Jumanne, 13 Februari 2018

MSAADA KWA WALIOWAI KUMWAGA DAMU YAANI KUUA

Na Mwalimu Oscar Samba #UgMinistry  #SHARE  #SAMBAZA Ili kueneza injili hii Zaidi.
Ujumbe huu ni sehemu ya kitabu changu cha SABABU ZA DAMU YA YESU KUWA NA NGUVU ILIYO NAYO.

  Kama uliwai kuua mtu, kwa kukusudia au bila kudhamiria, kwa njia ya ajli, au kutumia silaha, kutoa mimba, ukiwa kama mama wa mtoto, baba, dakitari, au kushiriki kiushauri ama kiuwezeshaji ama kwa njia yoyote ile.

Pia hata kama ulihusika katika mauaji ya mtu au watu, kwa njia yoyote, ikiwemo ya ushauri, kupanga mipango, au unafahamu fika na bayana kuwa damu ya mtu fulani ipo juu yenu, au juu yako, au katika eneo unaloishi njia hii itafanyika msaada kwako au kwenu Lakini pia hata kama wewe ni asikari, au mwanajeshi, na uliwai kumwaga damu, haijalisha uliona ina hatia au la, ila ujue ukweli wa hatia hiyo na uhalali wa mauaji hayo anayefahamu ni Mungu mwenyewe, Shetani na damu husika , kwa hiyo nawe yafanye haya maombi, ukijaribu kujihesabia haki kuwa ulikuwa ukitimiza wajibu wako sawa, au uliwajibika kufanya hivyo na haoni kosa lako, “it’s ok,” ila kwa ushauri wangu na waimizo la Roho Mtakatifu ndani yangu, huna budi kufanya hivyo:
Hakikisha unainyamazisha hiyo damu, ili isiendelee kunena mabaya au kulia kisasi au malipizi kwenye ulimwengu wa roho. Lakini kanuni ya kwanza;

1. Omba Rehema, tubia tukio hilo, muombe Mungu akusamehe, wala usijihesesabie haki, kwa namna yoyote ile. Tumia Damu ya Yesu katika kutubia hilo kosa, ombea rehema kutokana na umwajikaji wa Damu ya Yesu kwa ajili ya ondole la dhambi, Mathayo 26:28. Omba hadi upate mani ya kiungu moyoni mwako.

Jumamosi, 3 Februari 2018

Pata Dondoo za KITABU UCHUMBA SALAMA KATIKA KRISTO YESU Katika mada ya Namna ya Kuishi Salama Maisha ya Uchumba hadi Ndoa. Utajionea Hatua Muhimu za Kuchukua, Ikiwemo ya Kuchagua Mshenga Wajibu wake, Madili na Wasifu wake:

Namna ya Kuishi Salama Maisha ya Uchumba hadi Ndoa.
Kusudio la mada hii ni kukuwezesha kuishi vyema kiroho na kimwili, au kiushuhuda katika maisha ya uchumba.
Swala la ushuhuda ni muhimu sana katika hatua hii maana litawajengea heshima, kwa jamii, jamaa wako wa karibu kiundugu na kanisa kiujumla, kwa hiyo ipo haja ya kuwa salama kiroho na kimtazamo au machoni pa watu pia.
Maana ni vizuri kuhesabiwa haki na Mungu lakini pia wanadamu wakuheshimu. Maana hali hii itakupa haki kwao, lakini pia itaifanya huduma yako kukubalika, maana katika ulimwengu huu tunamuhitaji Mungu kweli ili tufanikiwe, lakini pia tunawahitaji wanadamu, na wanadamu hutazama kwa macho ya kimwili ili kuona, sio ya moyoni na nje kama Mungu.
Maana yangu hapa ni kukutaka kuepukana na mitazamo finyu ya vijana kadha kuwa anaishi kama vile atakavyo yeye madamu hatendi dhambi kwake sio mbaya.
Na kujaribu kutengeneza mazingira ya ushuhuda kwake ni unafiki, huku ni kukosa maarifa.
Hali ya kupita kila kona, au kukaa ovyo na mwenzako ama kukutana katika mazingira hatarishi kwa mujibu wa mboni za wanadamu, kwa madai kuwa nyie mpo vema kiroho hata kama hamtendi kosa la kukutana kimwili, lakini pia kufanya hivyo ni dhambi.
Inaweza isiwe na madhara au matokeo kama vile ya kujamiiana, ila hali ya kuharibu ushuhuda kwa makusudi ni kosa kiroho.
Paulo Mtume anasema sisi ni barua, licha ya hivyo, anatuambia kama akila nyama itamkwaza jirani yake, yupo tayari kutokuila, unaweza kujione uchaji wa mtumishi huyu ulivyokuwa mkubwa.
Kwa hiyo nawe unawajibika kujiwekea mazingira salama ili jina la Bwana lisitukanwe, hali ya kusema kuwa Mungu anatizama moyo, au ya kuku mayai na ya watu maneno, eti huwezi kuwazuilia kunena, unapaswa kuwa makini ili kumtetea Kristo.
“Madamu sitazini, si dhambi mtumishi.” Acha ujinga, linda ushuhuda.
Huduma nyingi za watu zimekufa, kwa kukosa hii hekima, zimeishilia kupakwa matope na uvundo wa kila namna.                      Karibu:
(a) Jinsi ya Kutenda Vyema.
(i) Zifahamu Sheria au kanuni za Kanisani kwako, makanisa mbalimbali yametofautia kivigezo, yapo ambayo ili ufunge ndoa au hata uchumba kutangazwa ni lazima, muhusika awe anaudhuria ibada za Ushemasi, Seli, au Jumuia, wenine huziita ibada za Nyumbani, au Kanisa la nyumbani.
Hususani makanisa makubwa huwa na sera hii ili kuweza kuwa na taarifa sahihi za mtu anayenuia kuchukuwa hatua hiyo, kwani kama kanisa lina watu wengi ni vigumu kwa uongozi wa kanisa la mahali pamoja, kujua tabia zake, na kama kweli ana vigezo na sifa za kufikia hatua hiyo, maana wengine huweza kuwa na ndoa nyingine au alishawai kuolewa, na muda wake katika wokovu, na pia hali yake ya kiroho.
Kwa mantiki hiyo, kikundi cha ibada za Jumuia, huweza kukufahamu vizuri zaidi.
Lakini pia wengine, ni shariti uwe umelipa au kutoa Zaka ama fungu la kumi, kwa kipindi kisicho pungua miezi 6.
Pia vigezo vya muda wako wa wokovu au kuabudu hapo kanisani ni muhimu sana.
Kufahamu kanuni na taratibu kama hizo, kutakusaidia kutokuingia katika malumbano ya kihoja na wahusika, pia kutakuokolea muda, licha ya kukuokolea muda kutakufanya kutenda vyema.
Maana nimewaona watu walioabudu makanisani muda wa miaka mingi lakini kwa kuwa walipohamia walihamia kienyeji, yaani bila barua ya utambulisho, walijikuta wakizuiliwa, kuchuku hatua hizi za Uchumba hadi ndoa, na swala lipo sana kwenye huduma zenye watu wengi.
Hatua za Kuchukuwa mkishakubaliana:
(ii) Nendeni kwa Mchungaji, kama mna abudu katika makanisa tofauti tofauti, ni vyema mkaanza katika kanisa la kijana wa kiume, au tumieni utaratibu kwa kila muhusika kumuendea mchungaji wake, na mara baada ya hapo ndipo muwaende walezi wate. Ila kibusara anzeni kwa wakiume.
Ili kulinda ushuhuda mnaweza kuamua kukutana kanisani, ama kutumia utaratibu wa kuambatana na washenga au mshenga.
 (iii) Tafuta Mshenga na uambatane nae, ni muhimu kuanza kutafuta mtu huyu maana atafanyika msaada mkubwa kwako, kama utatambua nafasi yake vyema.
Lakini mara baada ya kumpa, huna budi kuhakikisha kuwa unambatana nae, ili kutimiza adhima na dhima ya uwepo wake.
Sifa za Mshenga:
(1) Awe Mchamungu, sifa hii ni muhimu ili aweze kukubeba rohoni, na kukushauri kiroho, lakini pia aweze kukulinda vyema kiroho, pia asije kuhusika katika kukushawishi kuingia majaribuni, pia ili kumrahishia Mungu pale atakapotaka kufikisha jambo fulani kwenu aidha kwa njia ya mashauri na mahusia kutoka kwake.
(2) Awe na uelewa wa kutosha kuhusu Mambo haya, Anapaswa kuyafahamu kwa kiasi fulani maswala ya uchumba, ili aweze kukaa vyema kwenye nafasi yake.
(3) Awe na Uwezo wa Kukushauri na Ujasiri wa Kukukemea, Ajawe na Hekima lakini pia Busara, ili kukusaidia katika kuchukuwa maamuzi fulani, maana kuna majira mambo huweza kuwa magumu kiutatuzi, ila hekima yake na Busara zake huweza kutumika katika kuleta utatuzi.
Lakini pia ipo sifa ya ujasiri katika kukukemea au kukuonya, ni makosa kumtafuta mtu ambae unajua utampiga chenga au kumkwepa ukiwa na nia ya hila moyoni mwako.
Lakini pia mtu muoga hakufai, ni shariti awe na uwezo wakukukemea, na kukuzuilia kufanya jambo fulani au kuziende njia fulani.
AKikuona unataka kukata tamaa, au kutenda kinyume na maadili ya kiroho, kijamii ama kikanisa aweze kukwambia waziwazi, kuwa hivi na vile sio sawa, na wakati mwingine kuchukuwa hatua za kufikisha malalamiko yake katika ngazi husika ili kukulinda, huku wewe nawe ukiwa mwepesi na mwenye moyo mnyofu katika kuonyeka, na kuwekewa mipaka kiroho, kimwili, huku ukitambua ni kwa ajili yako, na kwa usalama wako, na huyo anatimiza tu wajibu wake, tena kwako.
(4) Awe Rafiki yako wa Karibu, yaani anayekujua vizuri, kitabia, kiimani, kiitikadi na hata kimaisha.
Licha ya mambo hayo kumuwezesha yeye kukuelezea vyema ukweni ama popote itakapohitajika bila kubabaika au kukurejelea mara kwa mara.
Pia itamsaidia katika kuchukulina nawe, kiudhaifu, kiuchumi, na hata kiitikadi.
Na jambo hili litamfanya kuwa mshauri, na mlinzi mzuri kwako, ukizingatia miongoni mwa dhima yake ni kukulinda kimwili, na kiroho pia.
Lakini urafiki huu usiwe wa kiundani kiasi cha yeye kukuonea haya katika kukulinda ama kukuzuilia kitu fulani.
Majukumu na Taswira ya Mshenga :
(1) Kukushauri, (2) Kukulinda kiroho ili msianguke dhambini, ni wajibu wake, kuwa karibu nanyi, ili kuwasaidia msiwe na ukaribu ambao unaweza kumpa Ibilisi au hisia zenu nafasi ya kuwatia majaribuni.
 (3) Kukusemea au kunena, ni msemaji badala yako ukweni au kukuwakilisha punde atakapo hitajika kufanya hivyo, popote kiuchumba.
(4) Kutatua Migogoro, Ngazi muhimu ya kwanza, punde kunapo tokea tatizo ni kwa mshenga, maana sio kila tatizo mtalipeleka kwa watumishi, walezi au wazazi ama wa dhamini watarajiwa wa ndoa.
(5) Kukulinda Kimwili, walioingia kwenye ndoa watakuwa wepesi wa kukubaliana nami, kuwa, wiki au siku chache kabla ya kufunga arusi, muhusika huwa katika wakati mgumu hususani katika usalama wa kimawazo.
Kwa hiyo anahitaji mtu wakutembea naye, ili kumsaidia kuepukana na kadhia ya kupigiwa honi kila wakati, na hata kumuepushia na kugongwa.
Lakini wapo ambao huishilia kuwa na mawazo mengi yamkini kutokana na baathi ya mambo kutoenenda sawa, kwa hiyo wanahitaji mfariji ili waweze kujipa moyo, lakini wengine hushindwa kula chakula, kwa hiyo mshenga ana dhima ya kumsaidia ili ale na wapo ambao hali hiyo hutokana na kuwa na mambo mengi.
(6) Ni Msaidizi kimajukumu, katika swala la kununua nguo au kushona, ni mtu muhimu kuongozana nae, maana licha ya kukushauri, lakini pia atakusaidia katika mambo mengi.
NB: Majukumu mengine hutokana na tamaduni na desturi za mahali unapo owa au muelewaji anapotoka.
Makabila mengine Mshenga huusika katika kumsaidia rafiki yake kutekeleza majukumu ya kimahari, kama kuchinja, kupika, kumbebea chakula na kumpelekea wakati wa sherehe za kimahari, na hata kubeba vitu vya mahari na kumpokelea zawadi. Kwa hiyo ni muhimu kuzifahamu zilizo za kabila husika ili kurahisisha utekelezwaji wake.
Tabia Madhubuti ama Sifa nyingine na Maadili ya Mshenga Mzuri:
(1) Awe wa Jinsia yako, yaani kijana wa kiume, awe na Mshenga wa kiume, na wa kike awe na Mshenga wa kike, hii ni sifa ya ulazima na umuhimu kuliko zote, na ipo wazi natumia haihitaji maelezo mengi.
Itakusaidia kuwa huru kwake, pili utakuwa katika mikono salama kihisia na kiroho pia.
(2) Awe anapatika kirahisi, Ni muhimu muda wake uwe haujambana sana, ili kurahisisha ufanyaji wa majukumu yake, maana kuna mipango mingine itamuhitaji kuwajibika usiku, mchana, na kila uchwao.
(3) Awe Tayari, jambo la utayari kwake ni muhimu sana, maana kazi hii haina malipo, na huchukuwa muda, na huvuruga ratiba pia, lakini pia, inahitaji kujitoa kiroho na hata kimwili, na kiucmi.
Maana kuna mahali atalazimika kwenda na nauli zake au gharama zake kulingana na uwezo wa kiuchumi wa muhusika.
Kwa hiyo sio busara hata kidogo kumlazimisha mtu ama kumshawishi kupita kiasi angali unajua hayupo tayari, kwani utakayeteseka au kukwama huko mbeleni ni wewe.
(4). Mwenye Lugha Nzuri, na Muongeji, “Msemaji.” Maneno yake ya kolee munyu, maana ukweni ni mahali panapohitaji heshima.
Lakini pia awe na uwezo wa kuongea hususani mshenga wa kijana wa kiume, maana ukweni atahitajika kupanga hoja zenye nguvu hususani linapofika swala la mahari, maana huyu hushirikiana na wazee katika kuhakikisha mahari inayopangwa utaimudu, ndiposa ni shariti awe ni mtu ambae anakufahamu vyema, ili akuongele vizuri.
(5). Awe Muombaji, Huu ni mtu anaye wafahamu kiukaribu mno, kwa hiyo ni rahisi kuwabeba kimaombi jambo ambalo litakuwa jema kwenu na kuwatulia mzigo.
(6)  Awe Mtu wa suluhu, sio mpenda shari, au mshindani wa mambo. Jambo hili litakusaidia katika utatuzi wa matatizo, pamoja na wakati wa kujenga hoja kama mwakilishi wako kwenye vikao, na kuzima mashauri yenye chembe chembe za shari kwenye vikao.
(7) Asiwe mwenye Wivu, Wivu ulimfanya Sauli kutengeneza hila dhidi ya Daudi, na kumpakazia yaliyo maovui ili amvurugie.
Kwa hiyo kuwa makini na tabia hii kwa unayemchagua maana kwa nafasi yake, huweza kukuvurugia au kutumiwa kuvuruga mipango yenu na Ibilisi.
Mwanzo 30
1 Naye Raheli alipoona ya kuwa hamzalii Yakobo mwana, Raheli alimwonea ndugu yake wivu. Akamwambia Yakobo, Nipe wana; kama sivyo, nitakufa mimi.
Hii ni tabia ya wivu, tazama mtu anatishia kufa, au kufikia hatua ya kutamani kufa, shauri ya wivu, na kwako huweza kufikia hatua ya kutamani kufanya lolote ili akuvurugie, hata kuwawekea sumu. Kaini alimua nduguye shauri ya wivu.
Umakini ni muhimu mno, Mithali 27: 4 Ghadhabu ni kali, na hasira ni gharika; Lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya wivu.
Onyo kwa wenye Wivu: Ayubu 5: 2 Kwani hasira humwua mtu mpumbavu, Nao wivu humwua mjinga.
(8) Asiwe Mtu ambaye Mlipishana kimasilai, wakati wa Kuchumbia, ama mwenye mahusiano ya kiundugu na wewe, au huyo mwenzako, lakini pia asiwe mtu ambae aliwahi kuwa na mahusinano ya kiurafiki ama kimapenzi na mchumba ako.
Akiwa ndugu yako, anaweza kukuonea haya baathi ya nyakati, au asitekeleze vyema wajibu wake, katika kukukaripia na hata kukushauri,  lakini pia akiwa ndugu wa mwenzako, ipo aibu itakayo mfunika wakati wakutekeleza majukumu yake, lakini pia, kiujumla, hataweza kutenda vyema, aidha kwakuegemea upande fulani, na kadhalika.
Lakini akiwa ni mtu ambae alisawai kuwa na mahusiano ya kimapenzi, au aliwai kuchumbiana na mwenzako, hakika hataweza kufanya majukumu yake kwa ufanisi na haijalishi amekuadia kutende vyema au ni mwaminifu kwa kiasi gani, kwani kuna mambo mengine moyo na nafsi ya mtu huwa na nguvu kuliko yeye.
(9) Asiwe ni wakuwaka Tamaa au Mwenye Pepo hilo, sifa hii ni muhimu ili kumzuilia kumtamani au kumpiga chenga rafiki yake. Yaani asije akateta na shemeji yake. Vijana wanamuita mtu kama huyu, “Penda-penda.”
(10) Ajuwe Mipaka Yake na Kuiishi Vyema, Ni muhimu kujifahamu kuwa yeye ni msenga wala sio bwana au bibi arusi mtarajiwa.
Kufahamu huku kutamfanya, kujua lugha za kunena na shemeji, uso wa kutazamana naye, majibu ya kumpa, pia wakati wahusika wanaonge au kupanga mambo fulani, atafahamu hatua za kukaa nao, au umbali na ukaribu, pia atahakikisha hawi kero, kizuizi ama kipingamizi cha mahusiano yao na hata tenda nje ya majukumu, wajibu na mwenendo wake.
Pia hata weza kuwa msemaji, mapangaji au mzungumzaji wa kila jambo, bali kuna mengine ni shariti aombe hizini ya muhusika au kumtaka kujinenea mwenyewe.
(11) Asijiweke au kujitegenezea mazingira yakutiliwa mashaka, Ewe mshenga, hakikisha unalinda ushuhuda wako, kama kuna umuhimu wa kukutana na shemeji bila rafiki yako kuwepo, basi hakikisha ni katika mahali ambapo hapata leta mashaka kifikra na kimtazamo, ikiwezekana iwe kanisani na rafiki yako lazima ajuwe. Usidhubutu kumficha hata kama ikiwa ni shemeji amekutaka kufanya hivyo, pia mshenga mwenza, yaani yule wa shemeji yako ni shariti afahamu na awepo eneo la tukio hata kama hatasikiliza ila awe karibu mahali ambapo upeo wa macho yake waweza fika bila kupapasa, kumbuka mazingira mazuri ni kanisani na maeneo ya wazi.
Taadhari: We! Mshenga shemeji akikutaka, usimlekezee macho, wala kutumia hata sekunde moja kumsikiliza, bali mkemee huku ukitimua mbio kama Yusufu kwa mke wa Potifa.
Lakini pia, hima vunja, Ushenga, ama jiuzulu haraka iwezekanavyo.
Mwisho mwambie rafiki yako ubaya wa shemeji, mwambie ili ajuwe kuwa nazi aliyoichagua ni korona.
Usi dhubutu kumficha kwa kuhofia Uchumba kuvunjika, maana madhara ya mateso atakayokuja kuyapata ni makubwa zaidi, nawe nafsi itakuhukumu pale utakapo yaona, na kumbwambia itamsadia kuchukuwa maamuzi mapema, na kama hata chukua zigo la lawama halitakuwa juu yako.
Wala usijiulize kuwa atakuamini au la, wewe sema kuamini au kukataa ni juu yake, yeye mwenyewe.
(12) Mwenendo Mwema, Utauwa, hali ya kujitoa, na hata nidhamu ya kimaisha ni miongoni mwa maadili muhimu sana kwake.
Pia swala la uvaaji vizuri ni muhimu ili asije kukuabisha ukweni, na kwa marafiki wa mwenzako na jamaa yake, maana rafiki wa mtu ni mtu, yaani jinsi watakavyomtazama yeye, ndivyo watakavyokuona wewe. Kwa ujumla unapaswa kushirikiana na Roho Mtakatifu, katika kumchagua Mshenga, maana dhima yake huweza kuendelea hata baada ya maisha ya uchumba kuisha, wengi hufanyika marafiki wa kudumu wa ndoa, na washauri, na walezi pia.
Hususani ndoa inapokuwa changa inahitaji sana watu wa karibu wanao wafahamu vyema, ili kuweza kushiriki mambo muhimu na nyeti vyema zaidi.
(13). Awe Mtunza siri, kwa makusudi kabisa nimeiweka sifa hii kuwa ya mwisho kwani kikanuni za kiuandishi nilipaswa kumalizia na maelezo yaliyopo kwenye pwenti iliyotangulia maana ina maudhui ya kihitimisho. Nami nimeiweka hapa ili isalie vyema moyoni mwako.
Kutunza siri ni muhimu sana, maana sio kila jambo lina wahitaji watu kujua, na utanzaji huu utadumisha heshima yako na ya wahusika pia;
Mithali 25: 9 Ujitetee na mwenzako peke yake; Bali usiifunue siri ya mtu mwingine.
Kuna swali linakuja nafsini mwangu, Je Mwalimu naweza kuwa na washenga zaidi ya mmoja, yamkini kwa sababu za kutofautiana kiuwezo, umri, na hata kupatika, “nafasi katika muda”.
Jibu: Nimewai kuliona hili, ila kuna hitaji umakini katika kupanga majukumu yao.
Kuna rafiki yangu mmoja ambae hivi sasa ni Mchungaji, ilikuwa hivyo kwake.
Mahali alipokuwa akiolewa, kulikuwa na tamaduni au desturi ngumu kwake, na wazazi wake walikuwa mbali, kwa hiyo alimtumia mshenga mtu mzima na anayezifahamu zile mila na taratibu vyema, maana hapa kijana, asingeweza kukamilisha jambo hili kulingana na baathi ya makabila wazee wake kutokuwa radhi kunena au kuteta na vijana mambo kama haya.
Lakini alikuwa na kijana mwenzake, ambae aliketinae siku ya kugw kwa mkewe mtarajiwa, na natumai pia katika maswala ya kukutana na mwenzake kuna utaratibu aliokuwa nao, maana huyu aliyemuwakilisha ukweni, alikuwa ni mtu mzima kwa hiyo hawezi kumuhitaji kila mara ili kumpa ushirikino anaoutaka anapokutana na mwenzake pia ukizingaia alikuwa ni mtu mwenye majukumu mwengi.
Ila ni muhimu kuwa na mshenga mmoja, na swala la mahari kuwe tu na wazee wa kanisa, au wazazi na watu wazima wa kwenu wakuwakilishe wakisaidiana na mshenga wako.
Maana wakiwa wengi wanaweza kukuvuruga, kiushauri na kadhalika.
(iv). Kapimeni Afya, Upimaji wa afya ni muhimu hususani ugonjwa wa UKIMWI/VVU. Jambo hili linapaswa kifanyika mapema kabla ya uchumba kutangazwa kanisani na utambulisho mwingine kwa jamaa zenu wa karibu.
Likichelewa ni hatari, mfano kuna wachumba ambao walienda kupima ikiwa imebakia siku kama 3, ili wafunge arusi, na mmoja wao alikutwa ni mwadhirika.
Ilibidi washindwe kuendelea, jaribu kuna jinsi lilivyo waathiri, maana jambo la arusi kila mmoja analifahamu, kwa hiyo ni rahisi kujua sababu ya kutokuendelea kwao na mchakato huo.
Lakini kwa kuwa watu waikuwa wameshajianda mmoja wao alilazimika kuchumbia kwa haraka na kufunga ndoa jambo ambalo pia ni hatari maana huweza kufanya hivyo bila kumfahamu muhusika, kwani akili na fikra zanu na saikolojia hazina utulivu wa  kutosha na kumuhusisha kwanu Mungu huwa ni vigumu zaidi.
Kwa hiyo jambo hili lifanyike hima au punde mara baada ya kutoka kwa Mchungaji.



(v). Katowe Posa na Kulipa Mahari, Kama upo kwenye kanisa makini na lenye utaratibu sawia, litakusaidia kukupa wazee, na wewe pamoja na mshenga wako na jamaa za kwenu mtaelekea ukweni kwa ajili ya posa na hatimae mahari.
Kitabu kikitoka, Usikubali kikupite maana yapo mengi zaidi ya hayo ikiwemo mbinu za kumpata huyu mwenzi, na kuhakikisha kama kweli katoka kwa Mungu.
Na Mwalimu Oscar Samba #UgMinistry #SHARE #SAMBAZA Ili kueneza injili hii Zaidi.
Kama hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na BWANA kwa upya leo, tafadhali fuatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU, ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
Na Huduma ya UKOMBOZI GOSPEL, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigospel@gmail.com Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigospel.blogspot.com 
Pia #Like #Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata habari hizi kwa haraka, zaidi. @ugukombozi Gospel 
PAGE: https://www.facebook.com/ugukombozigospel/ 
Kikundi: https://www.facebook.com/groups/2268418230050621/ 
Pia kwenye mtando Mpya wakitanzania wa 
2 DAY SKY: https://www.2daysky.com/ukombozigospel 
Pia TAZAMA VIDEO ZETU HAPAhttps://www.youtube.com/channel/UCv1tghnugOSpbmb5h6ebJtA (Ukombozi Gospel)