathayo 3:2


Hivi Ndivyo Tulivyoitimisha Mkutano wa Injili Katika Zahanati ya Mokala Rombo Klimamnjaro Tarehe 12 hadi 16 Aprili Mwaka 2023

 Ujumbe wa Mkutano huu ulikuwa ni UPENDO WA MUNGU KWA MWANADAMU 

Tukuongozwa na Andiko la Yohana 3:16.

Tazama Baadhi ya Picha za Matukio

Picha hii na Zifanazo na hii ni Watu Waliotoka kwa Ajili ya Kuokoka na Maombezi




Picha hii na hiyo tangulizi hapo juu ni Waimbaji wakiimba Wimbo wa Kichaga na Kucheza "Iriingi".

Naomba NiRepost NDOA NI ZAIDI YA UPENDO

Naomba NiRepost

#VIJANA_NISIKILIZENI_Haya_Nayo_Ni_Maneno_ya_Mwenye_Hekima


Moyo Unaweza Kumpenda Mtu Bila Kuwa na Sababu Yoyote ya Msingi ila Usikubali Kuoana na Mtu Asiyetosheleza Vigezo Vya Ndoa kwa Viwango Fulani.



Moyo wa mwanadamu kuna muda unavutiwa na mtu bila hata kukupa sababu zenye mashiko kwanini umempenda. Utamsikia mtu akisema basi nimepanda tu! Ni kweli ni jambo jema, na hatuwezi kuweka sababu kwa kila mtu au maamuzi ya moyo kupenda.

Ndiposa wengine wakasema mapenzi ni upofu, ikiwa na maana kwamba kuna mambo ya msingi mtu anaweza  kuya_overloock ama kuyapuuza ifikapo swala la kupenda. Hapa napo sina shinda napo.


Ila msemo huu ndio unaonipa shida; kipendacho roho hula nyama mbichi! Ndugu yangu, nyama mbichi huvimbisha matumbo, huleta kuharisha sanjari na hatari ya magonjwa ya minyoo.