Jumamosi, 17 Januari 2026

Usiogope Na Uwe Mwaminifu Hadi Kifo

Uwe Mwaminifu hadi kifo maana yake uwe na msimamo ambao utakuwa tayari kulipa gharama yoyote ile.

Pia tunaambiwa ya kuwa, ukishinda kuna madhara utaepukana nayo; hii inatupa kufahamu bayana ya kuwa, zipo faida za ushindi.

 Tazama Andiko : Ufunuo wa Yohana 2:10 Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima. 

11 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili. 

Ninalowiwa kukupatia Majira haya ni kukutia moyo ya kwamba USIOGOPE na nikutake kuwa Mwaminifu huku ukijua mwisho wake kuna ushindi tele.

Maumivu nyakati kama hizi ni muhimu, ila mwisho wake umejaa mafanikio tele...kuna majira unalazimika kuingia gharama kwa ajili ya kulinda kile ulichokibeba ....

majira kama haya sii lazima uaminike na kila mtu....sii lazima ueleweke na kila mtu...

Haikuwa rahisi kwa Yesu kuimili upinzani kutoka kwa Mafarisayo na Masadukayo pamoja na Wakuu wa Makuhani. Hawa kwa mujibu wa Mathayo 23 walikalia kiti cha Musa, kwa hiyo mfumo wa kiroho kipindi hicho ulikuwa "koraptedi". Kwa maana kwamba ulivamiwa na kuongozwa na waharibifu.

Lakini YESU akalazimika kuhakikisha anasimamia mapenzi ya Mungu, akakaza na hata kuuawa...lakini Bwana Akamfufua...(Tazama gharama iliyolipwa...kisha njoo katika ushindi.)

Zaidi Endelea Kututembelea katika Channel Yetu hii ya Wasapu ya ..

Follow the Jipe Moyo 🫀❤️ Utashinda 💪💪🤝 channel on WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029Vb7ZJLR9hXFGDfQuxT2D


Mungu Akubariki

Yamkini Hujaokoka na unaguswa kufanya hivyo Sasa...Karibu

Sema; BWANA YESU, MIMI NI MWENYE DHAMBI, NAKUOMBA UNISAMEHE SASA, AMINA.

Tafuta Kanisa la Watu Waliokoka Ukasali Hapo..

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni