Pichani ni Mwalimu Oscar Samba (aliyepo katikati kwenye picha ya Kwanza) akiongoza kikosi kazi cha Wanainjili wakiwa katika maandalizi ya mkutano kwa kufunga Jukwaa.
Mkutano huo ulianza hivi leo katika viwanja vya Kwarogati vilivyopo Shimbi Mashami. Ikiwa ni mfululizo wa mikutano 12 aliyonayo hadi kufikia mwezi wa tisa mwaka huu. Huu ni mkutano wa tatu ukitanguliwa na miwili iliyofanyika shuleni kwaikuru Sekondari juma lilopita na ule wa Shuleni Kwasondo uliotangulia.
Ujumbe: KUU NA UWEZA WA YESU JINSI ULIVYO Waefeso 1:18-23. (Kwa Rogati)
Ujumbe wa Kwasondo :MUNGU, MUNGU ANAYESAMEHE MAKOSA Isaya 43:25
Na Kwaikuru ni : HATIMA YA MAISHA YAKO Yohana 14:3
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni