Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Ratiba. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Ratiba. Onyesha machapisho yote

Alhamisi, 20 Aprili 2023

Jana tulianza Mkutano wetu hapa KWA TOKORA katika Kijiji cha MACHAME ALENI Keni Rombo Kilimanjaro Tanzania

 Umenza tarehe 19 hadi 23 (jumatano hadi jumapili) 2023


Ujumbe: UFALME WA MBINGUNI UMEKARBIA. Mathayo 3:2


Hivi Ndivyo Tulivyoitimisha Mkutano wa Injili Katika Zahanati ya Mokala Rombo Klimamnjaro Tarehe 12 hadi 16 Aprili Mwaka 2023

 Ujumbe wa Mkutano huu ulikuwa ni UPENDO WA MUNGU KWA MWANADAMU 

Tukuongozwa na Andiko la Yohana 3:16.

Tazama Baadhi ya Picha za Matukio

Picha hii na Zifanazo na hii ni Watu Waliotoka kwa Ajili ya Kuokoka na Maombezi




Picha hii na hiyo tangulizi hapo juu ni Waimbaji wakiimba Wimbo wa Kichaga na Kucheza "Iriingi".

Jumatatu, 2 Januari 2023

Rombo

#Mkutano #Mkutano #Mkutano Wiki hii; 4-8/1/2023 Katika Viwanja vya Zambia, Mengeni Chini Rombo . Muhubiri: Mwalimu Oscar Samba Walete wagonjwa na wenye mateso mbalimbali na Yesu Mtenda miujiza Atawaponya. Karibu Umsikie Mungu Akisema na Maisha Yako. Tafadhali watakatifu na Wengine

Alhamisi, 8 Desemba 2022

Mkutano Ubaa Posta ya Zamani au Mahakama ya Mwanzo Rombo

Jana Ndivyo Tulivyoanza Mkutano wetu wa 20 hapa Ubaa Posta ya Zamani au Mahakama ya Mwanzo Rombo. Hakika Sijawahi kuona mkutano wenye mwitikio mkubwa km huu! Watu wa Ubaa Hongereni. Nitajitahidi kuhifadhi matukio vyema km nitajaliwa. #Pia_tafadhali_Endelea_Kutuombea

Jumapili, 4 Desemba 2022

Mabadiliko Machache RATIBA ZA MIKUTANO YETU (iliyosalia)

Hadi sasa tangu mwezi wa 7/2022 tupo kwenye mkutano wa 19 18. Kitasha Kakfua (Chekechea) 23-27/11/2022 19. Kitasha; Shule ya Msingi Roya, (umeandaliwa na Kanisa la PSMA) 30/Nov -4/Dec /2022 20. Ubaa, Ushiri. 7-11/12/2022 21. Sio Makalema tena, (badala ya Yamerejea Mamsera ktk Kanisa la Kingdom kwa Mch Daniel.) 14-18/12/2022 22. Himo, 21-25/12/2022 (Moshi Vjjn) 23. Kinyauli, Kerio Mashati. 2-8/1/2022 Mingine Rombo Klnjaro. Na Mwl. O. Samba

Jumapili, 27 Novemba 2022

RATIBA ZA MIKUTANO YETU (iliyosalia)



Hadi sasa tangu mwezi wa 7/2022

 tupo kwenye mkutano wa 18

18. Kitasha Kakfua (Chekechea) 

Unaendelea  23-27/11/2022

19. Kitasha; Shule ya Msingi Roya, 

(umeandaliwa na Kanisa la PSMA)

30/Nov -3/Dec /2022

20. Ubaa, Ushiri. 7-10/12/2022

21. Mamsera Sokoni. 14-17/12/2022

22. Kinyauli, Kerio Mashati. 2-7/1/2022

Ni Rombo Klnjaro. Na Mwl. O. Samba


Jumamosi, 11 Juni 2022

TARATIBA ZA MIKUTANO YETU YA INJILI Shimbi, Maharo Makiidi, Mokala, na Ushirikiano Mkuu Rombo

 Kata ya Shimbi

1. Shuleni KwaSondo 11-24 June 2022

2. Shuleni Kwaikuru 15-19 June 2022

3. Kwa Rogati 22-28 June 2022 

Majira ya 10:30 Jioni 


Jumatano, 3 Julai 2019

JINASUWE KWENYE ROHO AU VIFUNGO VYA KURITHI, FAMILIA, KABILA NA UKOO.

Ujumbe huu ni matokeo ya kiu ya kijana fulani anayesoma kidato cha Sita kunitaka nimfundishe maana amekuwa akisumbuliwa na mkuu wao wa ukoo ambaye humtokea na kumtangazia kumkwamisha kimasomo, japo yeye hamjui maana ni wa miaka mingi, ila hujitambulisha hivyo, na amekuwa akipitia wakati mgumu kitaaluma, hata kugubikwa na usingizi mzito mwalimu aingiapo darasani na kadhalika !
Pia ni nimeelezea jambo hili kiupana sio kitaaluma tu, natumai litakusaidia namna ya kujinasua kindoa, kiuchumi, na hata kimaisha, unapojiona umeokoka ila maisha yako yamekwama kama ndugu zako, una ugonjwa ambao husumbua jamii zako, unatatizo la kindoa kama nduguzo, unakataliwa na ndugu, huna kibali kwao, uwe na hakika hizi roho zipo kazini.

Jumanne, 4 Juni 2019

Usiogope Adui MTAZAME MUNGU, NA TENDA KWA AKILI . Na Mwalimu Oscar Samba.


Zaburi 56:4
Aliinuka Sauli mfalme enzi za Biblia na kujaribu kupigana na shauri la Bwana akimuwinda Daudi aliyekuwa mfalme mtarajiwa kila kona lakini mwisho wake alijikuta akiishilia kwa mganga wa kienyeji na hatimae shauri la Bwana kushinda ndani ya Daudi !
Yamkini huyo anayepigana nawe hana hata cheo cha ubalozi wa nyumba kumi, na uwenda hakuwahi kuwa hata kiranja alipokuwa shule !

Sasa kwa nini uogope ! Ni kwa nini ukubali kutishwa na mwenye mwili wakati yupo awezae kuuzima kwa dakika ama sekunde moja na hata nusu sekunde !

Enzi za wakina Petro ama kanisa la kwanza aliinuka mtu mkoja aliyeitwa Herode, na kujipiga kifua mbele za Mungu wetu ila mwisho wake aliishilia kutafunwa na mdudu hadi kufa !
Farao alijifanya kupigana na taifa teule na mwisho wak

Jumatano, 29 Mei 2019

Usifadhaike, Mungu anajua Unayohotaji.


Mathayo 6:8.
Nami nakuhakikishia kuwa ni Kweli na dhairi kuwa Mungu anajua unayoyahitaji, kwa hiyo huna sababu ya kufadhaika, kukata tamaa, kuhuzunika wala kujawa na wasiwasi, maana Mungu anajua unayoyahitaji, usijisumbukie, wala kupoteza muda mwingi kwa kuwazia adha uliyo nayo, Mungu anajua unayoyahitaji, hii ndio kauli yangu na ya dhati itokayo moyoni mwa Mungu wangu, maana andiko hilo, la dhibitisha hili !
Huna sababu ya kukosa usingizi, kushindwa kula, wala kukosa amani kisa una ukata, au ukwasi

Jumatatu, 19 Juni 2017

RATIBA YA MIKUTANO YETU KUANZIA MWEZI WA 7 MWAKA HUU 2017 NA KUENDELEA

 MWEZI WA 7, TUTAKWEPO ROMBO KWENYE VIWANJA VYA SOKO LA MAMSERA NA MANDA PALE SOKONI KILESI. MWEZI WA 8 AU WA 9 TUTAKWEPO TANGA. NA MWEZI 3 MWAKA 2018 TUTAKWEPO KWENYE VIWANJA VYA RELI HAPA MKOANI ARUSHA. BAADA YA HAPO TUTAELEKEA ZANZIBAR ENEO LA DARAJANI KWENYE KIWANJA KILICHOPO MKABALA NA DARAJANI HOTELI. KUMBUKA MIKUTANO YOTE HIYO NI YA SEMINA YA NENO LA MUNGU. ILA KATKA MWAKA HUU PIA TUTAELEKEA KARATU NA TUTAKUJUZA TAREHE.

Jumanne, 16 Mei 2017

Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry aandaa Mkutano Mkuwa wa Semina ya Neno la Mungu kwa Morombo Arusha Tanzania.

Mwalimu wa Neno la Mungu Oscar Samba,wa Huduma ya Ug Ministry, anakuletea Semina kubwa ya Mkutano wa Neno la Mungu. Itakayofanyika hapa kwa Morombo Mkoani Arusha kuanzia tare 11-19/6/2017. Walete viwete, vipofu na viziwi pamoja na wagonjwa wote ikiwemo wa UKIMWI na Wakoma. Yesu Mtenda miujiza atakwepo katika Mkutano huo. Watu wote mnakaribishwa.