Alhamisi, 24 Novemba 2022

Utangulizi wa #Kitabu chetu cha VUMILIA WAMJUE MUNGU WAKO

Na Mwalimu Oscar Samba

Utangulizi

Hakuna eneo muhinu linalompatia Mungu utukufu kama matokeo ya wewe kushinda vita. Jaribu kufikiria Mungu angejisikiaje kama ujasiri huu aliokuwa nao kuhusu Ayubu kama usingalitimia! Ayubu 2:3 Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu?

 Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu; naye hata sasa anashikamana na utimilifu wake, ujapokuwa ulinichochea juu yake, ili nimwangamize pasipokuwa na sababu.

Najitoa moyo kurudia tena sifa tajwa hapo juu; na miongoni mwa maneno yaliyonigusa kiupekee nje ya hizo sifa ni hili hapa: ambapo nakiri kiuhakik kwamba japo nimekuwa nikikisoma kitabu hiki mara kwa mara lakini bado sikuwahi kukutana na jambo hili katika sura hii. Ya kwamba Shetani kumbe aliwahi kujaribu kumshawishi Mungu amuangamize Ayubu! Ona hili katika kipengele cha mwisho cha hilo andiko hapo juu; "...ujapokuwa ulinichochea juu yake, ili nimwangamize pasipokuwa na sababu."

Sasa katika mtu kama huyu, jaribu kufikiria mbinguni kungekuwa na msiba mkubwa kiasi gani kama Ayubu angemuangusha Mungu kwenye jaribu au pito lake? Shetani hapana shaka angalimrejelea Mungu na kumwambia kwamba ni bora tu ungalimwangamiza mapema kama nilivyokushauri pale awali.

Uvumilivu wa Ayubu ulimpatia Mungu heshima. Na wewe kuvumilia kwako kutakupatia heshima vivyo. Hakikisha unavumilia, ili Mungu aweze kukushindia pia. Usikubali kukwama kwenye pito lako, bali hakikisha unavumilia na hatimae kushinda.

Lengo kuu la kitabu hiki ni kukuwezesha kuwa na fikra na morali wa ushindi ili kumpatia Mungu heshima. Naye alishasema kuwa akiinuliwa, atawavuta wote kuja kwake. Hii inatupa kufahamu kuwa Mungu akiinuliwa na aliyelibeba jina lake naye anainuliwa. Huduma itapokea kibali maana watu watavutwa kuja kwake, na aliyelibeba jina lake anainuka na jina lililoinuliwa.

Heshima inakuja mwishoni, sio mwanzoni, mwanzoni ni kudharauliwa na kubezwa, kama ilivyokuwa kwa Ayubu, ni majira ya kuzingirwa na marafiki wataabishaji. Sio majira mazuri bali ni magunu, hakuna anayekuelewa. Ila ukishinda ndipo heshima huja. Kama ilivyokuwa kwa Ayubu, mwisho wake ulijawa na utukufu kiasi cha adui zake kuishilia kwenye matengenezo.

Kwa Meshaki, Shedraka, na Aberinego sanjari na Danieli ndivyo ilivyokuwa, waliinuliwa mara dufu mara baada ya ushindi wao. Na kwako inawezekana kama tu utaamua kumtazama Mungu kwa sura tajwa humu kitahuni. Karibu na Mungu akupe kuyaelewa haha:

Tafadhali Kitabu kikitoka  kinunuwe.. zaidi tembelea

www.ukombozigospel.blogspot.com

Jiunge nasi pia kwenye WhatsApp group letu la mafundisho ya neno la hapa: https://chat.whatsapp.com/E0eD0xegh1eIGMjRykPyRD


Kundi letu la Telegram https://t.me/+fft3GHXC9xIzYjhk


Namba ya Telegram au Mawasiliano: +255759859287

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni