Jumatatu, 13 Desemba 2021

SULUHU KWA JAMIII AU ENEO LENYE KUKABILIWÀ NA TATIZO LA WATU KUJIUA

Na Mwalimu Oscar Samba

Mithali 28:17 Aliyelemewa na damu ya mtu Atalikimbilia shimo; wala mtu asimzuie.

Andiko hilo hapo la Mithali linatupa kufahamu kuwa watu wanaojiua au kukimbilia mauti (ambao hapo imetumika au yametumika maneno kukimbilia shimo) ni matokeo ya kulemewa au kuwa na deni au mzigo wa damu iliyowahi kumwagika.

Sasa inawezekani aliimwaga yeye, au imemwaga kwenye eneo anaoloishi ama i juu ya uzao au jamii yake. Kwa ujumla ni kwamba kuna deni juu yake.

Damu huweza kukaa kwenye uzao nasi twajua hivyo, maana hata wale waliomsulibisha Yesu walikiri kuwa iwe juu yao na uzao wao. Pia eneo laweza kubeba damu maana hata aridhi iliyonunuliwa na fedha za usaliti wa Yuda ilitwa konde la damu.

Lakini pia damu ya Habili ililia kutoka aridhini. Kuna somo au kipengele cha kwenye kitabu fulani nichowahi kukiandika kinaitwa, ARIDHI KAMA KIUMBE HAI. Hapo nafunza vyema namna ya kushughulika na mambo kama haya.