Basi, Bwana ajua kuwaokoa watauwa na majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hata siku ya hukumu. 2 Petro 2:9.
Wakati wana
wa Israeli wanalia, wanalalamika, wanaumia ama wanaonyesha hisia zao kutokana
na ugumu wa mateso yale ya nchi ya utumwa wa Misri, Mungu kwa upande mwingine
alikuwa akitekeleza mipango ya kuwaokoa kwenye ile nchi!
Hakuna mtu
aliyekuwa akiona, kutambua, au kufahamu kuwa upande wa pili Mungu alikuwa
akimpatia Musa maelekezo ya namna ya kuwatoa kwenye ile ncchi!
Na hata kabla
ya hapo, Mungu alikuwa akimuandaa Musa kwa ajili ya swala hilo, sio kwamba tu
alilifanya hilo wakati Musa akiwa Midiani, bali hata kabla ya Musa kukimbilia
huko Mungu alishamuandaa, ndio maana yale mahubiri yake kwenye kitabu kile cha Matendo
ya Mitume yanaelelezea vyema kuwa Mungu alimuandaa huyu, ila hakumuelewa
mapema, na wana wa Isreali hawakulielewa lile ndio maana walimkataa kwa wakati
ule!