Jumapili, 1 Novemba 2020

MATESO, MAPITO SIO ISHARA YA KUPUNGUA, KUFIFIA AU KUTOKUWEPO KWA PENDO LA KRITO PAMOJA NAWE.

Na Mwalimu Oscar Samba.

Ujumbe huu ni sehemu ya kitabu chetu cha MUNGU ANAKUPENDA, chenye mukutadha wa kukujulisha hata katika taabu yako pendo lake lingali lipo hapo!

Wiki hii, (wakati mada hii inaandikwa) nilimuliza Mwalimu anayetufundisha kitabu cha Matendo ya Mitume swali gumu sana, ambalo lilisadifu ujumbe huu ambao ninauleta mbele yako siku ya leo!

Nilimuliza ama nalitaka kujua kuwa kweli ni Mungu huyu huyu liyejifunua kwa Stefano wakati anapiga mawe! Stefano anasema anamuona mwana wa Adamu au wa Mungu katika mkono wa kuume, tena tunaambiwa alikuwa amejaa Roho, kwa hiyo utatu mtakatifu ulikwepo ukimtazama au uwepo wake ulikwepo pamoja naye!